Je Zitto Amepoteza Uhalali wa kuwa Kiongozi?

PUMBA, watawadanganya akina Lunyungu tu!


Duh !!! Engineer , haya bwana wacha tudanganywe basi .

Nasema hii hadithi haina maana kuja hapa .Watu wamemaliza mambo ya Chama chao waachwe wajipange .Hizi ni tuhuma na nadhani hazina msingi kwa sasa .
 
Wakuu zangu mtamfuata Zitto hadi wapi jamani?... mwacheni Zitto wa watu hii habari ni uzushi mtupu kwa sababu nimesoma mambo kibao humu ndani hayalingani kabisa..

Kwanza Ikiwa Zitto alizungumza huko Ujarumani kuhusu uchaguzi wa viti maalum 2005 hivi kweli yeye ndiye mtu wa kwanza kuliongelea hilo?..
Kisha basi kubmukumbu yangu kutokana na swala hili la uchaguzi wa viti maalum nakumbuka viongozi wa Chadema wenyewe walikuja hapa na kutuambia viti maalum vilikuwa ni viti ambavyo chama kiliwapa nafasi hiyo WANAWAKE na wao ndio waliunda kamati yao na wakachagua wabunge, hivyo uongozi wa Chadema haukuhusika kabisa na uchaguzi huo. hii ndi kumbukumbu yangu ya maelezo tuliyopatiwa hapa JF..

Haya leo nasoma tena habari hii naona jina la Zitto kuwa alikuwa ktk kamati ya kutafuta wabunge wa viti maalum... Habari inasema hivi..
Unajua hizi tuhuma ni nzito. Zingefikishwa CC, Zitto angejimaliza. Kwanza, ni yeye aliyekuwa Katibu wa Kamati ya kutafuta wabunge wa Viti Maalum. Sasa kuna makosa yamefanyika, na yeye ndiye mhusika mkuu. Asingeweza kukwepa," zimeeleza taarifa za ndani ya chama.

Hii ikiwa na maana hata wale viongozi waliokuja hapa JF kutuambia kuhusu sababu kuchaguliwa Wabunge wa viti maalum toka Mkoa wa Kilimanjaro ilikuwa kamba na UONGO mtupu...sasa jamani tuamini kitu gani?... Je kuna ukabila Chadema au hakuna maanake hata ule ushahidi tuliopewa mwanzo tukaamini unaanza kugeuka! sisi tuamini lipi hasa lilitokea maanake inakuwa tena sii swala la Zitto ila Utawala mzima wa Chadema..
Ucheni Ujinga wenu nyie mnazidi kutuchefua tu.!
 
Tuhuma ya pili kubwa ilikuwa ujumbe wa simu aliomtumia Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Taarifa zinasema Zitto alimweleza Dk. Slaa kuwa hana “msaada wowote katika chama;” na kwamba kama kuna kiongozi ambaye ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa CHADEMA, basi ni yeye na Mbowe.

“Huyu dogo, nadhani ameanza kulewa sifa. Kweli ana ubavu wa kujilinganisha na Padri huyu (Dk.Slaa)? Jambo hili lingefikishwa Kamati Kuu, hakika angekutana na cha moto,” mbunge mmoja wa CHADEMA alilimbia gazeti hili.

Imeelezwa kwamba tuhuma za Zitto ndizo zilifanya hata pendekezo lake la awali kuwa Dk. Slaa agombee uenyekiti likataliwe.

“Lakini Dk. Slaa alikataa kugombe uenyekiti, akisema hataki nafasi hiyo. Sababu kubwa ni kule kushambuliwa na Zitto.




Chanzo: Gazeti la MwanaHalisi

Zito anamtuhumu Slaa kuwa hana mchango wowote, the same Zito anapendekeza Slaa awe mwenyekiti!

Again this is Mwanahalisi!

 
Kwa kuwa ni mara ya kwanza naingia ktk thread hii sijui iwapo haya yangu tayari yamesemwa. Zitto hafai kuwa kiongozi wa CHADEMA kwa sababu:

1. Alitakiwa kwanza kuonyesha umadhubuti wa uwakilishi wa voters wake jimboni kwa kugombea tena kiti hicho na kushinda. Kama vile akina Slaa na Ndesamburo. Anaogopa hilo, kwani hajiamini kama kafanya chochote jimboni kwake, na yumkini hajafanya chochote. Kinachoonekana ni kujaribu kupurukusha mambo tu ktk kutafuta namna ya kukwepa kugombea kiti hicho. Si bora lawama kuliko aibu?

3. Kukataa kujitoa Tume ya Bomani ya madini -- iliyotokana na suala la Buzwagi lililomsimamisha Bungeni. Angeshikilia msimamo wake. Ni mtu anayekubali kuyumbishwa mara moja.

3. Kujiingiza ktk suala lmitambo chakavu ya Dowans kwa kijisimika upande usio -- tofauti na wananchi walivyotarajia kwake -- kupigia debe serikali iinunue. Mitambo hiyo ni product ya ufisadi mkubwa ulioangusha mawaziri watati akiwemo PM. Bora angekaa kimya, hajui timing na mood ya wananchi ikoje kabla hajaongea.

3. Kujiingiza mabishano na watu wengine ktk JF kwa kutumia jina lake bila kujificha. Mabishano haya mara nyingi humwendea vibaya hasa yale kuhusu mitambo ya Dowans hadi akaanza kuonyesha jazba. hii haitarajiwi kwa mtu anayataka uongozi wa chama kama Chadema. Angebishana ktk JF kwa kutumia jina la kujipachika.

4.Kushindwa kubaini uwezo wa Mbowe, na hasa Mbowe alivyoweza kukifikisha chama kilipo kutoka Na 3 hadi No 2 ktk upinzani na kukiweka chama tawala kitikisike. Ushahidi ni tarime, Busanda na Biharamulo. hivi Zitto aliona dosari ya Mbowe ni nini? Au anafuata tu majungu ya eti ukabila ndani ya chama, matumizi ya pesa nk, vitu ambavyo bila shaka hutajwa sana na maadui wa Chadema.

HAFAI KUONGOZA CHAMA. ANAYUMBA, ANAWEZA AKANUNULIWA, IWAPO TAYARI HAJANUNULIWA.

Ninachoogopa sasa hivi ni kwamba ataingia CCM atasimamishwa jimboni kwake 2010 na atashinda kwa njia ya kawaida ya CCM kuiba kura.
 
.....Maane, Niagize mtoto aniletee Popcorn?? :)
....Shwanga kabisa mkuu....we agizia popcorn tu maana NaniHii....keshaanzisha kutunguana....sijui mwisho wake stelingi atakuwa nani??
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=qYRCkg0IlIw[/ame]
 
kazi kwelikweli....huu uchaguzi wa chadema umetuonyesha sura nyingine ya hiki chama, ila pia wameonyesha ukomavu mkubwa kisiasa kwa kuweza kuyamaliza matatizo yao kwa amani.....

Zito inabidi alichukue hili kama fundisho na awe anasikiliza pande zote, ndio maana ya kuwa kiongozi mahili....
 
Finally, Eric inaonyesha Zito hajapoteza uhalali wa kuwa kiongozi, au sio, just imagine tuhuma zote zile ulizomwelekezea wewe na chama chako, bado mnampa unaibu katibu mkuu!

Politics is a game!

Usiseme kuleta mshikamano, kama mtu hafai , ni hafai tu, kama mtu kaenda kinyume na katiba na anataka kubomoa chama hatakiwi.

So kwa tulio nje tunasema Zito alituhumiwa tuhuma za uwongo, hakupokea wala kutoa rushwa, na kama ilikuwa hiyo basi CHADEMA nanyi tabia zenu za kifisadi

kwa maoni yangu you need to be critical thinker in analysing political issue otherwise AIBU TUPU!
 
je zito angekuwa mwenyekiti kauli zake tata zingekomaa?je chadema kuwa na mwenyekiti mwenye kauli tofauti na misimamo ya chama italeta taswira nzuri kwa umma?
 
hapo kabwe alisukumwa na hisia na wala si hoja. hakukuwa na sababu ya yeye kutaka kugombea kisa tu ni demokrasia. demokrasia ina mipaka na tathmini zake. hakuona mbele kama angeweza kukivuruga chama wakati hapakuwa na mapungufu yoyote katika safu ya uongozi. mwisho tunamshukuru kwa kutambua wajibu wake katika chama na kukubali hali halisi. wakati wako ukifika, uongozo wa chama utaupata
 
Eric baba, hayo mawazo yako wala usifikiri kila mtu anawaza kama wewe!

Kwangu mimi Zito mpiganaji na kiongozi mzuri, andika weeeeeeeee jaza hata thread zote kwangu mimi ni hivyo hiyo haitabadilika; sijamjua leo wala jana!

Pili, weka dhamana au insuarance kuwa wengine woote wapiganaji hawawezi kuhudhiwa na kubadilika; ama sivyo kutakuwa hakuna mpiganaji !

swala la kuwa huyu jamaa atakufa kisiasa pia ni theory is not practical, na wote wanaosema hivyo ni kujaribu kutabiri kama akina Yahaya!

Tukiwa wakali kuwalinda wale wapiganaji wetu tutawaokoa wengi, tukiwa waandika nakala kama wewe tutaua wengi mwishowe utabaki wewe peke yako maana wooote watachukuliwa na upepo.

Uwazi wa Zito ni mzuri ndugu , ni picha tunapata kuwa ni jinsi gani vyama vinavyojiita mbadala vinaishi, Zito angekuwa wa kujikomba angekaa kimya!

KWA NAKALA YAKO UNAPROVE PIA KUWA ZITO YUKO JUU SANA ZAIDI YA CHADEMA, CCM huwa hawafanyi ujinga huu, angekuwa mdogo; why all this unconvicing articles!

Mwambie Mtei na Chadema wote kuwa habari zenu tumezipata na mnavyoishi humo, hamna tofauti na CUF, NCCR, TLP.

Shida ilikuwa nini si angeachwa ashindwe kwenye kibox cha kura, wewe hili hufikirii??

swali la kumalizia, tunawalindaje hawa wapiganaji?? maana juzi tu ulikuwa unampenda Zito , leo humtaki, kesho utamkacha Slaa, maana tuhuma zipo tu, na tusivyopenda vithibitisho!

why are we not believing in them, when then we will belive them as true dream leaders??

Mtu gani mkweli atakayeingia kwenye siasa na kuishi namna hii??

ETI KULINDA CHAMA THIS IS POPPYCOCK !!!, AKILINDE KISHA WAJE KUCHUKUA NCHI, SI KAMA YA KENYA YA KUMUONDOA MOI, THEN WAO HAWATAKI KUTOKA, THUBUTU !!! better this what is CHADEMA ANYWAY , mjinga sana wewe!!

Upumbavu huu anaouvumbua Zitto badala ya kufurahia ndio mnasema kulinda chama, TOFAUTI YA HII NA CCM ni nini then

Kwa wataka mabadiliko tusio na makundi this was good movies, kuona kumbe hakuna cha CHADEMA wala CCM, wala CUF , TLP, NCCR, we are long way to true revolution, lets think another way!

ETI KULINDA CHAMA!!! huu ujinga hausameheki, NDIO MNAISHI NA WANAWAKE WAZINZI ETI KULINDA NDOA!

mchaga nini wewe!!!!!!!!!!
waberoya ndivyo ulivyo huna hoja ovyoo.
 
zitto bado ni kidume

Ni kweli bado ni kidume. Tunahitaji dume siyo kidume. Alishapoteza mwelekeo tangu suala la mitambo ya DOWANS. Hana maana tena kwa aibu alishindwa hata kuwa muungwana na kukiri alichemka. Anashindwa hata na baba wa ufisadi Mkapa aliyekiri kuboronga kwenye ubinafisshaji.
 
Ni kweli bado ni kidume. Tunahitaji dume siyo kidume. Alishapoteza mwelekeo tangu suala la mitambo ya DOWANS. Hana maana tena kwa aibu alishindwa hata kuwa muungwana na kukiri alichemka. Anashindwa hata na baba wa ufisadi Mkapa aliyekiri kuboronga kwenye ubinafisshaji.
Capt. Pleeease!..yaani umemvuta hata Mkapa ktk hii kitu..
Hivi kweli unaweza sema Mkapa ni afadhali kwa sababu tu alikiri kuboronga kwenye Ubinafsishaji wakati yeye bado ameshikilia mali za Taifa, hataki kuachia hata moja wala kukubali kama yeye na mkewe wametuingiza mjini.

Mkuu wangu Mkapa hakuboronga.. Mkapa alifanya alichokusudia kufanya, alijua fika nini matokeo ya kubinafsisha na ndio maana akafungua Ofisi yake Ikulu..A Pre meditated act! wakati mkuu Zitto wala hajui makosa yake, hesabu zake zote zinampa 2+2=22 akilini, wakati Mkapa ni mtunzi wa formula hiyo..

Kumsifia Mkapa, huu ndio UCCM damu ukisikia..haiwezekani kabisa kumlinganisha Zitto na Mkapa, na yeyote anayefikiria hivyo bila shaka atasema hakuna kiongozi Chadema anayeweza kusimama na Mkapa.. ndio lugha ya wapenzi wa Mafisadi.
 
Capt. Pleeease!..yaani umemvuta hata Mkapa ktk hii kitu..
Hivi kweli unaweza sema Mkapa ni afadhali kwa sababu tu alikiri kuboronga kwenye Ubinafsishaji wakati yeye bado ameshikilia mali za Taifa, hataki kuachia hata moja wala kukubali kama yeye na mkewe wametuingiza mjini.

Mkuu wangu Mkapa hakuboronga.. Mkapa alifanya alichokusudia kufanya, alijua fika nini matokeo ya kubinafsisha na ndio maana akafungua Ofisi yake Ikulu..A Pre meditated act! wakati mkuu Zitto wala hajui makosa yake, hesabu zake zote zinampa 2+2=22 akilini, wakati Mkapa ni mtunzi wa formula hiyo..

Kumsifia Mkapa, huu ndio UCCM damu ukisikia..haiwezekani kabisa kumlinganisha Zitto na Mkapa, na yeyote anayefikiria hivyo bila shaka atasema hakuna kiongozi Chadema anayeweza kusimama na Mkapa.. ndio lugha ya wapenzi wa Mafisadi.

...........when things are so obvious..........kuukubali ukweli ni big step towards ufumbuzi wa matatizo and hence maendeleo ya oneself na jamii pia........unless tuwe tunafichwa jambo ambalo Zitto analijua yeye na selected few.........

i mean Zitto hawezi kukiri kuchemka kwani kuna kitu anakijua wakati sie akina "kapuku" hatukijui.......kama si hivyo basi ni kuchemkax100.......
 
Nilikuwa sina muda wa kuandika chochote leo lakini imebidi. Eric, Katiba ya CHADEMA inamruhusu mtu yeyote, ili mradi anakidhi masharti, kugombea uongozi ndani ya chama kama alivyofanya Mh. Zitto. Tatizo kwako ni nini? Kama unaona kuna mapungufu ya kikatiba, anza mchakato wa kupeleka hoja binafsi kwenye "BUNGE" la CHADEMA ifanyiwe kazi. Hata hivyo wanaoamua nani anasitahiri kukiongoza chama kama mwenyekiti ni wapiga kura. Kwa nini unaelekeza shutuma zako zaidi kwa Mh.Zitto na si Wah. Wazee wa CHADEMA waliomshauri Zitto aondoe jina, au Mh. Mbowe?

Mwisho, mimi siamini kuwa kumtukana mtu ni ishara ya kuonyesha kuwa huyo mtu amekosa sana au wewe umekasikarika sana kwa kile alichokifanya.
 
...........when things are so obvious..........kuukubali ukweli ni big step towards ufumbuzi wa matatizo and hence maendeleo ya oneself na jamii pia........unless tuwe tunafichwa jambo ambalo Zitto analijua yeye na selected few.........

i mean Zitto hawezi kukiri kuchemka kwani kuna kitu anakijua wakati sie akina "kapuku" hatukijui.......kama si hivyo basi ni kuchemkax100.......
Mkuu kuna kitu waswahili husema unapopigwa changa la macho ni kwa sababu umetaka upigwe changa laa sivyo usingetazama..
Zitto ni kidume kwa maana kwamba ukifumaniwa kataa hadi kufa hata kama ulikuwa uchi wa mnyama.

Now, Tofauti ya kukataa zipo mbili ipo ile unayokana kitu cha wazi kabisa kwamba hujafanya kitendo hicho kabisa hali umefanya na nyanga zote ziko nje!..Ukiwafanya wengine hamnazo....huyu sii Zitto!
Zitto anakana kutenda dhambi ama kukubali kafumalniwa kwa sababu mwanamke alokuwa naye alimwambia hajaolewa.. hivyo huwezi kumfumania mtu anayetembea na mwanamke msela..Hakatai kitendo isipokuwa haoni uharamu wa kitendo hicho. Na ili afikie Zitto kukubali makosa anataka kuona ushahidi ambao ungemweka hatiani kama vile pete ya ndoa, picha za harusi na kadhalika..

Mimi na wewe tunafahamu fika sii lazima mwanamke au mume avae pete ya ndoa au zibandikwe picha za harusi ukutani ila ndoa ipo na cheti ni ushahidi tosha.. mwenzetu anarudi na kusema kuna mtu huuliza cheti cha ndoa kabla ya kujituma?..Ukweli hakuna na ndipom Zitto anapodai makosa yake yako wapi?..

Haya kuna wapambe hapa hawayaoni yote haya kwa mtazamo kama wetu ila kinachowaudhi zaidi ni kwa nini Zitto katembea na mwanamke adui yao kisiasa..ina maana anauza habari, na Zitto hayaoni hayo pia kuwa ni makosa kwani mapenzi na siasa ni vitu viwili tofauti..Na atabisha hadi jogoo la kesho huku akiendelea kula denda!..
Umenipata mkuu!

Binafsi namwona Zitto kafulia kisiasa pale tu alipoanza kusema mambo mengi ya chumbani, kutaja uzembe wa wenzake ktk nyumba zao na kadhalika kututhibitishia kwamba yeye ni kidume kwa yale aloyafanya... Hapo ndipo anapoharibu..Zitto anataka kugombea Uenyekiti akijua wazi kwamba hawezi kugombea urais kutokana na Umri wake! Kisha anajitoa halafu anazidi kupaka uongozi ambao kawasikiliza ushauri wao kinyume cha hisia zake mwenyewe, ndio maana alichanganyikiwa walipoanza kumrushia madongo..

Sababu kubwa ilomsukuma Zitto nina hakika ni kutopenda mwelekeo wa chama Chadema kwa sasa hivi. Mkuu nimemsoma vizuri Zitto na nadhani hii kazi ya kupima hoja na kuchambua kulingana na WATU na MAZINGIRA inanifaa sana kwani hadi sasa inaonyesha watu wengi hawafahamu Zitto ana malengo gani..nawajua wapambe wa Chadema na jinsi wanavyofiiria! Zitto si mwenzao tena na kajijengea maadui kiasi kwamba yeye mwenyewe haoni makosa yake.

Nina hakika kuna agenda za siri ndani ya Chadema ambazo hazimfurahishi na pengine hana wafuasi wa kutosha kupingana na hali hiyo. Ni sawa na kina Mwakyembe wanaopigana na Ufisadi ndani ya CCM.. Yeye kaamua kugombea uenyekiti kuwachefua zaidi hasa kina Mpaka Kieleweke!
 
Last edited:
- Ngoja tujaribu kuchambua hoja nzito za hii ishu, naona hapa Raia Mwema wamejaribu kutusaidia na hoja zaidi.

Respect.

FMEs!


Maneno hayo yameandikwa Raia Mwema na Kada wa CCM Benard Mukasa, mdogo wa damu wa Oscar Mukasa aliyewekewa pingamizi Biharamulo katika suala la uraia. FMES, mukasa hajawahi kuandika makala yoyote gazetini, vipi ameibukia leo kwenye mjadala kuhusu CHADEMA? Alichaondika mukasa ndio hicho hicho kimeandikwa na waandishi wengine kwenye makala Sauti Huru, Nipe Habari, Hoja, Mtanzania, Tazama Nk. Kuna nini kinaendelea huko chama chenu CCM baada ya Zitto kujitoa? Mbona bado mnaendeleza mjadala kwa nguvu kubwa?

......ndiyohiyo
 
Kaka kwa umri wako kukumbatia theory za kuhalalisha ugandamizaji kam huu unatutisha sana endapo utapewa uheshimiwa wenye makali ya dola



Unataka kusema kuwa wanaCHADEMA hawana uwezo wa kuchagua viongozi wao?





Kaka hata mimi naomba utokee muujiza hili lifanikiwe. Lakini swali kwa unavyomjua MTUHURU wako unadhani anaaminika hata kumpendekeza Zitto kuwa Katibu wake? Na kama kulikuwa na mpango huo iweje Slaa aache kuchukua fomu za kugombe umakamo?



Kwa hiyo kwako wewe unaona ni sawa kabisa kuacha CHADEMA iliyojaa wasiokuwa tayari kupractice demokrasi kuwaongoza watanzania kufanikisha demokrasia pana. Unataka kusema wale mafisadi wa kenya walivyowalaghai wakenya na dudu lao waliloliita NARC na kuja na madudu kama ANGLO LEASING Scandals ndio mfano wa kuigwa kwa watanzania?



Kama sio kujua kuwa mmoja wao angekosa ustaarabu wa kutumia siasa safi kufanya kampeni zake, uoga wa kutowashindanisha unatokea wapi. Yaani mnataka kusema yale mawazo ya wahafidhina wa CCM kuwa kumshindanisha JK na mtu mwengine kutavunja chama yana maniki. Ilikuwaje mkaanza kuwabeza wale kina mama na wazee wa watu walipoandamana kuwatisha wanaCCM wengine wenye nia ya kushindana na JK 2010? Au kwa sababu huyu ni mswahili Jakaya ni sawa lakini sio "mstaarabu" FREEMAN AIKAELI?



Makundi hayakuanza na Zitto ila yameanza na utamaduni wa kufukuzafukuza kila anayetofautiana na maslahi ya wachache yanayopewa jina la maslahi ya chama. Na usimsingizie Zitto kuwa aligombea kukuza ama kumaliza kundi jingine. Kama kitu alichokuwa anasisitiza kuwa kinatia umuhimu wa yeye kugombea ni kusamehe wale wote walionewa kwa kufukuzwa ama kusimamishwa uanachama mara baada ya kuonyesha tofauti zao na mwenyekiti wao. Na hili amelisema hata alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari. Sasa hii ya kumaliza kundi jingine yametka wapi. Usitie shaka Zitto hana roho ya korosho na wala utamaduni wa kuweka vinyongo na pia best wako Mnyika kamwe hawezi kugeuka adui wa Zitto kwani wametoka mbali. Kidudu mtu ambaye anapaswa kunyamzishwa ni mwengine ambaye sidhani kama ana umuhimu sana kwako.



Dogo umefikia lini umri wa Wazee wa Chama unakuja na mawazo mgando kama haya. Yaani U-CCM umewaathiri namna hii. Kama ninyi mliokulia katika enzo za siasa za ushindani mnafikiria hivi iweje leo muwashangae MAGOGO yaliyofubaa ya CCM?



Aliyechukua fomu na kujaza kuomba ridhaa ya wanachama wake kuwa kiongozi wao na waliotumia bisara zisizo na hakima kumshinikiza ajitoe kwa kuogopa athari za siasa chafu za KIJANA wao na baadae wafuasi wake kuendeleza kumwaga sumu dhidi ya mwenzao, ni yupi ambaye anataka kukisambaratisha CHAMA?


Maandiko ya Zitto kama majibu ya Tuhuma dhidi zake JF


Ina maana huyajui haya kama yanatendeka?



Ni wapi Zittoa amesema hawa ni wabaya wake. Na kama wakati Zitto anakubali ushauri wa wazee wao wanaingia mitandaoni na kwa waandishi wa magazeti kuendeleza propaganda zao kama walizotumi kumfrustrate Kaborou na Chacha Wangwe ulitaka Zitto awanyamazie. Ili iweje? Watu wazoee uzandiki wao hadi waamini?



Unataka kuniambia kuwa Zitto angeenda kukimbilia kwa hao wazee ambao nao wanakuja kudai kuwa Zitto ana tuhuma za kuhonga vijana kwa ushahidi wa sms na vijikaratasi? Sijui kuhusu mauaji lakini unataka kusema CHADEMA hakuna tuhuma za matumizi mabaya? Hayo ya uchaga ni nani kama sio wenyewe wanayoyatengenezea mazingira ya kuyahalalisha. Tatizo hizi natural born arrigances zinawafanya muwe reckless kiasi cha kufanya yaleyale ambayo maadui zenu wangependa muyafanye ili muwathibitishie mapungufu yanu.

Hivi iweje mtu anayetumia fedha za chama vibaya, akatumia ukabila katika kufanikisha malengo yake akawa na mapenzi na chama chake na yule ambaye anamwambia kuwa acha kutumia ukabila ndiye akawa hana mapenzi nacho. Kwani haya yameanza kusemwa lini? jee kuna suluhu iliyofanyika kichama? Na imekuwaje kuwa hata alliances za utetezi wa MBOWE na mashambulizi dhidi ya Zitto zikawa na picha ya udini? sitaki nije kwa undani wake hapa lakini kama unahitaji nishtue nitakushukie the whole chain...

Ni kama anatuambia yeye haipendi CHADEMA kihivyo! wakiendelea kumgusa ataua chama! Huu ni ubakaji wa chama na kuibua hofu za kibazazi. Ni kama anawaambia wanaCHADEMA wasimuuzi lasivyo atanyea kisima?! Hatuwezi kuendesha chama kwa hofu na kuwaza ni lini Zitto atakunya katika kisima. Kuna maswala mengi ya kuwaza katika mustakabali wa nchi zaidi ya kunya kwa Zitto.


Ulitaka abaki ili mtimize mpango wenu wa kumchoma visu?


Tangu lini kumpigia kampeni mtu kukageuka kuwa kuhujumu uchaguzi?



Tangu lini aliyeshinda uchaguzi akalalamika kuwa kadhulumiwa? angewasilishaje taarifa wakati wenye chama wameshinikiza hata majibu yasitolewe.




Yaani sasa mnataka hata watu wasihoji makosa ya kikatiba? Kazi kwelikweli.



Kama msingeendelea na propaganda zenu dhidi yake ni wazi mambo yangekuwa shwari sasa. Kosa ni lenu mliochukulia uamuzi wake wa kujitoa kama weakness na mkaendeleza mpango wenu wa kummaliza kisiasa...Na msipoangalia mtaadhirika maana FREEMAN na ZITTO walijuana siku nyingi na wamefanya mengi pamoja.....wakati ninyi mnaendela na ujinga wenu huku wenzenu wanaangalia jinsi gani ya kufanya kazi pamoja huko mbele kuendeleza libeneke (ofcourse kama mmoja wao hajaendeleza chuki zake)




Wenye jitihada ya kuiua CHADEMA ni wale walio tayari kufanya lolote ili mradi kulinda vyeo vyao na maslahi yao hadi kuwafanya wazee kutumia busara isiyo na hekima kumshawishi Zitto kujitoa......

omarilyas

Omar

Hivi una nafasi gani ndani ya CHADEMA? Au ni mwanachama? Maana naona uko mstari wa mbele kweli. Profesa Baregu na Dr Kitila wameshinda ujumbe wa Kamati kuu, wewe uligombea nafasi gani?

Zitto amewataja humu yeye mwenyewe kwamba Dr Slaa, Mrema, Mnyika na Halima Mdee ndio wabaya wake.

Lakini hayo yalishapita, wewe naona bado unaendeleza kuandika humu. Wewe ndio unaendelea kumchonganisha Zitto na Wenzake.


.......ndiyohiyo
 
Back
Top Bottom