Je wewe ni mmojawapo? USIHOFU! Hauko mwenyewe.

WOS asante sana. Mada yako inabidi wengine tuichukulie serious mno!!! Again thanks!!! Itabidi wengine tupate muda wa kuanza kupitia warddrobe zetu na vyombo ndani!!!! Maplastic yale tulipewa send off na kitchen party tuanze nayo kwanza maana hayana nafasi kabisa!!! Wife jamani pelekeni kijijini mkienda kuamkua huko (kwa wale ambao wanafanya tour ya walikotoka wao au wazazi wao). Our junks are treasures to others!!! Let us maintain this spirit!!!
 
we are talking about how to get the unneeded junk to those in need.

who cares to those junks of yours?.....kama unabisha mpe hata mtoto wa mjukuu wako kijijini nguo zako zilizochoka uone atavyokusemea kwa watu...

simple way ya kudispose hizo junk ni kupiga moto..maana sioni logic ya mie kuvaa nguo ya mtumba kisha ikiwa hainifai nimpe mtu mwingine...

usimtendee mwenzio usichopenda kutendewa weye...na mwenye kanzu mbili na ampatie asiyenayo moja...sio mwenye malapulapu ya nguo, gari, furnitures ndio ampatie asiyekuwa navyo...

hiyo sio kwa maadili ya dini zetu nyingi hasa hizi za wavamizi wa bara letu la africa.
 
UMENICHEKESHA SANA Msanii!
Ina maana nywele zimepitwa na wakati wakaendelea kuzifuga na kuzificha chini ya wigi au?? hebu fafanua.

hapa haongelewi mtu mwanaume wala mwanamke... cha msingi angalia kama linakugusa uungame usaidiwe.
subutuuuu nani aungame?? ameshaungama maamuma naamini atasaidiwa na wanaookota vitu chakavu kwa matumizi anuai.

Hivi mmeangalia mabehewa ya reli ya kati nyie? ni old timer kinoma na tetenasi ya kusuuza moyo.

mie nimekusanyakusanya vitabu vya bulicheka ili wajukuu zangu waje kusoma nikiwa sipo tena sidhani kama hapo nitakuwa nimefanya kosa kukumbatia ya kale.
 
WOS asante sana. Mada yako inabidi wengine tuichukulie serious mno!!! Again thanks!!! Itabidi wengine tupate muda wa kuanza kupitia warddrobe zetu na vyombo ndani!!!! Maplastic yale tulipewa send off na kitchen party tuanze nayo kwanza maana hayana nafasi kabisa!!! Wife jamani pelekeni kijijini mkienda kuamkua huko (kwa wale ambao wanafanya tour ya walikotoka wao au wazazi wao). Our junks are treasures to others!!! Let us maintain this spirit!!!
naona unamtafuta MAXenxe wewe.
hivi alioa lini vile?
 
WOS asante sana. Mada yako inabidi wengine tuichukulie serious mno!!! Again thanks!!! Itabidi wengine tupate muda wa kuanza kupitia warddrobe zetu na vyombo ndani!!!! Maplastic yale tulipewa send off na kitchen party tuanze nayo kwanza maana hayana nafasi kabisa!!! Wife jamani pelekeni kijijini mkienda kuamkua huko (kwa wale ambao wanafanya tour ya walikotoka wao au wazazi wao). Our junks are treasures to others!!! Let us maintain this spirit!!!

Mkuu,
Hili ni tatizo ambalo wengi hatupendi kuliongelea au hatuko aware kuwa ni tatizo.
Watu wanakusanya hadi nyumba zinajaa na kumaliza hewa safi! Nakumbuka familia moja tena watu wenye uwezo, wasomi , well exposed.Kitu cha kusikitisha ni kwamba kwenye guest room yao ndiko waligeuza "stoo" ya kuhifadhi kila kitu walichokuwa hawahitaji.Hebu fikiria wewe ni mgeni unaandaliwa mahali hapo ulale! Sidhani kama wakikukaribisha tena kwao utakubali.Ni afadhali ukajikalie hotelini. Si ajabu wangepeleka "Ushaghooo" au "rizavu" wangeombewa dua.
 
who cares to those junks of yours?.....kama unabisha mpe hata mtoto wa mjukuu wako kijijini nguo zako zilizochoka uone atavyokusemea kwa watu...

simple way ya kudispose hizo junk ni kupiga moto..maana sioni logic ya mie kuvaa nguo ya mtumba kisha ikiwa hainifai nimpe mtu mwingine...

usimtendee mwenzio usichopenda kutendewa weye...na mwenye kanzu mbili na ampatie asiyenayo moja...sio mwenye malapulapu ya nguo, gari, furnitures ndio ampatie asiyekuwa navyo...

hiyo sio kwa maadili ya dini zetu nyingi hasa hizi za wavamizi wa bara letu la africa.

Huo ni mtizamo mmojawapo pia.Asante.
sijui kama ulisoma posts za wengine waliosema kuwa junk kwako yaweza kuwa lulu kwa wengine.

Unaposema kuwa namna ya kudispose ni kupiga moto, unaweza kusemaje kwa watu wanaonunua mitumba hata ya nguo za ndani zilizotoka ulaya?
Ina maana kwa vile mimi ni mwafrika basi sistahili kumpa bure ndugu yangu kitu kizuri ambacho sikitumii???
 
Jina halitoshi kukuambia unayejaribu kumuelewesha ni mtu wa aina gani? nadhani wengine wamekumbuka jukwaa lao la dini wafanye ligi ya hoja zisizo miguu wala kichwa..achana naye
 
asante ndugu yangu..nilikuwa sijui hilo.
Basi tumsamehe bure maana kakatiza kiwanjani kwetu kwa kukosea njia.
 
Some peoples junk is other peoples treasure

Mkuu ni kweli baadhi ni hobby but wengi wao ni katabia tuu!
Hii mentality ya kusema kuwa ipo siku nitakihitaji ndio inayofanya nyumba kujaa mazagazaga yasiyotumika. Sipati picha kama na bongo tungekuwa tunalipia kutupa mazagazaga/vifaa tusivyovihitaji stoo zingefurika....!
 
kuna makundi yafuatayo ya junk nawahusika wakuu kwenye mabano:
1. Nguo mpya na kuukuu - ( wote - ila hasa wanawake)
2. Vifungashio( containers) vilivyokwisha - ( wanawake)
3. Magazeti na machapisho mbalimbali ( wanaume)
4.vyombo vya nyumbani - ( wanawake)
5. Vifaa na vitendea kazi - ( wanaume)
6. Nguo za watoto na toys - ( wanawake wakishirikiana na watoto)
7.mapambo yaliyoharibika - ( wanawake)
8.vifaa vibovu kama TV,Magari, bicycle,computer/laptops,pasi -( wanaume)

Inaonekana pia kuwa kufuatana na michango ya wanaume wengi, wanawake ndiyo hasa wana hiyo hulka ya kung'ang'ania vitu na kuona vibaya kuviachia.Mara nyingi, hivi ni vile vitu vya kawaida vya kila siku ambavyo hata ukiviondosha bado unaweza kuvi replace kirahisi.Wanawake nao wanakubali kuwa iko haja kuachilia vitu badala ya kuvijaza kwenye majumba.
 
TUSOGEEE HATUA NYINGINE:
Ili tusafishe Junk tunatakiwa tuwe na maandalizi kisaikolojia kwanza ili wakati wa zoezi, tusirudi kuangalia nyuma.
Tuendelee kuchangia nisihodhi mjadala.
 
Nimeambiwa pia kwamba JUNKIES zinakaribisha magonjwa kwani hata yale mafriji tunayonunua mitumbani yanavijisha gesi ambayo ni hatari kwa afya zetu.
 
Kitu kama hujakitumia kwa mwaka au zaidi je unakihitaji? Mfano mzuri ni makabrasha/makaratasi/documents, magazeti ya zamani.

Hizo ni rejea/references. Tunafisadishwa kwa sababu hatuhifadhi nyaraka/documents. Tujifunze kutunza kumbukumbu/archives.
 
majuzi nilipita home kwa mzee kuwasalimu. nikakuta bado wanatumia antiques i mean nilipoomba maji nilipewa kwenye glasi nilizokua nazo miaka ya sabini themanini. ni ngumu kweli kweli na wana uwezo wa kununua mpya. ila wagumu tu! hapa niulize swali kwamba hivi vyombo vya ndani vinapaswa vitumike kwa muda upi?
 
Una point Mkuu,kuna documents na documents...
Lakini je unahitaji kila karatasi? - kuanzia mialiko ya kwenda kwenye tamasha la siku ya ukimwi duniani - 1998, mwaliko wa warsha ya kuandaa sera ya maendeleo ya vijana sijui mwaka 1989,mwaliko wa kitchen party.... magazeti......vipeperushi, writing pads... all that ??
 
umenikuna sana hapo,
leo nikifika home kazi moja tu!

WOS
nadhani hapa hauongelei yale makabati ya vyombo, nguo n.k. ambayo wengi walipewa kama zawadi za harusi miaka ya sabini huko...
 
majuzi nilipita home kwa mzee kuwasalimu. nikakuta bado wanatumia antiques i mean nilipoomba maji nilipewa kwenye glasi nilizokua nazo miaka ya sabini themanini. ni ngumu kweli kweli na wana uwezo wa kununua mpya. ila wagumu tu! hapa niulize swali kwamba hivi vyombo vya ndani vinapaswa vitumike kwa muda upi?

Huo ni utamaduni wa kiaristokrati. Inaonekana mzee wako alikaa sana na wakoloni au alikuwa anawahusudu sana. Mpaka leo huko ughaibuni kuna maduka ya hizo antikwado na huwa wanazinunua sana na kuzitimia hasa wanapoalika wageni. Zinawafanya wajione watu fulani - mambo ya sinia za shaba na sahani za kichina zilizokuwa zinatumiwa na wanoboli na wafalme!
 
umenikuna sana hapo,
leo nikifika home kazi moja tu!

WOS
nadhani hapa hauongelei yale makabati ya vyombo, nguo n.k. ambayo wengi walipewa kama zawadi za harusi miaka ya sabini huko...

Msanii,
Hayo makabati kama yalikuwa ya Hardwood - tunza mwenzangu maana hardwood ni mali kuliko MDF hahahah.Unaweza kuja kuuza kwa bei mbaya kama antique.
Tunachoongelea hapa siyo kwenda na fasheni bali kuwa na vile unavyovihitaji tu na kuepuka mlundikano.
 
Back
Top Bottom