Jengo la ghorofa kadhaa laanguka mjini DSM!

Kile kibao cha consult eng picha yake haijapatikana?
 
Huu ujenzi wa kubahatisha utaisha lini?

..utaisha pale tutakapo renew contract za city engineers kwa kiasi cha barabara walizotengeneza na kukarabati. pia,kwa ajali kama hizo kutokutokea kwa kipindi cha ajira zao.
 
kinachoshangaza zaidi ni pale watu wanaporuhusiwa kuwa eneo hilo wakati inaonekana wazi kuwa jengo linaweza kuendelea kuanguka. Mkuu wa mkoa pamoja na polisi wapo pale lakini hawazuiii watu kuingia na kutoka hapo bila mpangilio maalum...hii ni hatari kwani watu zaidi wanaweza kufa ikiwa sehemu zilizobaki zitaanguka. nguzo zinaonekana si imara na wakati wowote zitaanguka

Liz,

Umesema nilichokuwa nafikiria.Hivi kama ilijulikana kwamba ghorofa liko unstable, kwa nini hawakuwatoa watu wote walio karibu? Hili zoezi lingeweza kuepusha vifo na mostly ingekuwa hasara ya jengo.

Au ndiyo mambo ya wishful thinking kwamba the problem will go away, people have to sell stationery anyway, we cannot a day without business even at the expense of many lives?
 
Acha tu ndugu yangu! Hapa ukimsikiliza huyo Engineer wa manispaa ya ilala anavyojibizana na waandishi wa habari katika eneo la tukio utaelewa kabisa kwanini jengo hilo limeanguka. amechukuliwa na polisi nafikiri ni kuokoa maisha yake maana tayari wananchi walianza kupandwa na ghadhabu

wapo watu chini ya kifusi wanaweza bado kuwasiliana na waliopo nje lets hope watatoka salama
 
Na ile tume ya LOWASSA kuchunguza kilichotokea kule Changombe Villa ripoti iko wapi?

Lazima sasa tutake majibu ya serikali kwani huenda tukafa wote mpaka tukaisha siku sio nyingi wajameni.

Mungu awape matumaini wote waliopatwa na madhila haya makubwa.
 
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake..... Pole nyingi kwa waliokumbwa na balaa hili wakiwemo walipoteza maisha na majeruhi!!!
 
kweli watanzania tumeonyesha jinsi uwezo wetu wa kufukiri ulivyo.

Cha muhimu ilikuwa kupiga picha kile kibao ......

Duh!
 
Hali ni mbaya sana hadi sasa hv kuna watu wapo kwenye kifusi cha ghorofa na hawana hewa na hadi sasa hivi mkuu wa idara wa ukandarasi wa wilaya ya ILALA ameshikwa na polisi kwa uzembe pia hakuna na magari ya ujenzi ya wilaya ya ilala ni mabovu sema kuna watu watatu chini ambao wapo hai na wanafanyiwa mipango ya kupatiwa hewa hakuna mitambo ya kusukumia hewa sema pia kuna watu ambao idadi ya hajulikani wamakufa...vilevile inasemekana kuna rushwa ilipita kwa sababu jengo halina ubora wowote.
 
msingojee majibu ya tume ya lowasa, yalikuwa ni kusaka umaarufu tu. pia msikimbilie kumhukumu manispaa engineer. ninavyojua, kazi kubwa ya ujenzi wa ghorofa kubwa kama hili huwa inaangaliwa na wafuatao
1. architect-huwa anatengeneza michoro ya jengo lenyewe, na working drawings, kazi yake ni kuangalia kama ujenzi ukianza unafuata michoro aliyochora mwenyewe. ni kazi yake pia kuwasimamia washauri wengine walioko kwenye huo mradi(nitawataja hapa chini

2. quantity surveyor-huyu ni mtaalamu wa gharama za ujenzi, pia ni msomi katika karibu ya fani zote zilizoko kwenye ujenzi, ni wazi kuwa ili ufahamu gharama ya kitu ni lazima ujue kinavyotengenezwa na kinaavyofanya kazi, yeye humshauri cleint kuhusu mambo ya gharama.

3. structural engineer-huyu ndiye mtaalamu wa ubora wa jengo lenyewe, ni lazima atengeneze michoro ya nondo, asimamie ubora wa zege, na mambo mengine yanayohusu ubora na uimara wa jengo lenyewe

4. service engineer-hawa ni pamoja na mhandisi wa umeme, maji, airconditions, lift installation, alarms etc

5. municipa engineer/local authority-kuhakikisha ujenzi umefuata kanuni zote zinazohusu mahali hapo, building permit etc

6. mkandarasi aliyesajiliwa, kwa majengo makubwa kama hili angalau class 111, kutegemeana na gharama

ni wazi kuwa wa kwanza kukammatwa hapo juu ni structural engineer. lakini utashangaa wataanza kupoteza na muda na municipa engineer.

visit pia www.crbtz.com
 
Nasikia Mhandisi wa Manispaa alishatiwa ndani for negligence
 
mwikimbi unaonekana kuujua ujenzi na mtiririko mzima ulivyo.

Anyway, tayari Municipal Engineer kakamatwa na wale waliokuwa wanatazama thru ITV wameona akikamatwa live na kuchukuliwa palepale.

Hii ndiyo Bongo!

Ujenzi holela umeenea kwa kasi kubwa na nikipewa muda wa kupitia majengo mengi ya Dar naweza kuwatia ndani wengi kwa ujenzi wao wa kuudhi!

Mfano mwingine ni Mafuta House... Ni bomu litalolipuka siku za usoni. Kwa waliofika pale na wamesomea Engineering haswa waliosomea Ujenzi wanaweza kukiri jengo liko low quality ile mbaya!

Kariakoo hakuna jengo imara kabisa, nondo zilizojengea majengo mengi ya Kariakoo ni za chuma chakavu na ujenzi wenyewe umefanywa kwa deals tu ambapo ni wazi siku za usoni tuna matukio ya aina hii mengi.

Kwa wenye kumbukumbu nzuri (kuna wahandisi nawafahamu na mpo humu JF) mnaweza kukumbuka Linza Concrete Design walifutiwa leseni (sijui waliruhusiwa vipi) lakini mpaka naandika leo majengo mengi Structural Designer ni Linza!

Wahandisi wengi wanadharirishwa na wapuuzi wachache wanaoendekeza rushwa katika ujenzi na kuwa na upofu wa kufanya Quality Control. Inatia kichefuchefu kwa mhandisi mwenye akili timamu kusimama mbele ya magorofa ya Kariakoo na kuruhusu ujenzi uendelee huku akichekelea eti design nzuri akisahau kuwa linajengwa kwa vifaa dhaifu kabisa ili mradi ana 10% yake.

Tunaelekea kubaya zaidi na serikali isipochukua hatua madhubuti itajikuta kuna miaka kama 5 tu majengo zaidi ya 20 yameporomoka jijini Dar es Salaam.

Huu ni mwanzo tu, bado mengine yatadondoka kwa mwendo huu huu.

Inasikitisha lakini ndivyo tulivyo!
 
Asante mwaikimbi kwa analysis yako. Kuna jambo moja ambalo hata kama viwango vyote vya ujenzi vimefuatwa, jengo na hasa kama ni refu litaporomoka ikiwa hakuna "Verticality control" na kusababisha nguzo kupinda. Sasa ni mtaalamu gani anaye"control' verticality ya jengo? Lazima niseme ukweli kwamba A Professional and qualified Land Surveyor ndiye mtaalamu wa verticality control na ndiye anayejua quality assurance ya unyofu wa jengo kwenda juu (Verticality) hasa kwa majengi marefu. Kwa bahati mbaya katika fani ya uhandisi na ujenzi nchini Tanzania, Land Surveyor ni mtu ambaye hathaminiwi na huonekana kama kibarua tu.

Nini hutokea kwa miradi inayohitaji utaalamu kama hiyo, mara nyingi contaractors wanawachukua "technicians" na kuwafanya surveyors na wakati mwingine "civil engineering technicians' hutumika kama land surveyor. guess what will hapen.

Kwa hiyo katika kujadili suala hili ni lazime ijulikane ni jinsi gani verticality ya jengo ilikuwa controlled na nani alikuwa anafanya hiyo kazi na kwa kutumia vifaa gani na qualification yake.

Hapa lazima nisisitize pamoja na wanataaluma wote wanaohusika katika mabo ya ujenzi wa majengo marefu kwamba "Quality assurance of verticality of high rise building can only be controlled by a qualified and experienced land surveyor" and using high precision survey equipments. Contrary to this, you risk bending of the building, which can lead to collapse.

Cheap is expensive!
 
Last edited:
Nilikuwa mtaa huo wa tukio muda mchache kabla ya ghorofa kuanguka, jengo lenyewe ndo lilikuwa kwenye hatua ya kumalizika hasa sehemu ya paa. Wakati napita pale watu wa TBC1 walikuwa pale na mafundi wote walikuwa pembeni, ndani hakukuwa na mtu na kama kuna mtu atakuwa amekumbwa na mwanguko huo basi atakuwa ni wa ghorofa la jirani

Hapa namaanisha kuwa hali hii ilijitokeza mapema sana na sishangai kama kuna mtu ambaye ni jirani na akawa hana taarifa.

Madhara makubwa ni kwa nyumba za jirani kwani jengo lenyewe lipo katikati ya majengo mengine makubwa. Picha zikitumwa nadhani ,tajionea na kutathimini

HII NDO BONGO, MABAZAZI WANA NAFASI KUBWA KAMA CHUMVI BAHARINI
 
INVISIBLE,Unasema majengo mengi ya Kariakoo yamejengwa kwa kutumia chuma cahakavu, hapo sijakuelewa mkuu naweza pata ufafanuzi kidogo?
 
Mfano mwingine ni Mafuta House... Ni bomu litalolipuka siku za usoni. Kwa waliofika pale na wamesomea Engineering haswa waliosomea Ujenzi wanaweza kukiri jengo liko low quality ile mbaya!

Kuna wakati jengo hili la mafuta house wakati ujenzi ukiendelea kukawa na verticality problem na ndipo wakakurupuka kuajiri Land Surveyor kwa ajili ya ku-control verticality. Kama nilivyosema hapo mwanzo verticality ya jengo inapaswa ianze kuwa controlled tangu jengo linaanza kujengwa. Uimara wa majengo marefu pamoja na viwango vingine vya materials ni pamoja na quality assuarance of the verticality. Several high rise building had this problem Mafuta house (BMW) house and even BoT towers had this problem. Yawezekana yako mengi zaidi.
 
Ile stationary inayosadikiwa imefukiwa ipo upande wa kulia wa picha hizi ndo watu wanako hangaika kuwaokoa wakuu nimeshindwa kupiga picha ya ile bord kuonyesha contractors na client nitajitahidi kupenyeza camera ili nilete news hapa jamvini.

Mkuu hiyo stationery sio ile ilipokuwa marhaba zamani?marhaba ststionery i mean?maana wakati naondoka tz kuna jengo lilikuwepo linajengwa pale.Anyway yalikuwa majengo mawili,mbele ya kituo cha zamani cha mabasi ya kisutu palipo na tawi jipya la barclays na nyuma yake pia kulikuwa na jengo pale,ambapo kuna cul de sac ya kuelekea channel ten,ambapo upande wa nyuma kuna jamhuri street? wakuu ni eneo hilo au jingine?.Nielewesheni hapa
 
INVISIBLE,Unasema majengo mengi ya Kariakoo yamejengwa kwa kutumia chuma cahakavu, hapo sijakuelewa mkuu naweza pata ufafanuzi kidogo?
Ooops, nondo zake mkuu. Zimetengenezwa humu humu kwa kutumia chuma chakavu. They're not tested either.

Got me?
 
mwikimbi unaonekana kuujua ujenzi na mtiririko mzima ulivyo.

Anyway, tayari Municipal Engineer kakamatwa na wale waliokuwa wanatazama thru ITV wameona akikamatwa live na kuchukuliwa palepale.

Hii ndiyo Bongo!

Ujenzi holela umeenea kwa kasi kubwa na nikipewa muda wa kupitia majengo mengi ya Dar naweza kuwatia ndani wengi kwa ujenzi wao wa kuudhi!

Mfano mwingine ni Mafuta House... Ni bomu litalolipuka siku za usoni. Kwa waliofika pale na wamesomea Engineering haswa waliosomea Ujenzi wanaweza kukiri jengo liko low quality ile mbaya!

Kariakoo hakuna jengo imara kabisa, nondo zilizojengea majengo mengi ya Kariakoo ni za chuma chakavu na ujenzi wenyewe umefanywa kwa deals tu ambapo ni wazi siku za usoni tuna matukio ya aina hii mengi.

Kwa wenye kumbukumbu nzuri (kuna wahandisi nawafahamu na mpo humu JF) mnaweza kukumbuka Linza Concrete Design walifutiwa leseni (sijui waliruhusiwa vipi) lakini mpaka naandika leo majengo mengi Structural Designer ni Linza!

Wahandisi wengi wanadharirishwa na wapuuzi wachache wanaoendekeza rushwa katika ujenzi na kuwa na upofu wa kufanya Quality Control. Inatia kichefuchefu kwa mhandisi mwenye akili timamu kusimama mbele ya magorofa ya Kariakoo na kuruhusu ujenzi uendelee huku akichekelea eti design nzuri akisahau kuwa linajengwa kwa vifaa dhaifu kabisa ili mradi ana 10% yake.

Tunaelekea kubaya zaidi na serikali isipochukua hatua madhubuti itajikuta kuna miaka kama 5 tu majengo zaidi ya 20 yameporomoka jijini Dar es Salaam.

Huu ni mwanzo tu, bado mengine yatadondoka kwa mwendo huu huu.

Inasikitisha lakini ndivyo tulivyo!
Hivi Mafuta House ndiyo BWM Tower. Hili lilisimamisha kwa muda wakati wa ujenzi kwa kuwa wakaguzi waliliona limepinda na kushauri libomolewe. Ila baada ya mjadala ulionekana huo udhaifu ni mdogo kulingana na thamani ya jengo. Kama ulivyosema hili ni bomu litakalolipuka muda wowote mbeleni tulipe kama 20 years hivi tukisubiri breaking news.
 
Back
Top Bottom