Je, unapenda pilau kuku, biriani mbuzi, nyama choma, makange ya samaki, ugali dagaa na mbogamboga? Mbinguni hazitakuwepo.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,306
Kuna vitu na mambo yanayopendwa sana hapa duniani ambavyo sio dhambi lakini ni kuwa hivyo vyote havitakuwepo. Kwa mfano sisi tunaopenda misosi mitamu kama ile ya Shishi food, white rose na Marry brown ni kuwa haitakuwepo. Kitu nachosikia kinatajwa tajwa ni maziwa na asali. Pia huenda kikawepo chakula kiitwacho MANA walichopewa wana wa Israel jangwani. Kiukweli bado haijathibitishwa chakula gani kitakuwepo huko ila uhakika ni kuwa hizi biriani, pilau, makange, nyama choma, kitimoto rosti na vingine pendwa havitakuwepo. Kama unakula hakikisha unakula kwelikweli. Huko tuendako havitakuwepo.

Wale wapenzi wa mpira wa miguu mtambue pia nayo pia haitakuwepo. Kama kuna timu unaipenda hakikisha unaishangilia sana ukiwa hai. Kwa sisi wakristo tunaambiwa starehe kubwa itakuwa kuimba mapambio ya kusifu. Yaani shughuli kuu huko ni kusifu na kuabudu. Hata wale wapenda hela wajue kuwa dhahabu na almasi zitakuwa sio chochote kwa sababu hizo biashara hazipo.

Je, nini kifanyike? Biblia kupitia Mhubiri 9:10 inasema chochote utakachopata kufanya kifanye kwa nguvu zako zote kwa sababu huko uendako hautapata nafasi ya kukifanya. Lakini Je, ni wakati sasa wa viongozi wetu wa dini kubadili maneno ya hamasa kwenye kuhimiza safari ya kwenda mbinguni? Wenzetu nasikia wanasema tukifika huko tutakabidhiwa mabikra kadhaa. Hii kiukweli ni hamasa yenye uhalisia.
 
1698584468359.png

71. Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele.

(Qur-an 43:71)
 
Yaani mimi kibinafsi ile nimefika Mbinguni halafu kwa mbali namuona mke wangu halali wa ndoa naye kafika Mbinguni.
Haki ya nani vile siwatanii lazima NIMTONGOZE TENA ili mapenzi yetu yasiishe. milele.
 
Nasikia tunapewa mwili mpya. Wote mnakua mnafanana. Yaani watu ni Me wote mnafanana Ke wote wanafanana.
 
Maisha ni haya haya, hakuna cha mbingu wala nini, bali tunajifariji tu. Kula maisha, kufa kizazi kingine kije.
 
Watu wa dasalama siku hizi mna ulaji flani,naonaga Instagram yan utakuta mtu ameagiza lisinia lina chips,wali,vitumbua humohumo,kitimoto,samaki humohumo,dagaa,makande,pembeni Kuna supu, ugali,mayai ya kukaanga na kuchemsha,nyama choma yan mavitu kibao hadi yale mnayoita mabiliani,halafu mnamalizia na bia mbili au juisi ya parachichi....Sasa huo mchanganyiko mtu akienda chooni kukata gogo,au akipumua,watu mliopo karibu lazima mpoteane maana hali ya hewa itakuwa imechafuliwa vibaya mno
 
Kuna vitu na mambo yanayopendwa sana hapa duniani ambavyo sio dhambi lakini ni kuwa hivyo vyote havitakuwepo. Kwa mfano sisi tunaopenda misosi mitamu kama ile ya Shishi food, white rose na Marry brown ni kuwa haitakuwepo. Kitu nachosikia kinatajwa tajwa ni maziwa na asali. Pia huenda kikawepo chakula kiitwacho MANA walichopewa wana wa Israel jangwani. Kiukweli bado haijathibitishwa chakula gani kitakuwepo huko ila uhakika ni kuwa hizi biriani, pilau, makange, nyama choma, kitimoto rosti na vingine pendwa havitakuwepo. Kama unakula hakikisha unakula kwelikweli. Huko tuendako havitakuwepo.

Wale wapenzi wa mpira wa miguu mtambue pia nayo pia haitakuwepo. Kama kuna timu unaipenda hakikisha unaishangilia sana ukiwa hai. Kwa sisi wakristo tunaambiwa starehe kubwa itakuwa kuimba mapambio ya kusifu. Yaani shughuli kuu huko ni kusifu na kuabudu. Hata wale wapenda hela wajue kuwa dhahabu na almasi zitakuwa sio chochote kwa sababu hizo biashara hazipo.

Je, nini kifanyike? Biblia kupitia Mhubiri 9:10 inasema chochote utakachopata kufanya kifanye kwa nguvu zako zote kwa sababu huko uendako hautapata nafasi ya kukifanya. Lakini Je, ni wakati sasa wa viongozi wetu wa dini kubadili maneno ya hamasa kwenye kuhimiza safari ya kwenda mbinguni? Wenzetu nasikia wanasema tukifika huko tutakabidhiwa mabikra kadhaa. Hii kiukweli ni hamasa yenye uhalisia.
Ingekuwa Mwili wa nyama unaenda Mbinguni, hivyo vyote vingekuwepo. Lakini kwa kuwa kinachoenda ni Roho, hivyo haviusiani na Roho Wala Roho Haina kazi navyo.

Ujumbe wako ni mzuri kwamba tujiandae kwa maisha ya kiroho yenye vya rohoni Mbinguni.
 
Yaani mimi kibinafsi ile nimefika Mbinguni halafu kwa mbali namuona mke wangu halali wa ndoa naye kafika Mbinguni.
Haki ya nani vile siwatanii lazima NIMTONGOZE TENA ili mapenzi yetu yasiishe. milele.
Mbinguni hakuna kuoa wala kuaoana. Kama una mke piga sana paipu ukiwa hapa duniani
 
Mimi vyote hivyo vinazidiwa na kaka mzuri, sasa sijui nae atakuwepo mbinguni?
 
Yaani mimi kibinafsi ile nimefika Mbinguni halafu kwa mbali namuona mke wangu halali wa ndoa naye kafika Mbinguni.
Haki ya nani vile siwatanii lazima NIMTONGOZE TENA ili mapenzi yetu yasiishe. milele.
Same, natamani sana iwe hivyo.
Nikifikiria kuna mwisho napata stress!
 
Back
Top Bottom