Jenerali Ulimwengu: Hata kwenye upuuzi tuko dhaifu!

Just to make my point clear naomba angalia na hapa

Hapo inaonekana kwamba the works of art / talent ni some sort of upuuzi au some minor work.., ambapo sio kweli kila kazi ina faida zake.., kwahio hapa nadhani kwa mfano wa juu tungesema mpuuzi ni yule ambaye hafanyi kazi zake bali anakuwa mtu wa burudani au kuangalia burudani na sio mtoa burudani..

Kwahio kama wakuu wa nchi wanakula bata badala ya kufanya kazi basi wapuuzi ni wakuu wa nchi na sio mtoa bata (bali mla bata bila kuzalisha bata)

Unajua hata mimi nimeliona hili, nikataka ku critique, nikaona ngoja niangalie wengine watasemaje (Kiranga kimepause for once!)

Ukweli ni kwamba Ulimwengu hata kama ana a bigger, more general valid point, hii simplification ya kui denigrade art kama upuuzi amechemsha.

Kuna watu wanaoweza kumwambia hata yeye kama muandishi ni artist, kwa hiyo kama art ni upuuzi, hata anachofanya yeye ni upuuzi.

I like my articles crisp, and this feels like it was hurried to meet a deadline.

To the extent of reeking snobbery.

And such a put down for Congo, I mean I could understand if this was about the leaders, but he hammered a whole society with vast generalizations.

And this guy was supposed a huge Pan-Africanist!
 
Kama alivosema Father of All, hii inahitaji mtu mwenye uelewa wa hali ya juu. Maana nimesoma na bado nadiriki kukiri kuwa bado najiuliza kama hasa nimeelewa vile Ulimwengu alilenga uelewa uwe.

Labda alieelewa vema atudadafulie... Na kwa serkali yetu hii unaposema kui "Zaire" nchi yetu ina maana regardless ya tabia za Kiongozi mkubwa wa nchi kukumbatia upuuz (as per his say) pia in some way anakataliana na tabia ya wachache kuimiliki hii nchi badala ya majority... Hapo inanipa maswali kama akina J. Makamba pia ni walengwa...

Ulimwengu hajakandia Usanii au wanamuziki....isome makala vyema.msisitizo wake upo hapa.
Hata hivyo, hatutakiwi sote kuwa waburudishaji na watumbuizaji. Wengine hawana budi kufanya kazi nyingine ili taifa lisonge mbele, liweze kujilisha na kujilimbikizia amali kwa siku zijazo, kwa ajili ya vizazi vijavyo. Tukiwa sote ni watumbuizaji ni nani atatulisha, atatuvisha, atatujengea nyumba? Nasema, tunahitaji upuuzi kidogo, na tena huu ni upuuzi uliopangiliwa vyema, lakini upuuzi hautakiwi uwe ndiyo shughuli kuu ya jamii nzima.

Ulimwengu anaandika kwa tahadhari zaidi au mnataka apatiwe one-way ticket ya Kigali?
 
Kwenye upuuzi uliopangiliwa anamaanisha nini ? Its all about demand and supply kama jamii ina-demand viburudisho sio kosa la mburudishaji ku-provide kiburudisho, bali ni kosa la watumiaji kuburudika bila kufanya mambo mengine ya maendeleo..

Kwa hiyo mkuu narudia tena hapa ameshift the blame on the wrong people na kuita shughuli fulani kama ni ya kipuuzi na ya part time yenye manufaa kidogo, anasahau kuna nchi kama Jamaica (Reggae, na sasa Mbio) au Brazil (Football) kwa kufanya hizo kazi so called upuuzi kumeleta awareness na kutangaza nchi yao), bila kusahau other benefits za matangazo na fashion ambazo watu wananunua na kukuza uchumi kutokana na icon fulani tu kwamba amevaa au ame-endorse a certain product.

Its all about commodities / products na hizi kazi (upuuzi) zinaweza kuwa product tosha.., tatizo ni kwamba wengi hatufanyi kazi zetu sasa tunalaumu wanaofanya kazi zao (upuuzi uliopangwa)
 
1. Upuuzi kwa kiasi fulani ni jambo jema.
2.Ndiyo maana hata katika jamii zilizoendelea sana katika ujenzi wa uchumi wapo watu ambao wanalipwa kwa mabilioni ya dola ili wapangilie upuuzi utakaowaburudisha wenzao
3. Ni watu muhimu katika jamii kama ambavyo tulikumbushwa si muda mrefu uliopita alipofariki Kanumba.
4.Isitoshe, katika kujiliwaza na kujisahaulisha madhila waliyoyapata muda wote,..wananchi wa nchi hiyo.. wakaingia katika shughuli ya kujitumbuiza kwa muziki na ngoma.
5. Kongo ikajulikana kwa mambo manne makubwa:..........nne, muziki, ngoma na burudani..
6. Pamoja na yote, K0ngo/Zaire ilipata mafanikio makubwa sana katika upuuzi uliopangiliwa. Haiwezekani kuzungumzia muziki barani Afrika bila kuitaja Kongo/Zaire; hata barani Uropa, wapenzi wa muziki ambao hawana asili ya Afrika wanatafuta muziki wa Kongo/Zaire.
7. Mobutu, pamoja na kwamba alikuwa mshenzi, alifanya kazi kubwa ya kuhifadhi urithi wa kimuziki wa Kongo. Katika miaka ya 1970 nilikwenda mara kadhaa mjini Kinshasa na nikaweza kujikusanyia albamu kadhaa ya wanamuziki wa zamani wa Kongo, akina, Kabasele, Wendo na Boukaka, yote kwa sababu Mobutu alikuwa amefadhili kazi ya kukusanya nyimbo za zamani na kuziweka katika sahani za santuri.

Sun wu,
Ulimwengu hakandii wasanii katika makala yake hii, anamkandia Mabutu na Zairesation yake.
Amesifia sana muziki wa Congo na juhudi za wananchi(wasanii) wake katika fani hiyo. Na hata kumpa haki yake pale ilipostahiki (dikteta) Mabutu kwa kufadhili/ kuwezesha urithi wa muziki wa ki-Congo kuhifadhiwa.
 
Ulimwengu hajakandia Usanii au wanamuziki....isome makala vyema.msisitizo wake upo hapa.
Hata hivyo, hatutakiwi sote kuwa waburudishaji na watumbuizaji. Wengine hawana budi kufanya kazi nyingine ili taifa lisonge mbele, liweze kujilisha na kujilimbikizia amali kwa siku zijazo, kwa ajili ya vizazi vijavyo. Tukiwa sote ni watumbuizaji ni nani atatulisha, atatuvisha, atatujengea nyumba? Nasema, tunahitaji upuuzi kidogo, na tena huu ni upuuzi uliopangiliwa vyema, lakini upuuzi hautakiwi uwe ndiyo shughuli kuu ya jamii nzima.

Ulimwengu anaandika kwa tahadhari zaidi au mnataka apatiwe one-way ticket ya Kigali?

Nimeisoma makala vema, na ndio nilivoelewa… Na ndio mana nikataka udadavuzi kwa alieelewa zaidi; ili nisipotoke katika kuilewa. Hata hivo huo ufafanuzi inabidi uwe wa kina for me to understand in order to agree…

Tambua kuwa katumia neno ‘upuuzi' kwa kurudia rudia (ambayo katika uandishi ni moja ya njia ya msisitizo). Hicho kipengele ambacho umechagua kama msisitizo wake ni tokana tu na ile perspective yako kuwa uipe wapi uzito kufafanua na kuelewa makala nzima. Na hapo ndio anatowa wazi kabisa kuwa hao aliosema kuwa ni wapuzi ni Watumbuizaji (hivo kufuta was was wowote wa kudhani kuwa hamaanishi hao watu). Kama umeisoma veka katika mabandiko yangu nimesema ujumbe nakubaliana nao na upo sawia. ILA Sikubaliani na the way katumia neno ‘Upuuzi' IMO ipo extreme.

BTW hivi hapo kama wanania ya kumpa one way Ticket unadhani hawawezi manipulate hii Makala? Maybe nakosea but I feel like unamkubali sana Ulimwengu to the extent hata akikosea waona kama hajakosea. Hapo in black and white katoa dharau ya juu sana (bahati nzuri ama mbaya waliopo katika hio sector mara nyingi sio wasomi wa mambo kama haya for them to make a big deal out of the issue).
 
Hii ndo raha ya jf nami naburudika kwa upuuzi huu. kweli wape pombe maskini wasahau shida zao
 
namuunga mkobo jenerali kwa 100%. na tusiendeleze huu upuuzi wa kuwa na msanii wa bongo flaver kila baada ya nyumba moja mitaani. vijana tukalime tujenge nchi tuachaneni na upuuzi. nakumbuka kuna msanii alishawahi kusema " sio lazima tuwe sote wanamuziki, ingefaa kama wengine mbaki mashabiki" mashabiki twendeni shambani tukirudi tutakuta burudani tujiliwaze. lakini utakuwa upuuzi kama kila mmoja wetu ni mdurudishaji
 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?

I am sure ur going to die when the war start. U will die with ur upuuzi
 
nitaimalizia baadae ila najivunia kuwa na raisi promoter..

Hahahaha, JK=Janga la Kitaifa. Hapa ndo utajua kwa nini shuleni kuna mitihani na ndo utapata maana ya kwa nini kuna wa kwanza na wamwisho. Ila mimi naamini hakuna kisichokuwa na mwisho
 
Mie naona kama vile wanajamii wenzangu mnakwazika na neno "upuuzi" lakini hapa nadhani amelitumia ili kuleta utata (controversy) kuleta ujumbe. Sidhani kama anamaanisha neno upuuzi (literal) bali alitaka kutoa mkazo, ni kama vile kipanya anavyoziita katuni zake "upuuzi wa kipanya". Ukifuatilia katuni zake utaona zinaujumbe maridadi lakini anaziita upuuzi ili kuleta mazingira ya utata, ambao ni njia nzuri sana ya kupeleka ujumbe.

Kwenye upuuzi uliopangiliwa anamaanisha nini ? Its all about demand and supply kama jamii ina-demand viburudisho sio kosa la mburudishaji ku-provide kiburudisho, bali ni kosa la watumiaji kuburudika bila kufanya mambo mengine ya maendeleo..
kama viongozi wa juu hawaweki mkazo katika mambo ya maendeleo ya nchi na kulinda mali asili huku wakishadadia burudani huo ni upuuzi.

Kwa hiyo mkuu narudia tena hapa ameshift the blame on the wrong people na kuita shughuli fulani kama ni ya kipuuzi na ya part time yenye manufaa kidogo, anasahau kuna nchi kama Jamaica (Reggae, na sasa Mbio) au Brazil (Football) kwa kufanya hizo kazi so called upuuzi kumeleta awareness na kutangaza nchi yao), bila kusahau other benefits za matangazo na fashion ambazo watu wananunua na kukuza uchumi kutokana na icon fulani tu kwamba amevaa au ame-endorse a certain product.

Ukimsoma vizuri ulimwengu utaona hana ugomvi na wasanii bali Serikali ambayo haishadadii mambo ya maendeleo kama huduma bora za afya, mikataba mibovu ya madini na miundombinu. Viongozi wa serikali hawana nia wala sera ya maendeleo kwa vizazi vijavyo bali ni wakwanza kwenda kujivinjari na wasanii. Nchi ina nja wewe kama kiongozi mkuu unaserebuka kama sio upuuzi ni nini?

Its all about commodities / products na hizi kazi (upuuzi) zinaweza kuwa product tosha.., tatizo ni kwamba wengi hatufanyi kazi zetu sasa tunalaumu wanaofanya kazi zao (upuuzi uliopangwa)
Nchi haiwezi kula na kucheza muziki wakati watu wanakufa njaa, hizi product unazoziongelea zinamaana pale ambapo umeshiba ndio maana katika tamaduni zetu za kiafrika burudani zilikuwa na wakati wake, mfano wakati wa mavuno. Siku hizi nchi haizalishi kila kitu kinatoka ng'ambo halafu wewe unaongelea commodities, ni zipi hizo? Nchi haiweku kula CD bana.

Unapolinganisha na Hollywood elewa kwamba wale wameshika, wana barabara nzuri, watu wanafuata sheria (hakuna bla bla), shule zao nzuri na huduma zote za jamii poa. Tatizo letu waswahili tunapenda kudandia treni kwa mbele wakati mambo ya muhimu hatuyazingatii, huu ndio upuuzi wenyewe anaoungelea Jenerali.
 
Hii inahitaji uelewa wa hali ya juu. Ukikurupuka utadhani aliyeandika ndiye mpuuzi. Chunga sana kuna mtego!
 
Mara zote nakubaliana na Ulimwengu, ni mara moja tu nilipingana naye juu ya kutaka kuitoa FAT wakati huo (sasa TFF) katika shirikisho la dunia la mpira wa miguu (FIFA).

Hapa, natamani Salva Rweyemamu amsogezee "mkuu wa kaya" makala hii, ili aone kama nchi yetu ina"zaireshwa" ama la ?
 
Kuna kitu ambacho ni muhimu kujikumbusha. Katika jamii zetu burudani imechukuliwa kuwa shughuli yenye hadhi ya chini sana. Ndio maana neno kama vile msanii au mkata viuno wakati mwingine huchukuliwa kama tusi. Pamoja na kuwa jamii inahitaji burudani ila inapoendekeza mambo hayo lazima itaonekana kama iliyopotoka. Hata hivyo, msanii anayefanya kazi yake vizuri hawezi kuitwa mpuuzi.
 
Kwa muda mrefu sasa, nimekuwa msomaji mkubwa wa maandiko ya Jenerali Ulimwengu.Sijawahi,hata siku moja, kupata shida KUELEWA maudhui ya makala zake kwa kuwa huwa anatumia lugha rahisi na nyepesi kuwasilisha ujumbe mzito na wenye mantiki.Kwa hiyo,kila moja wetu,pasipo kujali tofauti zetu za viwango vya elimu, ana fursa ya kuelewa makala hizo.Hii haina maana kuwa huwa NAKUBALIANA mara zote na aandikacho.Makala husika NIMEILEWA na KUKUBALIANA na maudhui yake.
Jenerali anawataka wale wote wanaotuongoza , wenye dhamana na mustakabali wetu, na wa vizazi vijavyo, waache upuuzi na mizaha badala yake wafanye kazi wanazopaswa kufanya.Waonyeshe ,kuwa ,wanafikiri na kutafuta namna ya kutukwamua katika giza linalotukabili.Watu wanaofanya kazi bungeni, katika wizara mbalimbali,Taasisi ,Wakala,Idara,Mamlaka na vyombo mbalimbali hawapaswi na hawategemewi kujiunga na kundi la wapuuzi/wasanii lisilotumia akili sana.
Anasisitiza ,vile vile, kuwa jamii ifanye bidii za kujenga utamaduni endelevu wa kusaka maarifa kujiongezea maarifa na kukuza ufahamu na uelewa.Tuachana na silka yetu ya kujivunia ujinga (kutokujua mambo)na upuuzi.
Anasikitika, kuwa, kwa sasa ni kama vile sehemu kubwa ya jamii yetu imeamua kuwekeza katika kusaka upuuzi /ujinga endelevu.
 
...Hii ni kwa sababu nchi yetu inayo misingi ya kitaifa iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Misingi hiyo inakataa nchi yetu kugeuzwa kihamba cha mtu au watu wachache; ni kihamba chetu sote, na wala si chetu kiasi hicho, kwani tumepewa dhamana tu ya kukihifadhi na kukiendeleza kwa ajili ya vizazi vijavyo, kwa niaba ya Watanzania tusiowajua, kwa sababu hawajazaliwa...

Binafsi sidhani kwamba kuna nchi ya Kiafrika yenye MISINGI YA KITAIFA yenye tija kama Tanzania. Nafikiri iko highly rooted up to the Core of the Country itself! Ni kama mbegu ambayo inauwezo mkubwa wa ku REGENERATE hata kama mmea wa awali utakuwa umefifia au umekufa.

Inawezekana akatokea Mtu akaukata Mmea (Kwa sababu za kipuuzi) huo lakini kwa uwezo wake wa Ku regenerate au tusemea kuchipua na kuendelea kuota tena ..sio rahisi kuuangamiza. Naamini Utaifa wa Tanzania sio Mmmea unoweza kuchezewa na kutokomezwa kirahisi tu kwa uzembe/upuuzi wa sasa au siku zijazo.

Sidhani kuwa Zaire/Kongo wana mbegu inayoongela hapa. Kikuweli hawana na sidhani kuna mwelekeo wa karibuni kuwa nayo. Hawajawahi kuwa kitu kimoja kama nchi, hajawahi kuungana kupitia uasili wa mwanadamu mwenyewe ambao ni "Utu" wake... labda wamewahi kuuganishwa na kama hivyo ..labda kwa "upuuzi" anaousema Ulimwengu!

Taifa la Tanzania litayumba na kuonekana kama limepoteza mwelekeo kwa namna mbalimbali lakini lina MISINGI YA UTU NA UBINADAMU YA KITAIFA iliyowahi kutekelezwa kwa vitendo ambayo itahitaji KUREJEWA.

Utaifa wa Tanzania naouna kama umejengeka kwenye UTU ambao ndio Utanzania. Na Utu hauna dini, ukabila, ukanda, jinsia, rangi, itikadi nk. "Utanzania ni utu" unaozaa Utaifa na Uzalendo. Kufanikiwa kulijenga na kulirutubisha Taifa kwenye Thamani ya ubinaadamu ya juu kama hii ni mafanikio yasiyo badilika hadi milele! Kwani Kuungamiza Utu wa jamii utapata nini? Unyama? or May be Upuuzi!! Utu wa jamii ni kitu kisichofutika kwa namna yeyote ..kinazaa UTU WA TAIFA kama Uzalendo na UTAIFA usiovinjika na kutokomea kirahisi!

Nani anweza kuugamiza utu wa mtu? Nani anweza kuungamiza Utanzania? Nani anweza kuungamiza Utaifa .. HATA UPUUZI HUTWEZA!!!

Taifa la Tanzani tofauti na mataifa mengi, lina central rooted force ..the seed itself ... kama misingi ya kitaifa ambayo sio rahisi kuigamiza labda kwa mitazamo na attitude za kizembe tu ambazo finaly zitashindwa tu na bora kurejea Utaifa na utanzania wetu, sasa na bila kuchelewa ... anasema ::"Hii ni kwa sababu nchi yetu inayo misingi ya kitaifa iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Misingi hiyo inakataa nchi yetu kugeuzwa kihamba cha mtu au watu wachache; ni kihamba chetu sote, na wala si chetu kiasi hicho, kwani tumepewa dhamana tu ya kukihifadhi na kukiendeleza kwa ajili ya vizazi vijavyo, kwa niaba ya Watanzania tusiowajua, kwa sababu hawajazaliwa...;;;"

The living force is like force of inertia ... Nchi inaweza ikayumba na kuyumba lakini it will never escape its roots (the creative humanity on its core), it will come a time and will found its origin ..which is the force of Humanity in its community expression for future generation!
 
Back
Top Bottom