Je wewe ni mmojawapo? USIHOFU! Hauko mwenyewe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je wewe ni mmojawapo? USIHOFU! Hauko mwenyewe.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, May 7, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Jamani mmeshawahi kujiuliza ni kwa vipi naweza kuwa na vitu ninavyovihitaji tu badala ya kujaza kila aina ya unachoweza kuwa nacho – nguo, viatu, vitabu, makaratasi, michezo ya watoto, vyombo vya nyumbani, fenicha nzee,.vifaa vya kufanyia kazi –tool boxes, majembe,vifaa vya ujenzi, magari mabovu nk.
  Nimekutana na watu wengi tu wakiwa na tatizo hili na wengi wanakosa hata kufurahia mandhari ya nyumba zao kwa vile kuna msongamano wa vitu hivyo na wakati mwingine kuwa ni kero badala ya furaha. Kunazo njia mbalimbali za kupunguza tatizo hili.Lakini pa kuanzia ni kujiuliza yafuatayo:
  • Inakuwaje hadi unakusanya vitu ambavyo huvihitaji?
  • Kitu kama hujakitumia kwa mwaka au zaidi je unakihitaji? Mfano mzuri ni makabrasha/makaratasi/documents, magazeti ya zamani.
  • Unaponunua vitu ambavyo tayari ni second hand kumbuka kulikuwa na mtu alikuwa havihitaji.Je wewe ndiyo wa kusaidia kukusanya junk unless u really need it?
  • Kwa wale shopaholics wenye kupenda kununua nguo, viatu n.k. je unapojaza makabati na wakati mwingine wala huzivai? Huna mtu ambaye anahitaji ukampatia?
  • Kwa wenye watoto – je mwanao hawezi kuvaa nguo za aliyemtangulia kuzaliwa au ni mpaka ununue mpya hata kama zipo nzuri tu zenye kuweza kutumika bado?
  • Unajisikiaje pale ambapo wewe umelundika vitu ambavyo hutumii na wakati huohuo kuna watu maskini, wenye kuhitaji kama yatima, wazee, waathirika wa majanga nk.?
  Naombeni tuchangie
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Nyumbani kwangu kuna chupa za soda, madumu ya mafuta yalikwisha na containers za ice cream kila nikiomba watu wazitupe wife hudai kuna siku vitatusaidia nimesubiri hiyo siku naona uvumilivu umenishinda na hii ya WoS imenipa nguvu leo ni kutupa vyote.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  WOS
  unajua hata nguo za ndani pia zimo ktk fungu la junkies maana huko ulaya wakishazitumia na kuzichoka wanaexpert to afrika hahaha.
  Ila hii tabia ya watu kukusana mavitu ya zamani bila kutumia ni hulka na mara mwingine ni hoby.
  Serikalini napo ndo usiseme maana ukiangalia zile ndege zake utakuta nyingi zimeshakuwa chapter-closed kiwandani na hata behewa na vichwa vya treni ni vya adam na eva.
  Hata sisiem nayo ni mojawapo ya vitu vya kale ambavyo muda wake wa kutumika umeshaexpaya long kitambo
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Yaani! Nchi yetu ishakuwa dampo la vitu visivyohitajika hukoooo!

  Bado hatujafikia huko Mkuu.... tutatafuta solution tu wala uskonde..
  Hili la kukusanya containers za ice cream.. chupa mbalimbali... nimeliona sana kwenye familia nyingi.....
  hata vijijini utakuta hiyo tabia watu wanayo..je ni sentimental attachment na vitu fulani?
   
 5. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Vijijini wanaenda kununulia mafuta ya taa na kuhifadhi home....wengine yakisha kuwa mengi wanauza kuna watu hupita kwenye manyumba kununua kama makopo matupu na chupa za dasani..kama kuwa watu wanakunywa dasani home...mafuta ya kupikia tupu zake...mama anapata pesa ya mchicha soko la karibu...days goes on....ila kuwa na nguo usizo zihitaji kwa kweli ni sugu...uko nyumbani kuna mtu ana makabati ya nguo toka niko standard 7...mpaka sasa na kwangu na familia yeye anazo nguo zake za early 20s.Ukitaka kushauri kugawa hupati reception nzuri...sijui mama kama Wos amepata wapi hii ideal kwani wengi kama yeye ndio wanaongoza...kwa kuwa wao huenda na fashion...na ikiisha na nguo tena inakuwa haina thamani.
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani ni tabia zinazoletwa na insecurity flan aliyonayo mtu, mfano hayo makopo wanadhani kuna siku watayatumia kuhifadhia vitu. Lakini kwa ukweli kama tukipunguza hizi maisha yatakuwa simple sana.
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Buswelu,
  Ulivyosema ni kweli kabisa..kuna kukusanya kunakotokana na hitaji (1)
  halafu kuna kukusanya kama namna ya kurecycle na kupata chochote(2)

  ila kuna kukusanya tu hata kama huna haja nacho.....
  na inasemekana kuwa wanawake ndiyo wanaongoza kukusanya nguo(3)
  lakini ninajua pia kuna wanaume pia hufanya hivyohivyo.

  wanaume wanaweza wasikusanye nguo, wakakusanya magazeti ya zamani, magari mabovu, chuma chakavu etc.....
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mkuu wakati unajiandaa kuzitupa hizo chupa za soda nistue nianze kuvinjari maeneo ya huko shekhe.
  kuhusu vikopo vya ishkrimu ni conteina tosha kwa kuwekea sukari na takataka ndogo ndogo za maana. Ila kibaya ni pale ambapo wakulu wengi wa kibongo wanahifadhi masalia ya viatu vilivyoharibika ilihali wanajua hawatavivaa ndo maana siku hizi majalalani hatuoni tena viatu vikitupwa maana wenywe navyo wanahifadhi kumbukumbu. teh teh

  Ila najua kuna vibibi vinapenda sana kudunduliza pesa za ugoro kwenye vikopo vya redds au heinikeni. hiyo noma.

  WOS hebu nikumbushe, hivi hereni, na pete pete zako na vidani huwa unahifadhi ktk nini vile? (usikute umekata kikopo cha uhai nusu na kuvikusanyia humo) hahaha.
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  we mama wewe mbona unatutafuta sana sisi wanaume? haha. unajua magazeti ya zamani dili yanauzwa kilo moja buku unusu siku hizi.

  ninatilia shaka sana haya mawigi wanayovaa dada zetu maana kama nywele zao hazijapitwa na wakati walah wasingeyavaa. au vipi mkuu Burn?
   
 10. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  WoS umenisaidia sana. Maana nami ni mmojawapo. Nyumbani kwangu stoo imejaa hadi nimechukua bedroom moja kuwa stoo nyingine. Kwakweli siipendi hali ya nyumba nzima. Jicho halifurahii mandhari ya vyumbani.
  Kuna siku niliamka na azimio jipya kwamba 'leo ni usafi na kuondoa nisivyovihitaji'. Nikatoa vitu vyote nje ili niingize vile tu ninavyovihitaji. Ajabu ni kwamba vyote vilirudi ndani. Nilipoteza bure muda na nguvu zangu.
  Leo umenigusa, I'll do something. Asante sana.
   
 11. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  WOS,
  unanikumbisha ile drama mpya ya kule majuu THE CONFESSION OF SHOPPAHOLIC.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  hahaha Mkuu, nahifadhi kwenye kashubaka maalum ka vito!
  halafu kuna organisers maalum vya kuhifadhi na kupamba dressing table yako ikaonekana maridadi...haaa! hatujafikia huko Mkuu..tutajadili vyote hivi.
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  WOS..
  Umeleta mada nzuri na ukweli ndani yake. Binafsi, vitu vya zamani vimejaa ndani ya nyumba kuanzia pasi+feni zilizoharibika, viatu vimeisha au chanika,
  vyombo visivyotumika au masufuria yametoboka, nguo ndo usiseme ninazo hadi za sec(LOL) yaani ambazo haziivaliwi tena, madaftari ya shule tangia elimu ya msingi na mazaga zaga mengine nimebananisha stoo mpaka nahisi siku nitakuta nyoka!..
  Umenifanya nikumbuke hata kuvichoma moto au kutupa kabisa maana sivitumii hata kidogo zaidi nikiingia stoo nasikitika na kuahirisha siku ya kuvi-dispose..
  Asante itabidi nivishughulikie haraka..Ila sababu kubwa nadhani inakuwa unasema nitatupa kesho ngoja niweke hapa mara moja halafu muda unakwenda mtu unakuwa hukumbuki kabisa kudeal navyo. Pia kuna vitu vingine kama feni unaweza sema nitatengeneza, ila mpaka huyo fundi aje na kushughulikia mwaka unaweza kukatika hamna hatua iliyochukuliwa zaidi ya kurundika sehemu fulani nyumbani zaidi unanunua nyingine na kusahau kuishughulikia kama siyo kuitupa kabisa..
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Junius,
  si umeona matokeo ya kukusanyakusanya kila unachotamani -ni madeni na kukosa amani tu!Hii drama is a must see for all the shopaholics!They can also buy the book.
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hata ukiangalia mataulo ya watu wengi yameshabadilika asili yake baada ya kupigwa sana na jiki ili kutakatisha ukoko unaobanduka mwilini baada ya kuoga haha. yaani hata kandambili utakuta inatundu kubwa katikati lakini wadau wanasonga nyao tu kwenye vyoo vya shimo vya gesti bubu uswahilini bila kujali uchakavu wake.

  WOS
  hii topic haihusu UCHAKAVU kwenye vikao vya harusi?? maana ni uchakavu pia.
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  UMENICHEKESHA SANA Msanii!
  Ina maana nywele zimepitwa na wakati wakaendelea kuzifuga na kuzificha chini ya wigi au?? hebu fafanua.

  hapa haongelewi mtu mwanaume wala mwanamke... cha msingi angalia kama linakugusa uungame usaidiwe.
   
 17. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenikumbusha mimi nadhani hata hivyo vya harusi inabidi kuwe na kipimo, unakuta kwa mwezi unahudhuria vikao zaidi ya sita wengine hata huna uhusiano wowote kisa mdogo wake shemeji yake na work mate anaoa ili na wewe uonekane unazo unahudhuria. Kuna mengi juu ya hili la kuwa na vitu ili mradi tu uwe navyo wazee wengine wana mizigo kila baa ukiangalia uwezo wa kumridhisha mkewe tu hana, kung'an'gania tu ili mradi ajioneshe yeye kidume.
   
 18. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Some peoples junk is other peoples treasure
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  usikonde kabisa..tutaelezana vizuri namna ya kuondokana na junk.Usiondoke hapa.
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  La hasha ndugu.Topic inahusu kukusanya na kulundika vitu majumbani.
   
Loading...