Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Nakumbuka mimi nikiwa form one na mdogo wangu grade 2 tumeshuka kwenye school bus tunatembea kuelekea nyumbani. Ghafla njiani akatokea mkaka jirani yetu akaanza niambia kwanini unanikataa huku ananipiga akinituhumu najisikia sababu sisi tunapelekwa shule na gari.

Mdogo wangu akakimbia hadi nyumbani kumwambia baba na mimi nilifanikiwa kumchomoka yule kijana nikakimbilia nyumbani kufika nalia baba akinichukua hadi nyumbani kwao yule kijana, ile tunaingia tu na yule kijana kafika kwao aiseeeeee alipigwa makofi na mshua nikajua yameisha tunaenda nyumbani.

Mara baba akasema tunaenda polisi kufika polisi nikaandika maelekezo na hivi nilikua underage ikachukuliwa defender pale kuja kumkamata yule kijana yeye alikua mkubwa tukaenda polisi alichapwa fimbo na polisi jamani baadae wakanipa fimbo na mimi nijirudishie hehehehe. Tangu siku ile hakuna kijana mtaani kwetu alitusogelea kuongea ujinga.

Nakupenda sana baba Mungu akupe maisha marefu.
A responsible dad can do anything for his child
 
Nakumbuka mimi nikiwa form one na mdogo wangu grade 2 tumeshuka kwenye school bus tunatembea kuelekea nyumbani. Ghafla njiani akatokea mkaka jirani yetu akaanza niambia kwanini unanikataa huku ananipiga akinituhumu najisikia sababu sisi tunapelekwa shule na gari.

Mdogo wangu akakimbia hadi nyumbani kumwambia baba na mimi nilifanikiwa kumchomoka yule kijana nikakimbilia nyumbani kufika nalia baba akinichukua hadi nyumbani kwao yule kijana, ile tunaingia tu na yule kijana kafika kwao aiseeeeee alipigwa makofi na mshua nikajua yameisha tunaenda nyumbani.

Mara baba akasema tunaenda polisi kufika polisi nikaandika maelekezo na hivi nilikua underage ikachukuliwa defender pale kuja kumkamata yule kijana yeye alikua mkubwa tukaenda polisi alichapwa fimbo na polisi jamani baadae wakanipa fimbo na mimi nijirudishie hehehehe. Tangu siku ile hakuna kijana mtaani kwetu alitusogelea kuongea ujinga.

Nakupenda sana baba Mungu akupe maisha marefu.
A responsible dad can do anything for his child
 
Nakumbuka kuna siku tupo shambani tunamwagilia maji miti kwa kutumia dumu (lile la lita 20).

Tunachukua maji kutoka barabarani na kuleta shambani kumwagilia, sasa mimi nikiwa na dumu nmebeba mkononi namwagilia miti, na ili miti ilikua kwa laini sasa baba akataka niaze kumwagilia maji miti ya mwisho na kuacha ile ilikuepo mwanzoni, sasa pale nikawa nafanya ukaid kidgo sabab dumu zito na yeye anataka niende nalo mbali.

Daah bas ghafla tu ilitoka tu "FATA AMRI MOJA"

Duuh nilkua mdgo hapo hapo sabab sjawah kumskia akitoa amri za kijeshi kwetu ata siku moja.
Bas mpka leo namkumbuka faza .


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ambao wazee wetu bado wapo hai.. Tunadeni kubwa angalau kuwafanyia ihsani na kuwatendea mema kabla haujafika wakati tukasema "laiti angekuwepo ningefanya .... "

Na ambao tayari wametangulia.. Tuzidi kuwaombea dua kadri tuwezavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio wazee wote, wengine WASHENZI tu wacha wavune walichopanda/walale wanapostahili shubaamit.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mm nakumbuka kipindi hiko nna kama miaka 8 hv kama sikosei..mama aliondoka na mdogo wangu wa kike kwenda kilimanjaro kula sikukuu ya Christmas..Nyumbani tukabaki mm na baba...sasa kutoka nyumbani hd kazini kwa baba ni mwendo kama wa dk 15 hv..na dk 5 hv kwa baiskeli

Basi kwa vile mm nilikiwa nimefunga shule nipo tu nyumban..baba alikuwa kila akiamka asubuh lzm atengeneze chai ndo aende kazini..ikifika mchana atarudi nyumban atanipikia chakula then anarudi kazini..ikifika jioni atarudi kazn atapika chakula na soda ananiletea(inshu hyo ilifanyika kwa wiki 3)

Aisee nikikumbuka tukio lile linanifanya ni mmiss sana mzee...RIP

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi hizo daladala sio sana tulitoka kumsindikiza mtu umbali kiasi Sasa wakati wa kurudi ilikua muda umeenda ikabidi tupite shortcut katikati ya njia tukakutana na mto umechimbika ile mbaya na mvua za elnino na daraja liliondoka peegeshwa kamnazi kembambaa...

Yaani palikua panatisha ilikua hata kutazama maji yanayopita chini nilikua siwezi kwa woga na ile mzee ananiambia pita nakushika nikagoma akaona akinibeba nitamuangusha alichofanya akavua shati lake akanibeba kwa mtindo wa mbeleko japo halikufaa chochote ikawa kama kamba tuu...

Kisha akaulalia ule mnazi na kuanza kumove kama anaukwea kutoka upande mmoja kwenda upande mwengine......yaani alichunika na watu walikua wakishangaa kitendo kile mie nilikua nikifurahi kama turudie tena na tena....

Ni miaka imepita ila Hadi Leo natabasamu nikikumbuka tukio lile


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwa mayai wewe, dingi wangu katika umri huo utaanzia wapi kumwambia akubebe??!!, atakuambia; "pumbavu, wewe ni mlemavu??, watoto wa siku hizi bure kabisa!!, tembea huko!!., mimi nilipokuwa kama wewe nilikuwa natembea km 20, kwenda km 10 na kurudi km10."

May God rest him in peace, my Father who made me who I am.
ulikuwa unaishi kijiji gani?

Hittin Blunts And Bustin Nuts
 
Mi nakumbuka baada ya kututelekeza nilikua nikienda kwa wale family friend wa zamani wakati baba yupo.nikiulizia marafiki zangu wa utotoni.unaambiwa tu ..yupo nairobi anasoma huko...ukienda huku unaambiwa yupo sekondari fulani kampala.hata levo za vyuo ni huko huko.nikawa nawaza mzee asingetutosa tungesoma vizuri.kwakuwa alikuwa na kipato kizuri.na hata ajira isingekuwa ishu ni mtu mwenye koneksheni ya kibabe sana.nikikumbuka wakati wa kuomba misaada ya ada kwa marafiki zake wakati uwezo alikuwa nao kuwazidi .machozi yalikuwa yanamwagika sana.nilijenga chuki isiyokwisha mpaka leo.kwakweli simpendi hata kidogo.yaani simpendi kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
mzee wako aliamua kuchomoa betri.huwezi jua labda aligundua wewe sio mtoto wake

Hittin Blunts And Bustin Nuts
 
Nikimuelezea ntakuwa namkosea heshima sana amefanya mengi makubwa sana kwangu

Ikitokea ukifa unazaliwa sehem nyingne basi huyu mzee aendelee kuwa baba yangu na tena na tena had tena

Baba yangu ni mtu wa kwanza kumpenda kwenye hii dunia
Usiniulize kuhusu mama hiyo ni story nyingne

Ila mzee ww ni kila kitu kwangu sina wa kufananisha nae


Sent using Jamii Forums mobile app
 
My late father my hero made me to be gentleman,wise and kind guy he made me to be who iam everything i have money,power,respect with in the society because of him reposa in pace baba nakuombea dua kila napopata nafasi some of single fathers wanaitaj heshima kuu sana shukran muanzisha uzi nimemkumbuka baba yangu😭😭😭
 
Ila MUNGU awasamehe mama zetu wamekuwa mstari wa mbele kuwafitisha baba na watoto wao na kujiweka wao kuwa ndio waliplay role kubwa sana kumbe mzee ndie mshika usukani ambae amesababisha familia kufika mbali.

Ila wengi wa akina mama huwanza kuleta ajenda za kibaguzi ili kuwafitini watoto na baba zao ili wao waweze kupewa kipaumbele......!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom