Jenerali Ulimwengu: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina zaidi ya wanachama milioni 8, lakini kina mawazo ya kufikiri yasiyozidi matatu

Ningekuona una point kama ungekuja na fact katika kile unachompinga.
Kinyume chake ni bora ungekaa kimya.
Ccm huwa wanapakuliwa ubongo wanapoingia chamani. Huyu hajui ubongo wake upo shelfu gani. Halafu wamekaririshwa hoja zilezile zisizo na mashiko. Ukifuatilia humu utawajua ni wepi kwa kusoma tu hoja zaom
 
Jenerali Ulimwengu amenena ukweli ambao wana-CCM wajinga na wanafiki, hawawezi kuukubali. Lakini wale wachache wenye akili na wakweli wa nafsi, wanaujua ukweli huu, na unawaumizi, bahati mbaya ni wachache sana. WanaCCM wengi ni wanafiki walioamua kuacha kuziishi nafsi zao, na badala yake kuutumikia ujinga na unafiki.

Ukweli ni kuwa chini ya uongpzi wa CCM, ile faida ya kuwa wengi haipo kwa sababu mawazo, vipaji, na fikra, ambavyo laiti vingeweza kuwekwa pamoja ili kujenga Taifa, havina nafasi. Watu wote wanalazimishwa kutumia mawazo, fikra na vipaji vya watu wasiozidi watatu. Na bahati mbaya zaidi ni kuwa hao watatu unakuta wana weledi duni, fikra mgando na vipaji kibaba.
 
MWANDISHI wa Habari Mkongwe, Jenerali Ulimwengu leo Septemba 21,2021 amezindua Kitabu chake RAI YA JENERALI jijini Mwanza na kuhudhuriwa na Askofu Benson Bagonza.

𝗛𝗔𝗬𝗔 𝗡𝗜 𝗕𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗡𝗘𝗡𝗢 𝗬𝗔𝗪𝗔𝗟𝗜𝗬𝗢𝗭𝗨𝗡𝗚𝗨𝗠𝗭𝗔 𝗪𝗔𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗪𝗔 𝗨𝗭𝗜𝗡𝗗𝗨𝗭𝗜 𝗛𝗨𝗢....

"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina zaidi ya wanachama milioni 8, lakini kina mawazo ya kufikiri yasiyozidi matatu" - Jenerali Ulimwengu

"Hakuna uwezekano wa kizazi chetu kupata maendeleo na kupiga hatua ikiwa kitaendelelea kufundishwa kwa lugha wasioijua na pia wale wanaowafundisha nao hawaijui hiyo lugha"- Jenerali Ulimwengu

"Hakuna swali la kijinga ila majibu ndo ya kijinga"- Jenerali Ulimwengu

𝗔𝘀𝗸𝗼𝗳𝘂 𝗕𝗲𝗻𝘀𝗼𝗻 𝗕𝗮𝗴𝗼𝗻𝘇𝗮

"Mwalimu Nyerere aliwahi kusema marais wazuri waongoze kwa vipindi viwili ili waondoke na uzuri wao, lakini marais wabaya wao wataondolewa na wananchi" - Askofu Bagonza

"Tabia ya watu kusifia viongozi waliopo madarakani kufanywe kama kosa la jinai ili kupunguza watu kujipendekeza kwa viongozi kupata uongozi"- Askofu Bagonza

"Watanzania wanahitaji katiba yenye uwezo wa kuweka na kuwaondoa viongozi madarakani badala ilivyo kwa sasa" - Askofu Bagonza

"Muujiza wa elimu ya Tanzania kiongozi akichaguliwa leo akiwa hajui kitu, akishaingia madarakani kesho yake anakuwa anajua kila kitu"- Askofu Bagonza

"Tunaupungufu mkubwa katika Taifa letu la watu wenye Fikra na Uthubutu; Wapo wenye Uthubutu lakini hawana Fikra, kuna watu unawaona wana Fikra lakini hawana Uthubutu. Makundi haya yanahitaji daraja kuyaunganisha" - Askofu Bagonza

"Aslimia 60 ya wabunge wa CCM waliopo bungeni kwa sasa hawakushinda kura za maoni ndani ya chama chao, hata wanachama wao wanajua na wanaona kabisa hawakuwachagua na hivyo wanaona siyo wa wabunge wao"- Askofu Bagonza

"Bunge la sasa lina utata, kuna mabunge mawili (2), moja lipo mdomoni mwa watu na lingiine lipo mioyoni mwa watu," -Askofu Bagonza

Chanzo; Nipashe Mwanga Wa Jamii #NipasheHabari
Huyu mlevi wa kimbari kwa nini hatujamtimua arudi kwao. Kama hawaongozi basi hakuna mtu anajua kitu ni wao tu. Tangu njama zao kumsimika kugombea uongozi tanzania kuzimwa mdomoni kwake na akili yake ni chuki kwa dola ya tanzania. Ulevi na uzee sasa ndio unampa tabu.
 
Huyu mlevi wa kimbari kwa nini hutujamtimua arudi kwao. Kama hawaongozi basi hakuna mtu anajua kitu ni wao tu. Tangu njama zao kumsimika kugombea uongozi tanzania kuzimwa mdomoni kwake na akili yake ni chuki kwa dola ya tanzania. Ulevi na uzee sasa ndio unampa tabu.
Hata Nyerere ni Mburundi hivo kila mtu Ana haki
 
Ulimwengu anapaswa astaafu na apumzike. Yeye alishakuwa kiongozi mkubwa serikalini na hakuna alichofanya na vizazi vya eneo husika kumkumbuka. Ni sawa na Jaji Waryoba..wapiga kelele. Askofu anapenda kick na makofi.
Mbona kuna Viongozi wakubwa zaidi ya Ulimwengu husemi Wapumzike? Tatizo mkiambiwa UKWELI mnaumia sana

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Jenerali Ulimwengu amenena ukweli ambao wana-CCM wajinga na wanafiki, hawawezi kukubali. Lakini wale wachache wenye akili na wakweli wa nafsi, wanaujua ukweli huu,na unawaumizi, bahati mbaya ni wachache sana. WanaCCM wengi ni wanafiki walioamua kuacha kuziishi nafsi zao, na badala yake kuutumikia ujinga na unafiki.

Ukweli ni kuwa chini ya uongpzi wa CCM, ile faida ya kuwa wengi haipo kwa sababu mawazo, vipaji, na f fikra ambavyo laiti vingeweza kuwekwa pamoja ili kujenga Taifa, havina nafasi. Watu wote wanalazimishwa kutumia mawazo, fikra na vipaji vya watu wasiozidi watatu. Na bahati mbaya zaidi ni kuwa hao watatu unakuta wana weledi duni, fikra mgando na vipaji kibaba.
Kwenye siasa wingi wa watu ni hoja. Vema umeliona hilo. Wanaccm wanamuona jenerali ulimwengu kama mroho aliyekosa. Amebaki fitna na chuki. Mkimbizi aliyetaka kuongoza tanzania. Akajifanya mjamaa kuliko wajamaa. Baada ya kubainika amebakia hamaki na chuki. Tangu mkapa nchi haijawahi kua na uongozi mzuri kwa jenerali ulimwengu. Ni udikteta wa ccm na eti watanzania kwake ni wajinga kwa kuichagua ccm.
 
Ulimwengu anapaswa astaafu na apumzike. Yeye alishakuwa kiongozi mkubwa serikalini na hakuna alichofanya na vizazi vya eneo husika kumkumbuka. Ni sawa na Jaji Waryoba..wapiga kelele. Askofu anapenda kick na makofi.
Hawa jamaa ni muhimu sana sababu hawana shida na madaraka wao wanachochea watu kufikiri na hili ni jambo la afya Kwa jamii.
 
Kwenye siasa wingi wa watu ni hoja. Vema umeliona hilo. Wanaccm wanamuona jenerali ulimwengu kama mroho aliyekosa. Amebaki fitna na chuki. Mkimbizi aliyetaka kuongoza tanzania. Akajifanya mjamaa kuliko wajamaa. Baada ya kubainika amebakia hamaki na chuki. Tangu mkapa nchi haijawahi kua na uongozi mzuri kwa jenerali ulimwengu. Ni udikteta wa ccm na eti watanzania kwake ni wajinga kwa kuichagua ccm.
Umemshambulia binafsi,lakini nikwambie Jenerali ni mmoja wa viongozi wachache wa Ccm waliostaafu siasa mapema na wakafanyiwa sherehe ya kuagwa.
 
Huyu mlevi wa kimbari kwa nini hatujamtimua arudi kwao. Kama hawaongozi basi hakuna mtu anajua kitu ni wao tu. Tangu njama zao kumsimika kugombea uongozi tanzania kuzimwa mdomoni kwake na akili yake ni chuki kwa dola ya tanzania. Ulevi na uzee sasa ndio unampa tabu.
Hoja ya Jenerali Ulimwengu inatakiwa kujadiliwa na watu wenye akili timamu na uelewa mkubwa. Wewe hii hoja imekuzidi uwezo.
 
Huyu mrundi asituumize kichwa, ana uraia wa karatasi,hata kesho tunaweza kulichana
 
Back
Top Bottom