Je, wakati (time) una mwisho au ulianza lini?

Je, wakati (time) una mwisho au ulianza lini?

Ni wakati gani unausemea, kama nimuda ambao tunautumia kwa kujua muda kwa masaa; ulianza tangu dunia ilipo umbwa tu na kupewa sifa ya usiku na mchana. Na kama ni kuhusu mwelekeo wako wa maisha, muda ulianza ulipo zaliwa na utapata kikomo kwako wewe pindi utakapo kufa. Na ndomana wanasema "katika maisha yako chunga sana muda, maana muda ukiupoteza utakufanya ujute baadae kama ukiutumia vibaya."
 
“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” — Mwanzo 1:1
  • Mwanzo — Muda (Time)
  • Mbingu — Nafasi (Space)
  • Nchi — Maada (Matter)
Kwa maneno machache, mstari huu unaonyesha mwanzo wa vipengele vitatu vya msingi vya ulimwengu: muda, nafasi na maada. Vipengele hivi vinategemeana; maada haiwezi kuwepo bila nafasi, na matukio katika ulimwengu hayawezi kueleweka bila muda.

Kwa hiyo, Muumba wa muda, nafasi na maada hawezi kuwa amefungwa ndani ya vitu alivyoviumba. Ni lazima awe nje ya muda, asiyewekewa mipaka na nafasi, na asiyeumbwa kwa maada.

Hapo ndipo tunapomwona Mungu kama Muumba wa vyote, lakini Yeye mwenyewe hakuumbwa (Uncreated creator, uncaused Causer etc).
 
Back
Top Bottom