Nimeambiwa katika maswali mwanaume anayochukizwa nalo ni hili "ulikuwa wapi" actually ukichelewa na wakati najua ratiba yako lazima nikuulize ulikuwa wapi hili swali tuliwekeje ili lisiwaudhi.
Kwanza kabisa "ulikuwa wapi" siyo swali bali ni tuhuma. Ukiangalia hata wewe mwenyewe hukuweka alama ya kuuliza ili liwe swali. Kwa maana nyingine, unataka maneno mbadala ya kuelekeza tuhuma zako kwake kwa kuchelewa. Hapo bado mwanaume atataka kujitetea dhidi ya tuhuma zako. Lakini kimsingi mara nyingi mwanamke huwa anataka kuondelewa mashaka (reassurance) pale mwanaume wake anapochelewa kurudi nyumbani. Anakuwa na mashaka. Ukitaka kuondolewa mashaka hayo usituhumu bali mwulize.
Kunaweza kuwa na sababu za msingi ambazo zinakufanya ujisikie insecure anapochelewa na unastahili kuondelewa mashaka. Hata hivyo, unachotaka ni kuondolewa mashaka juu ya mapenzi yake kwako. Kwa sababu hiyo basi inakubidi umwulize kwa maneno ambayo yatamfanya akujibu badala ya kujitetea.
Mwandishi Michelle Davis katika kitabu chake cha
THE SEX-STARVED WIFE: WHAT TO DO WHEN HE'S LOST DESIRE, anasema badala ya kumtuhumu kwa kusema "ulikuwa wapi" unaweza kumwuliza hivi: "Najua labda kulikuwa hakuna chochote, lakini unapochelewa kufika nyumbani kutoka kazini huwa kunaniogopesha sana. Wakati mwingine mpaka naanza kufikiria labda umepitia kwa mchepuko. Nachukia sana kuwa feelings kama hizi, kwa hiyo, tafadhali nisaidie katika hili. Niambie kwa nini umechelewa?"
Mwandishi anadai kuwa swali hili litampa moyo mumeo kukupa mapenzi unayostahili. Lakini kwa upande mwingine nakubaliana na
FaizaFoxy hapo juu. Baba yangu alikuwa mchelewaji sana lakini sikuwahi kusikia hata siku moja mama akimwuliza kwa nini amechelewa. Never! Anamfungulia, anamsalimia, anamkaribisha, mara hao wanaanza kupiga story, sie tunaishia kwenye usingizi tukiamka asubuhi tunakuta chupa tupu za bia mezani.
Lakini pia siku hizi wanaume wengi huwa na vitambi bila sababu za msingi ni njia ipi ya kumwambia mume/mpenzi kwamba afanye mazoezi kupunguza mwili na uzito?
Kwanza kabisa huwezi kumhamasisha mtu mwingine apunguze unene. Watu wanaji-motivate wenyewe bana. Kama mtu hayuko tayari kupunguza unene hatafanya jitihada zozote hata kama ukimshauri. Na kama ni mumeo ukimshauri wala hatakusikiliza. Katika kupunguza unene, self-motivation is really important.
Na jinsi wanaume wengi walivyo stubborn anaweza kukuambia hayuko tayari kupunguza unene. Kumbuka kuwa wanaume wengi huwa wanajiona siyo overweight na tofauti na wanawake hawatachukua hatua za kupunguza unene. Kama yeye mwenyewe anaona kuwa anahitaji kupunguza unene unaweza tuu kumsadia kwa kutengeneza mazingira mazuri na kumpa msaada wa kufanya hivyo.
Pili onyesha mfano kwa vitendo. Kwa kuwa wewe ni mwembamba haina maana kuwa huna mafuta ya ziada mwilini. Kwa hiyo, madhumuni ya kufanya mazoezi yasiwe tuu kwa ajili ya kupunguza weight au unene, bali kuboresha afya zenu kwa ujumla. Akienda jogging na nenda nae. Akipunguza kunywa au kula vyakula vya mafuta na wewe punguza.
Kuna utafiti unapingana na hili kwa kudai kuwa
Want your husband to lose a few pounds? The solution is to nag him about it. Lakini ukiangalia comments za watu kwenye hiyo makala hazikubaliani na findings za huo utafiti. Muhimu kukumbuka kuwa kwa kuwa mtu amekuwa mnene hakumfanyi kuwa mtu mbaya. Kama alivyosema mchangiaji mmoja kwenye hiyo makala "nagging is a verbal abuse" and therefore you should not condone verbally abusing a spouse simply because they are fat.
Pia mavazi nyinyi wanaume inakua rahisi sana kutuambia usivae suruali au kimini au nguo ambayo hampendi ila nyinyi kuambiwa mnaona kama ni jambo zito sana. Je, ni njia ipi ya kufuata ili isilete mtafaruku katika swala la kumbadilisha mume/mpenzi avae kitu unachokipenda na unachoona kitampendeza?
Kwanza, nakushauri ukasome kitabu cha
MEN ARE FROM MARS, WOMEN ARE FROM VENUS. Kuna sehemu mwandishi anasema kuwa mwanaume huwa anamwoa mwanamke akitegemea kuwa hatabadilika na mwanamke huwa anaolewa na mwanaume akitegemea kuwa atambadilisha huyo mwanaume ili awe kama anavyotaka yeye. Sasa kasheshe linakuja pale mwanamke anapobadilika au mwanamke anapojaribu kubadilisha mwanaume. Hapo ndo ugonvi unaanza.
Kama ulishindwa kubadilisha uvaaji wake kabla ya kuoana basi usitarajie kufanya hivyo baada ya kuoana. Kama ulikuwa hupendi jinsi anavyovaa, then kulikuwa hakuna haja ya kukubali kuolewa nae. Ungetafuta ambaye anavaa kama unavyotaka wewe.
Having said that tofauti na wanawake, kwa wanaume wengi shopping na style are not on their list. Kuna baadhi ya wanawake wanapoteza makusudi au wanaziwekea madoa nguo ambazo waume zao wanapenda kuzivaa kila mara lakini wao (wanawake) hawazipendi. Never ever try to do that yo your man maana anaweza kukupotezea na wewe pia.
Tena ukute ni jezi ya timu yake kipenzi ya Man Utd ni original (siyo ya kichina) katumiwa na jamaa yake toka moja kwa moja Manchester utakiona. Hata kama timu yake ni Porto iliyotundikwa bao sita jana, bado ataendelea kuipenda mpaka kufa. (mwulize
everlenk au
BelindaJacob). Wengine tunaamini football is a beautiful game so what whatever which goes with it is also beautiful.
Wanaume wengi wanapendelea kuvaa nguo ambazo make them to feel comfortable na siyo kuonekana wamependeza. Kwa hiyo uzimlazimishe kuvaa nguo ambayo hataji-feel comfortable in it. Wengine wana self-image which identifies them who they are. Mfano, kama mumeo ni Mwanachadema kuna uwezekano akawa mara nyingi anavaa magwanda.
Labda njia mojawapo ya kukwepa mtarufuku ni siyo kumbadilisha anavyovaa, bali kumpa compliment. Hata sie wanaume baadhi yetu tunapowaambia usivae hii vaa ile, tunawaambia hivyo in a complimentary way. Kwamba hili gauni hali-match vizuri na viatu hivi, ila lile lingine lina-match fresh kweli. Hatusemi kuwa gauni ni baya au hatulitaki bali simply hali-match.
Pia kulingana na ucheshi wenu, you can be cocky and funny sometimes. Mfano, unaweza kuvaa gauni lako ukaja mbele yangu na kuniuliza "How do I look in it?". Nakujibu hebu linyanyue juu nione umevaa pichu ipi. Unanyanyua nakwambia hilo gauni hali-match na pichu uliyovaa. Wakati unafikiria kichwani kama ukabadilishe pichu nakuambia the pichu looks sexy on you, ila kama ungevaa na lile gani ulilovaa siku ile, I promise you darling nitahakikisha tunarudi mapeeeema so I can have plenty of time to undress you with my teeth.