Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,732
- 861,078
Utimilifu wa ndoto katika maisha ya mafanikio huanzia rohoni na si mafanikio tuu bali kila jambo katika maisha bila kujali uzuri ama ubaya wake! Kwakuwa roho ndio asili na ndio chanzo cha kila kitu katika ulimwengu wa mwili?
Je unaziishi ndoto zako? Ama bado hazijatimia? Je unaziona ndoto zako katika uhalisia wake! Ni kama vile upandavyo mazao kondeni.. Unajiona tangu maandalizi ya shamba, kupanda palizi kukomaa na hatimaye mavuno! Utimilifu wa ndoto..! Je unaiona hii picha kwa vipande? Hatua kwa hatua?
Hapa tofautisha ndoto hizi za rohoni na ndoto zile za kichwani. Ndoto za Alinacha. Ndoto za kuota una pesa mingi bila mipango, unaendesha ndinga kali unachukua bebes za viwango, kasri lenye kila aina ya starehe nknk.. Sio ndoto hizi ambazo waotaji wake hawawazi mwanzo wa kufikia kupata bali wanawaza mwisho wa matokeo ya kupata na kutumia..ndio maana ziko kichwani juu na sio rohoni ndani!
Unataka kuwa nani maishani.. Unataka kufanya nini maishani. Hiyo roadmap utaiona rohoni mwako kila uendapo, kila ufanyalo na hata katika usingizi na uchovu mwingi utajiona wewe katika uhalisia wako ndani ya hizo ndoto zako
Haijalishi utachelewa muda gani kuzifikia Kila mmoja wetu ana muda wake wa kupata. Wengine wanachelewa na wengine wanawahi. Sometimes ni heri kuchelewa lakini ufike milele kuliko uwahi kisha ufeli kabla kesho haijapambazuka. Kuchelewa kupata utakacho ni maono pia.
Usiishi kwa kihoro cha kuchelewa kutimiza ndoto. Usibabaike na waliokutangulia.. Jenga msingi wako rohoni ukitumainia yajayo. Lakini usibweteke ila usitumie mkato pia. Usiyalazimishe mafanikio yako kupitia njia zisizo sahihi. Usitumie kafara na nguvu za giza. Utapata kwa wakati huo. Lakini itakapofika kupata kwa halali. Haramu itakuwa imeshanajisi njia yako na anguko lako litaanzia hapo.
Maisha sio leo maisha ni kesho na kesho ni kubwa kuliko Jana, kuliko juzi, kesho ni kaka mkubwa wa leo. Usibweteke ila ziishi ndoto zako katika njia sahihi. Hata kama hujapata na hata kama muda haujatimia lakini ishi kwenye maandalizi ya KUWA utakaye kuwa!
Dressing code yako
Matendo yako
Mienendo yako
Maono yake vyote viashirie utakayekuwa baadae. Haijilishi ndoto zako ni kuwa
Mama wa nyumbani anza sasa
Msanii mkubwa anza sasa
Kiongozi mkubwa anza sasa
Mfanyabiashara mwenye mafanikio anza sasa
Mtu maarufu anza sasa
Paroko, Sheikh, mchungaji anza sasa
Mtunzi maarufu anza sasa
Mwanasayansi na jasusi anza sasa!
Kuna baadhi ya ndoto za rohoni hujidhihiri kwa watoto wadogo tangu mwanzo.. Maana matendo na mienendo yake huchora ramani inayoonekana!
Kumbuka hakuna ndoto za rohoni zinazojifunua uwe
Tena
Malaya
Jambazi
Mdangaji
Tapeli
Mwizi
Muongo nknk
Hayo ni matendo ya giza baada ya ndoto kufa kwa sababu zozote zile!
Kama kila ukijiangalia mawazoni kuna mahali unatamani kuwa lakini rohoni unaona kiza..achana na hizo fikra.. Hutafika popote..
Nawatakia Jumamosi njema ya Pasaka
Jr[emoji769]
16.04.2022