Viongozi acheni tabia ya kila kukicha kusimanga vijana

Bwana Bima

JF-Expert Member
Jul 29, 2014
418
885
Huu utaratibu wa mawaziri,manaibu waziri na viongozi wengine kuwasimanga vijana kwamba ni watumia pombe unapaswa kukemewa sana. Naongea hivi nikiwa na sababu za msingi kadhaa;

1) Si kweli kwamba vijana wote ambao maisha yamewachapa na kuangukia kwenye pombe ni wavivu kufanya kazi. Wapo wachapa kazi wanapata pesa zao so sio dhambi kutumia.

2) Hao mawaziri ndio wanapaswa kujihoji hasa kwa nafasi wanazopewa je kuna mifumo sahihi ambayo wanaumiza kichwa kuitengeneza ili kuzalisha ajira za kutosha? Kila siku tunasikia kuhusu ufisadi mkubwa unaopigwa na hao hao vigogo unategemea kutapatikana Maendeleo ambayo yatachagiza kupatikana fursa za kutosha kwa ajili ya vijana?

3) Majuzi zilitanganzwa nafasi kadhaa kuwawezesha vijana kupitia kilimo. Mpaka sasa haijulikani hao vijana walipatikana vipi kiasi cha watu wengi kudai ni vijana watoto wa vigogo na UVCCM.

4) Kila siku teuzi zimekua ni wazee tu, kupata ajira mpaka connection au rushwa. Happ sijaongelea mifumo ya elimu nchini ambayo mwanafunzi akimaliza hana anachoweza kufanya. Mbaya zaidi nafasi za kujitolea nowadays nayo ni connection ndo unapata je utapata wap ujuzi wa kukusaidia kwa namna hio?

PLEASE MAWAZIRI NA VIONGOZI WOTE MTUACHE KAMA TULIVYO. ENDELEENI KULA MEMA YA NCHI SISI TUPAMBANE NA HALI ZETU. MAMBO YA KUTUSIMANGA TAFADHALI TUACHENI!

Screenshot_20230922-132530.png
 
Hasa hizo pombe wanakunwa bure, si ndo kazi wanafanya wanapata Ela ya kupoza Koo.
 
Inabidi vijana muwaonyeshe viongozi kwamba nyie sio watu wa mchezomchezo, ingieni barabarani kwa umoja wenu kupinga ufisadi wa ccm, baada ya hapo hutomsikia mwanasiasa yeyote anaponda vijana
 
Inabidi vijana muwaonyeshe viongozi kwamba nyie sio watu wa mchezomchezo, ingieni barabarani kwa umoja wenu kupinga ufisadi wa ccm, baada ya hapo hutomsikia mwanasiasa yeyote anaponda vijana
😂😂😂Tz hatuyawez hayo. Ingekua kenya sawa.
 
Inabidi vijana muwaonyeshe viongozi kwamba nyie sio watu wa mchezomchezo, ingieni barabarani kwa umoja wenu kupinga ufisadi wa ccm, baada ya hapo hutomsikia mwanasiasa yeyote anaponda vijana
Hii Tanzania ndugu sio kwa wenzetu wanaruhusiwa maandamano ya amani, chezea lupango wewe.
 
Ndio maana wanasiasa wanawananga vijana, kuna mbunge mmoja wa kike alisema vijana wa tanzania hata nguvu za kiume hawana, jii ni dharau aisee
Inasikitisha sana kwa kweli. Ila tunawangoja kwenye masanduku
 
Inasikitisha sana kwa kweli. Ila tunawangoja kwenye masanduku
Mcherengwa kashasema hakuna jimbo litaenda ka upinzani na kura zote kwa mama, wanaweza kufanya kama alivyofanya John, ccm ni ileile mkuu
 
Back
Top Bottom