kuna habari mbaya juu ya kuanguka kwa jengo la ghorofa tisa, karibu na elia complex barabara ya titi mohamed dsm, inasemekana jengo hili liliangukia pia jengo lingine. maafa yawezekana kuwa ni makubwa
Ghorofa jipya lililokuwa likijengwa mitaa ya mtendeni/kisutu limeanguka na kuangukia jengo dogo ambalo watu walikuwa wanaishi. Jengo hilo linasemakana lilikuwa na ghorofa 7 au 8 lilionekana kuegemea upande moja hadi kufikia jana. Nitawaletea taarifa zaidi kadri nitakavyozipata.
Inasemekana hilo jengo ni lipya halijamallizika kujengwa na lilivyoanguka limeangukia gorofa dogo la pembeni na inasemekana wahanga wakubwa ni wale waliokuwa kwenye gorofa la pembendi ambalo nalo inasemekana limebomoka pia....
Kuna breking news hapa,
Kuna jengo la Gorofa kumi limeshuka na kutitia lilikuwa likijengwa.
Walio kuwepo wanadai dalili zilionekana toka asubuhi lilikuwa likitikisika.
Waliamuru mafundi wote watoke.
Lipo karibu na Stand ya Mabus Kisutu zamani mtaa wa Makunganya unaingia kwa ndani kidogo.Ngoja nichukue picha nawatumia.
Na ninafatilia news kamili kama kulikuwa na watu.
Inasadikika kuna watu wamefukiwa wenye stationary pembeni lakini bado haijajulikana idadi ya hao watu walio fukiwa.Ila wamiliki wa jengo nasikia walikuwa busy kutoa vitu baada ya kuona linatikisika.
Wamiliki wenyewe ni WaTZ wa kiasia.
wakuu mimi nimetoka eneo la tukio sasa hivi.
Nawaeeni Picha za kifusi kilicho bakia.
Inasemekana kuna watu wamefukiwa walikuwa na stationary kwa karibu idadi kamili haijapatikana.
Tatizo letu bongo kazi tunapeana kiujomba zaidi .... hii inanikumbusha ile habari ya kule maeneo ya Keko lile jengo nalo lilivyo anguka sijui yule mkandarasi alihukumiwa au kesi bado iko mahakamani uchunguzi haujakamilika....?
kama inawezekana, tuletee pia piicha za signboard, ule ubao unaonyesha client, consultant, structural engineer, nk. ni muhimu kufahamu hawa watu waliotufikisha hapa. kwa kuwa inasemekana tangu jana jengo lenyewe lilionekana kuegemea upande mmoja. baadaye nitwaambia wakuu wangu, majengi mengi yanayojengwa dsm, si salama, kuna uhuni mwingi. nitaupasua hapa jamvini kwa kuwa hii ndo taaluma yangu. tumepiga kelele mingi sana kwenye semina, warsha nk, lakini taasisi zinazohusika kama ERB, AQRB, CRB, NCC, wameweka pamba maskioni.
waokoaji wakujitolea kama kawaida wameshaanza kazi ingawa nimeliona hata gari la fire nalo limetia timu katika eneo la tukio.
Wamiliki ni wahindi wa hili jengo.Limetitia lote.
Ngoja tusubili taarifa rasmi kuhusu majeruhi na idadi kamili ya walio kuwemo.
mkuu fidel 80, kuna signboard inaonekana kwenye picha ya kwanza, tungeiwahi itatusaidia sana, kama ninavyojua, mwenye hili jengo na mhandisi wake watakimbilia kuingoa sasa hivi kuficha ushahidi, tafadhali muiwahi, wenzio tuko mbali sana na dsm.
Hii inanikumbusha jengo lingine pale Arusha linalomilikiwa na Mrema wa Impala, nasikia wamefungua hotel inaitwa Naura Spring! Jengo hilo manispaa na wahandisi walisema siyo salama likasimamishwa kwa muda mrefu. Mrema akawajengea CCM jengo pembeni yake lenye gorofa moja au mbili, akaruhusiwa kuendelea. Kesho na keshokutwa likianguka au likileta maafa mengine sijui itakuwaje. Tuwe serious basi kutetea taaluma zetu maana hawa wanasiasa wanakuwa wameziba masikio, sasa na sisi professionals kwa nini tuanaacha mambo yanaenda ndivyo sivyo?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.