Je unajua kinachoendelea katika siasa ya Tanzania?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,032
3,913
Kwa wale ambao hamfahamu leo nataka tuzushe mjada hapa unaoelenga zaidi kuchokoza mjadala zaidi;

Kwanza kabisa kuna Operation Maalum ya "Dethronement"ambayo inalenga kuhakikisha kwamba hakuna unpredictable and uncotrollable elements wanaingia katika mfumo wa Uongozi wa nchi.

Kitu cha Pili kinachoendelea ni "Consolidation" ya Mali pamoja na Mamlaka ya nchi ambapo mifumo ya kisheria na kikatiba na kijamii inatengenezwa chini ya uratibu wa watu wachache ambao wengine hata hawajui kama wanatumika katika kutengeneza mfumo kwa ajili ya wengine.

Kitu cha tatu kinachoendelea ni "Dis empowerment " ambapo inavyoonekana kabisa inalenga kuhakikisha kwamba ubora wa elimu,na uwepo wa fursa una didimizwa na kukandamizwa ili kuhakikisha kwamba hakutaibuka kundi au watu ambao watakuwa tayari kusimama na kupinga yanayoendelea.

Katika TREND inayoendelea ikiwamo shughuli za kisiasa ambazo zimebaki kwa Vyama vya CCM,CHADEMA na ACT huku kukiwa na Ndugu wawili kutoka mbeya kutaibuka Kundi la Tatu ambalo litakuwa a watu katika makundi yote ya vyama vya siasa pamoja na makundi mengine.

Inavoelekea kuna mawaziri,wabunge na hata watumishi waandamizi katika taasisi za serikali ambao wanatakiwa watoke katika mfumo kwa sababu wanaoneka kuvuruga hizi ajenda zinazoendelea.Kilichoafanyika ni kuhakikisha kwamba hili kundi la mawaziri na watumishi waandamizi wameachwa waumane wenyewe mpaka wamalizane kisiasa ili kutengeneza njia kwa ajili ya hao wanaotengeneza mfumo huu mpya.

Falsafa yao kwa sasa ni RAHISI "NEVER AGAIN"

Nimeandika mengi sana kwa codes rahisi sana kufungua so msione tabu kuzifungua hizi codes
 
Back
Top Bottom