Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Ni kweli mtumishi shemkunde ukijaribu kusoma katika matthew 26:36, na 26: 42 .inaonyesha ni jinsi gani Yesu alivyo kuwa kwenye wakati mgumu, alishindwa kabisa, alikuwa anajua nini kilicho mbele yake, Alijua nini uchungu wa majaribu ndo maana kwenye Matthew 26:41 akasema Kesheni mwombe msije ingia majaribuni. Akasema kuwa mara nyingi roho ya mwanadamu inaweza kuvumilia katika majaribu, lakini mwili katika hali ya kibinadamu ni vigumu sana kuvumila majaribu " roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu".
 
Hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea mkuu,naamini unakopita sasa yatakufanya kua imara zaidi...
Amina dada Valentina napenda sana kuangalia mfano wa Ayubu, Mungu aliangalia Maisha ya Ayubu akaamua kumfanya kama case study kumuonyesha shetani jinsi gani Ayubu alivyo kuwa mcha Mungu. Je sisi wa leo tuko teyari kuwa case study ya Mungu ili aweze kujichukulia utukufu kupitia sisi? Katika kitabu cha Ayubu 1:1 inasema kuwa Ayubu alikuwa Mkamilifu, mwelekevu, mcha Mungu na aliepuka uovu. Je sisi leo tunafiti katika wasifu wa Ayubu? Mungu wa Mbinguini aturehemu.
 
Ndugu, nashukuru sana kwa maelezo yako. Kiufupi, sio kweli kwamba muda wote naomba kwa ajili ya Kazi. Ukweli ni kwamba, toka nimeelewa siri za ufalme wa Mungu hata hamu ya kuajiriwa sina. ( Vyeti huwa naviweka tu mbele za Mungu ili mapenzi yake yatimizwe)

Mara nyingi huwa naomba kwa Rehema za Mungu, Anionyeshe ufalme wake, Anisamehe Makosa yangu, Anipe nguvu na Mamlaka za kufanya vitu hapa Duniani kama huko Mbinguni kwa ajili ya utukufu wake katika Kristo Yesu.

Ndugu, nielewavyo mimi, Mungu wetu ni mwema sana; Yeye yupo tayari kumsamehe Mwanadamu yeyote aliyetayari kuzifuata njia zake katika roho na kweli.

Ni kweli tunatakiwa kupatana na watu + kuishi nao vizuri. Kuna watu kama wakina Paul, walikua wakiwatoa machozi watu wengi sana. Mungu hafanyi Kazi zake kama wanadamu.

Yesu alidhaniwa kuwa kalaaniwa, kafungwa, katupiwa mikosi, n.k ; hivyo hivyo hata kwa kina ayubu na wengine.

Binafsi nafahamu kuwa , tunaishi katika Ulimwengu wa Uovu. Na ili tuweze kuushinda ni lazima kwanza tuutafute Ulimwengu wa Mema na Elimu yake yote. Kwahiyo basi ili tuweze kuyavuka mabaya ni lazima tujiandae ku - suffer, kuwa rejected, kuuliwa na kuwa resurrected kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Mtu yeyote ambae kaamua kweli kuwa karibu na Mungu lazima awe na mind set hiyo.

Kwahiyo basi ninayopitia ni sahihi kabisa mbele za Mungu , na ninafarijika sana kuona ananiongoza katika njia zake, sio kwenye njia za Uovu.

I mean, ningeweza kwenda kwa waganga au kuwa mharifu badala yake.

#GodKnowsTheBest
 
 
Nina IMANI utafanikiwa ili iwe funso kwa wengine....
DHAHABU lazima ipite motoni
Shukran
Nami pia nina amini hivyo. Let the will of God be done, in Jesus Christ Name. Amen & Shalom
 
Nina Vita kubwa sana katika Ulimwengu wa Roho, kwasababu shetani na majeshi yake yote wananifahamu vizuri sana , that I am a noble person ( A righteous branch and the repairer of the broken walls) ; Naelewa kuwa wanaumiza vichwa sana jinsi ya kunimaliza kwa muda mrefu wameshindwa.

Wakati nazaliwa, nilizaliwa nikatoka na chupa ya uzazi kama mnyama; na hata baada ya kuipasua chupa wakanikuta kondo la uzazi limeniviringa mara tatu shingoni.

Nikiwa na 3 years, niligundulika kuwa ni bubu, nikakatwa karimi.

Baadae nikapata mke mwenye HIV+ na nimeishi nae kwa zaidi ya 8 years bila kupata maambukizi wala watoto wangu kupata maambukizi. What a mighty God.

So nina elewa kuwa Mwili wangu sio wa kawaida, kwasababu ya kuepuka vifo vingi sana. Niliwahi kutekwa na Magaidi zaidi ya mara 2 na hawakuweza kunifanya kitu.

I know the truth, wa haya yote. Sio kwa nguvu zangu.
 
Kila jambo na wakati wake.....
 
Tumshukuru mungu kwa kila pitio tupitalo..,aidha kwa bahati mbaya au kwa makusudi yetu.,tumshukuru na kutoa sadaka ya shukrani kila inapobidi
 
Ukimya nao ni mbaya sana
 
Kwann ukiwa katika hali ngumu watu wansajiweka mbal nawe? na wanajisogeza kwa yule alie vizuri kiuchumi,kimaisha etc..
Binaadam tutaacha lini huu unafki?
Mi nshaapa hakyamama siku mtu anikute nashine mwenye pesa asijisogeze kwangu...Sitaki marafiki
watu wengi ndo wenye tabia hizi haswa watu baki (marafiki) ni wanafiki hatari
 
Hili nalo unatakiwa ulitazame kwa macho maneno...,
 
Your testimony is beyond imagination. Mungu anakusudi kubwa juu yako.
 
That's Bravoo Roger
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…