Jinsi ya kujibu swali la wewe ninani kwenye usaili

Nihaomedia7

Member
Jul 19, 2021
32
77
Kama ni mtafuta ajira ambaye umewahi kupata bahati ya kuitwa kwenye usaili, bila shaka swali hili sio geni. Ni swali la “wewe ni nani” ambalo mwajiri anauliza ili kufahamu taaluma, ujuzi na uzoefu wako.
Amini ninapokuambia kuwa, wala hahitaji kujua kabila na mkoa uliozaliwa. Anahitaji madini ya kung’amuliwa mchango ambao unaweza kuwa nao kwenye kazi unayoomba.
Hivi ndivyo vitu unavyotakiwa kujibu swali hilo:

Ongelea ujuzi na mafanikio yanayoendana na kazi unayoomba
Ni wazi kuwa hauwezi kufika kwenye swali hili ukiwa haujataja jina lako lakini kama ndiyo swali ulilolipata mara baada ya kuingia mlangoni, ni muhimu ukaanza na utambulisho ambao ni majina yako na elimu yako au cheo.
Tovuti ya masuala ya ajira, Resume Now imeeleza kuwa, ni muhimu kueleza historia yako kikazi na mambo uliyokuwa unajishughulisha nayo kabla ya kufika kwenye chumba hicho au eneo ulilofika.
Kama hauna, usijali. Unaweza kujitambulisha na kuelezea sifa ambazo zinaweza kukuongezea maksi kwa wanaokuhoji.
Ni muhimu kumsoma anayekuuliza maswali usoni kujua kama ni muda wa wewe kumaliza jibu lako au kama anahitaji kujua zaidi.
6078d9405ecc86aa6e30e76cce6842eb877a14a3.jpg
Usiwe mwenye stress. Tabasamu, jiamini na jieleze kimkakati. Picha| Mary Ellen Foundation.

Usiyafanye kuwa mazungumzo ya kuhusu wewe
Ni kweli umeulizwa swali linalokuhusu lakini swali hilo pia linahitaji kuambatana na maelezo ya namna gani utakuwa wa msaada kwenye kampuni ambayo unaomba kazi.
Kwa mujibu wa Programu ya masuala ya uongozi kwa wanawake ya She Lead, inashauriwa ujibu swali hili kwa ufupi lakin usisahau kuongelea mchango utakaoutoa kwenye kampuni hiyo endapo utaajiriwa.
Tovuti ya The Muse imetoa kanuni fupi ya kujibu swali hili ambayo ni “sasa + kale + yajayo”. Zungumzia unachokifanya kwa sasa na mafanikio uliyonayo, ongelea ya kale kwa kueleza wapi ulifanya kazi zamani na katika cheo gani na mwisho unachotarajia, kwanini unahitaji kazi hiyo na kwanini wewe na si wengine.
Chanzo Soma zaidi Hapa >>>>Jinsi ya kujibu swali la “wewe ni nani” katika usaili wa kazi
 
Hilo swali ukicomplicate utapata shida, unaweza kutumia hata dakika 10 kujielezea na usimalize,, jibu short uchapwe maswali mengine utambae..
 
Bondia aliyetrend sana week hii humjui mkuu?😂😂 alijitapa "Shaban kaoneka umeyakanyaga" akadundwaa. Vipi sura yake na yako vinatofautiana u private? 😂
hahahaha, tatizo me mpenzi wa movie movie, hayo maswala ya ngumi live me sio shabiki sana, Ndio nimemuona hata kwenye uzi wa mshana ule wa vichekesho, but huyo bondia amenizidi kidogo maana nimechanganya kasura ka mama kwa mbaali,🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom