Jengo la ghorofa kadhaa laanguka mjini DSM!

Jengo la ghorofa kadhaa laanguka mjini DSM!

Mimi nadhani tunaanza kuchanganya mambo. Hakuna haja ya kuunganisha issue hii na ya Kagoda. Hatari ni kuwa tukiipeleka huko itageuka kuwa suala la kiasi badala ya professional negligence and incompetence.

Hao watu wa bodi nao wana nafasi zao lakini mwenye mamlaka na maendelezi ya miji ni manispaa na si mwingine. Kwa hali hiyo, vibali vya ujenzi vinatolewa na yeye na ni yeye mwenye kuwajibika kuhakikisha ujenzi huo unaendana na malengo na sheria zake za maendelezi ya jiji. Hizo bodi wajibu wao ni kufuatilia ufanisi wa wale waliowaandikisha. CRB hawezi kumfuatilia architect au engineer na vile vile kwa AQRB. Wanachoweza kufanya ni kuwashtaki kwa bodi husika. Anayepaswa kubanwa hapa haswa ni manispaa, mwekezaji( kwa kuajiri na kutumia wataalamu na makandarasi wasiostahili na kutohakikisha usalama wa jamii) na wataalamu (architects na wahandisi) kwa kutotoa ushauri unaostahili. Napenda kutoa tahadhari kuwa inabidi hata michoro iliyopitishwa iangaliwe kama ilistahili kupitishwa. AQRB, wakishirikiana na AAT, wafuatilie suala la usimamizi wa architect. Kwa mfano,je palikuwa pakifanyika site meetings na inspections? Kama ndiyo, nani alikuwa akihudhuria na nini kilikuwa kikiamuliwa? CRB wamfuatilie mkandarasi wake kuhusu utendaji wake na kama alikuwa na haki na uwezo wa kazi hiyo. Bodi ya wahandisi wakishirikiana na IET na ACET wamfuatilie mhandisi wao. Hawa wote watoe taarifa itakayotolewa kwa wananchi.

Serikali kuu iangalie kwa undani taratibu za kutoa vibali vya ujenzi na usimamizi wa ujenzi. Mfumo tulionao tumeurithi toka kwa wakoloni, pengine kuna haja ya kuungalia tena. Manispaa zibanwe kuhakikisha kuwa watendaji wanapewa nyenzo za kufanya kile wanachopaswa. Ni aibu kuwa na building inspektaz wasio na usafiri (ingawa kwa hapa hilo halipo maana wangeweza kutembea kutoka ofisini kwao).

Sioni haja ya tume. Wasi wasi wangu ni bodi na mamlaka husika kuanza kunyosheana vidole na kutafuta ujiko kutokana na hii calamity.
 

Napenda kutoa tahadhari kuwa inabidi hata michoro iliyopitishwa iangaliwe kama ilistahili kupitishwa. AQRB, wakishirikiana na AAT, wafuatilie suala la usimamizi wa architect. Kwa mfano,je palikuwa pakifanyika site meetings na inspections? Kama ndiyo, nani alikuwa akihudhuria na nini kilikuwa kikiamuliwa? CRB wamfuatilie mkandarasi wake kuhusu utendaji wake na kama alikuwa na haki na uwezo wa kazi hiyo. Bodi ya wahandisi wakishirikiana na IET na ACET wamfuatilie mhandisi wao. Hawa wote watoe taarifa itakayotolewa kwa wananchi.

Fundi Mchundo,
Nilikuwa na jamaa yangu mmoja Mbongo akifanya kazi kampuni ya EC HARRIS. Huyu jamaa alikuwa akienda kukagua SITE na kukuta mabadiliko yoyote katika nondo au ujenzi, alikuwa akipiga picha na kuweka hayo mabadiliko kwenye michoro na Boss wa site aweke sahihi. Hivi vitu wanavitunza kama mboni ya jicho. Kikitokea chochote basi ujue UTAKUFA PEKE YAKO na wao kama Consultant wanakuwa safiii. Nafikiri kuna haja kwa hali ya ujenzi ninavyoisikia Tz basi mtu unakuwa na kumbukumbu zako zote na kikiwaka basi ujue utaponea wapi. Nikiwa nasomea Ufundi Mchundo miaka ya 80 mwishoni, nilienda practical pale Dar (IFM) wakati wakijenga lile ghorofa jipya. Hapo nikawa kwa mhindi aitwaje DB SHAPRIYA. Hawa jamaa siku ya kumwaga zege alikuja Mhandisi na kuangalia michoro kama iko safi, wakaja watu wa umeme na maji nk na kukuta kila kitu safi. Hao wakaandokoka. Siku iliyofuata nikaona maajabu. Kwanza kokoto no chafu na zina vumbi kweli kweli hadi zege linakuwa jekundu. Pia walikuwa wakikisikia tu na kuangalia rangi ya zege. Yaani waliweka kokoto na mchanga na baadaye cement. Sample kwa ajili ya CUBE TEST walitengeneza kwa kutumia Kokoto zilizosafishwa na kuweka katika ile real rate ya Sand, Agregate and Cement. Wakati huo nilikuwa nashangaa na kusema hili jengo MILELE sintakuja ingia. Ila naona huo ulikuwa mwanzo. Haya ya sasa uzembe hadi kwenye NONDO?? Kazi kwelikweli. Ila kwa USHAURI wangu ni kuwa WAHANDISI mkiwa na kazi na Wahindi au Waswahili basi tunzeni picha ya UZEMBE wanaofanya. Siku moja zitawaokoa.
 

...na iwapo hayo maghorofa wanayakatia bima, fikiria mabilioni watayokuja faidika nayo kwa ulaghai huo baada ya majanga kama haya!


Juu ya kulipwa na BIMA itategemea. Kama BIMA wakiwa NJE YA MTANDAO wao huo basi unaweza kukuta hawapati kitu. Bima na wao wana sheria zao. Kama wakiwa makini ni kiasi cha kusema "Mwenye jengo alifanya UZEMBE na kuonyesha kuwa kwa hali moja au nyingine aliHONGA na kupindisha mambo. Mfano ni hili la kusema Kampuni ya ujenzi haikustahili kujenga hapo kwani ni grade5. Sasa ukishaonyesha kuwa kuna kahongo kalienda, Wahindi na wale wote waliojenga kijinga, walie tu. Itabidi kama una Mjomba sehemu ya BIMA inayohusu kitengo cha Majengo basi muanze kutafuta kiwanja kipya maana MAPESA ya wahindi hayo yaja, SO LONGER MJOMBA ni FISAIDI.
 
Mkuu, Sikonge.
Katika site yeyote ya maana, picha zinapigwa wakati wa ujenzi. hii ni kumlinda mkandarasi na konsaltanti. Mara nyingi katika miradi mikubwa au iliyo nje ya miji, anajiriwa Clerk of Works ambaye ingawa analipwa na Client, anawajibika kwa konsaltant. Huyu anatakiwa kuwepo kila wakati na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya mradi. Huyu, kwa maelekezo ya konsaltant, ndiye anayehakikisha kuwa sample zinatengenezwa kutokana na zege itakayotumiwa. Ukumbuke kuwa si uamuzi wa mkandarasi kuwa ni batch ipi atakayotolea sample bali ni wa konsaltanti. Mkandarasi akifanya kinyume cha maelekezo, konsaltanti ana mamlaka ya kumuamuru afumue zege na apeleke ikafanyiwe uchunguzi. Kwenye miradi yote ya maana, mkandarasi anatakiwa kumuonyesha konsaltanti sample za vifaa anavyotarajia kutumia katika ujenzi. Konsaltanti ana mamlaka ya kuzikataa kama haridhiki nazo au kuamuru kuwa zikapimwe. Konsaltanti akikuta kokoto au mchanga ambao haufai kwenye site ana mamlaka ya kumuamuru mkandarasi aziondoe mara moja kwa gharama yake. Na si kwa hivi tuu, bali vitu vyote (nyaya za umeme, vyoo, taa n.k.) vinavyoingia kwenye mradi vinapaswa kuwa specified na konsaltanti kwenye tender documents na kupitishwa nae kabla ya kutumika. Ndivyo inavyotakiwa. Hatufanyi hivi wote ( nani katika sisi ambaye alijenga banda lake kwa kutumia konsaltanti au mkandarasi?) kwa mawazo finyu ya kukwepa gharama ingawa in the long run tunalipia. Inabidi tubadilike. Unajenga nyumba ya mamilioni lakini unataka mke wako, mume wako au mdogo wako ndiye asimamie!!!!!
 
Local contractors hapa mara nyingi huwa wanalalamika kuwa kazi nyingi zinaenda kwa foreign contractors...sasa kwa mtaji huu,si tunajiangusha wenyewe! Nani sasa hivi ataamini kupanga ofisi kwenye jengo kama hili lililoanguka.Na yako mengi sana haya mjini hapa.Sisemi kuwa ni wote,lakini pia hao wachache ndio wanaleta madhara makubwa zaidi kwa wenzao kwa kuwapa silaha foreign contractors
 
ninavyojua hakuna bima dhidi ya maafa kama hayo, ila kuna bima zifuatazo
1.professional indemnity insurance-hii inatilewa kama kinga kwa wataalamu waliofanya designya hilo jengo, kama mtaalamu anayo hii, na jengo limeanguka kwa ajili inadequtae design, mwenye jengo ata-sue mtaalamu kwa hasara hii, na bima iliyitajwa hapo juu itamlia mwenye jengo kama kinga dhidi ya professional negligence practised by thet professional, eg structural enginner.

2.0 contractors all risk insurance policy iko pia kumkinga contractor na vifaa vyake kama kuna losses

3.0 performance bond- in case performance is not good

anyway, ndo natoka kijijini nilikokuwa kwa week end, ukisiliza kila mwanachi anavyozungumza kwenye hili jambo utashangaa upeo wetu kwenye hayo mambo. kila mmoja anazungumza kuwa, hata zile picha za tv zinaonyesha kuwa cement ilikuwa kidogo, how do you recognized by merely looking at tv pictures?
 
ni rushwa tu hizo! hata kichaa angeweza kusema kuwa gorofa halipo kwenye kiwango
 
kwanza mm ni QS nafikiri mambo mengi sana kuhusu hilo gorofa ,kwanza kuna mangapi ya aina hiyo? Pili baada ya miaka kumi haya magorofa ya kariakoo itakuwaje?
 
kiongozi wa juu anaposhindwa kuongoza nchi ndio mambo kama haya yanatokea.
nchi inanuka ufisadi. kuanzia kwa viongozi wa juu hadi watu wa chini.
kampuni iliyojenga bila ya kibali waacheni warambe rumande na walipe fidia. ikitokea mara moja tu kampuni nyengine zitakuwa makini.
na uhakika ni kuwa kampuni ya ujenzi ikipandishwa kizimbani, mambo mengi yatafichuka na wafanyakazi wa manispaa nao watakuwa waangalifu wa kazi na sio kupokea rushwa
 
Pamoja na kusikitia tukio hili... na the fact kuwa watz hatukawii kusahau... hivi yake majengo yaliyoshikiwa bango kula Masaki na kubomolewa kishkaji...je, ubomoaji huo una manufaa yeyote kwa yeyote?..its such an ugly site..kama ni kuboma wangeyabomoa kabisa na kuondoa debris kieleweke.Au ni janja ili yaje yamaliziwe baada ya dust ku settle?
 
Wenye ghorofa lililoua kortini

2008-06-25 19:26:53
Na Waandishi Wetu, Kisutu

Watu watano wanaotuhimiwa kuhusika katika ujenzi wa Jengo la ghorofa 10 lililoanguka na kuua mtu mmoja Jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi ili kujibu mashtaka kadhaa yanayowakabili.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala Charles Mkumbo amesema tayari Polisi wamekamilisha upelelezi wao na wameamua kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani mapema leo.

Hati ya mashitaka iliyosomwa mahakamani leo asubuhi, imewataja watuhumiwa hao kuwa ni Injinia Brown Kundule, 43, Msanifu majengo Janas Mndeme,58, Atanas Mwageni, 55, na Mkandarasi wa jengo hilo Kantalal Laxman, 58.

Hati hiyo imeonyesha kuwa watuhumiwa wanakabiliwa na shitaka la kuua bila kukusudia.

Kwa mujibu wa hati hiyo, watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa Juni 21 mwaka huu katika mitaa ya Zanaki na Kisutu Ilala Jijini Dar es Salaam, walimuua bila ya kukusudia Shamte Nganoga.

Mpaka wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, watuhumiwa walikuwa tayari wamefikishwa mahakamani hapo wakisubiri kupangiwa Hakimu ili waweze kusomewa mashtaka yao.

Kutoka:http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/06/25/117202.html

Heading inasema wenye jengo lakini mbona siwaoni? Hili ni onyo kwa hao technocrats. Mkiwaendekeza hawa washitiri, when the day of reckoning comes ( as it sure will) mtasimama wenyewe.
 
Kutoka:http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/06/25/117202.html

Heading inasema wenye jengo lakini mbona siwaoni? Hili ni onyo kwa hao technocrats. Mkiwaendekeza hawa washitiri, when the day of reckoning comes ( as it sure will) mtasimama wenyewe.

Crummy press ya Bongo.

Pia linasema mashitaka yanaonyesha watuhumiwa walimuua Shamte Nganoga bila kukusudia.

Ilibidi wasema - na watu ndio wanataka kujua - mafundi wameshitakiwa kwa kufanya uzembe gani, vitendo gani, kumuua marehemu.

Shitaka lazima lilisema kitendo chenyewe, kwa sababu hakuna jinai kama hakuna tendo, mens rea. Journalists sio Wanasheria lakini gazeti la maana lazima liwe na legal reporters.

Magazeti ya Mengi ni feki, na Tanzania hakuna press.
 
Habari yenyewe si imetoka kwenye ALASIRI, hawa ni kawaida yao kudramatize habari, gazet la jion tena.

Ila mshangao wangu ni kwa nini mmiliki wa jengo Bwana Muhsin Somji hakufikishwa mahakamani?Maana kwenye kesi ya lile jengo la Chang'ombe village mbona mmilikia alifikishwa mahakamani? Au kwa kuwa Somji ana fedha nyingi maana yeye ndio owner wa MCSOMS Bureau na Royal Furnishers?
Pili kwa nini hao waliofikishwa mahakamani wameshtakiwa kwa manslaughter?kwanini sio murder? Maana mtu kafa, uchunguzi wa kilichosababisha jengo kudondoka ripoti haijatoka sasa polisi wametumia kigezo gani kuona hii ni manslaughter case? Au tena tunarudi pale pale kwenye influence ya mmiliki? na nia ya wazi ya polisi kutaka hawa wahusika wapate dhamana.
Huyu mjenzi bado anayo majengo kadhaa wa kadhaa anyoendelea kujenga tena marefu kama hilo lililodondoka, je kuna hatua gani madhubuti iliyochukuliwa kuyaaangalia yale yanayoendelea kujengwa na yaliyomalizika kuhusu ubora wake. Mimi mtizamo wangu kuishia kwa Engineer wa manispaa tu is not enough. Contractor Registration Board (CRB) pia wameonyesha udhaifu mkubwa wa kutokagua members wao wanafanya kazi kulingana na class ya leseni zao.
 
kuna habari mbaya juu ya kuanguka kwa jengo la ghorofa tisa, karibu na elia complex barabara ya titi mohamed dsm, inasemekana jengo hili liliangukia pia jengo lingine. maafa yawezekana kuwa ni makubwa
Taifa la wasiokumbuka na nchi ya wasiojifunza...
 
kuna habari mbaya juu ya kuanguka kwa jengo la ghorofa tisa, karibu na elia complex barabara ya titi mohamed dsm, inasemekana jengo hili liliangukia pia jengo lingine. maafa yawezekana kuwa ni makubwa
Miaka 16 mbele orofa lingine linaleta maafa karbia na eneo hilo hilo
 
This is very bad! Yaani jengo hadi lianguke engineer hajaona tu? Na watu wanaoshughulika na majengo walikuwa wanafanya ukaguzi wa hilo jengo pia?
Kisheria hakuna ujenzi usiokaguliwa na kuidhinishwa na city engineer
Hapa kuna watu wazito wawajibishwe moja kwa moja
 
Back
Top Bottom