PreGE2025 Jesca Kishoa atangaza kugombea ubunge Iramba Mashariki

PreGE2025 Jesca Kishoa atangaza kugombea ubunge Iramba Mashariki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,717
Reaction score
2,746
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Jesca Kishoa, ametangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Iramba Mashariki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, baada ya kupokea maombi ya wananchi kumtaka awanie nafasi hiyo.

Akizungumza Mei 24, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Iguguno, Wilaya ya Mkalama, Mhe. Kishoa alipokelewa kwa shangwe na wananchi waliomweleza bayana dhamira yao ya kutaka awanie ubunge, wakionesha mabango yenye ujumbe wa kumhimiza kugombea.

“Mheshimiwa Jesca, kama Mwenyezi Mungu atakujalia, tunakuomba ugombee ubunge kupitia jimbo hili. Umefanya kazi kubwa ukiwa mbunge wa viti maalum. Tuna imani kuwa ukiwa mwakilishi wetu wa moja kwa moja, utatutetea zaidi,” amesema mmoja wa wananchi waliokuwepo katika mkutano huo.

Naye mkazi wa eneo hilo, Zuber Athumani Juma, amesema wako tayari hata kumchangia gharama za fomu kwani wanaamini ujio wake ndani ya CCM utakuwa ni faida kwa chama na kwa wananchi wa kawaida.

Kishoa amesema amefarijika na mapokezi hayo na kwamba ametiwa moyo kuendeleza harakati za kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

“Leo, Mei 24, ambayo pia ni siku yangu ya kuzaliwa, natangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi. Naomba muendelee kuniunga mkono kama mlivyoniomba nigombee nafasi hii,” amesema Kishoa.

Hatua ya Kishoa inakuja wiki chache baada ya Mbunge mwingine wa Viti Maalum kutoka Mkoa huo, Mhe. Nusrat Hanje, kutangaza kujiunga na CCM na huku akiwa ameshatangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki.

Soma pia: Pre GE2025 - Mbunge wa Viti Maalumu CCM Jesca Kishoa: Kuna kiongozi alinishauri nisisaidie wananchi, alitaka nihonge wajumbe ili nishinde Uchaguzi
 
Huyu mtu inatakiwa akatwe na CCM na Jina lisirudi, alichoonesha ni uchu wa madaraka
 
Kichwa cha habari kinasema anagombea Iramba Mashariki,yeye anasema anagombea Iramba magharibi,kazi kweli
 
Back
Top Bottom