Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?


  • Total voters
    111
Kazi ya Waziri sio anayofanya Dr. Mwakyembe, nadhani hata scheme of work hana anajikurupukia tu. Japokuwa alikuwa mwalimu na mwalimu anaheshimu sana scheme of work lakini yeye ualimu wake haujamsaidia katika eneo hili. Hatutaki mawaziri wanaofanyakazi kwa mtindo huu. Itakuwa vurugu. Kwani mawaziri hawana job description? Kama wanayo sidhani tactic ni sehemu ya majukumu yao. Nani atatoa taarifa kwa nani? Nani ata atachanganua (analyse) taarifa ya nani? Nani atamsimamia nani? Ukishindwa kumsimamia mbwa abweke unabweka mwenyewe? Utendaji wa kutisha.
Ni homa hiyo, sio ya kuifagilia
 
[h=6]tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuwaua viongozi wa chadema.
Huku akihojisababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wwa taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana ini hasa idara ya usalama wa taifa ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.[/h]
 
1.Waliomteka ulimboka?
2.Waliomuwekea vinasa sauti dodoma Dr.slaa kwenye gesti ni nani?
3.walio mmwagia tindikali said kubenea nani?
4.walio muwekea sumu mwakyembe ni nani?
5.waliokuwa wakishuhudia machemuli na H.kiwia wakikatwa katwa mapanga ni nani?

Hayo maswali yanatosha kulituhumu jeshi la polisi kuhusika na unyanyasaji dhidi ya wapinzani wa serekali.
si hayo tu waliowauwa wachimba madini wa mahenge ni kina nani? wanaouwa majambazi bila wao kudhurika na bila uwepo wa ushahidi kuwa ni majambazi ni kina nani?

wanaoshindwa kuwakamata majambazi na kuwafikisha mbele ya sheria bali kujichukulia sheria mikononi mwao hadi wananchi wameiga ni kina nani/
 
Unajua ukishakuwa umevaa gamba huoni wala husikii uozo wowote unaolikabili Taifa na hili ndilo tatizo la Nchimbi na wenzake.. Kuwa na imani na jeshi la polisi Tanzania ni uwendawazimu.
 
Huyu kweli ni pimbi hivi hajui kuwa mwaka huu tena jeshi la polisi limeibuka kidedea kwa ulaji rushwa miongini mwa taasisi za umma hapa nchini? Tuliamini jeshi hili kwa ulaji rushwa?Inabidi huyu Dr. Love akapimwe akili.
 
Mi nasema wote yaani Dr Nchimbi na CHADEAM squared wapo sahihi, Nchimbi yupo sahihi kwa vile kila anachoagiza polisi yeye na magamba wenzie, police huwa wanafanya kama walivo elekezwa while CDM na wananchi wengine, yaani mimi na wewe tukipeleka shauri letu police kushugulikiwa huwa ni bahati nasibu, wapo pia wananchi wenzetu wengi tu waliobambikizi wa kesi na jeshi hili na sasa wapo magereza wakitumikia vifungo mbalimbali (mfano Babu Seya na wanaye) So kwa Nchimbi kuliamaini jeshi la police yupo sahihi because lifanya kile amabacho huwa analiagiza while sisi pamoja na CDM hatuwezi kuliamini jeshi kwa vile sometimes linaweza kutoa kibari cha mkutano na maandamano then wao wenyewe wanakuja na mabomu plus washa washa, tutaliamininje?
 
tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuwaua viongozi wa chadema.
Huku akihojisababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wwa taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana ini hasa idara ya usalama wa taifa ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.
Kwa hiyo ikiwa Dr.Ulimboka alikuwa mwiba ndio maana wakapanga kumuua....Aaaaaaaaaaaaaa, sasa nimemwelewa katibu mkuu kiongozi...Ikiwa utakuwa mwiba kwa serikali, basi usalama wa taifa wanakuua..... Hii njema...
 
Polisi wanaoibia wananchi wameongezeka, mauwaji yanayofanywa na polisi ni mengi mno...tutaliaminiye jeshi la polisi....
 
tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuwaua viongozi wa chadema.
Huku akihojisababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wwa taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana ini hasa idara ya usalama wa taifa ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.
Kumbe ukiwa tishio kwa wananchi unanyamazishwa (una uwawa) na serikali hii mara moja kama ilivyotaka kumnyamazisha Dr Uli.. hawa jamaa kweli wamepigwa upofu maana hata matamshi yao wanayatoa bila kuyapima na kujua kama yana madhara au la.
 
[h=6]tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuwaua viongozi wa chadema.

Huku akihoji sababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wwa taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana ini hasa idara ya usalama wa taifa ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.[/h]

Kumbe mtu akiwa tishio kwa wananchi na serikali anaweza kuuawa????
 
Kimsingi serikali inakubali kwamba huwa inaua raia wake pale inapojibu kwamba "huyo mtu anayelalamika hatuwezi kumuua kwa sababu siyo tishio kwa nchi"

Ina maana serikali ina kawaida ya kumuua mtu yeyeto inayomdhania ni "tishio kwa nchi". Nchi ni nani? Nani anayepitisha hiyo hukumu kwamba sasa fulani ni tishio? Je, huwa wanatangazia umma kwamba wamemuua fulani kwa sababu alikuwa "tishio kwa nchi"?
 
Kwako Mh. Nchimbi,
Salaam! Natumaini umzima wa afya na unaendelea vema na shughuli zako za kuiongoza Wizara Nyeti ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo Jeshi la Polisi liko chini yake. Mheshimiwa, inawezekana kabisa kuwa Dr. Slaa, Mnyika na Lema wamezusha madai kuwa kuna mpango wa kuwadhuru ambao unasukwa na Vigogo wa vyombo vya usalama. Siwezi kusema ni kweli au la mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Ila Mheshimiwa kwa kuwa tuhuma zimetolewa hadharani na wewe ukatoa kauli hadharani itakuwa vema uchunguzi ukikamilika taarifa nayo iwekwe hadharani.

Ningependa kukufahamisha kuwa wananchi walio wengi (mimi nikiwa mmoja wao) hawana imani na Jeshi la Polisi. Kuna viashiria vingi tu vya kukuonyesha kukosa imani kwa wananchi na chombo hiki muhimu ambacho kiesemwa na Katiba na sheria kuwa kina jukumu la kuwalinda raia na mali zao.

Moja ya viashiria Mheshimiwa ni kuongezeka kwa wimbi la kile kinachoitwa "raia wenye hasira kali" kutoa hukumu ya kipigo kikali na pengine hata kifo kwa watuhumiwa wa makosa ya udokozi na ukwapuaji wa mali za raia wenzao. Hujawahi kujiuliza kwanini raia wanapowakamata watuhumiwa huwa hawawapeleki Polisi na badala yake wanatoa hukumu wao wenyewe???

Kwa taarifa Mheshimiwa, wananchi walio wengi wanaona kupeleka mashauri yao polisi wakati mwingine ni sawa na kupoteza muda na hata fedha. Mara nyinigi utatakiwa kununua au kutoa fedha za jalada la kufungulia shauri lako na utatakiwa kutoa fedha au kununua karatasi za kuchukulia maelezo yako.

Hapo upelelezi haujaanza. Upelelezi ukianza utatakiwa kutoa fedha za usafiri kwa askari aliyepangiwa kufanya upelelezi wa shauri lako na wakati mwingine kuvunja shughuli zako na kuambatana nao wakati wa kile wanchokiita kumtafuta mtuhumiwa wako.

Wakati mwingine utatakiwa kutoa fedha za mawasiliano (kununulia muda wa maongezi) na posho ya kuwalipa watu wanoitwa informers wa Polisi ambao wengi wana record Mbaya katika jamii halafu upelelezi unaweza kuendelea milele hasa inapotokea mtuhumiwa naye anakuwa na uwezo wa kuwapooza wapelelezi.

Mheshimiwa, katika mazingira haya bado utasema kuwa mtu asiyeliamini Jeshi la Polisi kwa maana ya askari Polisi wanaotekeleza majukumu ya Ki-polisi ana matatizo? Ningekushauri ufanye uchunguzi uone ni mashauri mangapi yaliyofunguliwa polisi ambayo walalamikaji wameamua kumwachia Mungu matatizo yao baada ya kuona wamegeuzwa ng'ombe wa maziwa na wapelelezi wa polisi, kesi zilizotupiliwa mbali na mahakama baada ya wapelelezi kupeleka ushahidi wa kitoto kwa lengo la kutengeneza mazingira ya watuhumiwa kuachiwa huru na mahakama.


Nawasilisha hoja!

Okmnaya!

This is quite great thinking!

Nakushukuru kwa kuliona hilo. Dr. Nchimbi tatizo sawa na aliyemteua. Kunatakiwa kufanyike marekebisho makubwa ya Jeshi la polisi . We should start using own funds police reform like the one done in the public sector reforms. Lazima kwenye machakato aw kinachoitwa katiba mpya tuweke mambo Kama hayo.

We should go further including creating an independent body with binding laws which can investigate cases where police abuse individual rights . Such a body should be empowered to investigate independently cases against the police, state security . We can even allow private investigators etc etc
Kwa kesi Kama ya Ulimboka na hizo za akina Lema, Mnyika and Dr. Slaa it's a mockery of justice kumwambia aende polise wakati hana Imani nao. Ai hapenned to watch on you toube the speech by Dr. Slaa he referred to a bugging case more than three years ago in Dodoma and tidate the same police has not even conducted investigations and many others.

Nadhani pamoja nao kuwa wapinzani wana haki ya kusikilizwa na and independent body zaidi ya police. The problemI can see it is the constitutional limitations and absence of laws. Maybe you can go through the Tume business which has proved a failure.

Sijui let us exchange views. I might come back. Ila Serikali yatakiwa kuwafikiria hata wale ambao hawapendi kukubaliana.
 
Sijui watu wakiwa madarakani huchomwa sindano ya 'ganzi' ili wasigusike na mambo yanayotokea uraiani?

Nchimbi anaongelea Jeshi lipi la polisi? Kama ni Jeshi la polisi lilikuwa chini ya Mahita akisaidiwa na Zombe na baadaye kuongozwa na Mwema akisaidia na Kova basi ni vema azinduke na kutambuwa wananchi si tu hawana imani nalo bali hawataki kuona polisi. Wanahofia maisha yao wakiwaona polisi. Sasa hivi mtu ukipata simu kuwa ndugu yako yuko polisi unaanza kuwaza gharama za mambo mengine!

Ni makosa sana kwa viongozi wetu kuendelea kuimba wimbo ambao haufanani na hali halisi. Wanaonekana kuwa out of touch. Kwa kifupi ndugu Nchimbo wananchi wamechoka kuzika.
 
tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuwaua viongozi wa chadema.
Huku akihojisababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wwa taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana ini hasa idara ya usalama wa taifa ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.

Balozi Sefua ni msemaji wa Idara ya usalama wa taifa? Na kwanini hili la viongozi wa CHADEMA limemgusa Sefue na sio unyama aliofanyiwa Dr Ulimboka? Au Dr Ulimboka (kwa kutumia maneo ya Sefue) alikuwa 'tishio'? Naunganisha na kauli ya Stella Manyanya (mkuu wa mkoa - Rukwa) ya kumuita Dr Ulimboka Hitler wa Tanzania.
 
yuko sahihi.... jaribu kusema huna imani na chadema hapa JF kama hujaonekana una matatizo???

Mwamba ngoma huvutia kwake.

Mwambie Dk. Slaa huna imani na chama chake atasema una matatizo ya akili ... ndivyo nchimbi kasema.

hili jeshi kumbe ni chama!
 
Kusema huna imani na jeshi la si sawa. Ila huna imani na baadhi ya watendaji wa jeshi la polisi, lakini pia huna iman na serikali iliyowatelekeza askari poli na kuwaacha kufanys kazi katika mazingira magumu.

Kuna baadhi ya askari wanafanya kazi mpaka unakubali kazi zao, lakini wengine ni waovu. Tatizo si chombo, balli ni watu na serikali yao dhaifu

kaka walio wengi ni WAOVU na WAOGA hili wewe na GAMBA nchimbi mnalijua! wakipewa oda za kijinga na kidhalimu na mafisadi wanatekeleza sasa sisi mnatubishia nini hatuna mda wa kutafuta askar mwema 1 kati ya 100000 waovu tena wa ngaz za juu ndo waovu wananuka damu za mauaji plz achen kutuhadaa na kauli zenu za KIGAMBA GAMBA mgamba wakubwa nyie.
MWISHO WENU BADO KDOGO SANA, na sasa tunaandaa benghazi ya bongo kule kwa LEMA.
 
Viongozi wanajua kuwa wananchi hawana imani na jeshi la Polisi:
1. Polisi kuwaua wafanyabiashara wa madini na dereva wa teksi kulekule Mabwepande? -Jamaa wanatesa mitaani, victims wanaoza chini ya udongo.
2. Polisi kujaribu kumbambikia mtoto wa Mengi madawa ya kulevya ili wamkamate? -Jamaa bado anatesa kwenye kitengo.
3. Polisi kushuhudia kipigo kwa wabunge wawili wa Chadema kule Mwanza bila kutoa msaada wa haraka?
 
Salaam aleykum, Bwana Yesu asifiwe, Shaloom wana JF. Nategemea mmenikaribisha,
mimi nashangazwa na viongozi wetu katika kauli zao,1. wanajiridhisha wao kwa majibu wanayotoa au wanaamini kuwa watanzania wanawaamini! au pia hawajali jinsi watanzania wanavyoona na kuelewa?
2. Kuna polisi wema na wanaotimiza wajibu wao vyema, na wale wanaotumiwa na viongozi kutenda kinyume na haki, wao dhamiri zao zinawatumaje? haitoshi kusema wao ni wema lakini wanapewa amri ya kutenda maovu mfano kuuwa au kuumiza, nawaona pia ni wakatili na wasio na hofu ya Mungu na wataendelea hivyo hadi lini?
 
1.Waliomteka ulimboka?
2.Waliomuwekea vinasa sauti dodoma Dr.slaa kwenye gesti ni nani?
3.walio mmwagia tindikali said kubenea nani?
4.walio muwekea sumu mwakyembe ni nani?
5.waliokuwa wakishuhudia machemuli na H.kiwia wakikatwa katwa mapanga ni nani?

Hayo maswali yanatosha kulituhumu jeshi la polisi kuhusika na unyanyasaji dhidi ya wapinzani wa serekali.

umesahau walioua raia wasiokuwa na silaha jimboni kwake nani?
walioua wafanyabiashara wa madini na kuwatupa msitu wa pande nani?
wanaowabambikia kesi watu nani?
 
Back
Top Bottom