Je unajua siri hii kuhusu mafanikio

Je unajua siri hii kuhusu mafanikio

Siri ya mafanikio yako ni maamuzi tu basi usidanganywe sijui connection. Sijui freemason sijui nini. Hayo yote yanatokea baada ya kuchukua maamuzi tu. Wewe jaribu kuchukua maamuzi kwa kile unachokifikiria katika kichwa chako uone kama hizo connection na mengine hayotokufuata yenyewe.

Asanteni sana usiogope kuchukuwa maamuzi ya kutekeleza kile unachokifikiria katika kichwa chako.​
Asante sanaaaaaa nimeanza kufanyia kazi tukutane hapa December 1st 2026
 
Things change my brodah😅 kuna kupanda na kushuka unajua eeh, ukiyapatia maisha sio mbaya kujianika.. ukifulia unaomba upya connection..
Kitu kinachoomeshwa omeshwa sana mbele ya macho ya watu ninrahisi kukipoteza mana kinakuwa na maadui wengi tu.
 
Upo sahihi ,nakumbuka wakati nipo chuo bado nilikuwa nakaa nyumbani,

Nilikuwa nasoma huku nafanya biashara ndogo ndogo hvyo kiuchumi sikuwa vibaya,niliweza kujilipia ada mwenyewe na kujikimu kwa kiasi chake...

Kuna siku nimerudi nyumbani asubuhi nimepiga ugimbi haswa nipo hoi ,sasa nataka niingie msalani kujisaidia nikakuta kuna mtu ndani anaoga,maamuzi ya pombe yakanituma nikaingia chumbani kwa wazee(kwenye choo Chao)nikakata gogo fresh nikamaliza nikarudi chumbani kwangu nikalala,kumbe wao wananiona kila kitu ninachofanya mm hapo sina hili wala lile...

Nimekuja kuamkq jioni sikumbuki chochote, mama akaanza kunielezea A to Z kwa jinsi nilivyosikia aibu kesho yake nikatafuta dalali nikatafuta chumba nika nunua godoro na mashuka mawili ndoo na vitu vingine vidogo vidogo,mchana nikarudi nyumbani nikachukua begi langu nikaanza maisha mapya ya kupanga na mpk leo sijarudi nyumbani kurudisha mpira kwa golikipa...

Ni kweli ukidhamiria na ukaamua hakuna litakaloshindikana na hata ikitoke limeshindikana inakuwa ni tofauti na mtu ambae hajaamua...
 
Back
Top Bottom