Je, unafahamu sababu za computer kuzima ghafla unapoitumia?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,558
1666588729022.png


Kama wewe ni mtumiaji wa kifaa hiki, hili jambo halitakuwa geni kwako!

Changamoto hii tumekuwa tukikumbana nayo kwa kiwango kikubwa na hapo hapo tusijue nini chanzo chake. Leo hii hebu tupate ufafanuzi ni sababu zipi hupelekea kutokea kwa jambo hili.

Sababu hizi ni kama ifuatavyo;
1. Laptop kupata joto sana.
Vipo viashiria mbalimbali ambavyo hutokea kwenye mfumo mzima wa Laptop yako, ambapo hujumuisha.

(i) Feni kwenye laptop kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha, hii hujumuisha feni kushindwa kuipoza “Processor” pale laptop inapokuwa katika mfumo mzima wa kuchakata data kwenye Laptop.

(ii) Kutunza na kutumia laptop kwenye sehemu yenye joto sana, ambapo unakuta unatumia laptop kwenye sehemu yenye jua kwa kiwango kikubwa bila kutumia “Cooling Pad”.

(iii) Uchafu kwenye Laptop, kuna wakati kiwango cha Uchafu kwenye laptop kinakuwa kikubwa sana hasa kwa wale ambao hawana utaratibu wa kutofanya “Service” kitendo kinachopelekea kutengeneza mkusanyiko mkubwa kwenye “Motherboard” na hata kushindwa kupumua kwa laptop katika utendaji wa kazi.

2. Tatizo la “Hardware”.
Hasa pale ambapo utakuwa umebadilisha kifaa kikashindwa kufanya kazi kwa ufasaha kuendana na mfumo mzima wa Laptop yako. Mara nyini tatizo hilo likitokea ni vyema kufanya uchunguzi kwa kuangalia kifaa kimoja baada ya kingine kwenye Laptop yako, ili kujua kipi kinaleta hitilafu.

3. Tatizo la kukosa baadhi ya “Drivers” kwenye Laptop yako.Tatizo hili hutokea hasa kwa Laptop ambazo hutumia Window 10, Pale unapoweka window 10, hakikisha unatumia “Device Manager” kuhakikisha kama laptop yako ina “drivers”. Pia unaweza kutumia “ Window update” na “Windows Driver Verifier” Kuangalia kama laptop yako ina drivers zote muhimu.

4. Virus (Virus), kama laptop imeshambuliwa na kiwango kikubwa cha virusi huplekea kwa kiwango kikubwa laptop kuzima kabisa. Hakikisha unaweka Antivirus kwenye Laptop yako.

5. Tatizo la Betri, wakati mwingine kama betri sio mzima unapochomoa” Adapter” ghafla lazima laptop yako itazima ghafla.

6. “Adapter”/ Chaja kuwa na kiwango kidogo cha “Voltage”, ambapo hushindwa kuchaji laptop yako na kuplekea kuzima kabisa.

Credit: Cataux Computers
 
Back
Top Bottom