Teh teh kwa hiyo ni sahihi kabisa tuamini huu uarabu wako kama maana ya Afrika na sio Kilatini ama Kigiriki hapo juu ?
Huwezi kuutenganisha Uarabu Afrika.
Asili na fasili ya Uarabu ni Afrika na Asia Uarabu ulikwenda tu.
Uarabu ni nini?
Neno Arabia maana yake ni (caravan) msafara, Waarabu ni wasafiri na Uarabu ni lugha, misafara ya kibiashara ilikuwa ikijumuisha watu wa kutoka sehemu mbali mbali za hili bara ambalo sasa linajulikana kama Afrika lakini kabla likijulikana kwa vipande vipande na si kikontinenti kama ilivyo sasa. Haya makontinenti kihistoria ni mambo ya hivi karibuni tu.
Maarufu katika hivyo vipande ni Sheba, Habash, Sudan (Kurma, sehemu ya falme za Kush) Nubi/Nuba, Nri, Mali, Ghana, Senar, Saloum, Zimbabwe, Sahel, Magharibi, Barbara, Fulani, Sofala, Zenj, Kilwa, na nyingine nyingi ambazo sikuzitaja kwa sasa.
Misafara (Arabiya) ilipita kote huko na kuungana na msafara mmoja wapo unapofika unapokwenda hubaki na mingine kuunga na kuendelea, hakuna wakati misafara iliisha.
Na lugha kubwa iliyotumika katika hiyo misafara ni Kiarabu, kwa maana lugha ya msafara (Arabiya).
Hapo ndipo unapopata maana ya Uarabu.
Uarabu ni Uafrika to the dot.
Achana na historia za kujazwa ujinga na wazungu. By the way, hayo mataifa na miji niliyokuandikia hapo juu iliteketezwa kwa namna moja au nyingine na wazungu kwa makusudi kabisa.
Utakuta misafara iliyotoka Kaskazini, kwa asilimia nyingi ni jangwa na hakuna mapori au vichaka vya kujificha, na kuingia (au kutoka) Kusini ya Sahara basi iliitwa misafara inayoenda Afrikiya (kuliko jificha) kwa ajili ya mapori manene ambayo ukiingia mita moja tu huonekani. Ndiyo maana na jina Afrika lilipotokea.
Source, mimi mwenyewe.
Majina ya miji na falme niliyoyataja juu hapo, unaweza kuyapata uki Google.
Maana ya neno Ifrit / Afrit unaweza ku Google ukaipata.
Tarikh (historia) ya Afrika ni ndefu na pana kuliko ya kwingineko kokote duniani. Na nnakuhakikishia huwezi kuipata kiukamilifu ukiisoma kutoka kwa wazungu pekee. Kuna mbadala.