Uko wapi? Niko bar,
Uko na nani? Pumbaf sanaaaa
Sijawahi liuliza Gozi langu "ulikuwa wapi" hata siku moja. Nnamuamini na nnajiamini, si leo wala jana, toka ujanani.
Siioni sababu ya kumuuliza swali hilo, kwani limekaa kishari.
Vijana jiepusheni na maswali ya kiugomvi-ugomvi kwa waume zenu.
Usiwe unauliza
Usiniulize hovyo wakati wajua nilikuwa job....
Kitu ambacho wamekikosa wanawake wa karne hii ni hekima ndani ya nyumba...na ndio sababu kubwa inayopelekea nyumba ionekane kama jahanamu kwa kukosa amani....kwa kawaida mtu hukitunza kile anachokipenda na ndio maana wanaume tunahangaika kwa kadri ya uwezo wetu ili tu tuweze kuwatunza wake zetu....na katika harakati hizo tunajikuta tunatumia muda mwingi sana mapaka ule wa ziada ambao tungetakiwa tuwe na familia zetu...lakini tunayafanya yote haya kwa ajili yao...jambo la busara sio kumkemea anapochelewa kurudi bali kumpokea kwa upole kwani hujui ni masahibu gani mwenzio amekumbana nayo kwa siku hiyo..sasa unapomkemea ni sawa na kumwaga petrol kwenye moto...Wakati mwingine busara ndogo zinaweza kutuepusha na mambo makubwa sana na ya hatari...wanawake wajitahidi kuzitumia ndimi zao katika hali ya kujenga na sio kubomoa....
Gwali kuguu gwe ny'ambala gwangu gwa nalori, ngoganile figo. Hiyo ndiyo lugha nzuri ya kumuuliza mumeo
hapana kabanga
najua kabisa job unatoka saa 11
foleni za hapa na pale najua saa 1 upo home
sasa wewe unaingia saa 5 like eer day
Kuna kuangalia mpira, madili ya hapa na pale mbali na kazini.
ngoja nikupe airtime
Haya nimekujibu.
nolaka totire muresi
Ndiyo nini hiki mkuu mbona lugha mbaya, kwa hili ndiyo maana mumeo anakuwa mkali
nirushie tu vocha ya airtel
ULIKUWA WAPI limekaa kisharishari kidogo..nadhani ni bora kumuuliza mtu "mbona leo umechelewa?"..zen maswali mengine yanaweza kuja kulingana na majibu yake..
asante dada faiza kwa nini unamuita shem GOZI
gozi ndo jina lake?
Hapana, si jina lake, hata yeye ananiita mimi Gozi lake. Kisa kirefu kidogo, nilishawahi kuulizwa hili swali humu humu JF na nikalijibu, muda sasa. Kwa ufupi:
Jozi = Kiswahili fasaha ni "pair", hilo neno linatokana na Kiarabu likiwa na maana hiyo-hiyo. Mkioana kiarabu husema mmekuwa "pair" "Jozi". Na harusi huitwa Zawaj (to become into a pair).
Nilibahatika kutembelea Egypt na Gozi langu siku za mwanzo mwanzo baada ya kuolewa, na tour guide wetu kila akiongea anatu "refer" kama Gozi (accent ya Kiarabu cha Egypt Jozi wanatamka "Gozi"), basi ndipo nikashika hiyo "Gozi" ya ki Egypt.
He is my "Gozi" and I am her "Gozi", we are a pair.
Kuoana ni kuwa "jozi" hata kwa Kiswahili. Hata viatu kama havioani haviwi jozi.
We find it funy and to the point.
okey ray leee
ukamuuliza leo mbona umechelewa
kawa siku 4 mfulilizo kitafata nini?