Jenerali Ulimwengu: Hata kwenye upuuzi tuko dhaifu!

Hivi mtu akikufanyia vitu vya hovyo halafu ukamkenulia meno, mtu wa hovyo zaidi ni yupi??

Nadhani watanzania tunahitaji kuelewa hili!!

kwenye demokrasia watu wanapata serikali inayofanana nao. Watanzania wavivu, waoga wa maamuzi magumu, wanafiki (leo unamsema EL kesho ukimuona kanisani unakenua na kumsifia sana kwamba hamna mwingine kama yeye na unamtakia kila la heri katika mapambano yake ya Utawala wa juu). watanzania wanapenda mzaa na upuuzi kama alivyosema Jenerali hata kwenye kazi za muhimu, Watanzania wana chuki na maendeleo ya wenzao na hawapendi kushirikiana kwenye mambo ya maana ya kujenga maisha, kama wazairwaa tunapenda miziki yao, hulka zao, tunaiga majina yao kuitaana papaa nani sijui kwa sababu na sisi tukijiangalia kwenye kioo tunajiona hatuna tofauti nao sana.

Katika mazingira haya wezi wanashamiri na wanasifika na kuonekana ni mfano kwa jamii, wazalendo wanavunjika moyo na wenyewe wanakua wezi kwa sababu ya unafiki wetu, na viongozi tunaotengeneza wote wanakua wa sampuli hii.

Kitu kimoja tu Mungu alitupendelea ni kutupa Nyerere kama Rais wetu wa kwanza vinginevyo tungekua kwenye vita kama Kongo.
 
1. Upuuzi kwa kiasi fulani ni jambo jema.

Sun wu,
Ulimwengu hakandii wasanii katika makala yake hii, anamkandia Mabutu na Zairesation yake.
Amesifia sana muziki wa Congo na juhudi za wananchi(wasanii) wake katika fani hiyo. Na hata kumpa haki yake pale ilipostahiki (dikteta) Mabutu kwa kufadhili/ kuwezesha urithi wa muziki wa ki-Congo kuhifadhiwa.
Mkuu hakuna jambo jema katika upuuzi (upuuzi haufai wala hautakiwi)...

Mkuu nimemuelewa sana Jenerali na wala sibishi kwamba upuuzi haupo ila amejaribu kuweka kwamba kuna kazi fulani ambayo tija yake ni ndogo au haina manufaa.....

kwa kukupa mfano ngoja nichukue mfano wa jamii ya siafu / nyuki.. Utaona kwamba kwenye hawa wadudu kuna mgawanyiko wa kazi baina ya malkia (kutaga na kuhakikisha jamii inaongezeka) askari (kulinda jamii) na wafanyakazi (kutafuta chakula)

Sasa mkuu mfano kama malkia na askari wasipofanya kazi zao na wote wakawa wanafanya kazi ya kutafuta chakula na jamii ika-fail, tutasema kwamba jamii imeendekeza kazi ambayo haina tija au tutasema wafanyakazi ndio wenye makosa au ni (askari na malkia) ndio wenye makosa. Utaona kwamba hapa wafanyakazi wenyewe (ambao wanafanya kazi yao are the only heroes left).., In short there was no need kusema The Multi Billions Dollar Business (Hollywood / Movies) ni upuuzi uliopangwa sababu hii ndio the only commodity ya sehemu ile, na leo Hollywood ikifa uchumi utakufa na watu kukosa kazi...

Kwahio mkuu lets not dilute the issues nakubaliana na upuuzi unaotendeka lakini this slashing somehow imegusa heroes na kuita kazi zao ni kama kiburudisho kwa wafanya kazi wa kweli (just like a Puppet / Muppet pleasing the really wavuja jasho)
 
namuunga mkobo jenerali kwa 100%. na tusiendeleze huu upuuzi wa kuwa na msanii wa bongo flaver kila baada ya nyumba moja mitaani. vijana tukalime tujenge nchi tuachaneni na upuuzi. nakumbuka kuna msanii alishawahi kusema " sio lazima tuwe sote wanamuziki, ingefaa kama wengine mbaki mashabiki" mashabiki twendeni shambani tukirudi tutakuta burudani tujiliwaze. lakini utakuwa upuuzi kama kila mmoja wetu ni mdurudishaji
Mkuu tukalime ?, tukalime ambapo bidhaa zetu zikishakua miundo mbinu mibovu zinaozea mashambani ?
Tukalime ?, wakati mwisho wa siku mkulima analipwa peanuts ?
Tukalime ?, wakati ardhi imeshakuwa bidhaa adimu na kilimo cha kutegemea mvua (bahati nasibu unaweza kutoka bila hata senti....)

Mkuu its all about marketing na kujichuja.., kama wewe kazi yako ni mbovu hautauza na mwisho wa siku utaacha mwenyewe usanii (usanii ni talent huwezi kuamka asubuhi na kusema nakuwa msanii usipokubarika utakufa kifo cha kawaida)..

By the way kipi bora wale wanaojaribu every avenue to make a living au wale wanaobweteka na kukaa vijiweni ? (rest reward those who try na sio kuwaambia kazi hii haifai let them try wakishindwa naturally nao huenda wakajiunga na wenzao vijiweni au kwenye machinga complex) after all thats all the system is able to provide for its citizens baada ya kuua viwanda
 
Just to make my point clear naomba angalia na hapa



Hapo inaonekana kwamba the works of art / talent ni some sort of upuuzi au some minor work.., ambapo sio kweli kila kazi ina faida zake.., kwahio hapa nadhani kwa mfano wa juu tungesema mpuuzi ni yule ambaye hafanyi kazi zake bali anakuwa mtu wa burudani au kuangalia burudani na sio mtoa burudani..

Kwahio kama wakuu wa nchi wanakula bata badala ya kufanya kazi basi wapuuzi ni wakuu wa nchi na sio mtoa bata (bali mla bata bila kuzalisha bata)

AshaDii Nilivyomuelewa Jenerali ni kua ZAire ya Mobutu ilikua haina nafasi nyingine ya mtu kujiendeleza kijamii, kiuchumi au kisiasa na hapo wakatumia muziki, ngoma na sanaa nyingine kama ndiyo maisha yao huku wakiwa siyo waaminifu( wizi mkubwa na mdogo, kutokulipa kodi na uvunjaji mwingine wa sheria ukiwa ni kawaida ya kila siku na huu ni jumla ya upuuzi) Hadi leo upuuzi huu unaendelea kwa jeshi kutokua na nidhamu na huku rasilimali za kitaifa zikiachwa zikiibiwa kirahisi.

Sanaa siyo upuuzi ila itakua upuuzi kama ndiyo kitakua ni kitu pekee cha kujivunia kama taifa ambalo limeshindwa kujiendesha au taifa lililofeli. Huu utakua ni upuuzi. Na huku ndiyo Tanzania tunapoenda, tunalinda upuuzi kila mahali (wezi, rasilimali kuibiwa kirahisi, kuongezeka kwa udini, kushuka kwa elimu n.k) huku tukijiliwaza na sanaa ambazo zina mchango mkubwa katika jamii, lakini hamna jamii inayojulikana kwa sanaa tu pekee yake huku ikiwa imefeli kujiendesha na huu utakua upuuzi na sisi wapuuzi.

Kwa sababu Kongo kisanaa hatujaifikia au hatuifikii, ikifika wakati tukaja kushindwa kujiendesha kama Taifa na kujulikana kwa sanaa tu kama taifa basi sisi tutakua wapuuzi dhaifu (kwa sababu hatuifikii kongo kwa sanaa).
 
nimemsoma jenerali nimepitia walimuelewa pia ambao wanapata taabu kumuelewa na hatawale waliopita tu kikubwa ni kuwa kuna ujumbe kwa watanzania kwa ujumla wetu pamoja na haowalioamua kuwa viongazi wetu makala hii ukitaka kuielewa jaribu uisome kwa kuurudiarudia na uiangalie jamii yetu na matendo ya hao viongozi wet huenda ukauona huo upuuzi unazungunziwa kwenye makala hii
 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!
Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?[/

Hii ndo akili ya watanzania wengi,............akiguswa "panapo" atakimbilia Utaifa, au dini yake.

Ukisoma kwakutafakari utaona neno UPUUZI limetumika vyema ktk kufikisha ujumbe aliodhamiria, sasa kwavile ukweli unauma..........Pole bana...........Tafakari...........chukuwa hatua ......Vua gamba..............Vaa uzalendo.

SERIKALI LEGELEGE.........................
 
Kama alivosema Father of All, hii inahitaji mtu mwenye uelewa wa hali ya juu. Maana nimesoma na bado nadiriki kukiri kuwa bado najiuliza kama hasa nimeelewa vile Ulimwengu alilenga uelewa uwe.

As much as namkubali sana Jenrali Ulimwengu somehow naona hii article kaenda extreme in trying to make his point kwa kui label 'upuuzi' hio entity... Nashindwa kuelewa ni kwa nini ka label "Upuuzi" kwenye sector ambayo ingawa imelenga burudani zaidi ina manufaa yake makubwa tu kwa taifa kwa serkali na wananchi wenyewe kwa pande zote. Je amekuwa inspired na hasira tokana na kujihusisha kwa mkuu wa kaya na mtoa burudani ambae kwa kiasi kikubwa ni maarufu kwa kuuza sura? au ni kweli anaona kama hio sector ni upuuzi?

Labda alieelewa vema atudadafulie... Na kwa serkali yetu hii unaposema kui "Zaire" nchi yetu ina maana regardless ya tabia za Kiongozi mkubwa wa nchi kukumbatia upuuz (as per his say) pia in some way anakataliana na tabia ya wachache kuimiliki hii nchi badala ya majority... Hapo inanipa maswali kama akina J. Makamba pia ni walengwa...

Mara zote dada AshaDii huwa unanitangulia, kiasi kwamba siwezi kutoa maoni mapya bila ya kurefer mchango wako.

Yaliyomo ndani ya mistari katika makala hii ni mambo ya busara na kuzingatia kwa makini, kiasi kwamba kama tuna viongozi waelewa kiwango cha Ulimwengu, wangejifunza mengi badala ya kuendelea kufanya upuuzi, hasa pale anapomalizia:
Tunao watoto tayari ambao kila wakituchunguza tunavyoenenda ki-Zaire hawaoni mustakabali wao na wa watoto wao; wanatuuliza maswali, tunashindwa kuwajibu; wanaasi, hatuelewi.
Tungekuwa na busara ya kusikiliza vyema wanachosema, tungezisikia sauti za watoto watakaozaliwa mwaka 2099, wakisaili: Mbona mnaigeuza nchi yetu Zaire?
, lakini nje ya mstari makala inaweza kuonekana ya kipuuzi kwa kuita burudani upuuzi.

Mwandishi ametaja shughuli za kujipatia riziki na pengine utajiri mkubwa kaam vile Hollywood na Bollywood, uchezaji ngoma, ususi, ushoni wa nguo na viatu, uchoraji, uchezaji mpira...kuwa ni upuuzi (foolishness, useless). Nimemulewa mwandidhi alichotaka kusema, akimaanisha hayo kama burudani (entertainments) na vitulizo (distractions), lakini kuviita upuuzi nahisi kama ni upuuzi.
 
Last edited by a moderator:
Shida ni kitendo cha kuwa na audacity ya ku-entertain vitu kama entertainment in a time ambayo taifa inakumbana na matatizo kila Nyanja, kila sector, ndani/nje and between hizo Nyanja na sector¡* Sad.
At the same time industry ya entertainment ambayo inaonekana upuuzi inaweza kwa namna moja kuchangia maendeleo. Hollywood, Bollywood zinaingiza kiasi gani kwenye serikali zao?
Mtu kama Eto'o analipwa zaidi zaidi ya $200,000 kwa wiki, mtu kama huyu aki invest kwenye nchi yake atasaidia kwa namna moja nchi yake kutengeneza ajira.
Tusiende mbali angalia pesa wanazotengeneza wasanii wa Uganda, Kenya au Nigeria unakuta hata watu tunaowaona wanafanya issue za maana (sio upuuzi) hawawafikii hata robo..
Kwa kifupi sijapenda sekta ya burudani kuonekana ya kipuuzi na isipewe kipaumbele kisa kuna vitu vingine vya maana vya kufanya, wakati hao hao wenye matatizo wanatumia burudani kujifariji na matatizo yao.
 
Nchi haiwezi kula na kucheza muziki wakati watu wanakufa njaa, hizi product unazoziongelea zinamaana pale ambapo umeshiba ndio maana katika tamaduni zetu za kiafrika burudani zilikuwa na wakati wake, mfano wakati wa mavuno. Siku hizi nchi haizalishi kila kitu kinatoka ng'ambo halafu wewe unaongelea commodities, ni zipi hizo? Nchi haiweku kula CD bana.

Unapolinganisha na Hollywood elewa kwamba wale wameshika, wana barabara nzuri, watu wanafuata sheria (hakuna bla bla), shule zao nzuri na huduma zote za jamii poa. Tatizo letu waswahili tunapenda kudandia treni kwa mbele wakati mambo ya muhimu hatuyazingatii, huu ndio upuuzi wenyewe anaoungelea Jenerali.

Mkuu ndio hapo hapo ninapobishia kwamba, usanii (so called upuuzi unakuja pale baada ya kushiba au kufanya so called jobs/productive works)

Tuongelee watu individually Je ni makosa yao kwamba hakuna viwanda / miundombinu wala ajira ? na kama sio makosa yao kwanini tusilaumu cause (wanasiasa na viongozi ambao hawaleti mazingira ya ajira na kulinda resources zetu?).., Kazi ya Usanii sio kila mtu anaweza kufanya (kama hauna talent utabakia kuchemka) kwahio hii kazi sio ya upuuzi wala upuuzi uliopangiliwa (its a job like any other which needs talent) na kama wale ambao kazi yao ni kulima / kulinda mipaka / kuhudumia jamii hawafanyi kazi zao ila wanaburudika na wengine kuiba kazi za (upuuzi uliopangiliwa) maybe wenyewe ndio wapuuzi na sio wenye kazi au ambao wapo kwenye hii tasnia...

Kwahio we can feed the words to Jenerali all we want we can try to enter his brain and see what he might have meant lakini what remains ni kwamba hakuna kazi ambayo ni upuuzi uliopangwa (be it kushona nguo, viatu kuimba au kukata viuno) its a job like any other job., its a professional na hakuna tofauti ya tija zote zina manufaa be it a doctor, mchimba kaburi au mkata viuono its all a means to an end (mtu kupata pesa kwa familia yake na maisha yake) kutokuwa na viwanda na other means of production sio makosa ya tabaka la watu wanaojaribu kufanya kazi ili wapate mkate wao wa kila siku.., bali ni system mbovu ya viongozi na policy makers (lets call a spade a spade) na kama kwenye kazi moja inampatia kipato (then its his right job) kama wewe unafanya kazi fulani hupati kitu (be it kulima, uhasibu au usanii) then you are in the wrong proffession and its time to look elsewhere.
 
Hata mimi sina hakika kama nimemuelewa vizuri, !

Sasa Babu, hapo hapo unasema umelipenda hili andiko la Twaha na kumbe huna uhakika kama umemuelewa..... lol

Wengi tunaliogopa neno "UPUUZI"...

Wabongo wengi hatupendi kukaripiwa, hatupendi kuambiwa ukweli katika hali yake halisi.....

Tunapendwa kuambiwa kila kitu katika sura ya kinafiki-nafiki huku tukichekewa chekewa....

Jamani neno UPUUZI si limenyambuliwa kutoka kwenye neno "KUPUUZA", "KUPUUZIA".

Labda tukiangalia kutokea hapo, ukakasi wa hii makala utapungua...

Na nadhani tutakubaliana kuwa ni kweli kuna wakati sanaa inatumika kwenye kujenga "UPUUZI" kuna wakati inaweza kutumika kujenga "UZINGATIAJI".....

Mi naona Mzee Twaha, ameimulika sanaa ya Congo, kipindi kile ilipotumika kwenye UPUUZI hasa...

Mfano wa Bollywood na Hollywood ni kweli kuwa ile ni sanaa iliyoratibiwa na iliyogharamiwa ili kupumbaza watu baada ya shughuli zao za kujenga uchumi imara wa mataifa yao...
Ndio maana ameanza na hoja ya kisaikolojia pale mwanzo kuwa binadamu yeyote aliyekamilika kiafya ni lazima anahitaji kiasi fulani cha upuuzi katika maisha yake.

 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?

Hapana shaka wewe ni mmoja kati ya watu wanaohujumu Taifa hili, hivyo sitegemei wewe na genge lako muipende makala hii kwani inawaacha uchi wa mnyama!!
 
Mwandishi ametaja shughuli za kujipatia riziki na pengine utajiri mkubwa kaam vile Hollywood na Bollywood, uchezaji ngoma, ususi, ushoni wa nguo na viatu, uchoraji, uchezaji mpira...kuwa ni upuuzi (foolishness, useless). Nimemulewa mwandidhi alichotaka kusema, akimaanisha hayo kama burudani (entertainments) na vitulizo (distractions), lakini kuviita upuuzi nahisi kama ni upuuzi.

Nakushukuru kaka kwa acknowledgement... Naomba ni kiri kuwa nje ya matumizi ya neno 'upuuzi' ujumbe ni mzito na ni kitu hasa cha kuzingatia kwa waliolengwa na hii habari. Hio iko wazi, hata hapa jamvini kuna watu mbali mbali wamepost kuhusu swala zima lilopelekea hata Jenerali Ulimwengu kutoa makala juu ya jambo lenyewe. Nakubaliana na wewe kuwa ni 'Upuuzi' kuita hizo sekta 'upuuzi' just to make a point ni namna gani kaona hazina tija.
 
Sasa Babu, hapo hapo unasema umelipenda hili andiko la Twaha na kumbe huna uhakika kama umemuelewa..... lol

Wengi tunaliogopa neno "UPUUZI"...

Wabongo wengi hatupendi kukaripiwa, hatupendi kuambiwa ukweli katika hali yake halisi.....

Tunapendwa kuambiwa kila kitu katika sura ya kinafiki-nafiki huku tukichekewa chekewa....

Jamani neno UPUUZI si limenyambuliwa kutoka kwenye neno "KUPUUZA", "KUPUUZIA".

Labda tukiangalia kutokea hapo, ukakasi wa hii makala utapungua...

Na nadhani tutakubaliana kuwa ni kweli kuna wakati sanaa inatumika kwenye kujenga "UPUUZI" kuna wakati inaweza kutumika kujenga "UZINGATIAJI".....

Mi naona Mzee Twaha, ameimulika sanaa ya Congo, kipindi kile ilipotumika kwenye UPUUZI hasa...

Mfano wa Bollywood na Hollywood ni kweli kuwa ile ni sanaa iliyoratibiwa na iliyogharamiwa ili
kupumbaza watu baada ya shughuli zao za kujenga uchumi imara wa mataifa yao...
Ndio maana ameanza na hoja ya kisaikolojia pale mwanzo kuwa binadamu yeyote aliyekamilika kiafya ni lazima anahitaji kiasi fulani cha upuuzi katika maisha yake.
Hapo kwenye blue, umetumia neno hasa ambalo Ulimwengu angelitumia kwenye makala yake badala ya neno UPUUZI ambalo sikubaliani nawe hapo kwenye red kuwa neno hili limenyembuliwa kutoka KUPUUZA.

Neno Puuza kwenye kamusi linamaanisha: acha kutia maanani, bekua, beua, beza, dharau na minyambuliko yake ni puuz-ana, -ia, -zika, -zisha, -iwa, -wa, ​na upuuzi hauingii hapa.
 
Hapo kwenye blue, umetumia neno hasa ambalo Ulimwengu angelitumia kwenye makala yake badala ya neno UPUUZI ambalo sikubaliani nawe hapo kwenye red kuwa neno hili limenyembuliwa kutoka KUPUUZA.

Neno Puuza kwenye kamusi linamaanisha: acha kutia maanani, bekua, beua, beza, dharau na minyambuliko yake ni puuz-ana, -ia, -zika, -zisha, -iwa, -wa, ​na upuuzi hauingii hapa.

Sasa Mkuu MAMMAMIA ungeweka basi maana ya "upuuzi" kabisa kwa msaada wa kamusi yetu uliyonayo!

Ila naamini katiko andiko la J.U. kuwa sanaa isiyojenga fikra madhubuti zinazoweza kufanya watu wajitazame kama taifa na kuimalisha nguvu kazi na kujijengea maendeleo ni UPUUZI.....

Ni neno sahihi tu haijalishi linatuumiza kiasi gani na wala tunatafsiri vipi au kamusi yetu inasemaje
 
Last edited by a moderator:
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?

upuuzi wa kugomea sensa mbona hawakuwahi kumfanyia Mkapa au Nyerere?!!

Kama huna jibu sahihi, basi na wewe utakuwa na mtazamo na mawazo ya kipuuzi.
 
wapuuzi wataikashifu hii makala but truth be told, this is one of the many best features Jenerali wrote. Ukweli haupingiki, tunaizairesha nchi.
 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?

kwa upotoshaji wako .napata shida KUELEWA kama unatuona wana jf kama wapumbavu vile au unapotosha kwakuwa umeelewa kuwa general anaisaga serekali ya ccm na wewe ni magambazi hivyo unajaribu kutetea ?? .
 
Sasa Mkuu MAMMAMIA ungeweka basi maana ya "upuuzi" kabisa kwa msaada wa kamusi yetu uliyonayo!

Ila naamini katiko andiko la J.U. kuwa sanaa isiyojenga fikra madhubuti zinazoweza kufanya watu wajitazame kama taifa na kuimalisha nguvu kazi na kujijengea maendeleo ni UPUUZI.....

Ni neno sahihi tu haijalishi linatuumiza kiasi gani na wala tunatafsiri vipi au kamusi yetu inasemaje
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la Pili (2004), uk. 440 Oxford University Press,
UPUUZI maana yake ni jambo la kijinga lisilo na maana.

Na ni kutokana na maana hiyo ndio ninakakataa kuwa kucheza ngoma, filamu, mpira, ususi, uchongaji, uchoraji n.k, n.k, ni upuuzi. Kama ninemfahamu J.U ni kuwa Watanzania tunafanya upuuzi tunapocheza soka, na tunapocheza mziki, na tunapocheza filamu, na tunapotia saini mikataba, na tunapotakiwa kutoa maamuzi magumu, na tunapotafuta ufumbuzi wa tatizo sugu ...orodha inachosha.

Binafsi, kama nilivyoeleza kwenye post yangu huko nyuma, ninakubaliana kabisa na content ya J.U; ambapo kama nimemfahamu na ninakubaliana naye sana ni kuwa Watanzania tuwapuuzi na dhaifu. Na anaposema tunakuwa dhaifu hata katika upuuzi hakukosea. Atakayepinga hilo atakuwa na upofu wa akili. Tujiulize kwa mfano, sisi tumefika wapi kwenye huo upuuzi wa soka? Hata Mwinyi, raisi mzima alisema kuwa TZ ni kichwa cha mwendawazimu kwenye soka, hii haina maanakuwa kucheza soka ni upuuzi bali ipo kucheza soka kipuuzi.

Kwa hivyo kama umenifahamu, sipingani na J.U kwenye mantiki ya kile alichozungumzia, bali kutumia neno upuuzi kwa amali ambazo zenyewe sio upuuzi bali namna ya utendaji wake unaweza kuwa wa kipuuzi.
 
Hili linaitwa kapu la mjanja mjinga hatii mkono. Bila shaka kuna waliotoka kapa hapa. Bt kwa uelewa wangu jenerali hajawalenga wasanii(wakata kiuno na waburudishaji) bali anataka awakurupue watazamaji kua hii burudani na tamthilia inayoendelea (mafisadi na visa vyao) havipaswi kuangaliwa kwa jicho la mzaha kwamaana tukiendelea hivi rasilimali zetu zitaendelea kuwa chini ya wachache.........
 
The Case of an Emperor has no Clothes....

Ku-hit the nail kwa hii habari kwenye pande tofauti hakubadili upotokaji wa hii habari kwenye upande mwingine regardless ya message yoyote aliyotaka kuleta....

Kutaka kuaminisha watu kwamba Usanii ni Uburudishaji, kitu cha kufanya baada ya kazi ni kusahau kwamba msanii yupo kazini...
Kutaka kuaminisha kwamba baada ya kushindwa kufanya mambo mengine watu walikimbilia hii tasnia kujiburudisha
Kutaka kuaminisha kwamba sehemu kama Hollywood, Bollywood na sehemu nyingine Entertainment imepangwa ili kuburudisha wale wanaofanya kazi fulani za maana

Sasa no matter what the end message is.., hapa kuna kupotoka kwa hali ya juu sababu hii tasnia (entertainment) ni Industry na Biashara kama ilivyo biashara nyingine na mara nyingine inaweza ikawa na faida kuliko tasnia nyingine zozote kwa individual (na wala mtu huchagui kufanya hii kazi.., sababu you need something extra.., ) its an art / talent.

Sasa tukiacha meaning zote nyingine ambazo ni za kweli na kila mtu anaziona bottom line amepotoka kwa kuonyesha hii kazi its a mere extra au something to fall upon if everything else does not work out..

Ni kupotoka kutaka kutuaminisha kwamba sababu ya shida ndio watu walikimbilia hii tasnia kujiburudisha.., si kweli sababu this is not the factor behind mtu kuingia kwenye usanii, bali fame, money and talent are the ingredients zinazompelekea mtu kuingia kwenye hii industry.

In short the failure of Congo / Zaire has nothing to do na Usanii wala kuburudishana hata kama Congo isingetawalia na Mobutu asingetokea sio kwamba tungekosa wasanii wa Congo, watoto wanazaliwa na kuona jinsi idols wao walivyo they try to imitate na kama talent ipo they make kama hawana talent they die a natural death...

Narudia pamoja na ujumbe wa hii article kuna upotoshaji wa hali ya juu na associations ambazo hazina ukweli Usanii (waburudishaji) has nothing nor association of the leaders failing to do their jobs, also Sanaa (Entertainment) mfano Holiday haipo pale kuburudisha watu baada ya kazi, bali its an industry, money making business yenye full time professionals, with the capability of exporting its work world wide.

By the way among the top money making industries in the world Entertainment is among the top.., sijui bila huu usanii (upuuzi) kama kungekuwa na kampuni kama za Sony, Game Consoles n.k.
 
Back
Top Bottom