Jenerali Mabeyo, unayasikia yasemwayo na makomandoo wetu mahakamani kwenye kesi ya Mbowe?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
 
Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia;
Wengine hawajulikani walipo kama Komandoo Moses.

1638514807659.png
 
Niliwaahi andika humu, ila shida ni kutafutana.

Mimi Kaka yangu ( mtoto wa mama mkubwa)

Wakiwa pale kambi ya ukomandoo Morogoro...

Posho zao wakawa hawapewi, wakaamua kuja Dar makao makuu JWTZ kulalamikia.

maajabu, wakapewa Kesi za Uhaini, uhujum, uasi, uporaji wa Mali za Raia.

Walikua vijana 60 wa Mafunzo ya ukomando

30 wakasamehewa ...30 Wakafungwa jela mwaka 2015 akiwemo Kaka yangu huyo.

Waziri Mkuu anajua, Mwinyi anajua, Mwanasheria Mkuu wa wakat huo anajua,Mkuu wa Majeshi alopita anajua ..maana suala lao lilijitokeza 2013 .

WAKAFUKUZWA KAZI BILA KUPEWA BARUA YA KUACHISHWA KAZI, BILA KUPEWA MAFAO YAO, IKUMBUKE TOKA HUO MWAKA 2013 MPAKA 2015 ,MISHAHARA YAO ILISIMAMISHWA.

Walikua kuachiwa mwaka 2017 kwa msamaha

mpaka naongea hii Leo, Hawa vijana wamejitahidi kutafuta haki zao sanaaa ,wametumia wanasheria wapiiii..suala lao linaminywa chini chini.

KWA sasa wamebaki vijana 29. ..baada ya mmoja maisha kumchanganya, akaungana kwenye ujambazi,... Alipigwa risasi.
 
Jeshini kunasheria zao
 
Mtani wangu na mkuu wangu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo, nakusalimu na kukutakia kazi njema. Nakuuliza tu kizalendo: unayasikia au kuyasoma maneno yasemwayo na makomandoo wetu walio washtakiwa na mashahidi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake? Hakika, makomandoo hawa (ingawa kwasasa wote hawako tena jeshini/kazini) wanazungumza vya kushangaza na kuogofya.

Kuanzia Kusekwa/Adamoo, Ling'wenya hadi Mhina wa jana wamezungumzia kukamatwa kiholela; kuteswa; kutwezwa; kudhulumiwa na madhila mengine. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watulinde. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watupiganie. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili watutetee. Hawa walifunzwa kwa fedha zetu ili waendeleze uzalendo na utii wao kwa nchi yetu. Kwanini wamepitishwa kwenye njia waisemayo?

Makomandoo wetu wamelalamika; wamelia; lakini hawana la kufanya hadi mwisho wa kesi. Wenzao wa 92 KJ na kwingineko wanajifunza nini? Wanapata ujumbe gani? Wanawaza nini? Wanawataja wenzao wengine kukamatwa na kuteswa pia. Wako wapi wale waliotajwa? Kazini? Hai? Ndugu yangu Mabeyo, utumishi wako umetukuka. Sina shaka nawe wala na jeshi unaloliongoza. Makomandoo hawa, kwa mujibu wao, waliathirika vitani. Wapewe haki zao. Wakumbukwe. Watendewe yaliyo mema.

Unaandika lakini mtani wangu Jenerali Mabeyo? Nitakuja pia nyumbani na ofisini kusisitiza hili

Wasiojulikana sasa wamejulikana?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Semeni nyie mnaoweza kusema. Tangazo la juzi la Msemaji wa Jeshi lilionesha mapungufu makubwa sana. Tulitaraji kama jeshi letu pendwa wangekuja na majina ya matapeli waliokuwa na nia ovu ya kulichonganisha jeshi letu na wananchi.

Jeshi hili lenye heshima kubwa nchini na nje ya nchi lina mbinu nyingi za kiintelijensia na kimedani zingewatia hatiani hao matapeli wanodanganya umma ahadi za ajira
 
Back
Top Bottom