Kampuni ya NALA yapata uwekezaji wa bilioni 106

Under-cover

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2023
Posts
2,211
Reaction score
3,527
Leo Julai 9, 2024 saa tatu asubuhi kwa saa New York Marekeni, Kampuni ya NALA iliyoanzishwa na Kijana Mtanzania Benjamin Fernandes, imetangazwa kwenye soko la hisa la Marekani NASDAQ kupata uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni 40 ( Tsh. Bilioni 106) uwekezaji ambao utaiwezesha kutimiza lengo lake la kukua zaidi kimataifa na kuboresha ubora na usalama wa malipo barani Afrika kwa kupita mfumo mpya wa malipo uliotengenezwa na Kampuni hiyo uitwao Rafiki.

NALA imepata uwekezaji huu kutoka kwenye Kampuni kubwa za Uwekezaji duniani kama vile Acrew Capital, DST Global, Amplo na nyinginezo ambapo itatumia uwekezaji huu kutimiza malengo yake ya kimataifa kwa kufanya vitu vikuu viwili kwa sasa ambavyo ni kuongeza huduma za kutuma na kupokea fedha nje ya Afrika na kutengeneza huduma za kibenki kwa ajili ya Wahamiaji na Watu waishio ughaibuni.

Taarifa ya NALA imesema mfumo wake mpya wa kimataifa wa malipo uitwao Rafiki unatarajiwa kutumiwa na Watu Bilioni ambapo utawahakikishia Wateja huduma za malipo zenye ubora na usalama wa kiwango cha juu, huduma nzuri za fedha za kigeni, gharama nafuu za miamala na kuwezesha biashara kutuma na kupokea malipo kwa urahisi sambamba na kuleta mapinduzi kwenye huduma za malipo barani Afrika kama yale yaliyofanywa na kampuni ya dlocal Amerika kusini pamoja na AirWallex huko barani la Asia.

NALA imeendelea kufanya vizuri zaidi kwa miezi 12 iliyopita na kushuhudia idadi ya miamala inayochakatwa kwenye NALA ikiongezeka mara 34 zaidi, idadi ya Wafanyakazi ikiongezeka kutoka watu 7 hadi 100 huku idadi ya Wateja ikifikia Watu laki 5 na kuongeza Matawi kwenye nchi 21 za Ulaya.

Benjamin akiongea na millard ayo amesema yafuatayo “Uwekezaji huu wa Bilioni 106 utatuwezesha kuongeza huduma zetu za kifedha, yaani mbali na kutoa huduma za remittances (kutuma fedha kutoka ughaibuni kwenda nyumbani Afrika) tutatoa huduma mpya za malipo za kimataifa nje ya Afrika, tutatumia hii pesa kuboresha miundombinu ya mfumo wetu mpya wa malipo (uitwao Rafiki), kuboresha ubora na uharaka wa huduma za kifedha pamoja kupunguza gharama za miamala, NALA hatushiriki tu kwenye mabadiliko ya huduma za kifedha ila sisi ndio tunafanya hayo mabadiliko" #MillardAyoUPDATES

FB_IMG_1720559089597.jpg
 
huyu kijana wa kumtumia sana. samia amshike mkono, kuna maeneo mengi tu samia hawezi kuingia ila huyu kijana anaingia. kuna marais wengi tu samia hawezi kuonana nao ila huyu kijana anaonana nao, kuna wafanyabiashara wakubwa mno na wenye uwekezaji mkubwa kijana anaonana na kunywa nao chai ila samia hawezi. ni Mtanzania, babake kazaliwa Tanga, mchungaji fernandes wa kanisa la Agape kule mbezi.

wengi wakimwangalia wanamwona kama mhindi, hapa nchini huyo ni generation ya 4 inavyosemekana, ni Mtanzania kuliko watanzania wengi sana, babu yake alikuja hapa hata kabla wangoni hawajaja hapa nchini n.k, na kote anakoenda amejitangaza Utanzania wake, serikali imshike mkono kwa kumtangaza zaidi kwasababu uwekezaji alioufanya utaitangaza Tanzania pia. haiwezekani vijana kama hawa wawe wao ndio wanajibembeleza kwenye Utanzania badala ya Tanzania kujibembeleza kwao. wamepambana kwa jasho lao, Mzee fernandes kajinyima pale haven of peace kamsomesha hadi akapata scholarship marekani, kasoma vizuri.

kwa wale tuliokuwa tunasali Agape pale mbezi, tunakumbuka alivyokaweka wakfu uchungaji kipindi fulani, na namna mzee fernandez alivyopigania hata injili ya Tanzania na kuanzisha tv za dini. Mungu ambariki. ana mkono wa Mungu na atafika mbali zaidi ya hapo hata kama serikali itakaa mbali naye. ana Mungu, ana kibali cha MUngu.
 
apo samia anaingiaje acha upumbavu sio kila kitu samia samia
 
Unahasira mkuu au kuna tatizo!?
 
Hongera sana, nafatilia huduma zako nami nitakuwa sehemu ya kutumia app yako kutuma pesa Tanzania
 
Vijana wenye akili kubwa kama hao ni mwiba kwa watawala wengi wa Afrika. Kwa mtu yoyote mwenye akili kubwa Afrika sio sehemu sahihi ya kuishi. Yeye mwenyewe sio mjinga kuweka makao makuu ya kampuni yake uko Kenya hii ni kwa sababu anajua figisu za wanasiasa wa bongo ni mabingwa wa kupenda kuvuna ambapo hawajashiriki kupanda, kampuni yake angeweka Tanzania izo bilioni 100 Mwigulu angeshazitolea macho. Vijana wa aina ya mwijaku na Lucas Mwashambwa ndio wanahitajika zaidi na watawala wa Afrika
 
Back
Top Bottom