Je, unaweza kumpa mtu nafasi ya kumiliki utambulisho wako milele kwa gharama ya Ksh. 7,000 (sawa na Tsh. 120,000/-)?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
jichooo.jpg

Watu wengi wajitokeza katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi, Kenya kuandikisha utambulisho wao wa kipekee kupitia mboni ya jicho kwenye Kampuni inayoitwa Worldcoins, ambapo kama malipo wanapewa sarafu za kidigitali zenye thamani ya 7,000 za Kenya na mpaka sasa zaidi wa watu 50,000 wameshawasilisha utambulisho wao.

Worldcoin pia imeahidi kuwapatia sarafu nyingine zenye thamani ya 7,000 za Kenya kila wiki kwa yoyoye atakaekubali kushiriki zoezi hili na kutumia program yao.

Worldcoin ilizinduliwa Jumatatu, Julai 24 2023 ikiwa na mashine za kuandikisha utambulisho wa watu kupitia mboni za macho katika maeneo mmbalimbali yaliyotambulishwa duniani Kenya ikiwa moja wajo, ambapo inawapatia watu sarafu za kidigitali bure kwa watakaokubali kuthibitisha wao ni binadamu kupitia mboni za macho yao.

Sarafu hizi za kidigitali wanazopewa baada ya kutoa utambulizo wao, wanaweza kuzitumia au kuziuza kama zilivyo au kuzibadilisha kuwa pesa taslimu.

Baadhi ya Wakenya hasa vijana, wamejitokeza kwa wingi kuchangamkia ‘fursa’ hiyo na kupata pesa za ‘bure’, wakisema hii ni hela ya bure ambayo huitolei jasho wala hutakiwi kufanya kazi ngumu, sasa kwanini wasichangamke!

jicho.png

Mmoja wa waanzilishi wa kampuni hiyo, ambae pia ni mmiliki wa mtandao wa ChatGPT amesema lengo la kuanzisha Worldcoin ni kuwa na sarafu ya kidigitali ambayo itapatikana kwa watu wote duniani bila kujali hadhi zao au sehemu wanapotokea na kueleza kuwa itasadia kueleza kama shughuli zinazofanywa mtandaoni ni za binadau au akili bandia katika dunia hii ambayo ni vigumu kututofautisha kutokana na maendeleo ya teknolojia.

Lakini je, ni kweli kuwa hakuna cha kupoteza kwa yoyote anaetoa utambulisho wake kama wengi wanavyoamini? Swali hili hata wamiliki wa kampuni hiyo hawana jibu, wakisema kuwa wanajua watakutana na changamoto nyingi na hawajui matokeo yake yatakuwaje!

Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi imewatahadhirisha Wakenya juu ya jambo hilo sababu ukishatoa utambulisho wako ina maana huna udhibiti wa taarifa zako ten ana unaweza kutumika vibaya milele na utakuwa huna la kufanya kuzuia hilo. Hii ni kwasababu mboni zetu zina utambulisho pekee kama ilivyo kwa alama za vidole, ambapo mtu akiwa nazo anaweza kujitambulisha kama wewe na kutumia utambulisho kwenye jambo lolote atakal ikiwemo kufanya uhalifu.

Je, kiasi chochote cha fedha kinatosha kuuza utu wako? Kumbuka bila Ulinzi wa taarifa binafsi na faragha yako hakuna uhuru wa kweli, maisha yako yanakuwa yanashikiliwa na mtu milele sababu anaweza kufanya chochcote kama wewe na kukuingiza matatizoni muda wowote.

Nation Africa
 
Waafrika hasa wale waliokata tamaa wanafanya jambo lolote hata la hatari lengo apate mkate wake wa siku.

Hii issue ya kupewa kipande cha mkate na kutoa taarifa zako haikupaswa kuruhusiwa na washika mpini, ila kwa sababu wanapewa ahadi basi ndiyo hivi tunaona.

Tuweke kabatini hii story kwa siku za usoni.
 
Back
Top Bottom