Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)

Acha kupotosha hao ni raia kitendo cha luwahusisha na jeshi au kuwaita majina ya ngazi wslizokuwa wamepewa jeshini kabla ya kufukuzwa kazi ni upotoshaji mkuu. walikwisha fukuzwa siku nyingi hata kabla ya kushtakiwa kwa tuhuma zinazoeakabili. Hapo mkuu wa majeshi anahusika vipi na raia? Wenye control kwao sasa ni viongozi wa serikali ya mtaa, nzengo , ukoo wake na ndugu zake
 
kufukuzwa kazi ni upotoshaji mkuu. walikwisha fukuzwa siku nyingi hata kabla ya kushtakiwa kwa tuhuma zinazoeakabili
tunahoji namna ya kufukuzwa kwao, je misingi ya utumishi wa JWTZ ulifuatwa, shahidi anasema hata barua ya kuachishwa kazi hajapewa, stahiki hata mia hajapewa - mtu ambaye kalitumikia taifa hadi kimataifa - hii si haki kabisa na cha zaidi si ajabu hata huo ugonjwa wa akili ulitokana na mafunzo yao pamoja na utekelezaji wa majukumu yao.

Sababu wakati wanaanza jeshi kawaida walipimwa afya, kama wangekuwa na ugonjwa huo wasingepokelewa na jeshi. JWTZ huwa halipokei wagonjwa.
 
Inaumiza sana.mafunzo waliyopitia ni magumu sana na kazi zao ni ngumu sana hata hawapati fursa ya kuwa na familia.
 
Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Ni dhahiri Kingai ndiye kiongozi mkuu wa Wasiojulikana, ndiyo maana alikuwa na kiburi hata dhidi ya IGP.
 
Kiufupi askari wa cheo cha chini ni umbwa tu hawana haki wala hawatetewi ila likifika swala la masahibu na vita wanaonekana lulu, kwa sasa majenerali na mameja na makanali ndio wanaonekana wa maana ila hili ni bomu ambalo wanalitengeneza wenyewe kwa kuendekeza sisasa za maji taka
 
Acha kupotosha hao ni raia kitendo cha luwahusisha na jeshi au kuwaita majina ya ngazi wslizokuwa wamepewa jeshini kabla ya kufukuzwa kazi ni upotoshaji mkuu. walikwisha fukuzwa siku nyingi hata kabla ya kushtakiwa kwa tuhuma zinazoeakabili. Hapo mkuu wa majeshi anahusika vipi na raia? Wenye control kwao sasa ni viongozi wa serikali ya mtaa, nzengo , ukoo wake na ndugu zake
watu wanachojadili kule kuondolewa kwao kwa kukutwa na matatizo ya akili ndio sababu iyo,je walishindwa kuwatibia,sawa wanaumwa basi wangeweza kuwapa kazi ambazo zinaendana na vile walivyo na sio kufukuzwa,sawa u8memfuka je unategemea uko mtaani ataishije
 
Niliwaahi andika humu, ila shida ni kutafutana.

Mimi Kaka yangu ( mtoto wa mama mkubwa)

Wakiwa pale kambi ya ukomandoo Morogoro...

Posho zao wakawa hawapewi, wakaamua kuja Dar makao makuu JWTZ kulalamikia.

maajabu, wakapewa Kesi za Uhaini, uhujum, uasi, uporaji wa Mali za Raia.

Walikua vijana 60 wa Mafunzo ya ukomando

30 wakasamehewa ...30 Wakafungwa jela mwaka 2015 akiwemo Kaka yangu huyo.

Waziri Mkuu anajua, Mwinyi anajua, Mwanasheria Mkuu wa wakat huo anajua,Mkuu wa Majeshi alopita anajua ..maana suala lao lilijitokeza 2013 .

WAKAFUKUZWA KAZI BILA KUPEWA BARUA YA KUACHISHWA KAZI, BILA KUPEWA MAFAO YAO, IKUMBUKE TOKA HUO MWAKA 2013 MPAKA 2015 ,MISHAHARA YAO ILISIMAMISHWA.

Walikua kuachiwa mwaka 2017 kwa msamaha

mpaka naongea hii Leo, Hawa vijana wamejitahidi kutafuta haki zao sanaaa ,wametumia wanasheria wapiiii..suala lao linaminywa chini chini.

KWA sasa wamebaki vijana 29. ..baada ya mmoja maisha kumchanganya, akaungana kwenye ujambazi,... Alipigwa risasi.
Daaah inasikitisha sana
 
Semeni nyie mnaoweza kusema. Tangazo la juzi la Msemaji wa Jeshi lilionesha mapungufu makubwa sana. Tulitaraji kama jeshi letu pendwa wangekuja na majina ya matapeli waliokuwa na nia ovu ya kulichonganisha jeshi letu na wananchi.

Jeshi hili lenye heshima kubwa nchini na nje ya nchi lina mbinu nyingi za kiintelijensia na kimedani zingewatia hatiani hao matapeli wanodanganya umma ahadi za ajira
Mkuu mwenyewe anateuliwa na mwanasiasa inafikiriwa sana
 
watu wanachojadili kule kuondolewa kwao kwa kukutwa na matatizo ya akili ndio sababu iyo,je walishindwa kuwatibia,sawa wanaumwa basi wangeweza kuwapa kazi ambazo zinaendana na vile walivyo na sio kufukuzwa,sawa u8memfuka je unategemea uko mtaani ataishije
Hakuna mtu yoyote mwenye ajira rasmi ya serikali atafukuzwa kazi kwa sababu ya ugonjwa. Watu hufukuzwa kazi kwa vitendo ambavyo ni kinyume na sheria kwa mujibu wa sheria za ajira mtu akiugua kazini na baada ya kupewa likizo mbalimbali za matibabu na kuona haiwezekani kupona au kutekeleza tena wajibu wake hustaafishwa kwa heshma na kulipwa haki zake zote na sii kufukuzwa kazi. Jeshi lina mahakama yake na hawamafukuzi mtu kabla ya kumsikiliza, haya anayoyasema kwamba ni kichaa ni ili jamii imuone kwamba hana tatizo lakini ni deffence ambayo haisaidii chochote. Kma ni kichaa basi chadema waliajiri mwehu na hata anayoyaongea sii ya mtu mwenye akili timamu
 
Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Hee kumbe mtani mzito hivyo
 
Niliwaahi andika humu, ila shida ni kutafutana.

Mimi Kaka yangu ( mtoto wa mama mkubwa)

Wakiwa pale kambi ya ukomandoo Morogoro...

Posho zao wakawa hawapewi, wakaamua kuja Dar makao makuu JWTZ kulalamikia.

maajabu, wakapewa Kesi za Uhaini, uhujum, uasi, uporaji wa Mali za Raia.

Walikua vijana 60 wa Mafunzo ya ukomando

30 wakasamehewa ...30 Wakafungwa jela mwaka 2015 akiwemo Kaka yangu huyo.

Waziri Mkuu anajua, Mwinyi anajua, Mwanasheria Mkuu wa wakat huo anajua,Mkuu wa Majeshi alopita anajua ..maana suala lao lilijitokeza 2013 .

WAKAFUKUZWA KAZI BILA KUPEWA BARUA YA KUACHISHWA KAZI, BILA KUPEWA MAFAO YAO, IKUMBUKE TOKA HUO MWAKA 2013 MPAKA 2015 ,MISHAHARA YAO ILISIMAMISHWA.

Walikua kuachiwa mwaka 2017 kwa msamaha

mpaka naongea hii Leo, Hawa vijana wamejitahidi kutafuta haki zao sanaaa ,wametumia wanasheria wapiiii..suala lao linaminywa chini chini.

KWA sasa wamebaki vijana 29. ..baada ya mmoja maisha kumchanganya, akaungana kwenye ujambazi,... Alipigwa risasi.
Duh
 
Back
Top Bottom