Jenerali Ulimwengu: Hata kwenye upuuzi tuko dhaifu!

Which war are you talking about? no matter how this Rwandan refugee try to instigate war in TZ he will not succeed.

Pole sana Eddie anayekulipa mshahara na posho ndiyo huyo ataanzisha vita. Ipo siku moja kama mwenyezi atatujalia uzima utakuja hapa nakunena. CCM mnatufanya watanzania wapuuzi sana na elimu zetu ni hakuna kitu
 
Tuongelee watu individually Je ni makosa yao kwamba hakuna viwanda / miundombinu wala ajira ?
Siyo makosa kabisa kwa wasanii hujipatia ridhiki.

....na kama sio makosa yao kwanini tusilaumu cause (wanasiasa na viongozi ambao hawaleti mazingira ya ajira na kulinda resources zetu?)..,

...kutokuwa na viwanda na other means of production sio makosa ya tabaka la watu wanaojaribu kufanya kazi ili wapate mkate wao wa kila siku.., bali ni system mbovu ya viongozi na policy makers (lets call a spade a spade) na kama kwenye kazi moja inampatia kipato (then its his right job) kama wewe unafanya kazi fulani hupati kitu (be it kulima, uhasibu au usanii) then you are in the wrong proffession and its time to look elsewhere.

Ndiyo maana nikasema...

Ukimsoma vizuri Ulimwengu utaona hana ugomvi na wasanii bali Serikali ambayo haishadadii mambo ya maendeleo kama huduma bora za afya, mikataba mibovu ya madini na miundombinu. Viongozi wa serikali hawana nia wala sera ya maendeleo kwa vizazi vijavyo bali ni wakwanza kwenda kujivinjari na wasanii. Nchi ina nja wewe kama kiongozi mkuu unaserebuka kama sio upuuzi ni nini?
 
upuuzi wa kugomea sensa mbona hawakuwahi kumfanyia Mkapa au Nyerere?!!

Kama huna jibu sahihi, basi na wewe utakuwa na mtazamo na mawazo ya kipuuzi.


..... tena bora kwenye hiyo sensa wangeweka "dodoso" ya level za upuuzi, huu wa kwako ungepata alama za juu!
 
Pole sana Eddie anayekulipa mshahara na posho ndiyo huyo ataanzisha vita. Ipo siku moja kama mwenyezi atatujalia uzima utakuja hapa nakunena. CCM mnatufanya watanzania wapuuzi sana na elimu zetu ni hakuna kitu

Pole wewe na mpuuzi mwenzio wa kinyarwanda
 
Kwa hivyo kama umenifahamu, sipingani na J.U kwenye mantiki ya kile alichozungumzia, bali kutumia neno upuuzi kwa amali ambazo zenyewe sio upuuzi bali namna ya utendaji wake unaweza kuwa wa kipuuzi.

Labda kama nimejaribu kukuelewa ni kuwa kosa la kiufundi kwenye makala yetu pendwa ni kuwa J.U. hajatofautisha aina za sanaa amabapo angeweka wazi zipi ni upuuzi na zipi ni za maana!!!??

Nadhani angeenda sana huko hiyo makala ingepoteza maana maridhawa...

Binafsi naona amelifanya kwa kupitia mifano aliyotoa ambapo amezungumzia sanaa ile iliyojikita kwenye kusifia na kusujudu watawala.... hichi ndio amejaribu kukiita upuuzi...

Ndio maana pia kwenye jibu langu nikasema kuwa hakika kuna sanaa ambazo ni upuuzi hasa zile zisizojenga wala kuleta tafakuri yoyote ya kuamsha watu.
 
Upuuzi !!!!

Its true kwamba tunafanya upuuzi, its true kwamba mengi yafanyikayo ni upuuzi lakini tusiite hata mazuri ni upuuzi.., he is right in some scenarios lakini tusisahau kwamba what matters is making a living, kwahio si vema kuita skills za mtu ni upuuzi.. Upuuzi wa Mobutu hauwezi kupunguza sifa za Franco, Pepe Kalle wala Papa Wemba
NADHANI WENGI HAMJAMUELEWA Mr ULIMWENGU KTK Wossia WAKE. neno kubwa alilosema ni watu wachache katika nchi hii wasiigeuze nchi yetu kama ni vihamba vyao. Rasilimali za nchi hii ni za wote na ziwe kwa ajiri ya vizazi vijavyo. nimeguswa sana na article yake yote na driving force behind him to write hii article ni kuhusu swiss bank ya mambilion ya watu walivyozipata kimabutulism.

kitu ninachopinga ni asiwape sifa waasisi wa nchi hii eti wameweka misingi imara. misingi imara ni katiba bora ambayo ingekuwa ina mshitaki kila raisi aingiaye madarakani akiboronga. toka waasisi walikikwepa kifungu cha kumshitaki raisi aikimaliza muda wake asishitakiwe, madhara yake ni makubwa kuliko hata kupigana vita vya wenyewex kwa wenyewe. kwa hiyo ndugu yangu, chakupigania katika kuweka katika bora, lazima kipengere cha kumshitaki raisi akimaliza muda wake kiwekwe ili wachache wasifanye mali za nchi ni zao na kuwafanya watoto wetu wakose maisha bora baadaye.

Mafuta, uranium na madini yanaozidi kugunduliwa kila kukicha yatalindwa vema na kifungu kitakacho mshitaki raisi akimaliza muda wake tuu na sio kelele za wabunge za kulaani rushwa.

bado generali ulimwengu nakuvulia kofia kwa article yao ambayo ni nzuri sana na umetumia hekima ya william shakke spear kuwaelimisha wananchi.
 
kitu kizuri walichofanya wa zaire mwaka 1964 ni pale walipomuua Lumumba tuu. Maana huyu Lumumba alikuwa komunisti lililo kubuhu ambalo lilimkana mungu. kama lumumba angechukua nchi tuu basi zaire isingewika katika usanii barani ulaya. maana wakomunisti kitu cha kwanzan akipata nchi ni kufuta haki miliki kwa wanamuziki na aina yeyote ile ya usanii.

hata soka hufukuzia migogoro mpaka vilabu kuzoorota. anagalia jinsi wakomunisti wa kongo ya ngwabi walivyouwa klabu ya kalamu FC ilitamba barani africa, angalia jinsi wakomunisti wa Guinea walivyoiuwa klabu ya Afia fc ya gunea. kweli kabis shetani alitaka kuitawala dunia kwa kutumia ukomunisti jamani.
 
Haya ndiyo matatizo ya fikra finyu za watu wachache wenye majigambo kama ni wao wasomi. Yale yale mawazo kama ya Samwel Sitta.

Ni ufinyu wa mawazo na ukosefu wa hekima kutaka kujenga hoja kwa ghalama ya dhalau kwa jamii nyingine. Hata alichokiandika hapa ni upuuzi mtupu. Watanzania siyo Wazaire na Wazaire siyo Watanzania. Hata kihistoria ni tofauti.

Ama kweli mgema akisifiwa, tembo hulitia maji
 
Hivi ni kweli kabisa Jenerali hajaeleweka au kuna kingine cha ziada?
Any way,hii ni kawaida kwa kuwa hatuwezi kufikiri kwa namna inayofanana.Hata kama angefanya nasi mazungumzo ya ana kwa ana bado kuna miongoni mwetu wangepata tabu kumwelewa.
Labda nifupishe ujumbe wake:anatutaka sote tuache na tusishabikie upuuzi.Upuuzi wa aina yoyote haufai.
Anatutaka tuwe watu makini,watu tunaojitambua,tunaojistahi, tunaowajibika ,watu wa kupigiwa mfano.
 
kitu kizuri walichofanya wa zaire mwaka 1964 ni pale walipomuua Lumumba tuu. Maana huyu Lumumba alikuwa komunisti lililo kubuhu ambalo lilimkana mungu. kama lumumba angechukua nchi tuu basi zaire isingewika katika usanii barani ulaya. maana wakomunisti kitu cha kwanzan akipata nchi ni kufuta haki miliki kwa wanamuziki na aina yeyote ile ya usanii.

hata soka hufukuzia migogoro mpaka vilabu kuzoorota. anagalia jinsi wakomunisti wa kongo ya ngwabi walivyouwa klabu ya kalamu FC ilitamba barani africa, angalia jinsi wakomunisti wa Guinea walivyoiuwa klabu ya Afia fc ya gunea. kweli kabis shetani alitaka kuitawala dunia kwa kutumia ukomunisti jamani.

Mkuu unaamini kuwa kuuawa kwa Lumumba ilikuwa ni jambo jema?

Pitia hizi link Patrice Lumumba: the most important assassination of the 20th century | Georges Nzongola-Ntalaja | Global development | guardian.co.uk

link 2. The Assassination of Patrice Lumuba - YouTube

Je pia lilikuwa jambo zuri kupinduliwa kwa Nkrumah kwa msaada wa CIA?

Afrika itaendelea kuwa shamba la US na wazungu kwa miongo kadhaa kama tuna mawazo haya.

Libya ilitumia mfumo wa arab socialism chini ya Gaddafi na huwezi kupinga kuwa Libya ilikuwa mbali kwa huduma za kijamii na kimaendeleo. Na kama haikuwa vikwazo vya US na Europa basi ile nchi ingekuwa mbali sana.

China na Cuba nazo zimetumia siasa za uchumi wa kijamaa(ukommunisti) ingawaje zinabadilisha mfumo kwa sasa lakini kwa kuamua wenyewe na kulingana na mazingira yao leo.

Na nchi zinazotumia ubepari nyingi leo ziko kwenye misukosuko ya kiuchumi /zinaporomoka, mfano Greece, spain, France, Italy na hata US

Pia kama unafatilia vizuri historia kila kiongozi wa Afrika anayepigia debe umoja wa waafrika na Afrika basi anakwenda na maji. US na Wazungu humuona ni hatari kwa maslahi yao na unayajua maslahi yao(kuvuna shamba la bibi bila mikwala au kuulizwa chochote).
 
Pole wewe na mpuuzi mwenzio wa kinyarwanda

Hahahahaha, kweli wewe Eddie, jamaa uko poa although unamuita mpuuzi ila sisi wenye akili zote(Class+kazini+Maisha) tunajua thamani yake katika hii inji yetu
 
Hahahahaha, kweli wewe Eddie, jamaa uko poa although unamuita mpuuzi ila sisi wenye akili zote(Class+kazini+Maisha) tunajua thamani yake katika hii inji yetu

Kama ungekuwa na hizo sifa usinge mwaga ***** humu
 
Ndiyo maana nikasema...
Ukimsoma vizuri Ulimwengu utaona hana ugomvi na wasanii bali Serikali ambayo haishadadii mambo ya maendeleo kama huduma bora za afya, mikataba mibovu ya madini na miundombinu. Viongozi wa serikali hawana nia wala sera ya maendeleo kwa vizazi vijavyo bali ni wakwanza kwenda kujivinjari na wasanii. Nchi ina nja wewe kama kiongozi mkuu unaserebuka kama sio upuuzi ni nini?
Mkuu with all due respect haya maneno ni ya kwako..

Na hakuna ubishi kwenye article kuna maneno yafuatayo.....

Hata kwenye upuuzi tuko dhaifu (heading) (By the way one should think kwamba if that is the case then we are okay au alitaka tuongoze kwenye upuuzi, yaani tuwe mabingwa wa upuuzi ?)

Upuuzi Uliopangwa Hapa akiongelea sehemu kama Hollywood (which means he does not think highly kwa kazi za hawa watu au tija ya kazi zao

Upuuzi kidogo Kuburudisha watu baada ya kazi Kana kwamba hii kazi ipo pale kwa ajili ya refreshment kwa wachapa kazi wa kweli

Kila binadamu anahitaji upuuzi kidogo
katika maisha yake kujiburudisha baada ya kazi ngumu.....

Kwahiyo mkuu you can't dispute kwamba ametaka kutuaminisha kwamba hii kazi its just like a second rate work (although he is entitled to his opinion na tungeweza kusema okay...) ila kwenda a one step further na kuita ni upuuzi uliopangwa nadhani there was no need for it...

Na issue kwamba wote hatuwezi kuwa wasanii., nadhani its obvious, kama vile vile wote hatuwezi kuwa wanasiasa, madaktari, waalimu au machinga.. (there is always specialization and division of labour) vile vile kumbuka kwamba kila mtu anaweza akawa mkulima au mwalimu lakini sio kila mtu anaweza kuwa msanii (upuuzi uliopangwa) sababu one can be learnt but the other needs talent.....

Kwahio mkuu ku-brand hii kazi Upuuzi Uliopangwa was uncalled for and nonsensical and there was no need for it, and it has diluted the message and for some have made the article upuuzi (as there is no such thing as upuuzi uliopangwa)
 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?


General is on another level for you to grasp his arguments. If this is the case it would be wise not to divert the attention of wise and brilliant readers " the greater thinkers". No country has ever developed for not investing in real sector of the economy and such investments must largely be made by her own people! In the next morning you will be empty-handed with no lucrative land to farm. Is this what you argue against Ulimwengu? What a shame!

It is better to think big that no God Father from abroad will help to feed and develop your kids. Please think!
 
General is on another level for you to grasp his arguments. If this is the case it would be wise not to divert the attention of wise and brilliant readers " the greater thinkers". No country has ever developed for not investing in real sector of the economy and such investments must largely be made by her own people! In the next morning you will be empty-handed with no lucrative land to farm. Is this what you argue against Ulimwengu? What a shame!It is better to think big that no God Father from abroad will help to feed and develop your kids. Please think!
It does not need to be a rocket science to know that..., its a no brainer everyone knows that our country is lost and going wayward BUT there was no need to call some art is Upuuzi Uliopangwa or its mere existence is to entertain those who does the so called productive work.., this was uncalled for.., and even if it was a work of Shakespeare himself branding the Industry of entertainment as Upuuzi Uliopangwa ni Kupotoka to say the least and those words has added nothing to the article but just diluting it and will not get well with the some people (and the accusation is baseless and untrue) as this upuuzi uliopangwa is an industry which supports many other industry (the so called kazi za akili na kazi za kweli) including manufacturing (just stop and think without movies / music would there be cd's and dvd and what about the millions who are working for these industries and the business men who sells these...There the guy could have got his message accross without this bashing (upuuzi uliopangwa)
 
Hivi ni kweli kabisa Jenerali hajaeleweka au kuna kingine cha ziada?
Any way,hii ni kawaida kwa kuwa hatuwezi kufikiri kwa namna inayofanana.Hata kama angefanya nasi mazungumzo ya ana kwa ana bado kuna miongoni mwetu wangepata tabu kumwelewa.
Labda nifupishe ujumbe wake:anatutaka sote tuache na tusishabikie upuuzi.Upuuzi wa aina yoyote haufai.
Anatutaka tuwe watu makini,watu tunaojitambua,tunaojistahi, tunaowajibika ,watu wa kupigiwa mfano.
Mkuu hakuna mtu ambae hajaelewa message ipo wide open, lakini kuna some elements kwenye hii article ambazo zilikuwa hazina umuhimu wala hasina basi na ni kupotosha...

Moja wapo ni Upuuzi Uliopangwa (kazi kama za wasanii wa hollywood)..., kwahio mkuu you can not dadavua au kuelewa vipi in order ku-dilute kwamba kuita kazi za wasanii tuseme hollywood ni upuuzi uliopangwa au ipo pale kuridhisha watu wanaofanya kazi za kujenga nchi.. (hapa alipotoka) hata kama ameandika article worth winning a nobel prize ila katikati ya habari kuna mstari unaopotoka.., umuhimu au uzuri wa habari yake hakubadilishi mstari aliopotoka... we have all seen the message aliyotaka lakini tumeona na zaidi ya hio message.., kwamba kwenye hii article kuna vipengele ambavyo havina uzito wala ukweli wowote at best vimetoka nje ya mada
 
Nionacho ni mgongano wa maana ya mwandishi na maana ya neno “upuuzi” kama tunavyolifahamu ktk maisha ya kila siku.

Tatizo la Ulimwengu ni kutaka kila andiko liwe la kifasihi. Mfano ktk The East African makara zake hutokea ktk ukurasa ambao kuna waandishi wengine wawili. Napenda sana kusoma uandikaji wao, unaburudisha na unafundisha vizuri sana. Lakini uandikaji wa Ulimwengu kila wakati ni kama fasihi tofauti na wengine. Burudani ya fasihi huja baadaye sana baada ya mtu kupata tafsiri ya ndani ya maudhui ya mwandishi. Najikuta sifurahii uandikaji wake maana siyo lazima kufanya hivyo kila nakara ya gazeti.

Ktk hili la upuuzi tunajikuta wengine tukichukia matumizi ya neno lenyewe kabla hata ya kupata maana ya mwandishi. Tunadhani katukana wacheza muziki na sinema. Lakini mwishoni utaona maana ya upuuzi huu anaousema. Anazungumzia maendeleo ya nchi ambayo kwa uhakika ukiyataka huwezi kuimba, kucheza n.k halafu ukasema utaendelea. Ni upuuzi. Hata USA haiwezi kuendelea kwa Holywood. Hapa kwetu ndo kabisa maana hata hawalipi kodi. Bahati mbaya sasa nao wako Bungeni wakipanga sera na sheria za nchi.

Jamani naona Ulimwengu yuko sahihi. Sera sasa ni mbinu za kuwaburudisha wananchi wake. Muziki (studio), Redio (---FM), Mpira (makocha toka nje ya nchi), uwanja mkubwa wa kuvutia sana. Baadaye tuko majukwaani wanatuimbia na tunacheza na kucheka jukwaani. Sasa kundi la usanii limekuwa kubwa ktk mfumo wa serikali na ukiwagusa wanakuja juu. Hatuwezi kupoteza muda na usanii tukidhani tutaendelea!

Wasanii ndo viongozi wa nchi. Hawa ni waburudishaji tu! Anayetafuta ushuhuda asubiri miaka mitatu iliyobaki kama kweli CCM italeta meli tatu; Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, na moja kubwa kuliko Victoria huko Ziwa Victoria. Bado yapo mengine; Kiwanja cha ndege kwenye lile bonde la Nkenge Bukoba, Kiwanja cha ndege Singida, na yoote tuliyodhani ni ahadi kumbe ni ahadi toka kwa msanii. Alikuwa akitoa burudani.
 
Hata mimi sina hakika kama nimemuelewa vizuri, ila kajaribu kusema baadhi ya mambo tuliyoyasema kwa Kanumba tunaonekana wabaya...Tuliona kama vile jamii inaelekea ndiko siko. Inawezekanaje watu makini wakamiminika kumsindikiza msanii na kumsahau mtu ambaye alikuwa mkuu wa majeshi wa nchi??

Katika kuendesha maisha ya kila siku, kuna mambo siyo ya lazima (huwezi kufa au kupata madhara makubwa kwa kuyakosa). Mfano wa mambo haya ni burudani za aina zote. Pamoja na kwamba sijafurahia neno alilolitumia, ila kwa namna fulani naweza kumuelewa kwa sababu ni kama vile tumeweka kipaumbele kwenye mambo yasiyo ya lazima na kuacha mambo muhimu. Na katika hali kama hiyo, tunaweza kusema tumefanya upuuzi na kwa maana hiyo, tunaendekeza mambo ya kipuuzi!!

Nadhani siyo rahisi kuelewa makala kama hizi, na endapo ukihisi kwamba umekuwa offended!

Nakuhakikishia ya kuwa wewe umemuelewa vilivyo El General del Mundo! hao wenye kujihisi offended ni kwamba ile level ya uzaireshwaji imeshakuwa ya juu hawana wakijuacho zaidi ya upuuzi anao uzungumzia jenerali,isitoshe makala imekaa kiutuuzima watu wa mipasho na hoja mkato hawaoni kitu lazima uwe mtu wa ku-reflect and refer nyakati na matukio mbali mbali,pia unatakiwa uisome kwa akili si kwa macho!
 
I always like this dude, huwa haogopi makunyanzi ya walioko kwenye madaraka- ukienda hovyo lazima akulime tu. Mzee wa kiwira anamjua vizuri ilibidi akimbilie kumnyang'anya uraia lakini haikusaidia kitu jembe liliendelea kutifua tu!!!!

Yeah, hana uoga kwa sababu ana hakika na anachoongea,na bado anatumia uhuru wake kikatiba. Nilipata bahati ya kuhudhuria mijadala yake kadhaa akipiga shule pale UDSM miaka ya 90s! Wakati huo yeye, Prof. Seith Chachage(Al Marhum),Tundu Lissu(issues alizianzia huko) na bwana mmoja anaitwa Ramadhani Kingi(cjui yu wapi). Hawa ni watu waliokuwa wanachambua siasa za nchi hii mpaka unapata hamasa ya kuwa mwanamapinduzi. Nafikiri mbegu hyo imepandikizwa vyema kwa Mh. Lissu.
Bother Jenerali ni chachu ya uchambuzi yakinifu juu ya mwenendo na mustakabali wa siasa za nchi hii japo najua wanaoguswa na makala zake hawazipokei positively!
 
Back
Top Bottom