May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,820
Ingawa baadhi yetu twaweza kuleta ubishi juu ya hili lakini ni ukweli unaowakuta zaidi ya asilimia 80 kama sio 90 ya Wanandoa wamejikuta wameoana kutokana na sababu moja au nyingine, wengi ikiwa ni baada ya kuona miaka inasonga bila kupata Mwenza anayekidhi ndoto zake.
Binaadamu yeyote mwenye mipango ni lazima atakuwa na mipango ya namna anavyotamani aishi siku za usoni, miongoni mwa mipango hiyo ni kupata Mke/Mume wa aina fulani, kimuonekano, asili yake, imani yake n.k.
Huenda nyote wawili mnalijua hilo lakini hakuna anayethubutu kuweka hisia zake hadharani ili kutomkwaza Mwenza wake.
Labda kwa zile ndoa zinazoingia kwenye misukosuko ya mara kwa mara inayopelekea kutoleana maneno makali yasiyojali hisia za mwingine.
Bila shaka mpo wengi mnaoweza kukiri kuwa hamuishi na Wenza wa ndoto zenu.