Je, umeweza kujibu swali hili maarufu? Kati ya kuku na yai nini kilitangulia?

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,553
Umewahi kujiuliza kati ya kuku na yai nini kilitangulia? Hili swali sio geni, ila umewahi kulifikiria na kutafuta jibu lake? Kwanini wenye jibu sahihi hawataki kulitoa?

1. Ni kuku kwanza, halafu yai. Kimamtiki ni sawa na ndivyo tunavyoona kila siku, kuku anataga yai.

2. Ni yai kwanza, halafu kuku. Hii nayo pia ni sahihi kimantiki, na ndivyo tunavyoona kila siku yai likitotolewa halafu kuku hutokea.

Ukiweza kujibu swali hili utajua mambo mambo mengi sana yanayotatiza ulimwengu na yanayokutatiza wewe binafsi.

Kwa mfano utajua:
a. Ulimwengu na vyote vilivyomo vilitokeaje,
b. Kwanini upo duniani,
c. Kwanini maisha yako yapo jinsi yalivyo,
d. Utaelewa pia namna ya kuanzisha chochote kile,
e. Utajua nini maana ya maisha na kwanini watu na viumbe wengine huzaliwa na kufa,
f. Kifupi, utajua majibu ya maswali yote tatanishi katika ulimwengu huu, Mungu, Shetani, uchawi, n.k.
g. Utakuwa huru.

Je, ni kuku kwanza, au ni yai kwanza? Kwanini?
 
Hakuna kitu au jambo linaloitwa "Mwanzo" au "Mwisho" kwenye huu ulimwengu.
haya maneno yote ni dhahania tu

Yaani namaanisha Kila kitu hakina mwanzo wala mwisho, bali kipo katika "Loop" yaani kinabadilika tu form au hali na kuwa kitu kingine au kinachofanana na kitu cha Awali.
 
Unataka tulijibu vipi, kidini kisela ama..

Kidini mungu kasema katika quraan aya siikumbuki, kwamba aliumba viumbe kwanza. Yai si kiumbe.

Kihuni.. kati ya mimba na binadamu nani alizanza, kama ni mimba basi yai lilianza ila kama ni mtu basi kuku ndio alianza.🤣😂
 
Umewahi kujiuliza kati ya kuku na yai nini kilitangulia? Hili swali sio geni, ila umewahi kulifikiria na kutafuta jibu lake? Kwanini wenye jibu sahihi hawataki kulitoa?

1. Ni kuku kwanza, halafu yai. Kimamtiki ni sawa na ndivyo tunavyoona kila siku, kuku anataga yai.

2. Ni yai kwanza, halafu kuku. Hii nayo pia ni sahihi kimantiki, na ndivyo tunavyoona kila siku yai likitotolewa halafu kuku hutokea.

Ukiweza kujibu swali hili utajua mambo mambo mengi sana yanayotatiza ulimwengu na yanayokutatiza wewe binafsi.

Kwa mfano utajua:
a. Ulimwengu na vyote vilivyomo vilitokeaje,
b. Kwanini upo duniani,
c. Kwanini maisha yako yapo jinsi yalivyo,
d. Utaelewa pia namna ya kuanzisha chochote kile,
e. Utajua nini maana ya maisha na kwanini watu na viumbe wengine huzaliwa na kufa,
f. Kifupi, utajua majibu ya maswali yote tatanishi katika ulimwengu huu, Mungu, Shetani, uchawi, n.k.
g. Utakuwa huru.

Je, ni kuku kwanza, au ni yai kwanza? Kwanini?
Hili swali mi huwa nalionaga la kijinga sana

Siku zote kati ya mzazi na mtoto nani anaanza kuwa na maisha/uhai?
Jibu ni mzazi....sasa kati ya kuku na yai its obvious wa kwanza ni kuku
 
Ilo swali lako lijibiwe kwa mantiki ipi? 😂 Kuna namna mbalimbali za kulijibu😀😀
Namna yoyote yenye kutosheleza uelewa wa binadamu mwenye akili nzuri na timamu.
 
Hakuna kitu au jambo linaloitwa "Mwanzo" au "Mwisho" kwenye huu ulimwengu.
haya maneno yote ni dhahania tu

Yaani namaanisha Kila kitu hakina mwanzo wala mwisho, bali kipo katika "Loop" yaani kinabadilika tu form au hali na kuwa kitu kingine au kinachofanana na kitu cha Awali.
Una point.
 
Jibu ni kwamba yai lilikuja kwanza.

Hii ni kwa sababu mayai yamekuwepo kwa mamilioni ya miaka na yametagwa na wanyama ambao hawakuwa kuku. Kuku wa kwanza, kwa maneno ya mageuzi, angeweza kuanguliwa kutoka kwa yai lililowekwa na aina tofauti kidogo ya ndege, kutokana na mabadiliko au mabadiliko ya maumbile yaliyotokea wakati wa ukuaji wa kiinitete ndani ya yai.

Kwa hiyo, yai lililoanguliwa kuku wa kwanza lilipaswa kuwepo kabla ya kuku yenyewe.

Chanzo: ChatGPT
 
Yai lifaalo kutotolewa na hatimaye "dogo" kifaranga kuja duniani hutokea tu baada ya Bw. Jogoo na Bi. Mtetea kujivinjari na kupeana mambo ya kiutu uzima. Na tena yai hilo hutamiwa na bibiye mtetea kwa siku 21, ukizingitia enzi hizo hakukuwa na teknolojia ya utotoaji kwa njia ya mashine.

Sasa katika hoja yako, ebu tufafanulie kidogo ni aina gani ya kuku yupo katika dhana yako ya utangulizi. Ni kuku KE ama ME!?
 
Hili swali mbona halina utata Tena lilishajibiwa wa kwanza ni kuku walivyofanya utafiti waligundua yai haliwezi kujileta lenyewe bila kuku na ata kwenye biblia Mungu aliumba viumbe sio mayai

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimba na binaadamu Nani? Alianza then ukipata jibu usijibu tena
 
Hili swali mimi nalionaga la kipuuzi Sana, unajua vizuri kwamba yai haliwezi kujiangua lenyewe bila kuatamiwa na kuku afu utasikia mtu anasema eti yai lilitangulia kuumbwa kabla ya kuku.

Jibu Ni rahisi Sana,kuku aliumbwa ataga yai,akakwatamia Hilo yai Kisha akaangua kifaranga.
 
Umewahi kujiuliza kati ya kuku na yai nini kilitangulia? Hili swali sio geni, ila umewahi kulifikiria na kutafuta jibu lake? Kwanini wenye jibu sahihi hawataki kulitoa?

1. Ni kuku kwanza, halafu yai. Kimamtiki ni sawa na ndivyo tunavyoona kila siku, kuku anataga yai.

2. Ni yai kwanza, halafu kuku. Hii nayo pia ni sahihi kimantiki, na ndivyo tunavyoona kila siku yai likitotolewa halafu kuku hutokea.

Ukiweza kujibu swali hili utajua mambo mambo mengi sana yanayotatiza ulimwengu na yanayokutatiza wewe binafsi.

Kwa mfano utajua:
a. Ulimwengu na vyote vilivyomo vilitokeaje,
b. Kwanini upo duniani,
c. Kwanini maisha yako yapo jinsi yalivyo,
d. Utaelewa pia namna ya kuanzisha chochote kile,
e. Utajua nini maana ya maisha na kwanini watu na viumbe wengine huzaliwa na kufa,
f. Kifupi, utajua majibu ya maswali yote tatanishi katika ulimwengu huu, Mungu, Shetani, uchawi, n.k.
g. Utakuwa huru.

Je, ni kuku kwanza, au ni yai kwanza? Kwanini?
Shahawa na binadamu nani alianza? Ukipata jibu hilo.. na swali la kuku umepata....
 
Back
Top Bottom