Zingatia haya wakati unatafuta mke/mume mwema

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
11,556
Reaction score
7,113
MARA nyingi vijana hupata taabu sana katika suala la kuchagua mchumba. Vijana wa kiume ndio hasa hupata wakati mgumu zaidi kwani jamii imewapa wajibu wa kuanzisha mazungumzo yahusianayo na mapenzi. Hata hivyo, vijana wa kike nao wanao wajibu wa kuchagua ili kuhakikisha kuwa hawaanguki mikononi mwa mabazazi wa kuwalaghai na kuwatumia kwa raha za miili yao kisha kuwaacha kwenye mataa.

Ni jambo la kawaida kwa vijana walio wengi, wawe wa kike au wa kiume, kuangalia sura na mwonekano wa mtu. Lakini unapotafuta mchumba kwa malengo ya kuishi naye maisha yako yote kama mume na mke haipendezi kuangalia tu mwonekano, maana Waswahili husema si kila king'aacho ni almasi. Kwa sababu hiyo, hapa yatabainishwa mambo muhimu ya kuangalia na kuzingatia katika suala hili.

1.MCHA MUNGU.
Vijana wengi huwa wanasema kuwa ni ngumu kumpata mwenza ambaye kwao wanaona ni mwenza ambaye anamjua Mungu, mwenza ambaye anatambua nafasi ya Mungu katika maisha aya kila siku.Tatizo hilo huchangia kuwa na watu amabao baadaye wanakuja kuwa tatizo pale ambapo matatizo yameikumba familia.Pia kunakuwa hakuna hofu ya Mungu kati yenu hivyo kupelekea mambo kwenda mrama kwa sababu mnakuwa hamumshirikishi Mungu katika mambo yenu.. Ni vyema kuwa makini sana katika hilo.Mshirikishe Mungu katika chaguo lako

2. UADILIFU

Pamoja na sifa zote za uzuri zinazoweza kubainishwa na kufanywa kuwa vigezo vya uzuri wa mwanamke na mwanaume na hata zikatumiwa kumpata Miss au Mr Tanzania, sifa kuu impasayo mtu anayefaa kuwa mchumba kuwa nayo ni sifa ya uadilifu.

Mtu anapokuwa na uadilifu (pengine uaminifu), maana yake ni kwamba tabia ya mtu huyu anayoionesha nje ndiyo tabia yake halisi na anapofanya jambo jema analifanya kwa roho yake na si kwa unafiki.
Mtu anapokuwa mwadilifu ataheshimu maadili na kufanya wema, hata pale inapokuwa rahisi kwa wengine kukengeuka na kufuata njia za mkato ambazo mara nyingi si za halali.

Mtu mwadilifu pia huwa na sifa za ukweli na kujitolea kuwasaidia watu wengine bila kujali faida – haya yote ni mambo muhimu ambayo mtu mwenye kuwa nayo huwa na msingi wa ujenzi wa uhusiano imara na wa kudumu.

Watu wanaoweza kujivunia furaha ya kweli katika maisha yao ya ndoa, ni watu ambao wamekutana wote wakiwa na sifa ya uadilifu ambayo hujumuisha mambo mengi.

Zipo ndoa nyingi zenye furaha ya bandia. Furaha hii mara nyingi hutokana na ridhiko la kimwili alipatalo mtu kutokana na kukidhiwa kwa mahitaji yake ya kimwili yanayohusiana na haki za msingi za binadamu – yaani chakula, mavazi na malazi. Lakini furaha ya kweli ya maisha ya ndoa, watu hawaipati isipokuwa katika uhusiano ambao wenza wamethibitishana kuwa waadilifu.

3. HEKIMA

Mtu mwenye uadilifu wa kweli, mbali na kuwa mwema kwa mwenzake, pia huhakikisha anakabiliana kwa busara na hekima na matatizo yote yanayoweza kusababisha kuyumba kwa uhusiano, hususan yale yaliyo nje ya uwezo wake.

Uzoefu unaonesha kuwa wapenzi, hususan wanandoa walio katika uhusiano wa muda mrefu wanaoendelea kufurahia unyumba wao si wale ambao walipendana kwa mvuto na wala hawana mambo mengi ya asili yanayowaunganisha kuliko wale wanaotengana. Lakini la muhimu ni kwamba watu hawa huwa wamejifunza jinsi ya kukabiliana kwa hekima na matatizo yanayojitokeza, hususan yale yanayotokana na tofauti zao kimtazamo.

Ukiachilia mbali sifa ya uadilifu, watu hawa huwa wamejifunza kukabiliana na matatizo kuhusiana na uzazi na ulezi wa watoto, uhusiano na ndugu, jamaa na marafiki, suala la ngono, fedha na maisha ya unyumba kwa ujumla.

Habari njema ni kwamba uadilifu na hekima ni mambo ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza na kisha kufanyia kazi. Ndiyo maana wanandoa hufundishwa kabla ya ndoa na hata wanapokuwa tayari wameoana huendelea kuhudhuria semina za kidini na kijamii kwa ajili ya kujiimarisha.

Kwa hiyo, kama mume/mke wako mtarajiwa anaonekana kuwa na utayari wa kujifunza kuhusiana na jinsi ya kuishi na mtu wa jinsia nyingine, ana nafasi kubwa ya kuwa mke/mume mzuri baadaye.

4. UPOLE

Mfalme Suleiman katika mojawapo ya semi zake za hekima alisema mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake. Yamkini ndivyo ilivyo pia kwa mwanaume mpumbavu, maana upumbavu haujengi.

Siku zote kitu kinachovunja uhusiano wa kindoa si makombora ya nyuklia, bali ni ulimi. Kwa kadri mtu anavyoutumia ulimi wake anaweza kuijenga au kuibomoa nyumba yake.
Katika kumwangalia mtu ambaye unaweza kujenga naye nyumba ya kudumu, ni vema kumchunguza na kuhakikisha kuwa si mtu mwenye kupenda kurefusha maneno, maana hakika huyu atasababisha ugomvi mara kwa mara na uhusiano hautadumu.

Wapo watu ambao ndoa zao zina sifa ya ugomvi na karibu kila mtu anafahamu na hata wamekuwa kero kwa ndugu, jamaa na majirani zao, mara kwa mara wakiwaamsha watu usiku wa manane wakitafuta suluhu.
Mara nyingi wanaume ndio huanzisha ugomvi, lakini ugomvi huwa na nguvu zaidi kama mwanamke ni msemaji. Dawa ya kuzuia ugomvi usiokuwa na mpango ni kupunguza maneno na kuepuka kutafuta ushindi katika ubishi. Lakini kinga ya tatizo hili ni kuepuka kujiingiza katika uhusiano na mtu ambaye umejihakikishia kuwa si mwingi wa maneno.

Bahati nzuri, jamii huwatambua wanawake/wanaume ambao wanaweza kuwa wake/waume bora baadaye kwa hiyo ni wajibu wa mtafutaji kuhakikisha kuwa anafanya uchunguzi wa kina kabla ya kujitosa kwa mtu ambaye baadaye atamtaabisha.

Mwanandoa aliyeifahamu vema dhana ya ndoa – kwamba ni maisha ya kuvumiliana na kuchukuliana, hufahamu ni wakati gani wa kusema na wakati gani wa kukaa kimya. Mtu huyu pia hufahamu njia nzuri na salama ya kujiondoa kwenye tatizo anapoona mwenzake anaelekea kubaya, ili hatimaye uhusiano wao uendelee kuwa salama japo wao wanaweza kuwa wamekwaruzana.

Mtu huyu mwenye upole hujiweka katika mkao wa upatanishi na huhakikisha kuwa kila mjadala mkali unapita na kumalizika salama. Ni wazi kuwa katika kutafuta, kama hukukurupuka, utamwona mtu mwenye hulka hii – upole.

5. MVUTO

Hisia za mvuto wa kimapenzi ni muhimu katika kujenga uhusiano. Mtu mmoja akauliza, ni yupi bora – yule anayenivutia sana au yule anayenipenda sana? Maisha ni ya ajabu sana. Huwa inatokea kuwa mtu unayevutiwa naye sana yeye havutiwi nawe, bali anavutiwa na mwingine ambaye naye hana mpango naye!

Haya ndiyo maisha. Uzoefu unaonesha kuwa asilimia kubwa ya watu walio katika ndoa hawajawaoa/kuolewa na watu waliokuwa wakiwapenda sana enzi za ujana wao, au wale waliotimiza ndoto za ujana wao. Bahati njema miongoni mwa wanandoa hawa wapo wale wenye ndoa imara sana.

Mvuto wa kimapenzi ni muhimu sana, lakini watu husema maji yakisema usininywe yajibu kuwa wewe pia huna kiu nayo. Japo inaweza kuonekana kama ni aina ya ‘sizitaki mbichi hizi' lakini si vema kujisumbua na mtu asiyekupenda.

Badala ya kujihangaisha na mtu asiyekupenda, kaa chini na umsubiri anayekupenda hata kama huhisi kuvutiwa naye sana. Baadaye utamzoea na maisha yatakuwa mazuri, kisha utajiuliza baadaye yule aliyekuringia alikuwa na nini cha ziada?

Lakini iwapo mambo mengine yote yatakwenda sawa, ni vema na muhimu kabisa kuhakikisha kuwa mtu unayepanga kuwa naye maisha yako yote ni mtu anayekuvutia kimwili na kiakili, maana vinginevyo unaweza kupata sababu ya kukidhi kiu yako nje – jambo ambalo si maadili mema katika ndoa na maisha.

NI MUHIMU KUWA MAKINI

Katika nyakati za ujana, watu wengi hubabaishwa kwa mengi. Vijana wa kiume hubabaishwa na sura, maumbile na pengine rangi na kusahau mambo muhimu yaundayo orodha ya sifa za mke mwema.

Kwa upande wao, vijana wa kile pia waweza kubabaishwa na pesa, maumbile, sura, utanashati, umaarufu au kuchoshwa na shinikizo la umri, hivyo kujikuta wakijitumbukiza kwa wanaume wasio na sifa za waume wazuri.

Lakini tukirejea kwenye msemo wa zamani kuwa uzuri si hoja bora tabia, ni wazi kuwa tutafikia mahali tutajenga mahusiano imara na yasiyotikiswa na sunami zozote za kimaisha. Ilimradi tu uhakikishe kuwa mtu mwenyewe anakupa mvuto kimapenzi, maana vinginevyo kutakuwa hakuna maana.

Bora ukosee kujenga nyumba kuliko kukosea kuoa/kuolewa..
Mr Rocky, FP , snowhite, gfsonwin, Mtambuzi, Kaunga, Dark City, bi mkora, AshaDii, Maxence Melo, na wengine ambao mpo kwenye ndoa naomba muongezee mambo mengine muhimu ambayo mtu anapaswa kuangalia wakati anatafuta mke au mume..
 
Last edited by a moderator:
Nicas Mtei nakubaliana na wewe katika mchanganuo ulioutoa hapo juu
Suala kubwa katika wakati wa kutafuta mke ni lile la ucha Mungu maana mengine yote yatazalishwa iwapo utakuwa na mke au mume ambaye ana moyo wa ucha Mungu.

Maisha ambayo tunajuka kuyaishi wakati na kwenye ndoa zetu tunahitaji sana uwepo wa Mungu katika nyumba zetu. hatuchagui mke tuu kwa kuwa sura yake ni nzuri au ana miguu mizuri au ana macho mazuri au ni mpole tuu au ana hekima tuu then ukaacha kuangalia vigezo vingine. Je huo upole wake ni kweli au ni geresha tuu wakati anakuingiza kwenye libne zake au uadilifu/ uaminifu wake ni wakati huu tuu mkiwa wachumba akishavaa ile pete ndo anaonyesha makucha yake
Vyote hivyo inategemea kama ana roho ya Mungu ndani mwake hatabadilika hata ndani ya ndoa yako. Mpime mchumba wako kwa mengi kabla hujakubali kuingia kwenye kiapo na yeye na ujue kama mengi anayoyafanya anaiga au ni kweli ni ya moyoni mwake.

Usimpende mtu kwa kuwa ana macho mazuri au ana miguu mizuri au ana sura nzuri bila kujua ndani ya moyo wake ameweka nini au anakuwazia nini wakati hampo pamoja. Sura yake ya nje iendane na moyo wake iendane na kila alicho nacho ili kuja kudumisha ndoa yako maana ni kiapo cha kufa na kuzikana.
 
Ahsante sana Mr Rocky kwa mchanganuo mzuri katika mada niliyoiweka... Kwa kweli vijana sasa tunayo changamoto kubwa sana wakati tunaelekea kwenye ndoa
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana kwa somo hilo zuri. Wanawake wengi kwa sasa hawana hekima kabisa, utakuta mtu mkikosana kidogo tu anakimbilia JF utadhani ndo kuna mganga wa matatizo yake-sijui ni kwa sababu ya usomi?. ACHENI HIZO
 
Hakuna kitu kizuri kwenye mahusiano ya aina yoyote kama mkiwa na uwezo wa kutumia busara na hekima na ucha Mungu katika kufikia kusolve matatizo yenu na migogoro yenu bila hata sisimizi walioko vyumbani mwenu kujua kuwa mligombana au mlikuw ana differences ndani ya nyumba.

Mahusiano mengi yanavunjika kw avitu na viugomvi vidogo vidogo kama eti siku nzima hajanipigia simu au kunitext au nilimtumia text hakunijibu au nilimpigia hakurudisha simu yangu hata alipokuta missed call. Au alichelewa kwenye miadi nimekaa nimemsubiri muda mrefu bila kuonekana. Au hanisifii hata kama nimevaa kiatu kipya au nguo mpya. dah sasa unajiuliza alikaa akatulia au wote mkatulia mkaulizana kwa nini hajajibu your sms or your call au kwa nini alichelewa kwenye miadi inawezekana mama yake alikuwa mgonjwa au alipata dharura kazini.

Ukiwa kwenye uhusiano jifunze sana uvumilivu na kusamehe na kujifunza kutulia kabla hujakurupuka kufanya jambo lolote. Tulia na uliza kwa makini wakati hasira zako zimepoa. Msijibizane au kupandishiana maneno maana hapo mnafurahisha umati na hasira zako hazisaidii. tengenezeni magomvi yenu taratibu mkitoka kugombana watu hata wasijue kuwa mligombana au kulikuw ana tatizo. Usiku usipite mchana uingie mkiwa na maugomvi ya jana yake ndo yale mambo wachumba au mke na mume wanaandikiana vimemo niamshe saa kumi na mbili na mke anaamka saa kumi na mbili anaandika kimemo saa kumi na mbili imefika amka sasa sijui hicho kimemo ndo kitamuamsha mumewe
 
as for me wakati wa kutafuta mchumba jambo kubwa moja ni hili angalia mtu ambaye ni MWAMINIFU na MVUMILIVU basiiiii.
kwanini haya nayasema ni ya muhimu sana kwangu??
mtu akiwa mwaminifu ni wazi kwamba atakuwa mkweli kwako na kwa Mungu pia. akisema nipo nyumban ni wazi kwamba yupo nyumban, sipo ina maana kweli hayupo. akiwa mwaminifu kwa Mungu ni wazi kamba atakuwa mcha Mungu manake ili utimize kipengele cha uaminifu kwa Mungu basi lazima uwe ni mcha Mungu.

atakuwa mwaminifu hata kwenye heshima kwa Mungu na wanadamu pia, atamuheshimu Mungu kwa kipato chake, atakuwa muaminifu ata kwa mume/mke na kwa kumtolea mungu basi ataleta baraka ya kipato na neema ndani mwako.

uvumilivu: mchumba akiwa mvumilivu basi ni wazi kwamba atakuwa ni mtu asiyehesabu gharama katika makosa ya mwenzie na mara zote hatakasirishwa na mwenzie bali atalikasirikia kosa lililotendeka.always ataangallia kwanini kosa hili litokeee?? na kwanini ilihali bado mwenzangu ni mzuri na hajabadilika kutoka kuwa fulan kwenda kuwa mtu mwingine??
kwake yeye kosa ni kosa na mpenzi wake ni mpenzi wake. daima hatomchanganya mpenzi na makosa bali atataka kuvitofautisha ili aweze kuvitenganisha. ni makosa sana kuchanganya kosa la mtu na mtu mwenyewe manake hii huzaa chuki kwa mtu jambo ambalo sio jema.

ikumbukwe kwamba uvumilivu hauhesabu gharama wala hauna chuki.
 
perfect sana... nimejifunza jambo hapo
 
Uaminifu na Uvumilivu... nazingatia sana pia....
 
yay!! i have one of those attributes to large extent, hiyo nyingine ninayo moderate. umeongea pointi nzuri
 
nakupenda sana mwanangu. ngoja tu nikupende ili ufaidi matunda ya kupendwa kwa dhati bila unafiki manake sijui wadada utakao pata watakupendaje.

but nakuombea sana Mungu akupe wa kufanana na wewe. ila aongezewe zaid uvumilivu.
 
Nicas Mtei, Dah!
Umenifumbua macho na masikio.
Ila nauliza hv, suala la kipato haliingii hapo?
Maana kuolewa au kuoa mtu asiye na kipato kbs huoni kwamba ni tatizo kwa baadhi ya wenza!
 
Last edited by a moderator:
UPOLE - moyo wa upole unaweza kusamehe kweli na kuvumilia mapungufu yote ya mwenzako.
 
Leo akili yangu haijakaa vizuri, sijui kwanini?
 
Nicas Mtei, Dah!
Umenifumbua macho na masikio.
Ila nauliza hv, suala la kipato haliingii hapo?
Maana kuolewa au kuoa mtu asiye na kipato kbs huoni kwamba ni tatizo kwa baadhi ya wenza!

Mimi nadhani mtu hawezi kukosa kipato kabisa, labda useme kisichokidhi mahitaji yanayohitajika.

Katika mapenzi kitu tunacho kiangalia ni mapenzi ya dhati yanayoshabihiana na ukweli usiyo jificha, kama mtu ulimempenda kweli na kumridhia sidhani kama suala la kipato litakuwa kigezo chakutengana au kuto kamilisha ndoto zenu.
Kitakacho wakomboa ni uvumilivu wa hali ya juu ambao utachochea jitihada zizizokua na mwisho, naamini ukifanya hivyo utaweza kuzitimiza ndoto zako na kufanikiwa kwa hali ya juu.
 
[/B]

Asante sana saudari kwa Ushauri wako.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom