kama inawezekana, tuletee pia piicha za signboard, ule ubao unaonyesha client, consultant, structural engineer, nk. ni muhimu kufahamu hawa watu waliotufikisha hapa. kwa kuwa inasemekana tangu jana jengo lenyewe lilionekana kuegemea upande mmoja. baadaye nitwaambia wakuu wangu, majengi mengi yanayojengwa dsm, si salama, kuna uhuni mwingi. nitaupasua hapa jamvini kwa kuwa hii ndo taaluma yangu. tumepiga kelele mingi sana kwenye semina, warsha nk, lakini taasisi zinazohusika kama ERB, AQRB, CRB, NCC, wameweka pamba maskioni.
Ghorofa jipya lililokuwa likijengwa mitaa ya mtendeni/kisutu limeanguka na kuangukia jengo dogo ambalo watu walikuwa wanaishi. Jengo hilo linasemakana lilikuwa na ghorofa 7 au 8 lilionekana kuegemea upande moja hadi kufikia jana. Nitawaletea taarifa zaidi kadri nitakavyozipata.
waokoaji wakujitolea kama kawaida wameshaanza kazi ingawa nimeliona hata gari la fire nalo limetia timu katika eneo la tukio.
View attachment 1712
Wamiliki ni wahindi wa hili jengo.Limetitia lote.
View attachment 1713
Ngoja tusubili taarifa rasmi kuhusu majeruhi na idadi kamili ya walio kuwemo.
kama sikosei iliundwa tume ya kuchunguza magorofa yote yaliyojengwa dar,lakini hiyo ripoti mpaka leo hatujui ilisema nini.
mkuu fidel 80, kuna signboard inaonekana kwenye picha ya kwanza, tungeiwahi itatusaidia sana, kama ninavyojua, mwenye hili jengo na mhandisi wake watakimbilia kuingoa sasa hivi kuficha ushahidi, tafadhali muiwahi, wenzio tuko mbali sana na dsm.
utasikia amefukuzwa kazi mhandisi wa manispaa! na wasaidizi wake wote, tume imeundwa kufanya uchunguzi.
Tatizo letu bongo kazi tunapeana kiujomba zaidi .... hii inanikumbusha ile habari ya kule maeneo ya Keko lile jengo nalo lilivyo anguka sijui yule mkandarasi alihukumiwa au kesi bado iko mahakamani uchunguzi haujakamilika....?