Makinda: Makarani wa Sensa 10 walifariki wakati wa utekelezaji wa zoezi la Sensa 2022

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,877
Kamisaa wa Sensa Spika mstaafu Anne Makinda amesema jumla ya Makarani wa Sensa 10 walikufa wakati wa utekelezaji wa zoezi la Sensa.

Source Star tv

=====

LICHA YA MAFANIKIO KATIKA SENSA, MAKARANI 10 WALIJIUA NA KUUAWA:

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Nchini, Anne Makinda amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyoonekana kwenye kazi ya Sensa la 2022 kuzifikia kaya, jumla ya makarani kumi walipoteza maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiua na kuuawa.

Makinda ametoa ripoti hiyo huko mkoani Manyara wakati alipokutana na Kamati ya Sensa mkoani hapo kwa minajili ya kupokea taarifa ya zoezi la Sensa ambapo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amesema kwamba zaidi ya kaya 300,000 ziliweza kufikiwa kwenye kazi hiyo.
 
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022, Anne Makinda amesema katika zoezi la Sensa mwaka huu jumla ya Makarani 10 wamepoteza maisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiua na kuuawa.

Makinda ametoa taarifa hiyo akiwa mkoani Manyara wakati alipokutana na Kamati ya Sensa Mkoa wa Manyara kwa lengo kupokea taarifa ya zoezi la Sensa.

"Mmoja wa Tabora alijinyonga mwenyewe na kuacha ujumbe, wengine walikufa kwa maradhi na mwingine aliuawa baada ya kupata vijisenti kidogo wenzie wakadhani ana mamilioni," ameeleza Makinda.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amesema Mkoa wa Manyara umefanikiwa kukamilisha zoezi la Sensa ambapo wamezifikia zaidi ya Kaya 300,000 ikiwa ni sawa na asilimia 126 ya lengo. #habarizote
8YFLZmOP.jpg
 
Kinachonichanganya awamu hii asilimia zote zinavuka 100 kwa kila jambo utasikia tumefanikisha kwa asilimia 100 na point
 
Kinachonichanganya awamu hii asilimia zote zinavuka 100 kwa kila jambo utasikia tumefanikisha kwa asilimia 100 na point
Inwezekana kabisa, wameenda wakiwa na makisio ya kaya zitakazohesabiwa. Ni sawa ma makusanyo ya Halmashauri kuvuka lengo, lazima itakuwa > 100%
 
Back
Top Bottom