Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Nilikuwa nawaza tu kwa sauti (just thinking aloud):
"Kuna kama kusua sua kwa zoezi hili la sensa ya watu na makazi kwenye baadhi ya maeneo. Kuna uwezekano baadhi ya kaya zisiweze kufikiwa ndani ya muda uliopangwa wa siku saba. Kuna kaya ambazo makarani wa sensa watazikuta zimefungwa kwani wanakaya watakuwa kwenye pilika pilika zao.
Jee tungalitumia mabalozi wa nyumba kumi au watendaji wetu wa mitaa/ vijiji hatungaliweza kweli kuzifikia kaya zote nchini ndani ya siku moja tu? Kwani hawa wangalishindwa kutumia hivyo vishikwambi baada ya mafunzo? Wangaliweza hata kujaza hizo takwimu manually kwenye jedwali lililoandaliwa ambazo baadaye zikaingizwa kwenye vishikwambi".
Hawa watendaji wa mitaa/ vijiji ni waajiriwa wa serikali na hivyo figisu figisu tunazozisikia zikitokea kwa baadhi ya makarani wa sensa hazingalitokea. Hawa wanazifahamu sana kaya zilizo kwenye maeneo yao.
Hata namba za simu za wakuu wa kaya wanazo na hivyo hizo takwimu za sensa wangaliweza kuzipata hata kwa njia ya simu tu.
Mojawapo ya kazi za watendaji hawa ni kutunza hizo takwimu kwenye maeneo yao na kuzi update mara kwa mara, na si kusubiri hadi baada ya miaka 10.