Je viongozi wengi kuwaponda vijana ni mbinu ya kuwanyong'onyeza ili waendelee kula keki ya taifa peke yao?

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,590
15,385
Kumponda kijana, kumvunja moyo na kumtamkia kauli za kumkatia tamaa ni kushambulia uti wa mgongo wa taifa.

China imepromote vijana, hadi leo ndio nchi inayoongoza kuwa na malaki ya mabilionea under 30.

Tukumbuke wakina Nyerere, Salim etc walianza kung'aa wakiwa vijana.

Kumeibuka kundi la wazee na watu wa makamo wenye hofu za maisha na kustaafu. Watu hawa wamekuwa mwiba mkali kwa vijana. Kila siku ni kuwaponda na kuwavunja moyo ili waonekane hawafai.

Je hili vuguvugu ni matokeo ya hofu za maisha za watu wazima au ni mbinu ya kuwapa motisha hasi vijana ili wajitutumie?

Nini maoni yako.
 
Back
Top Bottom