Je, wanaume tuwaulize vipi hili swali? "Ulikuwa wapi"

Je, wanaume tuwaulize vipi hili swali? "Ulikuwa wapi"

babu ukishapiga supu asubuhi na chapati ndukiiiii mpaka usiku

Yani bibi yako akitaka nimchefue basi aniulize hili swali "Ulikuwa wapi". Kawaida mi huwa namtaarifu mapema kama nitahisi nachelewa.
 
Suala la mwanamke kupenda sana hela huwa linanishangaza.

kama ujaoa
usioe ambaye hajishughulishi

why nasema hivyo
HAJUI UCHUNGU WA KUTAFUTA ELA NDO MAANA ATATAKA AZICHEZEE CHEZEEE

ila pia usioe gumegume lenye mlengo wa kujenga kwao na familia yake huko badala ya kufocus kwenye familia yenu na future ya watoto wenu.
unaoa mwanamke ana taka kuwaringishia wenzie kanzini new handbags na less wigi kila kukicha ???
unaoa mwanamke kila kitu kabla ya kufanya lazima awaulize mashosti zake?????

kuwa makini....katika kuoa
 
Ntajaribu kujibu kama vile ndo mimi sasa, sijui kama itafanya kazi kwa wote........!



Nimeambiwa katika maswali mwanaume anayochukizwa nalo ni hili "ulikuwa wapi" actually ukichelewa na wakati najua ratiba yako lazima nikuulize ulikuwa wapi hili swali tuliwekeje ili lisiwaudhi.

{Binafsi sina tatizo na hili swali kabisaaa, maana nikiulizwa nikalijibu ndo huwa nakuwa huru zaidi kama nimetokea kusiko, lakini nisipoulizwa nakuwa na wasi wasi zaidi kwani sijui unajua kiasi gani au unawazaje kuhusu kuchelewa kwangu, hata hivyo ni vema kuwa na desturi ya kuhadithiana siku ya kila mmoja wenu ilivyokuwa hapo ndo utakuwa unauliza kwa akili upate unachokitafuta}


Lakini pia siku hizi wanaume wengi huwa na vitambi bila sababu za msingi ni njia ipi ya kumwambia mume/mpenzi kwamba afanye mazoezi kupunguza mwili na uzito?

{HAPA SIJUI NIAMBIWE VIP KWA KWELI..., labda kama utani vile, mfano..., 'mmmh unavonenepa siku hizi, ntakushindwa jaman' kuwa makini na mood hapo kabla hujaanza huo utani}



Pia mavazi nyinyi wanaume inakua rahisi sana kutuambia usivae suruali au kimini au nguo ambayo hampendi ila nyinyi kuambiwa mnaona kama ni jambo zito sana.


{ni ngumu sana kumwambia mtu kuhusu mavazi kama hushiriki kwenye ununuzi wake, uchaguzi wake n.k, wewe ndo uonyeshe kwa mfano ungependa atokelezee vip? taratibu ataingia kwenye formula tu}


Je, ni njia ipi ya kufuata ili isilete mtafaruku katika swala la kumbadilisha mume/mpenzi avae kitu unachokipenda na unachoona kitampendeza? Tujulishane juu ya hili.


 
Mimi mwanamke akiniuliza eti "Ulikuwa wapi? huwa namuuliza pia "Kama wapi?
 
Mmmmmmmhhhhh me nadhani kukiwa na "consensus ad idem" katika mahusiano hakutakuwa na makumbano kama hayo hata iwe iweje
 
twende kwenye hali halisi UMERUDI SAA 6 nisiulize chochote kweli?

Kiukweli hata mi kati ya maswali ninayo yachukia na ya mfumo huo.
Mara mia kenda uanze kwanza kwa kunipa pole, alafu uniulize mbona umechelewa.
Ila ulikua wapi, na nani, unafanya nini muda wote.??? Hapa utaona vumbi tu, hata kama mvua imenyesha.
 
mambo mengine yanamalizwa kimasihara ingawa ndio unakuwa ukweli unahitajika. Wanawake wengi huuliza hayo maswali huku wakiwa na sauti fulani ya kukereka au kwa kupandisha sauti zao, hicho ndio kikubwa kinachotukera sisi wanaume. Uliza kwa utaratibu na upole, utapewa jibu.

Mfano: "Mume wangu mwenzako mi tangu saa hizo nimejiweka tu hapa najua mda wako wa kurudi ni saa fulani, mda umefika nimeona mwenzangu kimya basi sina raha wala amani, vipi ulikutwa na maswahibu gani?". Utaona utakavyojibiwa. Uliza hivyo au mfano wa hivyo utaona matokeo yake.

Hayatakagi hata kuelewa sasa, pamoja na kufundwa kote huko yatokako. Agrrrrrri
 
Kitu ambacho wamekikosa wanawake wa karne hii ni hekima ndani ya nyumba...na ndio sababu kubwa inayopelekea nyumba ionekane kama jahanamu kwa kukosa amani....kwa kawaida mtu hukitunza kile anachokipenda na ndio maana wanaume tunahangaika kwa kadri ya uwezo wetu ili tu tuweze kuwatunza wake zetu....na katika harakati hizo tunajikuta tunatumia muda mwingi sana mapaka ule wa ziada ambao tungetakiwa tuwe na familia zetu...lakini tunayafanya yote haya kwa ajili yao...jambo la busara sio kumkemea anapochelewa kurudi bali kumpokea kwa upole kwani hujui ni masahibu gani mwenzio amekumbana nayo kwa siku hiyo..sasa unapomkemea ni sawa na kumwaga petrol kwenye moto...Wakati mwingine busara ndogo zinaweza kutuepusha na mambo makubwa sana na ya hatari...wanawake wajitahidi kuzitumia ndimi zao katika hali ya kujenga na sio kubomoa....

Faza hawa wa siku hizi, mwalimu wao "Matonya"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom