Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,026
- 12,337
Yes, kama kichwa cha uzi kinavyosema" Chama cha siasa kisicho tofautiana mitazamo baina ya wanachama ni chama kilicho kufa".
Chama chochote cha siasa hapa duniani ambacho wanachama wake wote wanakubalina kila kitu anachosema sema mwenyekiti au katibu bila pingamizi lolote hata katika mambo ya kipuuzi ni chama kilicho kufa kinajiendea bora liende tu.
Moja ya mapungufu makubwa ya vyama vya kikomunisti au vyenye chembechembe za ukomunisti wana kauli mbiu yao moja hivi inayosema" zidumu fikra za mwenyekiti".
Sasa katika hiyo kauli mbiu yao ya" zidumu fikra za mwenyekiti" anaweza tokea mwenyekiti mwendawazimu au mwenyekiti aliyepo madaraka yaka mlevya na kupeleka kuwa mwendawazimu wa madaraka aliyo nayo anaweza sababisha maafa kwa fikra zake za hovyo na asiwe na pingamizi zaidi ya "zidumu fikra za mwenyekiti".
Chama bora ni kile chama kinacho ruhusu challenge baina ya wanachama kukubaliana na kutokubaliana kwa baadhi ya mambo na sio kauli mbiu ya kipuuzi ya" zidumu fikra za mwenyekiti" au " mwenyekiti kasema".
Historia
Historia ya dunia inatueleza kuwa kauli mbiu ya" zidumu fikra za mwenyekiti" au " mwenyekiti kasema" imeweza kuleta matokeo hasi mengi tu katika mataifa mbalimbali.
Wakati mwalimu Nyerere kafika uchina na kuvutiwa na ukomunisti kipindi cha mwenyekiti Mao kwa mbwembwe akarudi bongo na kulazimisha kuifanya bongo kuwa nchi ya ukomunisti uchwara uliopachikwa jina la "ujamaa"
Mwalimu alikutana na pingamizi kubwa kwa baadhi ya wanachama kuona mawazo ya mchonga meno kuwa ni mawazo ya kipuuzi na yasingeweza leta matokeo tarajiwa ila kutokana na kutumia cheo chake cha uenyekiti aliweza ku force mawazo yake kutekelezwa huku yakisindikizwa na kauli mbiu ya "zidumu fikra za mwenyekiti"
Wale wote waliompinga mchonga meno aliwachukia na kuwachukulia hatua za ajabu ajabu alizo zijua yeye waliiona nchi chungu.
Utekelezaji wa mawazo yake ulileta hali mbaya kijamii na kiuchumi na mwisho nchi ilimshinda mchonga meno.
China napo upuuzi huu alio uchukua mchonga meno ulikuwa kwa kiasi kikubwa uliopelekea maafa katika utekekezaji wa cultural revolution/mapinduzi ya kitamaduni.
Mwenyekiti Mao kupitia cheo chake alitoa mawazo ya utekekezaji mapinduzi ya kitamaduni kwa sababu alizo ona yeye pasipo kujali njia na matokeo ya mawazo na maamuzi yake ya kipuuzi.
Bwana bwana Mao kupitia genge lake ndani ya chama cha kikomunisti cha uchina alinyamazisha kimya wanachama wote walio mpinga kwa kuwafunga vifungo vya majumbani, magerezani, wengine kunyongwa, wengine kupotezwa, wengine kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya chama na serikali na kupakwa matope wanachama mbalimbali nchi nzima kama wasaliti.
Mfano rahisi kwa China ni familia ya kina Xi Jinping huyu rais wa sasa wa China baba yao ali valishwa bango na kutembezwa sehemu mbalimbali za nchi na kuchafuliwa kama msaliti na mwisho kifungo cha nyumbani.
(Huyo hapo Baba yake Xi Jinping akiwa na bango lake)
Dada yake na Xi alijiua na Xi Jinping kutengwa na familia katika umri mdogo na kupelekwa maporini huko.
Hata yule anaeitwa Deng Xiaoping kama mwana mageuzi wa China naye alikutana na moto wa operation ya Mao.
Chama cha kikomunisti cha Uchina na nchi nzima ilipitia katika kipindi kigumu sana katika cultural revolution kutokana na maamuzi ya Mao yakisindikizwa na zidumu fikra za mwenyekiti ambazo hazikutakiwa kuwa na pingamizi toka kwa wanachama zaidi ya kuzitekeleza.
Mwisho mawazo ya Mao yali fail vibaya na kuleta matokeo mengi negative katika jamii, jambo la kushukuru ni kuwa Mao alikata moto na hio ndio ponea ponea ndipo Deng akarudisha nchi katika mstari.
Bongo wakina Oscar, Titi, Sanga n.k ni matokeo hayo hayo ya mwenyekiti kasema hivyo hakuna pingamizi zaidi ya kukubali na kutekeleza hata upuuzi.
Mwisho: Chama bora kinajengwa kwa wanachama kukubaliana na kuto kukubalina kwa baadhi ya mambo yasiyo na afya.
Chama kinacho amini katika "zidumu fikra mwenyekiti" au "mwenyekiti kasema" kwa kila jambo ni chama mfu.