Tuendelee kusubili kuhesabiwa na tutoe ushirikiano kwa makarani wa sensa watakapotufikia

Lucas mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
14,196
8,562
Ndugu zangu watanzania zoezi la Sensa limeanza Leo na litaendelea katika wiki yote hii, Najuwa Kuna ambao hatujabahatika kufikiwa na makarani wa Sensa katika siku ya leo, ndugu zangu naomba tutambue kuwa sote tutafikiwa na kuhesabiwa bila kuachwa Wala kurukwa kaya yoyote Ile

Ndugu zangu pamoja na kuwa Mimi siyo kiongozi Wala karani wa Sensa lakini Kama kijana na mpenda nchi yangu napenda kuwasihi nanyi ndugu zangu kuwa Tuwe na Subira na tuhakikishe kuwa tunakuwepo au anakuwepo mtu atakaye toa ushirikiano wa taarifa kwa karani wa Sensa atakapo pita

Tukumbuke kuwa zoezi hili limetumia mfumo mpya, kwa Mara ya kwanza makarani wamepewa vishikwambi,hivyo changamoto za hapa na pale haziwezi kukosekana,

Mimi moyo wangu umewiwa kumsaidia mh Rais kuwaelemisha watu juu ya umuhimu wa Sensa hasa majirani zangu ambao tulikaa kusubiri makarani, nimefanya hivyo hata kabla ya zoezi hili kuanza siku ya leo,

Tuhesabiwe wote ili Tumpe picha mh Rais wetu ya uhalisia wa Taifa analoliongoza, ili ajuwe afanye Nini na wapi, ajuwe Ni wapi apeleke huduma zaidi, Ni wapi asogeze huduma kupunguza adha kwa wananchi, ajuwe Hali yetu ya kiuchumi Sisi watanzania, ajuwe Ni vipi kundi fulani lipewe kipaombele

Sisi vijana ndio tunatakiwa Tuwe msitari wa mbele kuhamasisha watu wahesabiwe ili mh Rais wetu ajuwe Ni vipi atunge Sera na Sheria za kutusaidia sisi vijana wake, Sote tunatambua adhima na dhamira ya mh Rais wetu ya kutaka kujenga Taifa na uchumi utakao mgusa kila mtu, niwajibu wetu kumuonyesha Hali ya vipato vyetu watanzania ili ajuwe afanye Nini kutusaidia sisi

Natamanii hata ningepita Tanzania nzima kaya kwa kaya kuhamasisha watu wahesabiwe lakini uwezo wangu hauniluhusu kufanya hivyo, ndio maana natumia jukwaa hili kuwaomba watanzania wenzangu tuhesabiwe

Mimi Lucas Mwashambwa nipo Tayari Kuhesabiwa, Nawe pia mtanzania mwenzangu jiandae kuhesabiwa ili keki ya Taifa igawanywe kwa usawa na kwa makundi yote na kwa maeneo yote bila kuachwa mtu nyuma au pembeni ya meza ya Taifa
 
Upate uteuzi, na kama unao upande cheo zaidi. Ina maana sasa hivi keki ya taifa haigawanywi sawa kwakuwa idadi ya watu haifahamiki au? Ni maendeleo gani mmeshindwa kufanya kwakuwa hamjui idadi ya watu?
Uongozi unatoka kwa Mwenyezi Mungu ndugu yangu, lazima tumsemee mh Rais wetu, sisi tuliopo huku mitaani tunaona kazi kubwa inayofanywa na mh Rais ambapo kiukweli anahitaji kupewa ushirikiano na faraja, tusimkatishe tamaa, lakini pia Sensa inatoa taswila ya watu unaowaongoza kitakwimu kwa kila kundi na vipato vyao, hata ukitaka kupika na kupakua chakula Jambo la kuzingatia Ni idadi ya walaji waliopoo au mpo wangapi
 
Hili zoezi liende vizuri na kwa mda mfupi ingefaa wananchi kupitia serikali za mitaa wagawiwe form za maswali wazijaze mapema baada ya kujaza mabalozi wa nyumba kumi wazikusanye wazipeleke serikali ya mtaa maana changamoto ya kuwakuta watu wote nyumbani nayo ni kikwazo, mabalozi na wajumbe wao ndio ujua idadi halisi ya wakaazi wa eneo husika kupitia madaftari yao.

Then makarani wa sensa ndio waende ofisi za serikali za mtaa wazifeed SAsa data kwenye system, ni mabalozi wa nyumba kumi kwa kushirikiana na wajumbe wao pamoja na makarani wa sensa wangeweza fanya zoezi hili kwa ufanisi zaidi.
 
Uongozi unatoka kwa Mwenyezi Mungu ndugu yangu, lazima tumsemee mh Rais wetu, sisi tuliopo huku mitaani tunaona kazi kubwa inayofanywa na mh Rais ambapo kiukweli anahitaji kupewa ushirikiano na faraja, tusimkatishe tamaa, lakini pia Sensa inatoa taswila ya watu unaowaongoza kitakwimu kwa kila kundi na vipato vyao, hata ukitaka kupika na kupakua chakula Jambo la kuzingatia Ni idadi ya walaji waliopoo au mpo wangapi

Mungu ndiye anayeratibu wizi wa kura ili CCM wakae madarakani? Huu ujinga bado kuna watu mnawalisha? Mpaka sasa maendeleo yako duni ni kwakuwa hamjajua idadi ya watu?
 
Mungu ndiye anayeratibu wizi wa kura ili CCM wakae madarakani? Huu ujinga bado kuna watu mnawalisha? Mpaka sasa maendeleo yako duni ni kwakuwa hamjajua idadi ya watu?
Tumepiga hatua kubwa sana kimaendeleo Kama nchi na bado safari yetu ya kimaendeleo inaendelea mbele na haiji kufika mwisho, kwa kuwa matatizo na kero za kuzifanyia kazi zitakuwa zinabadilika kulingana na wakati kwa kuwa hata watu tunaendelea kuongezeka idadi yetu siku Hadi siku

CCM imebeba Imani na matumaini makubwa ya watanzania ndio maana unaona ukiendelea kuaminiwa kila uchaguzi, hii Ni kutokanaa na kwamba CCM inabeba ajenda na Sera zinazogusa maisha ya watu,

Inafanya kazi na kuweka vipaombele vinavyo gusa maisha ya watu wengi, pia inajenga uchumi unaogusa maisha ya watu wengi bila kumwacha mtu nyuma
 
Nikweli ni week nzima ila maandalizi ni hafifu, manpower ni ndogo sana,ukilinganisha na kazi yenyewe
 
Tuwe wavumilivi naamini sote tutakuwa tumeshafikiwa ndani ya wiki hii
Kwa manpower iliyopo hasa mijini,ukiwasikiliza wahusika wenyewe Makarani labda wapike data tu,ila Kwa kufuata utaratibu ni ngumu wakatoboa Kwa siku Saba,labda waache form majumbani watu wajaze taarifa zao wenyewe
 
Naamini
Kwa manpower iliyopo hasa mijini,ukiwasikiliza wahusika wenyewe Makarani labda wapike data tu,ila Kwa kufuata utaratibu ni ngumu wakatoboa Kwa siku Saba,labda waache form majumbani watu wajaze taarifa zao wenyewe
Naamini kinachohitajika Ni taarifa zetu wote watanzania ,hivyo naamini serikali inafuatilia kwa ukaribu zoezi Hili na ikiona watu wengi bado hawajafikiwa katika muda husika Ni Imani yangu na Iman kwa mh Rais wetu kuwa ataongeza muda ili watu wote tufikiwe na zoezi litoe matunda tunayotarajia ya bila mtu kubaki bila kuhesabiwa
 
Tuwe wavumilivi naamini sote tutakuwa tumeshafikiwa ndani ya wiki hii
P
 
P
 
P
Ngoja tuangalie mpaka kesho mkuu wangu na Tathimini ya serikali juu ya zoezi hili na asilimia zitakazokuwa zimefikiwa, Naamini serikali yetu Ni sikivu na inaweza ikaongeza siku endapo itaona inafaa kufanya hivyo
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom