Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

Mdogo wangu Zitto... CHADEMA is NOT for you!!!, You are smart, talented, visionary and ambitious; Just move on; soma, fanya biashara zako na ukiamua kurudi siasani; angalia kilicho bora!!!!

The storm coming from people supporting Mbowe, show that the hatred is toooo deep to be ignored!!
SIKUJUA!!!
 
Dude appears arrogant, self-righteous, ego-tripping and not least has a tendency to draw (and relish in) attention to himself.

I bet in the back of his conceited mind he believes himself to be some kind of charismatic, young, uniquely ambitious, next generation political animal in the local political scene.

All the hype he receives on a daily basis in the tabloids as some sort of an up-and-coming political stalwart and stud (among the usually grey-haired CCM geezers and rest of the aging, tired-looking and boring political talking-heads) no doubt contributes to his big-headedness (or inflated sense of self-importance if you will)

But one thing I know for sure (and you can all agree with me - more or less), ni kwamba jamaa ana sura mbaya kama kiatu cha Baniani! Damn!

Bwa ha ha ha.. sasa sura ya Zitto inaingiaje hapa tena wajameni? Mboni sielewi?
 
Mie naomba mijadala ya ZIITO na CHADEMA isitishwe kama kweli tunataka kuokomboa nchi hii!!!!
 
Kama ambavyo wengi wetu humu hatukumwomba/kumshauri Zitto achukue fomu kugombea nafasi ile, ni vizuri sasa tukaheshimu uamuzi "wake" wa kujitoa kugombea.
 
Sisi vijana wa CCM ni kicheko na furaha tele. Tukiona watu wanao tutuhumu kuwa sisi mafisadi, kumbe wao pia wanahilo. Pambaneni ila msiumizane yetu macho. Kwa hali hiyo tuna miaka 60 mbele ya kutawala nchi hii
 
The title is very misleading. Hiyo first lady inge paswa kuwekwa katika quotations. Title inakua kama magazeti yanavyo fanya kuattract readers.
 
Naogopa yoyoooo, o kaka naogopa yoooo
toka lini tofali la barafu likajenga nyumbaaaaa

Naogopa yoyoooo, o kaka naogopa yoooo
toka lini tofali la barafu likajenga nyumbaaaaa

Dharau yako CHADEMAAA, tegemeo lako ni bure (bure!)
toka lini tofali la barafu likajenga nchiiii!!!
 
Sisi vijana wa CCM ni kicheko na furaha tele. Tukiona watu wanao tutuhumu kuwa sisi mafisadi, kumbe wao pia wanahilo. Pambaneni ila msiumizane yetu macho. Kwa hali hiyo tuna miaka 60 mbele ya kutawala nchi hii

Mkuu inabidi hii "sisi vijana wa CCM" uielezee vizuri. Kwani kuna "sisi vijana wa CCM tunaopinga ufisadi" ambo kwa ajenda hiyo tunaungana na wapinzani wanaopinga ufisadi kwa kuwa our common interest is to see a better and a well of Tanzania. Na Kuna "sisi vijana wa CCM tunaotetea ufisadi" ambao akili zetu zimechafuliwa na hela, na tunaona tuibe tu na tutunishe mifuko yetu na akaunti zetu. kutoijali Tanzania na watanzania.
 
The title is very misleading. Hiyo first lady inge paswa kuwekwa katika quotations. Title inakua kama magazeti yanavyo fanya kuattract readers.

Hapa umenena mkuu.Na hilo jina la first lady nani amempa?

na naona huko CHADEMA chama kimekuwa family business sasa not ve sonn utasikia mamake zitto ni mwenyekiti wa wanawake chadema!
 
Mhh mbona makubwa haya!!!! Kama ni kweli alitakiwa kuweka mambo wazi kuhusu huo uchafu wa makao makuu.
 
1) I concur with M/falsafa1

2) kama ni family business sasa wale wanaosema ni chama cha wachaga, na huyu mamani mcgaga?

3) blaa blaaa blaaaa!! nyiiingi? wenyewe wanafanya wanajiandaa na mkutano wao wanavyojua wao.
 
What if is true?? jamani kunya anye CCM akinya CHADEMA karanga? wote tunapige kelele ili kusiwa na ukabila, kama Zito angeruhusiwa huoni kuwa wangeondoa hilo wingu maana lipo na lilikuwepo! kama CHADEMA tunakiamini kwa nini tusikionye leo?


NDIO AWE KATIBU MKUU UKABILA UTAKUWA UMEPUNGUA.

I ssue ya ukabila wa wachaga na wanyakyusa imekuwa ajenda si kwenye chama tu ila hata kwenye sekta nyingine ila kwa wale wasomi wa hesabu wanajua mkiwa wengi mahali, probability ya kuchaguliwa wengi inakuwa kubwa. Mara TRA, mara Wizara ya Fedha tunalalama kuna uchaga. Tuelewe wanyakyusa, wahaya na wachaga wengi zaidi wameenda shule na mambo haya yanahitaji shule hivyo uwezekano wa kuwa wengi mahali sioni shida. Tujenge mashule mengi na kwetu ili tupunguze makali hayo

Kwa hiyo hata kama wachaga wanastahili wasipewe nafasi? kwa nini tuwabague?
 
Mkuu inabidi hii "sisi vijana wa CCM" uielezee vizuri. Kwani kuna "sisi vijana wa CCM tunaopinga ufisadi" ambo kwa ajenda hiyo tunaungana na wapinzani wanaopinga ufisadi kwa kuwa our common interest is to see a better and a well of Tanzania. Na Kuna "sisi vijana wa CCM tunaotetea ufisadi" ambao akili zetu zimechafuliwa na hela, na tunaona tuibe tu na tutunishe mifuko yetu na akaunti zetu. kutoijali Tanzania na watanzania.

Maana yake tunamsubiri zitto kwa HAAAAAAAMU atue UVCCM! Ni suala la Muda tu.

Congrats Hussein Bashe
 
Kaka kwa umri wako kukumbatia theory za kuhalalisha ugandamizaji kam huu unatutisha sana endapo utapewa uheshimiwa wenye makali ya dola



Unataka kusema kuwa wanaCHADEMA hawana uwezo wa kuchagua viongozi wao?





Kaka hata mimi naomba utokee muujiza hili lifanikiwe. Lakini swali kwa unavyomjua MTUHURU wako unadhani anaaminika hata kumpendekeza Zitto kuwa Katibu wake? Na kama kulikuwa na mpango huo iweje Slaa aache kuchukua fomu za kugombe umakamo?



Kwa hiyo kwako wewe unaona ni sawa kabisa kuacha CHADEMA iliyojaa wasiokuwa tayari kupractice demokrasi kuwaongoza watanzania kufanikisha demokrasia pana. Unataka kusema wale mafisadi wa kenya walivyowalaghai wakenya na dudu lao waliloliita NARC na kuja na madudu kama ANGLO LEASING Scandals ndio mfano wa kuigwa kwa watanzania?



Kama sio kujua kuwa mmoja wao angekosa ustaarabu wa kutumia siasa safi kufanya kampeni zake, uoga wa kutowashindanisha unatokea wapi. Yaani mnataka kusema yale mawazo ya wahafidhina wa CCM kuwa kumshindanisha JK na mtu mwengine kutavunja chama yana maniki. Ilikuwaje mkaanza kuwabeza wale kina mama na wazee wa watu walipoandamana kuwatisha wanaCCM wengine wenye nia ya kushindana na JK 2010? Au kwa sababu huyu ni mswahili Jakaya ni sawa lakini sio "mstaarabu" FREEMAN AIKAELI?



Makundi hayakuanza na Zitto ila yameanza na utamaduni wa kufukuzafukuza kila anayetofautiana na maslahi ya wachache yanayopewa jina la maslahi ya chama. Na usimsingizie Zitto kuwa aligombea kukuza ama kumaliza kundi jingine. Kama kitu alichokuwa anasisitiza kuwa kinatia umuhimu wa yeye kugombea ni kusamehe wale wote walionewa kwa kufukuzwa ama kusimamishwa uanachama mara baada ya kuonyesha tofauti zao na mwenyekiti wao. Na hili amelisema hata alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari. Sasa hii ya kumaliza kundi jingine yametka wapi. Usitie shaka Zitto hana roho ya korosho na wala utamaduni wa kuweka vinyongo na pia best wako Mnyika kamwe hawezi kugeuka adui wa Zitto kwani wametoka mbali. Kidudu mtu ambaye anapaswa kunyamzishwa ni mwengine ambaye sidhani kama ana umuhimu sana kwako.



Dogo umefikia lini umri wa Wazee wa Chama unakuja na mawazo mgando kama haya. Yaani U-CCM umewaathiri namna hii. Kama ninyi mliokulia katika enzo za siasa za ushindani mnafikiria hivi iweje leo muwashangae MAGOGO yaliyofubaa ya CCM?



Aliyechukua fomu na kujaza kuomba ridhaa ya wanachama wake kuwa kiongozi wao na waliotumia bisara zisizo na hakima kumshinikiza ajitoe kwa kuogopa athari za siasa chafu za KIJANA wao na baadae wafuasi wake kuendeleza kumwaga sumu dhidi ya mwenzao, ni yupi ambaye anataka kukisambaratisha CHAMA?


Maandiko ya Zitto kama majibu ya Tuhuma dhidi zake JF


Ina maana huyajui haya kama yanatendeka?



Ni wapi Zittoa amesema hawa ni wabaya wake. Na kama wakati Zitto anakubali ushauri wa wazee wao wanaingia mitandaoni na kwa waandishi wa magazeti kuendeleza propaganda zao kama walizotumi kumfrustrate Kaborou na Chacha Wangwe ulitaka Zitto awanyamazie. Ili iweje? Watu wazoee uzandiki wao hadi waamini?



Unataka kuniambia kuwa Zitto angeenda kukimbilia kwa hao wazee ambao nao wanakuja kudai kuwa Zitto ana tuhuma za kuhonga vijana kwa ushahidi wa sms na vijikaratasi? Sijui kuhusu mauaji lakini unataka kusema CHADEMA hakuna tuhuma za matumizi mabaya? Hayo ya uchaga ni nani kama sio wenyewe wanayoyatengenezea mazingira ya kuyahalalisha. Tatizo hizi natural born arrigances zinawafanya muwe reckless kiasi cha kufanya yaleyale ambayo maadui zenu wangependa muyafanye ili muwathibitishie mapungufu yanu.

Hivi iweje mtu anayetumia fedha za chama vibaya, akatumia ukabila katika kufanikisha malengo yake akawa na mapenzi na chama chake na yule ambaye anamwambia kuwa acha kutumia ukabila ndiye akawa hana mapenzi nacho. Kwani haya yameanza kusemwa lini? jee kuna suluhu iliyofanyika kichama? Na imekuwaje kuwa hata alliances za utetezi wa MBOWE na mashambulizi dhidi ya Zitto zikawa na picha ya udini? sitaki nije kwa undani wake hapa lakini kama unahitaji nishtue nitakushukie the whole chain...

Ni kama anatuambia yeye haipendi CHADEMA kihivyo! wakiendelea kumgusa ataua chama! Huu ni ubakaji wa chama na kuibua hofu za kibazazi. Ni kama anawaambia wanaCHADEMA wasimuuzi lasivyo atanyea kisima?! Hatuwezi kuendesha chama kwa hofu na kuwaza ni lini Zitto atakunya katika kisima. Kuna maswala mengi ya kuwaza katika mustakabali wa nchi zaidi ya kunya kwa Zitto.


Ulitaka abaki ili mtimize mpango wenu wa kumchoma visu?


Tangu lini kumpigia kampeni mtu kukageuka kuwa kuhujumu uchaguzi?



Tangu lini aliyeshinda uchaguzi akalalamika kuwa kadhulumiwa? angewasilishaje taarifa wakati wenye chama wameshinikiza hata majibu yasitolewe.




Yaani sasa mnataka hata watu wasihoji makosa ya kikatiba? Kazi kwelikweli.



Kama msingeendelea na propaganda zenu dhidi yake ni wazi mambo yangekuwa shwari sasa. Kosa ni lenu mliochukulia uamuzi wake wa kujitoa kama weakness na mkaendeleza mpango wenu wa kummaliza kisiasa...Na msipoangalia mtaadhirika maana FREEMAN na ZITTO walijuana siku nyingi na wamefanya mengi pamoja.....wakati ninyi mnaendela na ujinga wenu huku wenzenu wanaangalia jinsi gani ya kufanya kazi pamoja huko mbele kuendeleza libeneke (ofcourse kama mmoja wao hajaendeleza chuki zake)




Wenye jitihada ya kuiua CHADEMA ni wale walio tayari kufanya lolote ili mradi kulinda vyeo vyao na maslahi yao hadi kuwafanya wazee kutumia busara isiyo na hekima kumshawishi Zitto kujitoa......

omarilyas

Omary, unapotumia wingi unaniwekwa mimi katika kundi gani? Kama una aamini mimi nimeandika kwa msukumo wa makundi au kutumia na kama huo ndio msingi wako wa kuamini kuwa kuna makundi basi ya makundi hayapo na ni hewa.

Binafsi siamini kama kuna makundi.Hata hivyo wewe unalazimisha kuwepo makundi na kujipachika katika kundi la kubuni la zito. Mtazamo wako huu umekupofusha na usione mantiki ya hoja zangu. Nimekuonyesha mwezi wewe umetazama kidole.

Msingi wa hoja zangu ni maandiko yalikosa mwelekeo ya Zito.Nimempima zito na Zito mwenyewe. Matendo yake, misimamo yake, muonekano wake katika jamii na matarajio ya jamii kwake ndio msingi wa maandiko yangu. Amepwaya dhidi ya mizani aliyoibuni mwenyewe.


Nimesema mwanzo kuwa sitetei ukiritimba na naamini ushindani ni chachu muhimu kwa ustawi wa chama. Hoja zangu zimejikitka katika uwezo wa kitaasi kwa sasa kubeba ushindani huu? Pia ni nimehoji msukumo halisi wa Zito kugombea(wewe unakaribia kusema aligombea kwa kuwa hakuwa na uhakika wa kuteuliwa kuwa katibu mkuu!) na mwisho nimemlaumu Zito wa kutofanya maandalizi ya kutosha kama mgombea, kushindwa kwake kusoma mazingira ya chama anachokiongoza alikuwa tayari majiandalia mazingira ya kushindwa kwa maksudi! Na hapo ndipo ninapoibua shaka ya lengo lake...........



Suala la Zito kuzungumzia kusimamishwa/kufukuzwa kwa viongozi na wanachama ni hoja inayomkaba Zito pia. Nakumbuka Zito ni moja ya watu waliotetea umuzi ule Tanga na alitoa mifano ya CCM kuwahi kufanya maamuzi kama hayo huku nyuma kwa kina ml0o, seif, jumbe n.k.

Jitihada za kumuibua Zito kama shujaa kwa uzembe wake aliofanya hazitasaidia. Nimekusoma unajaribu kujengwa taswira kuwa Zito amefanya vyema kusema aliyoyasema kwa minajili ya kusafisha chama? Eti anatetea Ukweli ? Huu ndio uwezo wako kweli Omar?

Suala hapa ni je Zito anafaulu kuwa muumini na mtetezi wa ukweli kwa maelezo aliotoa? Kama yeye ni muumini wa ukweli kwanini awe anasema "ukweli" akiwa amekasirika tu? Ni pale tu inapothibitishwa kuwa ana nyama ndio ukweli unatoka? Ukweli ungetoka kwa msimamo wake halisi(as a matter of principal) ningemuunga mkono. Zito hajafanya hivyo, kaandika kwa muskumo wa hasira, mazingira aliyotumia hayampi uwanja sawaia wa kufanya ukweli wake ukaaminika, hizi ni hujuma kwa ukweli(kama upo) anaojaribu kuutetea, uwezo wake wa kuvumilia uovu na kuutoa pale tu anapokasirishwa ni kielezo cha udhaifu wake.

Isitoshe hajaeleza ukweli wowote zaidi ya umbea. Kama angekuwa na nia ya kutoa ukweli angefafanua suala la "kumtenda wangwe" na masuala ya ubadhirifu kinagaubaga,yeye kugusia na kuwaaacha watu wafikiri watakavyo sio sifa ya mwkeli, lengo lake ni kupandikiza hisia mbaya dhidi ya chama na sio kukisafisha. Kama amaamua kusafisha asafishe kwa ustadi tuliouona kwenye uwasilishaji wa hoja ya Buzwagi na sio kutoa madokezo ya kimbea yenye mguso wa kishangingi. Uamuzi wake wa kueleza maneneno nusu na kutafuna maneno hapa hatuwezi kusema ana nia ya kusafisha chama. Hapa ametweta.


Suala la Zito kumfahamu Mbowe na Mnyika mda mrefu sio hoja,na sijui inaingia vipi hapa, wandelee kufahamiana maana mahuisiano ni hitaji la kiutu.Sikuandika kwa minajili ya kuhoji mahusiano yao nimehoji weledi na uwezo wa Zito kioungozi.

Hilo swala la Zito kuchoma kisu linatokea wapi? Kwanini unakuwa mwepesi kupandikiza hoja zisizo na maana yoyote ile? sikuona mazingira ya hatari kwenye uchaguzi wa BAVICHA. Sehemu kubwa ya hoja zako ni za kufikirika na kuweweseka nakosa pa kuanzia kuzijibu. Invayolekea mvutano ulipo sasa umechangiwa na umbea na majungu. Umbea wako kama huu wa Zito kutaka kuchomwa kisu unanipa picha ya mchango wako katika kumpotosha Zito na kumjaza majungu. Inalekea kiu yako ya kuwa na msisimko wa kisiasa wakati wote inakulazimisha kubuni mambo ambayo hayapo wakati wote na kisha kuyaamini kama ni ya kweli. Ni aibu kwa mtu wa taaluma yako kujidhalilisha katika kiwango hiki. Pengine ushauri wako ndio mwiba kwa mustakabali kisiasa wa zito. Hakika kikulacho……….
 
Back
Top Bottom