Je, unaziona ndoto zako rohoni?

Je, unaziona ndoto zako rohoni?

Utimilifu wa ndoto katika maisha ya mafanikio huanzia rohoni na si mafanikio tuu bali kila jambo katika maisha bila kujali uzuri ama ubaya wake! Kwakuwa roho ndio asili na ndio chanzo cha kila kitu katika ulimwengu wa mwili?

Je unaziishi ndoto zako? Ama bado hazijatimia? Je unaziona ndoto zako katika uhalisia wake! Ni kama vile upandavyo mazao kondeni.. Unajiona tangu maandalizi ya shamba, kupanda palizi kukomaa na hatimaye mavuno! Utimilifu wa ndoto..! Je unaiona hii picha kwa vipande? Hatua kwa hatua?

Hapa tofautisha ndoto hizi za rohoni na ndoto zile za kichwani. Ndoto za Alinacha. Ndoto za kuota una pesa mingi bila mipango, unaendesha ndinga kali unachukua bebes za viwango, kasri lenye kila aina ya starehe nknk.. Sio ndoto hizi ambazo waotaji wake hawawazi mwanzo wa kufikia kupata bali wanawaza mwisho wa matokeo ya kupata na kutumia..ndio maana ziko kichwani juu na sio rohoni ndani!

Unataka kuwa nani maishani.. Unataka kufanya nini maishani. Hiyo roadmap utaiona rohoni mwako kila uendapo, kila ufanyalo na hata katika usingizi na uchovu mwingi utajiona wewe katika uhalisia wako ndani ya hizo ndoto zako

Haijalishi utachelewa muda gani kuzifikia Kila mmoja wetu ana muda wake wa kupata. Wengine wanachelewa na wengine wanawahi. Sometimes ni heri kuchelewa lakini ufike milele kuliko uwahi kisha ufeli kabla kesho haijapambazuka. Kuchelewa kupata utakacho ni maono pia.

Usiishi kwa kihoro cha kuchelewa kutimiza ndoto. Usibabaike na waliokutangulia.. Jenga msingi wako rohoni ukitumainia yajayo. Lakini usibweteke ila usitumie mkato pia. Usiyalazimishe mafanikio yako kupitia njia zisizo sahihi. Usitumie kafara na nguvu za giza. Utapata kwa wakati huo. Lakini itakapofika kupata kwa halali. Haramu itakuwa imeshanajisi njia yako na anguko lako litaanzia hapo.

Maisha sio leo maisha ni kesho na kesho ni kubwa kuliko Jana, kuliko juzi, kesho ni kaka mkubwa wa leo. Usibweteke ila ziishi ndoto zako katika njia sahihi. Hata kama hujapata na hata kama muda haujatimia lakini ishi kwenye maandalizi ya KUWA utakaye kuwa!
Dressing code yako
Matendo yako
Mienendo yako
Maono yake vyote viashirie utakayekuwa baadae. Haijilishi ndoto zako ni kuwa
Mama wa nyumbani anza sasa
Msanii mkubwa anza sasa
Kiongozi mkubwa anza sasa
Mfanyabiashara mwenye mafanikio anza sasa
Mtu maarufu anza sasa
Paroko, Sheikh, mchungaji anza sasa
Mtunzi maarufu anza sasa
Mwanasayansi na jasusi anza sasa!

Kuna baadhi ya ndoto za rohoni hujidhihiri kwa watoto wadogo tangu mwanzo.. Maana matendo na mienendo yake huchora ramani inayoonekana!

Kumbuka hakuna ndoto za rohoni zinazojifunua uwe
Tena
Malaya
Jambazi
Mdangaji
Tapeli
Mwizi
Muongo nknk
Hayo ni matendo ya giza baada ya ndoto kufa kwa sababu zozote zile!

Kama kila ukijiangalia mawazoni kuna mahali unatamani kuwa lakini rohoni unaona kiza..achana na hizo fikra.. Hutafika popote..

Nawatakia Jumamosi njema ya Pasaka
Jr[emoji769]
16.04.2022
Mshana samahani natoka nje ya mada,naomba kufahamu kuhusu mimea ifuatayo na je kwa uzoefu wako wapi naweza kuipata. Kwenye vitabu vitakatifu tumepewa vitu vyote vilivyopo chini ya ardhi tuvitawale lakini pia kuvitumia.

Screenshot_20220508-025902.png


Screenshot_20220508-030503.png


Screenshot_20220508-030612.png


Screenshot_20220504-051025.png
 
Aisee pole sana, wakati nasoma shahada yangu ya pili niliteseka na kupata machungu nusu niache shule na nilipata depression na kuugua kisa shule, but I was farting and praying na nikakumbuka kutoa sadaka na fungu la kumi na nilikuwa nasali naiombea sadaka iondoe kikwazo chochote a day nimetoa sadaka hyo baada ya kutoka kanisani mikitembea mjini nilikutana na mtu akaniombea simfahamu that day I vomited na weak hiyo nikapigiwa simu nikakusanye vitabu ni graduu Hadi nilishangaa, na kazi yangu ilikuwaga Haina makosa imepitia editing had za ma Prof ila ilikuwa ngumu kutoboa, I believe Kuna vitu watu hufanyizia wengine Ili ucheleww kufia kusudi na destiny yako, so Anza maombi ufunge na utoe fungu la kumi pia usisahau kusoma Malaki 2 inazungumzia kuhusu sadaka ilinisaidia sana

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
Wanadamu tunatesana sana, Ahsante sana kwa ushauri cariha
 
Nakuombea sana hili nalo litapita
Mkuu em nisaidie hapa,tangu nianze tiba ya chumvi matokeo nimepata mazuri sana tu,ila imejitokeza shida moja(hii sikuinuia ktk tiba,imekuja tu yenyewe),watu wananiangalia sana toauti na zamani,yan mtu ananangalia tangu natokeza ktk upeo wake mpaka nikisha mpita yeye alipo nikageuka nyuma nakuta bado ananiangalia tu.Hii inaninifanya nijishtukie hadi naona aibu,nakosa ujasiri.

Kwamfano nikienda kuhemea mboga mboga,hao wamama wauzaji wananitazama wote kwa pamoja usoni,bas me nabaki najistukia nashindwa nimuungishe nani biashara yake sababu wote wana ntazama,bas najkaza naenda kwa mmoja,nikishafika ktk meza yake ananihudumia utafikiri mimi ni Malkia,ananikaribisha na kuonesha kunijali kupita kiasi sana tofauti na zamani nilivokuaga.

Funga kazi ni jana kanisani, yaani nimeingia tu waumini badala ya kutazama mbele wakageuka kuniangalia wakanishindikiza na macho mpaka nilipoketi,(sikua na kasoro yoyote ktk mavazi wala sikuvaa viatu vya kwa kwa kwa).Yaani muda wa sadaka ulipofika sikusimama kwakweli dah!!

Sasa mkuu hakuna sehemu nilikosea kweli ktk tiba??Watu wananiangalia sana(sikunuia hili).Nifanye nini hapo ili hali irudi kawaida??Maana tiba siwezi kusimama,niliyo yanuia yanaendelea vizuri na mengine bado hayajakamilika ila naona mwanga kuwa yatatimia. Shida ni watu kuniangalia sana tu!
 
Mkuu em nisaidie hapa,tangu nianze tiba ya chumvi matokeo nimepata mazuri sana tu,ila imejitokeza shida moja(hii sikuinuia ktk tiba,imekuja tu yenyewe),watu wananiangalia sana toauti na zamani,yan mtu ananangalia tangu natokeza ktk upeo wake mpaka nikisha mpita yeye alipo nikageuka nyuma nakuta bado ananiangalia tu.Hii inaninifanya nijishtukie hadi naona aibu,nakosa ujasiri.

Kwamfano nikienda kuhemea mboga mboga,hao wamama wauzaji wananitazama wote kwa pamoja usoni,bas me nabaki najistukia nashindwa nimuungishe nani biashara yake sababu wote wana ntazama,bas najkaza naenda kwa mmoja,nikishafika ktk meza yake ananihudumia utafikiri mimi ni Malkia,ananikaribisha na kuonesha kunijali kupita kiasi sana tofauti na zamani nilivokuaga.

Funga kazi ni jana kanisani, yaani nimeingia tu waumini badala ya kutazama mbele wakageuka kuniangalia wakanishindikiza na macho mpaka nilipoketi,(sikua na kasoro yoyote ktk mavazi wala sikuvaa viatu vya kwa kwa kwa).Yaani muda wa sadaka ulipofika sikusimama kwakweli dah!!

Sasa mkuu hakuna sehemu nilikosea kweli ktk tiba??Watu wananiangalia sana(sikunuia hili).Nifanye nini hapo ili hali irudi kawaida??Maana tiba siwezi kusimama,niliyo yanuia yanaendelea vizuri na mengine bado hayajakamilika ila naona mwanga kuwa yatatimia. Shida ni watu kuniangalia sana tu!
Hilo si tatizo umetakasika sasa unangara kila mtu anakuona
 
Mshana nimeikubali sana hii life changing post.ila vijana tulio wengi hatutakuelewa,tunaweza kuja jua baadae sana wakati tukiwa mwishoni mwa uzee wetu.

All in all ,mungu pekee ndio anatimiza ndoto zetu licha ya ugumu wa ndoto zetu.tuzidi kuomuomba mungu amen.
 
[mention]Mshana Jr [/mention] naomba unisaidie mkuu hivi upande wa juu wa jicho la kushoto ukiwa unacheza cheza ni nini maana yake ( nyusi)
 
Mshana nimeikubali sana hii life changing post.ila vijana tulio wengi hatutakuelewa,tunaweza kuja jua baadae sana wakati tukiwa mwishoni mwa uzee wetu.

All in all ,mungu pekee ndio anatimiza ndoto zetu licha ya ugumu wa ndoto zetu.tuzidi kuomuomba mungu amen.
Aaamen
 
Utabarikiwa na hiki nitakachoandika usiku huu tulivu.
Uono wa macho ya rohoni na usikivu wa sauti ya rohoni.. Hivi ni vitu viwili vyenye nguvu kubwa sana kwenye mustakabali wa maisha yako... Kesho yako...
Kesho yako kazini kwako
Kesho yako kwenye biashara yako
Kesho yako kwenye kipaji, kipawa chako
Kesho yako kwenye usanifu, ubunifu wako
Kesho yako kwenye mahusiano nknk

Chukua muda utulie na kusikiliza sauti rohoni zinasema nini... Ni muhimu sana
Chukua muda utulie uangalie macho ya rohoni yanakuangazia wapi.. Msingi wa mustakabali wa kesho yako huanzia hapo

Maisha ni hatua.. Maisha ni mchakato.. Ziamini ndoto zako kwakuwa ndoto ni uhalisia wetu wa ndani kupitia ufahamu maizi.. Ndoto zinazungumza.. Ndoto zinatuonesha tuendako.. Ndoto hizi hutafsiriwa kupitia macho na sauti za rohoni
Natambua hujanipata vema kuhusu ndoto... Kuhusu sauti za rohoni.. Kuhusu macho ya rohoni.... Nisikilize tena.
Katika hatua za makuzi kila wakati kuna sauti zinakwambia wewe unapaswa kuwa fulani.. Halafu kuna uono unakuonesha vile unavyotakiwa kuwa... Kweli si kweli? Hivi viwili ndio hutengeneza ndoto yako katika tafsiri yake.

Twende na mifano michache upate kunielewa vema.
Wote tunamfahamu vema mwanzilishi wa JamiiForums ndugu yetu Maxence Melo.. Natamani nipate wasaa wa kuhojiana naye.. Nina hakika alijiona akisimama toka kwenye kigoda mpaka kukaa hapo alipo
Wote tunamfahamu mtoto wa Mbagala Diamond Platnamuz... Alipotoka... Alipo sasa na huko aendako.. Anaziishi ndoto zake
Mifano ni miwili tu lakini naamini ni kiwakilishi cha wengi kwenye kuziishi ndoto... Kusikiliza sauti za rohoni na kuangalia kwa macho ya rohoni

Kuna swami moja maarufu watu huulizwa.. Swali husika ndio hubeba uhalisia wa mustakabali wako maishani... UNATAKA KUWA NANI? Jibu la kwanza bila kuwaza ndio huwa sahihi. Kwakuwa kufumba na kufumbua hujiona wewe pale unapotaka kuwa na automatically jibu hukutoka.. Ni kitendo cha split of seconds.

Usijaribu kuwa tofauti ni kile kinachokuambia rohoni mwako.. Usijaribu kuwa tofauti ni kile kinachokupa mwanga wa uono rohoni mwako.. HUTAFANIKIWA.. Kwakuwa unakuwa mpangaji kwenye NAFSI yako mwenyewe

Ujanani kwenye hatua za makuzi ndoto huwa nyingi lakini ukitulia kuna moja hujirudiarudia.. Ifuate hiyo kwakuwa hiyo ndio wewe wa baadae

Usikimbilie kufanikiwa katika hatua za mwanzo za makuzi kabla hujahakikisha ndoto yako.. Wengi wamekwama hapa na kuharibikiwa kabisa
Natambua wazi uko kwenye ajira lakini unajiona kabisa hapo sio kwako.. Unajiona ukiwa kwenye nafasi nyingine kabisa
Natambua uko kwenye biashara lakini unajiona kabisa kuwa unahitaji kukua na kuwa mfanyabiashara mkubwa
Natambua uko kwenye fani lakini kila ukijitazama unajiona kabisa level yako unayostahili ni ya kimataifa

Natambua uko kwenye mahusiano rasmi ama yasiyo rasmi lakini kila ukiangalia mbele unaona giza ama unajiona mkiwa na mwenza wako kwenye maisha fulani ya furaha na mafanikio makubwa.. Kurunzi la rohoni kwenye mahusiano lina nguvu kuliko chochote
Kurunzi la rohoni kwenye mahusiano linaimulika vema kabisa kesho yako.. Hebu liangalie kama linawaka ama unaona giza

Hatua hii ya utambuzi wa kiroho kwenye maisha yako ni muhimu sana sana kuichunga kwakuwa ukifanya kosa tuu.. Umekwisha... Kwakuwa ni katika hatua hii wengi wetu hutaka ndoto zitimie haraka
Kwenye usanii
Kwenye ubunifu
Kwenye vipawa
Kwenye mahusiano
Kwenye ajira
Kwenye biashara
Kwenye siasa
Usijaribu kabisa kulazimisha hapa... Maana yangu ni kwamba usipaniki ukataka kutafuta njia za mkato.. Kama wizi, dili chafu na kubwa kuliko yote USHIRIKINA...

Natambua kuna wakati ndoto hukusukuma kwa nguvu sana utoke hapo ulipo na kukaa kwenye nafasi yako... Hilo halizuiliki... Lakini kamwe usiangukie kwenye mtego wa nguvu za giza
Tamaa ya kutimiza ndoto haraka ni ibilisi anayekusukuma uende uelekeo usio sahihi... Tamaa inakutia upofu wa kuona ATHARI za mbeleni utapokuwa umesimana sasa... Utahubiriwa habari za waliofanikiwa kupitia USHIRIKINA... Usiwasikilize hao ni madalali wa ulozi.. Kama ni mafanikio kwani wao hawayataki? Umeshawahi kujiuliza hili swali? Huko gizani ni utumwani.. Wewe unakuwa mtumwa na mateka wa maagano na makafara na miiko migumu

Unaweza kusema nimechoka mimi ngoja nijilipue.. Lakini majuto yatakuja baadae.. Hakuna kitu kibaya kama viapo na maagano ya damu... Kiwango huongezeka kila hatua... Mwisho wa yote ni anguko kubwa na lenye mateso makubwa na sometimes fedheha na aibu. Si kila umuonaye amefanikiwa ana furaha na amani kama unavyodhani

Ziishi ndoto zako katika njia sahihi.. Katka mstari mnyoofu... Jicho lako na kurunzi la rohoni vikumulikie uelekeo sahihi.. Sauti ya rohoni isibebe mwangi unaotisha bali kila uisikiapo ile loud and clear

Je umekumbuka chumvi yako leo?
Nakuombea ndoto zako zikatimie katika mstari sahihi.. Kumbuka una kipimo chako kwenye maisha yako.. Usilazimishe kuongeza.. Utaharibu chombo...

Alamsiki....!!!
 
.
 

Attachments

  • FB_IMG_1697545821033.jpg
    FB_IMG_1697545821033.jpg
    12.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom