Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

Invayolekea mvutano ulipo sasa umechangiwa na umbea na majungu. Umbea wako kama huu wa Zito kutaka kuchomwa kisu unanipa picha ya mchango wako katika kumpotosha Zito na kumjaza majungu. Inalekea kiu yako ya kuwa na msisimko wa kisiasa wakati wote inakulazimisha kubuni mambo ambayo hayapo wakati wote na kisha kuyaamini kama ni ya kweli. Ni aibu kwa mtu wa taaluma yako kujidhalilisha katika kiwango hiki. Pengine ushauri wako ndio mwiba kwa mustakabali kisiasa wa zito. Hakika kikulacho……….

Eric, niliisha kuelewa tangu ulipoanza article ya kwanza , ila wengine hatuna kiswahili na mvuto wa maneno.Tunandika tunachowaza kama unavyofanya.

Hoja yangu ni kuwa nini msimamo wako kuhusu walilofanya Chadema?

Je unayaamini maneno ya mtei kuwa fedha ilipenyezwa, nani alipewa fedha na nani? au hayo si majungu, au kuna rank za majungu.CHADEMA siku zote wanatafuta documen wakionozwa na Slaa, leo swala la watu kuwapewa rushwa linazungumzwa tu, kama unavyosema 'kufikirika' linamweka wapi Zito? Na je Mtei anaposema hivyo si anamsema Zito?

Una kithibitisho gani kuwa pengine Zito alishajitahidi kuyaweka mambo sawa yakashindikana?

Unasema swala la 'kumtenda Chacha' Umeniangusha, haiwezekani uandike nakala ndefu hivi then usiweze kuelewa sentensi fupi alizosema Zito! Zito alimaanisha na alikuwa anamjibu Asha kuwa '' kama yeye CHADEMA SASA INAVYOMSEMA YEYE ANACHUKUA HELA CCM?NDIVYO WALIVYOMFANYIA WANGWE, Eric usichoelewa hapa ni nini jamani! sina kundi, nataka ukweli! kwa hili umekosea hata kama utaandika mashairi mia! period!

Unnapokuja na kutosaidia future ya wapambanaji wengine siyo CHADEMA tu, naingia na wasiwasi, TUNAWALINDAJE HAWA WAPAMBANAJI WETU? MAANA KWA tuhuma, kuumizwa na kufanyiwa yooote mabaya wataweza?

Ngau Zito ameweza hat kama leo atakaa bench, je anayekuja nani na tuna proof gani? ili swala lisiwe la kiitikadi ukiwaza globally utaona kama kuna MAKOSA ya Zito we need to know the source! kama CHADEMA haifai kama CCM, why not say it! kwanini kijiko kisiitwe kwa jina lake?

Woote Chadema, akina Zito naona wanacheza tu, wamerudi mwaka 90' belive me when I say this.

Message sent, auwezo wa kujibizana na wewe!
 
Pole sana Zitto, lakini hizo ndio siasa kuna ups and downs. ndio kukomaa kwenyewe huko
 
1) I concur with M/falsafa1

2) kama ni family business sasa wale wanaosema ni chama cha wachaga, na huyu mamani mcgaga?

3) blaa blaaa blaaaa!! nyiiingi? wenyewe wanafanya wanajiandaa na mkutano wao wanavyojua wao.
kuku akinya fresh ila bata-ataambiwa kaharisha
 
............................ Suala hapa ni je Zito anafaulu kuwa muumini na mtetezi wa ukweli kwa maelezo aliotoa? Kama yeye ni muumini wa ukweli kwanini awe anasema "ukweli" akiwa amekasirika tu? Ni pale tu inapothibitishwa kuwa ana nyama ndio ukweli unatoka? Ukweli ungetoka kwa msimamo wake halisi(as a matter of principal) ningemuunga mkono. Zito hajafanya hivyo, kaandika kwa muskumo wa hasira, mazingira aliyotumia hayampi uwanja sawaia wa kufanya ukweli wake ukaaminika, hizi ni hujuma kwa ukweli(kama upo) anaojaribu kuutetea, uwezo wake wa kuvumilia uovu na kuutoa pale tu anapokasirishwa ni kielezo cha udhaifu wake......................……….

Hiyo paragraph inabidi isomwe mara mbilimbili na Mh Zitto.........

Good point Mkuu Eric Ongara......unanikumbusha mbaali kwenye ule mjadala wa Majimbo..........
 
Eric;

Well said on Zitto. We are now waiting for the otherside of the coin.

Mbowe naye hajafanya lolote kama Zitto "alivyofanya" hayo uliyotaja?

Jamani leteni basi BALANCED STORIES. Hicho tu ndio sisi wakongwe tunataka humu jamvini.

Au weka toka mwanzo kuwa "mimi nipo pamoja na Mbowe" thing kisha endelea/anza kumshambulia Zitto.

FP

ni vema sana kusimamia hoja badala ya kutegemea "mtu"........hivyo basi tuwe huru kusoma hoja na tuzichambue kama kawaida yetu JF......au vipi Mkuu
 
ni vema sana kusimamia hoja badala ya kutegemea "mtu"........hivyo basi tuwe huru kusoma hoja na tuzichambue kama kawaida yetu JF......au vipi Mkuu

Umesahau jina la huyo bwana alokuwa akitumia kule bcstimes? heheheheheee.....ukilikumbuka wala hutashangaa tena...

Kwa kifupi mimi nadhana Zitto ni unstable and erratic politician. Hafai kabisa kushika nyadhifa za juu za serikali ya taifa! Ubunge ndio uwe kikomo chake.
 
Mkuu lakini twende mbele tukitazama nyuma.
.
Unajua naposoma maneno ya mzee Mtei, kisha nifikirie anayezungumzwa ni mtani wa jadi Ngabu ndio Zitto!.... Loooh ingekuwa kasheshe.. mzee wa watu pengine angekuwa amelazwa Hospital Pressure imepanda!.. hapo hapo sina hakika kutokana na reaction yako itakuwa ndio sababu ya kukuhukumu wewe uwezo wako ktk kuongoza...

Hata mimi kuna wakati hujiuliza kama ningeweza kuvumilia matusi ya Mzee Mtei na huyo Kibanda!
 
kavimba sana kichwa nae,tulimuona wa maana naona taratibu kesha boa watu sasa.........utajuuta kuingia siasa.
 
Eric, niliisha kuelewa tangu ulipoanza article ya kwanza , ila wengine hatuna kiswahili na mvuto wa maneno.Tunandika tunachowaza kama unavyofanya.

Hoja yangu ni kuwa nini msimamo wako kuhusu walilofanya Chadema?

Je unayaamini maneno ya mtei kuwa fedha ilipenyezwa, nani alipewa fedha na nani? au hayo si majungu, au kuna rank za majungu.CHADEMA siku zote wanatafuta documen wakionozwa na Slaa, leo swala la watu kuwapewa rushwa linazungumzwa tu, kama unavyosema 'kufikirika' linamweka wapi Zito? Na je Mtei anaposema hivyo si anamsema Zito?

Una kithibitisho gani kuwa pengine Zito alishajitahidi kuyaweka mambo sawa yakashindikana?

Unasema swala la 'kumtenda Chacha' Umeniangusha, haiwezekani uandike nakala ndefu hivi then usiweze kuelewa sentensi fupi alizosema Zito! Zito alimaanisha na alikuwa anamjibu Asha kuwa '' kama yeye CHADEMA SASA INAVYOMSEMA YEYE ANACHUKUA HELA CCM?NDIVYO WALIVYOMFANYIA WANGWE, Eric usichoelewa hapa ni nini jamani! sina kundi, nataka ukweli! kwa hili umekosea hata kama utaandika mashairi mia! period!

Unnapokuja na kutosaidia future ya wapambanaji wengine siyo CHADEMA tu, naingia na wasiwasi, TUNAWALINDAJE HAWA WAPAMBANAJI WETU? MAANA KWA tuhuma, kuumizwa na kufanyiwa yooote mabaya wataweza?

Ngau Zito ameweza hat kama leo atakaa bench, je anayekuja nani na tuna proof gani? ili swala lisiwe la kiitikadi ukiwaza globally utaona kama kuna MAKOSA ya Zito we need to know the source! kama CHADEMA haifai kama CCM, why not say it! kwanini kijiko kisiitwe kwa jina lake?

Woote Chadema, akina Zito naona wanacheza tu, wamerudi mwaka 90' belive me when I say this.

Message sent, auwezo wa kujibizana na wewe!

Kumbe mkuu ukitulia una pointi!!!!!
Hapa umeongea vizuri sana, tofauti na mabandiko yako mengine. I wish watu wangekuwa wanakaa chini na kuja na hoja kama hii hapa. U can post ten times kumbe ni posti yako moja au mbili ndo iko constructive.
Kwa namna hii JF ni jamvi kweli kweli, lakini sio kwa kushambulia watu wa kabila au dini fulani....
Hongera kwa hii posti...
 
Last edited:
Ukiacha suala la Dowans, kujitoa kwenye kugombea nafasi ya uenyeketi CHADEMA - Taifa, kumeonyesha kukosa kwako principles. Huku kunapelekea wewe kuyumba na kupoteza sifa za uongozi bora.

kati ya controversial ambazo hana budi kurethink the direction in political race ni hizo; 1.dowans2.vying for chairmanship.
1.Dowans; ulitaka tununue tu mitambo wakati wanaharakati wote wakikataa, na kufikia kuongea lugha zisizo na nidhamu kwa mh. Mwakyembe-people discredit for that!

2.Chairmanship;nakuunga mkono kujitoa kwa sababu ulikuwa umejichimbia kaburi la kisiasa, too eary kwa sisi kukuamini kama unaweza kuongoza chama cha vijana na wazee. nimestudy the way unawatreaty wazee, nikaona, bado, huwezi. the way ulivyodili na mwakyembe, sitta na slaa hivi majuzi, bado

wayfoward; stop politicing youth wing, sababu your very senior to them in national issues, ikiwezekana achana na vyeo ndani ya chama, show that u r loyal even out of system. stop connection with untrusted networks.
otherwise mwakani utakuwa mwisho wa siasa zako, wakati siasa zitapokuwa tamu zaidi-when smart, neat and intellectual politics will prevail.

Kuna mifano mingi sana ya watu waliokuja na kuvunja PRINCIPAL zilizokuwepo. Hawa walipelekea nchi kufanikia au kuangamia. Mtu kama Hitler amesaidia sna German kuwa sehemu ilipo. Leo wanalaani kuwa hata wao waliteseka, yes. Ila hawa akina BMW, VW, makampuni ya madawa nk walifaidika sana wakati wa Hitler na hilo technologia limewapa uwezo mkubwa sana wa kufika hapo walipo.

Ndiyo maana ninaipenda sana advertising SLOGAN ya Apple Comp. Inc ya miaka ya 90 isemayo "THINK DIFFERENT."
Tunahitaji mtu ambaye ataanza kuwabadili Watanzania mawazo ya kizamani yaliyopitwa na wakati. Ndiyo maana huwa nalaani Mrema kukosa Urais. Huyu bwana Tanzania ya leo kwa vyovyote vile ingelikuwa imebadilika na mentality za watu zingelikuwa tofauti. Tanzania ni kama Congo vile. Tumeridhika na kila kitu. Sasa mabadiliko yatoke wapi?
 
Umesahau jina la huyo bwana alokuwa akitumia kule bcstimes? heheheheheee.....ukilikumbuka wala hutashangaa tena...

Kwa kifupi mimi nadhana Zitto ni unstable and erratic politician. Hafai kabisa kushika nyadhifa za juu za serikali ya taifa! Ubunge ndio uwe kikomo chake.

NN umenikumbusha kitu muhimu sana hapo.
 
Kwa kifupi mimi nadhana Zitto ni unstable and erratic politician. Hafai kabisa kushika nyadhifa za juu za serikali ya taifa! Ubunge ndio uwe kikomo chake.

Napenda kutofautiana na wewe mkuu....

Kusema ukweli nimemsoma Eric, Omar, NN, Ogah, Waberoya etc. vizuri sana. Hapa mtakubaliana na kutofautiana, ila ni vizuri watu wakajaribu kumtazama huyu Zitto kwa uzito unaotakiwa.

Kwa kilichojiri hapa majuzi naona Zitto kakosea sana. Ila kukosea huku ni kutokana na hulka yake ya kufanya mambo...KUJARIBU. Sio mtu wa kukaa nyuma na kuangalia watu wakifanya kwa sababu zozote zile ambazo unaweza kuzifikiria, mfano kuahirisha, uoga wa KUKOSEA, au ngoja tuone watakavyokosea etc etc. Pia naona experience kidogo kaikosa. Lakini bado yuko step ya mbele sana zaidi ya wengi wanaoongea kumponda hapa na kwingine kote.

Nachotamani kukiona kikitokea mbeleni ni kwa Zitto na wenzake huko CHADEMA kukaa chini na kujiangalia wapi tumekosea. We always learn from mistakes. Kilichotokea kisiwarudishe nyuma na kusambaratika. Wanatakiwa waonyeshe ukomavu kwa kutoka katika hii crisis kifua mbele, kuwashangaza wale wote waliokuwa wakiwaombea mabaya.

Kingine kitazamwe kwa nini hii ishu ya CHADEMA imekuwa kubwa namna hii?? Naweza kusema ni kutokana na nguvu yao ambayo walishajikusanyia. So huu ni wakati wa watu kumeza pride zao, kushuka chini, kukiweka chama mbele, kujisafisha na kikubwa kujifunza kutokana na kilichotokea kisitokee tena....
 
Zitto moyo na mapenzi yake kwa sasa yako CCM na kwa Kikwete:

1. Kamati ya madini
2. Dowans
3. Bajeti iliyopita ya serikali

and on and on
 
Kwa kilichojiri hapa majuzi naona Zitto kakosea sana. Ila kukosea huku ni kutokana na hulka yake ya kufanya mambo...KUJARIBU. Sio mtu wa kukaa nyuma na kuangalia watu wakifanya kwa sababu zozote zile ambazo unaweza kuzifikiria, mfano kuahirisha, uoga wa KUKOSEA, au ngoja tuone watakavyokosea etc etc. Pia naona experience kidogo kaikosa. Lakini bado yuko step ya mbele sana zaidi ya wengi wanaoongea kumponda hapa na kwingine kote.

Mkuu Techmaro,

Chukua 5 kabisa. Kuna watu kibao tuna tabia hata kusema asante tunasubiri kwanza kuangalia nani kaweka asante ili kuficha msimamo wetu. Tukishaona fulani na fulani wako wapi (kama Mbunge wetu wa Sikonge - Nkumba) basi ndiyo na sisi tunaibuka kusema.

Ndiyo sababu pekee inawafanya wengine wampende Lowassa kwani na yeye huwa hasubiri. Ila Lowassa ana ujinga mmoja. Yeye atafanya jambo lolote limwijialo kichwani hata kama watamwambia kuwa hapa hapafai kwa hilo. Alilia Richmonduli na pamoja vitu kibao kukosekana, alipindisha kila mstari hadi ikapatikana. Watu kama hawa ni HATARI sana. Hawaambiliki wala hawashauriki.
Zitto na yeye pia ana PUPA. Hakai kusubiri wengine wanasemaje. Anaruka na kufanya lile ambalo yeye anaona linafaa. Ila pamoja na hayo, anaonekana ni mtu anayeweza kupokea USHAURI mara akionyeshwa kuwa hili dogo umechemka. Wengine wanamlaani kwa hilo. Anyway, kila mtu na mawazo yake. Ila ukweli lazima usemwe kuwa "ZITTO ANAFIKIRI TOFAUTI. Yes, Apple computer wanasema "THINK DIFFERENT".
 
Sijui ni lini tutaanza kuwashangilia mashujaa badala ya kuwanyamazisha na kuwakebei.

Mrema alipoyamwaga mapungufu ya CCM miaka ya 90 alitolewa mbio na kunyimwa mkate hadi sasa kakonda kiasi kwamba mafundi cherahani wameacha kuendelea kupunguza size ya kofia yake.

Leo hii Zitto anapoyamwaga matatizo ya Chadema (rushwa, ukabila na udini) wengi tunaona katenda dhambi! Ati tunataka akaongelee chumbani kwa Chadema, kana kwamba Taifa ni Chadema.

Huu ni upumbavu husiopimika; nchi inaliwa, ukabila na udini unaenea ndani ni nje ya Chadema, kadhalika democracy inanyanyaswa ndani na nje ya Chadema. Wachache wanaojitoa mhanga kukemea mambo haya hadharani tunawafanya wawe apologetic, kwa visingizio vya "kukeuka maadili" au kutunza "heshima ya chama". Huu ni upumbavu kwa herufi kubwa.

Chama kinatunza maadili gani kama wanachama wake niwapika majungu, wala rushwa, wakabila, wadini, na wazee wake hawatoi baraka zao kwa mwanachama anayetumia haki yake ya kimsingi ya kugombea uenyekiti?

Halafu hii kitu nayo inanisumbua: Hivi wazee wa Chadema ni akina nani na wana mamlaka gani ndani ya katiba ya Chadema? Mkutano wa wazee hawa huitishwa na nani? Mbowe? Slaa? Na ili niwe "mzee" wa Chadema natakiwa niwe wa namna gani? Wazee hawa ushauriwa na nani?
 
Leo hii Zitto anapoyamwaga matatizo ya Chadema (rushwa, ukabila na udini) wengi tunaona katenda dhambi! Ati tunataka akaongelee chumbani kwa Chadema, kana kwamba Taifa ni Chadema.

Unataka kubadili historia au wewe ndiye unataka Zitto akaongelee chumbani kwa Chadema? Zitto kaflip flop, kajichanganya, karopoka na zaidi ya yote, kaonyesha mapenzi yake yako mbali na chama chake.

Akikosolewa hapa ni makosa? Zitto si MUNGU kwamba hakosei na JF haina mtu ambaye haguswi. Zitto kachemka na anapata vidonge vyake kama wengine woooote.
 
Hivi kukemea kwake dhidi ya maovu ya Chadema ndio kigezo cha kumshutumu kwamba hana mapenzi na Chadema? Kumbe ukiwa kiongozi wa Chadema kamwe hutakiwi kukemea maovu ya Chadema hadharani hata kama maovu hayo ni pingamizi la juhudi za kumletea maendeleo Mtanzania!!

Nisingependa nishawishike kwamba ni Kweli chadema ina wenyewe...na nisingependa nishindwe kukubali kwamba "na wenyewe ni wachaga".
 
Back
Top Bottom