Eric Ongara
Senior Member
- Sep 19, 2006
- 165
- 8
Wengi wamepongeza baadhi kuhoji na kubeza uamuzi wa Zitto kugombea. Na badae wamebeza uamuzi wa Zitto kujitoa sambamba na kushangazwa na ushauri wa kamati ya wazee waliomshauri Zitto ajitoe katika kinyanganyiro cha uenyekiti wa taifa dhidi ya mwenyekiti wa sasa Freeman Aikael Mbowe( Mtuhuru).
Sikubaliani na waliompinga Zitto kwa msukumo wa mazoea na kukumbatia ukiritimba. Ushindani ni hitaji muhimu katika ustawi wa chama. Ni kweli Zitto alikuwa na haki ya kugombea na anakidhi vigezo vya jumla vya kugombea. Kinachogomba ni wajibu aliojaribu kuupuza wakati anafanya maamuzi ya kugombea. Lazima tukumbuke haki huambatana na wajibu.
Zitto anafahamu kwa sasa CHADEMA haina anasa ya kuchagua kati yake na mtuhuru. Pamoja na ukuaji unaovutia kwa nje,CHADEMA bado haina watu wenye mitaji mikubwa ya kisiasa.Inawahitaji wote(Mtuhurum,slaa na Zitto) kwa pamoja katika timu moja ya kiuongozi.Jaribio lolote la kulazimisha wanachama wachague kati ya mtuhuru,Zitto au slaa ni fikra muhali za kihuni ambazo zinaweza kukijeruhi chama.
Zitto alipaswa kutekeleza vyema wajibu wake kwa kutafakari.Pengine hakujipa mda wa kutosha kutafakari kwani alikamilisha maamuzi yake akiwa uwanja wa ndege. Wengi wanoasukumwa na nadharia zaidi ya uhalisia, walitaka Zitto ashindanishwe na mtuhuru kama kielelezo cha kukidhi matakwa(na sio mahitaji) ya demokrasia kwa tafsiri na matamanio yao.
CHADEMA ina wafuasi wengi lakini ni wachache waliojitokeza mbele katika siasa za moja kwa moja.Hivyo CHADEMA inahitaji majabali haya machache kuendelea kuwemo katika safu moja ili kukiandaa chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu.Tayari kulikuwa na wazo la kutumia "utatu mtakatifu" yaani Mtuhuru,Slaa na Zitto katika kuipasua na kiitesa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwakani na hatiame kukiandaa vyema chama na mwaka wa mavuno mwaka 2015.
Zitto alikuwa ana wajibu wa kutafakari namna ambavyo "haki" yake ya kugombea ingesababisha mnyukano ambao ungeibua athari za muda mrefu kwa chama na wagombea. Hatuwezi kuhujumu demokrasia ndogo kwenda kuathiri demokrasia Pana.Hatuwezi kutetea udhofishaji wa CHADEMA Kwa kiisngizio cha demokrasia na kwa wakati huo tukiua demokrasia pana yani ushindani wa CCM na CHADEMA.
Kugombea kwa Zitto kungefaidisha zaidi CCM zaidi ambavyo ingefaidisha CHADEMA. Kama CCM wangeombwa ushauri basi wangesisitiza Mtuhuru na Zitto washindane. Hivyo uamuzi wa awali wa Zitto kugombea ulikuwa tayari una manufaa kwa wapinzani wa CHADEMA Hususani CCM.
Inalekea kulikuwa na makundi ya muda mrefu ambayo Zitto anayafahamu kwa mujibu wa maandiko yake hapa, na pengine ndio msukumo wake kugombea. Kama ndivyo,Zitto amepwaya kiungozi kwa kuamua kugombea kwa msukumo wa kukuza na kumaliza kundi jingine.Umbea, majungu na husda haviwezi kamwe kufaulu kama kichocheo cha kuwa mwenyekiti wa chama kitaifa.
Zitto anaelewa kanuni, mazoea na taratibu za uendeshaji wa chaguzi zake za ndani. Kama alikuwa na nia njema alipaswa kuwa ameepika michakato hii ili isije ikadhuru nia yake ya kugombea na pengine kuwa na athari hasi kwa taathira ya chama kwa ujumla wake. Uzembe wake katika kutathmini hili ni hujuma za wazi dhidi ya haki yake kama mgombea na ustawi wa chama kwa ujumla wake. Ushauri uliotolewa na kamati ya wazee wa chama ni jambo ambalo Zitto alipaswa kulingamua hata kabla.Pengine lengo lilikuwa kukivua nguoa chama au kuwashwa na msisimko wa ndani.
Ipo changamoto ya chama ya kuwa na utegemezi usio wa kwaida kwa mtuhuru, slaa na Zitto kutokana na mitaji yao mikubwa ya kisiasa. CHADEMA inao watu wengi wenye weledi wanaoweza kutoa mchango mkubwa katika medani ya siasa, hivyo kunapaswa kuwa na mkakati kambambe wa kuzalisha na kutambulisha kwa umma wanasiasa wengi zaidi.Utatu mtakatifu uliapaswa kuwa nyenzo ya kutengeneza mabingwa wapya. Zitto kwa uzembe au kiburi aliamua kupuuza hali halisi ya chama na kuamua liwalo na liwe! Suluhisho lake la mvutano wa ndani lilikuwa ni kusambaratisha wapinzani wake wa ndani na pengine kukisambaratisha kabisa chama kwa ujumla wake.
Maandiko ya Zitto kama majibu ya Tuhuma dhidi zake JF
Hakuna maelezo yoyote yanaoweza kuhalalisha ujinga wa Zitto alioufanya hapa. Kwa maelezo yake amethubitisha maamuzi ya wazee yalikuwa ni sahii juu yake. Ni utovu wa nidhamu usio na kikomo na ni ishara ya kutokuwa na mapenzi yoyote na chama anachokiongoza.
Utetezi kuwa yeye ni binadamu ana nyama na kuwa anaudhika kama binadamu ni upumbavu. Ni sawa na mlevi anaebaka kwa kisingizo cha msukumo wa pombe, kwanini hakuna msukumo wa mlevi mwanaume kulazimisha kulatiwa? Kwa nini bado kuna uangalifu wa kuchagua vitendo?
Ikiwa wabaya wake ni John Mrema na John Mnyika, kwanini ameamua kugombana na chama kizima? Uchaguzi wake makini wa maeneo ya kugusa katika majibu yake ni kielelezo cha mpangalio uliojaa uovu, fikra duni na nia mbaya, mathalan maelezo yanayoibua hisia kama suala la marehemu wangwe ni kielelezo halisi kuwa Zitto ana nia mbaya na CHADEMA. Huwezi kujisaidia katika kisima ambacho unatumia kwa maji ya kunywa na kupikia kisa umekasirishwa na mwanakijiji mmoja.
Ikiwa ni kweli Mrema na Mnyika wamemtuhumu Zitto ni kwa nini kama kama kiongozi ameshindwa kutumia miundo ya chama kutataua? Na mbona amekishambulia chama kwa ujumla wake? Amekihusisha chama na uchaga( ni sawa na kuthibitisha propaganda za CCM au kuunga Mkono msimamo,mkakati na mtazamo wa CCM dhidi ya CHADEMA), maauji na matumizi mabaya ya fedha. Hizi sio tuhuma za kwa watu binafsi! Inaelekea anaowalenga wana mapenzi makubwa kwa chama zaidi yake, hivyo kete yake yeye ni kwa kuumiza kile kinachopendwa na hao maadui zake wa kubuni.
Ni kama anatuambia yeye haipendi CHADEMA kihivyo! wakiendelea kumgusa ataua chama! Huu ni ubakaji wa chama na kuibua hofu za kibazazi. Ni kama anawaambia wanaCHADEMA wasimuuzi lasivyo atanyea kisima?! Hatuwezi kuendesha chama kwa hofu na kuwaza ni lini Zitto atakunya katika kisima. Kuna maswala mengi ya kuwaza katika mustakabali wa nchi zaidi ya kunya kwa Zitto.
Kwa makusudi Zitto ameamua kupotosha suala la BAVICHA. Ushindi wa kafulila anauzungumzia anaujaje?. Nilibahatika kushuhudia uchagauzi ule, matokeo hayakutangazwa kutokana na idadi za kura kuzidi idadi ya wapiga kura. Hali ilivyoanza kuwa tete Zitto alitoa kauli tata kuwa vijana leo watatupiana ngumi na kutokomea, yeye kama kiongozi wa kitaifa anaamua kukimbia hali ile ulikuwa ni udhaifu mwingine mkubwa wa kiungozi wa Zitto.
Msiamazi baada ya kutangaza hali halisi ya zoezi la kura, aliwaapa wajumbe nafasi ya kutoa maoni yao ambao wengi walimtuhumu moja kwa moja Zitto pasipo kutafuna maneno kuwa alishiriki kuhujumu uchaguzi ule. Kipindi hicho sio Zitto wale Kafulila waliokuwepo, wagombea wengine walikuwepo na kuzunguma, hatukumsikia hata wakala wa kafulila akilalamikia kudhulumiwa. Ni aibu kwa Zitto kufanya jitihada za kuhalalisha uhuni ule. Ikiwa alibainie jitihada za hujuma dhidi ya Kafulila ni kwanini hakuziwasilisha katika kikao cha jumapili cha kamati kuu?
Kuhoji kamati ya wazee chini ya Mtei kuendelea kusimamia uchaguzi zinaozendelea wakati tayari baraza la wazee limechagua viongozi wake ni kielelezo cha kukosa uwajibikaji wa pamoja. Yeye kama kiongozi hakushiriki katika kuandaa ratiba na mchakato mzima wa uchaguzi? Kwanini anajitenga? Inaelekea Zitto amepoteza Imani na chama chake au amejifungua imani mpya.
Baada ya kikao cha kamati kuu jumapili iliyopita umma ulielezwa kuwa tofauti kati ya Zitto na Mtuhuru zimefutwa. Sasa hapa Zitto anaposema siku wakipatana na Mtuhuru wapambe nuksi watakoma anataka kusema nini? Kwamba walituzuga? Walifanya unafiki?
Kimsingi Zitto amepoteza uhalali wa kuwa kiongozi. Mtuhuru ameandamwa sana na kuandikwa mno lakini hajawai payuka nama hii kwa kisingizo kuwa na yeye ana nyama! Kiongozi lazima uwe na moyo mkubwa. Zitto angekuwa Mwenyekiti (Mungu katuepuesha) angekuwa ndio mlengwa mkuu wa tuhuma toka kwa washindani wake, angetupeleka wapi na mihemko ya aina hii ya kisiasa? Na je ni kwanini amekuwa mkali sana kwenye tuhuma hizi na sio wakati wa Dowans au ule wa mahusiano? Je kuna msukumo wowote wa hatia? Zitto anapaswa kutafakari kwa kina kwa nini nembo/Bango(Brand) yake/lake ya kisiasa imekuwa dhaifu kiasi cha kubeba tuhuma kirahisi hivi na hatime baadhi ya watu kukaribia kuziamini ikiwemo yeye mwenyewe kiasi cha kuweweseka namna hii?
Jitihada za Kuiua CHADEMA ni jambo lisilovumilika kwa hali yoyote ile.Ni ushenzi na laana iliyo kuu. Naami hili ni jaribio la mwisho la CHADEMA kudhihirisha ukomavu wake wa kisiasa na kuwarejeshea matumaini watanzania. Upuuzi na udhaifu wa Zitto unaweza kusahihishwa.

Last edited by a moderator: