Mchungaji Msigwa aliondoka CHADEMA kwa kukosa Cheo na anaondoka CCM kwa kukosa Cheo na anarudi CHADEMA kusaka Cheo

Mchungaji Msigwa aliondoka CHADEMA kwa kukosa Cheo na anaondoka CCM kwa kukosa Cheo na anarudi CHADEMA kusaka Cheo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
37,675
Reaction score
24,547
Ndugu zangu Watanzania,

Ambacho Hamkijui Ni Kuwa Mchungaji Peter Msigwa aliondoka CHADEMA kutokana na Kukosa Cheo cha Uwenyekiti Wa kanda ya Nyasa baada ya kudondoshwa na kugaragazwa vibaya na Sugu. Alipoona Amekosa Cheo Mkononi Mwake akaamua kutimua Mbio kali sana Kuja CCM kwa matarajio ,imani na Matumaini ya kuwa atapata nafasi ya Uteuzi kwa haraka sana.

Tena alitarajia pengine angeweza kuteuliwa kupeperusha Bendera ya CCM kuwania Ubunge Jimbo la Iringa Mjini ambalo aliliongoza Bila mafanikio kwa Miaka Kumi Mfululizo. Sasa Baada ya Kukaa CCM na kuona hapati uteuzi wala Matumaini ya kupata uteuzi wa aina yoyote ile. hasira zikamjaa na kuanza kuandika porojo mitandaoni ili pengine aangaliwe na kukumbukwa kwenye Uteuzi wa haraka na Dharura. Lakini akaona hakuna mwenye habari naye wala wa kumpa sikio wala wakumzingatia wala kumbembeleza.

Akaona watu wapo Bize na ujenzi wa CCM tena kwa kujitolea kwa bidii pasipo malipo wala kudai malipo .jambo ambalo yeye alikuwa hajalizoea hata siku moja . Kwasababu yeye kwa asili ni mjasiriasiasa na mchumia tumbo anayefanya siasa kwa ajili ya kushibisha na kuneemesha Tumbo lake. Alikuta CCM tunafanya kazi kwa moyo wa kujitolea bila kuuliza malipo ama fadhila ama kuomba uteuzi wala kulalamika kwa kunyimwa Uteuzi.

Wakati yeye kwa akili yake alijua kuwa pengine kuwepo kwake ndani ya CCM pengine watu watampapatikilia au kumshobokea na kuanza kumpa Uteuzi wa haraka Haraka.

Alichokuwa hakijui ni kuwa CCM ina Hadhina kubwa sana ya watu wenye Uwezo wa kuwa viongozi na wenye uwezo wa kushika nafasi mbalimbali za kiuongozi ndani ya chama na ndani ya serikali. CCM haijawahi kuwa na upungufu wa rasilimali watu hata siku moja. CCM haijawahi kuwa na uhaba wa watu wa kuongoza ama kushika nafasi fulani ya kiuongozi. CCM ni Tanuri la kupika viongozi wake kuanzia chipukizi hadi ndani ya chama.

CCM haigawi vyeo kama Njugu ama kama Fadhila ama kama hisani ama kama zawadi . Bali hugawa Majukumu kwa mtu kulingana na uwezo wa mtu husika na uwezo wa kumudu majukumu ya kazi husika na mahitaji ya nafasi . Mtu anapimwa kwa uwezo wake ndipo anapewa nafasi ya kuongoza eneo fulani na siyo kwa upendeleo.

Tofauti na CHADEMA ambako kule ni zoazoa kama madodoki yasiyoweza kuchuja uchafu. CCM unapimwa katika mizani ndipo unapewa nafasi wakati CHADEMA wao hata ukihamia leo unapewa nafasi ya kugombea Urais hata kama bado hujajua hata salamu ya chama na imani ya chama ama falsafa ya chama ama katiba ya chama na hapa mnaweza kurejea kilichotokea na kufanyika 2015.

Hii ni kwa sababu CHADEMA ina uhaba wa rasilimali watu wenye uwezo wa kiuongozi na kuweza kushika nafasi za kiuongozi. Ukitaka ujue hili angalia na fuatilia hata Elimu za viongozi wake . Utakuta ni wale wenye Elimu za hapa na pale na ambao hata hawaeleweki walianzia wapi wakaishia wapi. Utakuta Historia za Elimu za watu wake ni za kuunga unga kama Gundi na kukatika katika kama Moshi angani .

Ndio maana watu kama Msigwa wanajikuta wakipata vyeo ndani ya CHADEMA kwa sababu watu wa kuongoza na wenye sifa za kiuongozi ndani ya CHADEMA hawapo. Lakini alipokuja CCM akajikuta hana sifa wala uwezo wa kupata uteuzi na kwa ufupi ni kuwa alikuwa hateuliki, kwa sababu hana uwezo na sifa za kuwa kiongozi ndani ya CCM na serikali ya CCM. Wenye uwezo ni wengi sana ndani ya CCM. Peter msigwa alikuwa hana uwezo wa kuwa hata Balozi ndani ya CCM kwa sababu ni mkurupukaji, Mropokaji,mwenye mihemko ba asiye na utulivu kichwani unaomhitai kiongozi kuwa nao kabla ya kufanya maamuzi ya jambo lolote lile.

Sasa utakuwa wewe ni Mwendawazimu na kichaa ikiwa utamuamini leo Msigwa . Ikumbukwe nimesema kinachofanya msigwa akae na wewe ni cheo na maslahi tu na maslahi yakiisha ama akikosa cheo lazima akukimbie na kukusaliti. Ndio maana CCM baada ya kulijua hilo ilimpokea tu na kumuweka kabatini mpaka alipoamua kukimbia Mwenyewe.

CCM itaendelea kubakia chama kiongozi barani Afrika katika kuandaa viongozi wake na kuwakuza na siyo kusubiria Marejects ama watu wenye uchu wa madaraka.

Hata huko CHADEMA atawavuruga sana atakapokosa Cheo maana ikumbukwe ya kuwa msaliti ni msaliti tu siku zote na hawezi kubadilika hata siku moja. Ndio maana wasaliti huwa wanauwawa Majeshini maana mwenye akili Timamu haupaswi Kumuamini msaliti . Ukimuamini msaliti atakuona wewe ni Mjinga sana kwa sababu anajua kesho atakusaliti Tena.

Alikuja peke yake CCM na ameondoka peke yake kama alivyokuja Mwenyewe. Ametuacha wana CCM kama alivyotukuta wana CCM tukiwa na umoja ,upendo , ushirikiano na mshikamano. Huo ndio utamaduni wetu CCM na ndio historia yetu ilivyo. Hatupapaliki na mtu .

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

1779604884468.png
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ambacho Hamkijui Ni Kuwa Mchungaji Peter Msigwa aliondoka CHADEMA kutokana na Kukosa Cheo cha Uwenyekiti Wa kanda ya Nyasa baada ya kudondosha na kugaragazwa vibaya na Sugu. Alipoona Amekosa Cheo Mkononi Mwake a moto nyumba na magari yangu
Siasa ni cheo, ukimuona mwanasiasa hataki cheo huo sio mwanasiasa, mtizame Nape hivi sasa anavyoishambulia ccm, akipata uwaziri tu atabadilika
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ambacho Hamkijui Ni Kuwa Mchungaji Peter Msigwa aliondoka CHADEMA kutokana na Kukosa Cheo cha Uwenyekiti Wa kanda ya Nyas

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Ila huko CCM alivuta hela ndefu kuliko makombo unayotupiwa wewe mbwakoko.
 
Maccm ndiyo masenge kabisa Msigwa alikuwa anayatukana na yalimpa mamilioni kuingia CCM. Manina zenu.
Kwenda zako huko wewe. CCM haina huo ujinga hata siku moja na ndio maana unaona huyo. Msaliti amekimbia Mwenyewe baada ya kuona kakosa kila kitu alichotegemea atakipata ,
 
Malengo ya kisiasa ya Mchungaji Msigwa na Joseph Selasini ndani ya chadema yatafikiwa kabla ya mwaka 2026 kwisha?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom