Kama unajiona uko sawa, unawasha mishumaa kuombea vyeti siku nenda, siku rudi, unaona vitu vitakavyotokea na nini na nini basi sawa. Ila kuona kitu kuwa kitatokea hakiondoi uwezekano wa kuwa na msongo maana ubongo ni huo huo. Basi kila la heri kenye safari yako ya kiroho mtumishi.Ndugu, nashukuru kwa mawazo yako mazuri. Kiufupi ni kwamba, baadhi ya matukio mengi kabla hayajayokea huwa nayaona.
Mara nyingi sana huwa naomba yaniepuke ... mengine hutoweka kwa huruma za Mungu na mengine hutokea kama nilivyoyaona , lakini baadae nakuwa naelewa kwanini yamenitokea.
Suala la bafuni nililiona , na sikuelewa itakuwa wapi ; Kwasababu kila siku lazima niote ndoto za matukio ya mbele au kuwa na Visions ( Nina diary huwa naziandika kila siku ) .
Hata Yesu walidhani kuwa ana msongo wa Mawazo wakati ule, lakini ukweli ni kwamba mtu yeyote akiwa karibu na Mungu lazima Awe na Sober Mind ( Sober reflection) , aishi a Righteousness life + A Godly life katika Kristo Yesu. Hatua hii si kila mtu anaweza kukuelewa because, what people don't understand they always call names , and what they know they destroy
Ngoja awashe mshumaa uangukie kwenye cheti. Teh!!Kama unajiona uko sawa, unawasha mishumaa kuombea vyeti siku nenda, siku rudi, unaona vitu vitakavyotokea na nini na nini basi sawa. Ila kuona kitu kuwa kitatokea hakiondoi uwezekano wa kuwa na msongo maana ubongo ni huo huo. Basi kila la heri kenye safari yako ya kiroho mtumishi.
Daah still Mshukuru Mungu kwa ajili ya watu hao. Hata kama ulisoma kwa masimango, mwisho wa siku umemaliza salama. Ni wengi waliotamani kusoma kama wewe, ila hawakuweza kwa sababu moja au mbili. And make sure unawasamehe, na kwa chochote Mungu atakachokujalia, usiwasahau. Usiishi kwa kinyongo wala uchungu, wapende tu.Huu uzi umenikumbusha mbali sana!! Usiombe ukafiwa na wazazi ukiwa mdogo alafu uishi na ndugu mwenye roho mbaya na hana huruma! anaweza kukutolea maneno ambayo hayawezi kufutika ktk ubongo wako! sitasahau nikiwa kidato cha pili niliomba ada kabla sijapewa niliambiwa maneno haya(wengine wazae wengine walee) niliumia sana siku ile nililia siku zima,anyway nawashukuru walinisomesha kwa masimango ila nimetoka huko kwa nguvu za Mungu,na sasa ninaishi kwa amani na furaha nikwa na familia yangu na watoto wangu.
Asante NDUGU; kama umesoma maelezo yangu vizuri, lengo sio kuombea vyeti.Kama unajiona uko sawa, unawasha mishumaa kuombea vyeti siku nenda, siku rudi, unaona vitu vitakavyotokea na nini na nini basi sawa. Ila kuona kitu kuwa kitatokea hakiondoi uwezekano wa kuwa na msongo maana ubongo ni huo huo. Basi kila la heri kenye safari yako ya kiroho mtumishi.
hahahaaa.....Ngoja awashe mshumaa uangukie kwenye cheti. Teh!!
Baada ya kujifunza mambo ya ufalme wa Mungu; Nimegundua vitu vingi sana, na vyeti vyangu naviona vya kawaida sana.Ngoja awashe mshumaa uangukie kwenye cheti. Teh!!
Vanity possessions.hahahaaa.....
Hayo yote uliyoyaandika , ndio nayapitia sasa. Tena yamekuwa kwa muda mrefu sana.
Ilifika mahala nikaenda SCOAN Nigeria kwa PTB Joshua kwa njia ya bara bara ( nilitumia siku 76 kufika)
Nimekuwa kiroho sana. But matatizo yapo pale pale. Na yanazidi kuongezeka mpaka kukimbiwa na watu wa karibu kabisa, uliowasomesha na kuwainua juu.
Wakwe kukuona kama mwehu, mke kukuona hufai , na kuudharau Wokovu wako.
Mara waseme sitaki Kazi, na kwamba nachagua Kazi. Wakwe wanamsisitiza mke wangu aachane na Mimi kuwa nampotezea muda, sina Kazi.
Nakuwa karibu sana na Mungu kila mara. Na ninafunga na kuomba kila mara.
Hii ni sehemu ambayo naitumia kusali mchana na Usiku..., asubuhi mchana jioni.
Usiku kabla ya saa 6 , Then saa 7-8 , na saa 9-10.
Nimetandaza vyeti vyangu vyote kuanzia chini hadi Postgraduate, na mahitaji ya watu wengine.
Natumia muda kuwaombea maadui
Me too ulishawahi kupitia lakini?aisee hali hyo ni mbaya vibaya mno!!! ukitaka kuchomoka ni MUNGU tu ndo atkuchomoa kwa njia zozote.
Usisubiri kuajiriwa fanya shughuli zako mwenyewe maana ajira ni chache watu wengi.Elfu 30 inakutosha kabisa kwa mtaji wa kutembeza njegere na utatoka.Usisubiri kupewa bora kutafuta.mimi bado napitia sijaweza kuchomoka kwenye tatizo la ajira
Hadithia tu mkuu watu tujifunze maana naamini hadi umeandika hii leo haupo kwenye ugumu uliopitia awali.Kuna watu wamelala juu ya miti na leo ni matajiri.Maisha niliyopitia mimi nikiamua kuhadithia hapa wote mtamwaga machozi.
Inaweza kuwa yuko sahihi! Unajua duniani kuna mambo mengi sana mengine ni ya ajabu sana! Baba yangu mkubwa ambaye ni "Role model" wangu kwa masuala ya imani, alifanana na huyu kwa kiasi fulani. Alipenda kusema "kama imempendeza Mungu yeye kupitia mateso,mimi inanihusu nini? " Hakupenda nisikitike kwa yeye kuteseka na magonjwa yasiyopona! Tangu napata akili yeye anaumwa tu, mpaka nafika Sekondari bado anaumwa tu! Lakini ajabu aliamini kuwa kuteseka kule ilikua ni mpango wa Mungu na alishukuru kwa ajili hiyo! Baadae sana nilielewa kwamba utukufu wa Mungu wakati mwingine huja kwa namna za ajabu! Kwamba kuna watu Mungu huwapa mateso ili jambo Fulani liwe!Kama unajiona uko sawa, unawasha mishumaa kuombea vyeti siku nenda, siku rudi, unaona vitu vitakavyotokea na nini na nini basi sawa. Ila kuona kitu kuwa kitatokea hakiondoi uwezekano wa kuwa na msongo maana ubongo ni huo huo. Basi kila la heri kenye safari yako ya kiroho mtumishi.
nami pia kweli napita kwenye hali ngumu! mimi naishi karbu na dada yangu, hali ilikuwa mbaya sana siku moja ikabidi wife aende kwa wazazi kuchukua mahindi nikabaki na mtoto, siku hiyo sina hata kumi nikamwomba dada yangu ikifika jioni anisaidie kumwekea mtoto wangu maji ya kuoga! akanijibu sawa na nikampa nguo za mtoto za kubadilisha! huwezi amini siku hiyo nikaenda kutafuta chochote mjini nikachelewa kurudi nikamkuta dogo kalala! asubuhi nikamuuliza jana aunt alikuwekea maji ya kuoga! dogo akasema aliniambia baba ako kasahau kukuachia taulo na sabuni! jamani iliniuma sana!Hapa nina maanisha kufirisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku kutengwa na ndugu. Kukosa kazi muda mrefu, kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba/mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uongo
kudharauliwa na mambo kama hayo.
Je uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?
Nimefiwa na wazazi nikiwa dalasa la nne na mdogo wangu la kwanza, mali zote zilipotelea mikononi mwa ndugu za baba, kwa kweli ni long story , ila nisicho kisahau mwaka 2000 nilikuwa naishi na wapwa zangu pamoja na shangazi, siku moja mpwa ana muuliza mama yake ambaye ni shangazi yangu, hivi mama kama huyu mtoto wa kaka yako angekuwa binti mpaka sasa angekuwa kesha kuletea wajukuu wangapi ?shangazi akajibu kama wawili hivi .yaani mimi nilikua mzigo mzito kwao, najaribu kusahau haya maneno ila nashindwa, nashukuru Mungu nina mke na watoto wawiliHuu uzi umenikumbusha mbali sana!! Usiombe ukafiwa na wazazi ukiwa mdogo alafu uishi na ndugu mwenye roho mbaya na hana huruma! anaweza kukutolea maneno ambayo hayawezi kufutika ktk ubongo wako! sitasahau nikiwa kidato cha pili niliomba ada kabla sijapewa niliambiwa maneno haya(wengine wazae wengine walee) niliumia sana siku ile nililia siku zima,anyway nawashukuru walinisomesha kwa masimango ila nimetoka huko kwa nguvu za Mungu,na sasa ninaishi kwa amani na furaha nikwa na familia yangu na watoto wangu.