Je, tunahitaji Vazi la Taifa?

Mimi naona tuachane na hili suala, miaka 50 imepita tumechelewa ni wakati muafaka kuangalia zaidi maendeleo ya kiuchumi! watu bado maskini sana, maliasili za taifa zinaibwa, siasa inapoteza pesa nyingi wananchi wanaumia na kupanda kwa vyakula, mafuta n.k.
Hili vazi halina tija yoyote, labda kama kuna great-thinker anieleweshe, ukiangalia sehemu nyingi mavazi wanayoyaita vazi la taifa ni vazi linalotumika na kabila fulani kubwa, hivyo tuangalie sana kukuza uchumi.
Na ukisema tutumie Suti n.k haya mavazi tumeyarithi tu, mfano suti zimeanzia ulaya na marekani, kuna watu wanaofata mlengo fulani watasema tuvae suti, lakini wengine watakuambia tuvae msuli na wengine watakwambia lazima tufate haki za binaada, tutembee na vimini na blauzi fupifupi, kwa hiyo labda kama ni lazima saaana tuwe na hilo vazi, tunaweza kuwa na kitambaa fulani ambacho ni vyema kingezalishwa/kutengenezwa hapahapa nyumbani kila mtu ashone anavyojua ikiwa kimini au suti, hijabu , nikaab n.k
 
Nina uhakika tutakuja kuishia kwenye bendera ya Taifa, yani rangi za bendera, ngoja kwanza tutumie mahela, hayana kazi.

Niko very pessimistic na hii issue, naomba mnisamehe, kwani sioni jinsi waTanzania, bara na visiwani tulivyo na culture tofauti, tupate VAZI moja, ambalo sio rangi za bendera ya Tanzania.

Huu usiwe mkakati wa kutafuta vazi, kama ningekuwa mie ningehamasisha tu wazalendo wavae kuendana na bendera yetu, au viongozi wazidishe kuivaa wakati wa shughuli za kitaifa na kimataifa.

Designers watakuja na vitambaa na trends kuendana na muda na ocassions, umri shughuli nk.

Anyway nadhani ni mtazamo zaidi, na iko mitazamo ya aina nyingi
 
Hii mijadala inaletwa na uvivu wetu tu wa kupenda kutumia tekinolojia, mimi nime-gugo kidogo tu, tayari nina opshenz mbili tatu

short.jpg very short.jpg funny clothes.jpg

Mimi sioni haja ya mijadala, ni suala la kuingia kwenye mtandao na kuchagua. Mbona bei ya umeme haikujadiliwa kwenye runinga?

Tumeshindwa Timu ya Taifa, sasa tunataka vazi la Taifa.
 
hapa kazi ipo, Ndugu zangu kwa wabunifu tulionao hapa bongo sioni muelekeo wowote wa kupatikana vazi la Taifa labda kwa hicho kitambaa. Na endapo hakutakuwa na mshono wa aina moja kama ilivyo kwa wa Nigeria, malaysia, scotland, japan, china, india na kwingineko, basi sidhani kama kutakuwa na mantiki yoyote ya hicho kitambaa kuwa cha Taifa. Nadhani kinachomtambulisha mtu zaidi ni mshono wa vazi na sio kitambaa, Mfano, sketi wanazovaa waskotland kitambaa chake ni mithiri ya lubega za kimasai, sasa je, kufanana kwa aina ya kitambaa kati ya wamasai na hawa jamaa inawafanya wamasai waonekane kama waskotland?, jibu nadhani ni hapana, wapo tofauti coz ya aina ya kushona............... Ndugu zangu, mm nadhani pia hawa wadau waliopo kwenye huu mchakato wapo kiwestern zaidi...............Mapendekezo yangu mimi, nadhani tusipoteze muda zaidi wa kuhangaika kutafuta kitu ambacho mwisho wa siku hakitatufoutisha sisi na watu wa magharibi, ni bora tuchukue vazi la kimasai (lubega na nginyara) na kuliboresha kidogo na kisha kulitambulisha kama vazi rasmi la Taifa, najua wamasai wapo hapa Tz na kenya, lkn Tz ndio wapo wengi zaidi. Nadhani hata hawa wenzetu wenye mavazi yao ya Taifa, ukichunguza kwa undani unaweza kuta mavazi yao yana asili ya kabila fulani huko kwao. Vuta picha hii, upo sehemu unaangalia Bunge kupitia Tv, unaona wabunge wote wametupia modern lubega, hv unadhani kutakuwa na muonekano gani ndani ya Bunge? huku zito, mbowe, mdee, lowasa, pinda, cheyo, na wengineo wote wapo ndani ya lubega na bila kumsahau babu Wasira a.k.a. Tyson etii nae katupia lubega yake............... Huu ni mtazamo wangu tu
 
Mimi naona tuachane na hili suala, miaka 50 imepita tumechelewa ni wakati muafaka kuangalia zaidi maendeleo ya kiuchumi! watu bado maskini sana, maliasili za taifa zinaibwa, siasa inapoteza pesa nyingi wananchi wanaumia na kupanda kwa vyakula, mafuta n.k.
Hili vazi halina tija yoyote, labda kama kuna great-thinker anieleweshe, ukiangalia sehemu nyingi mavazi wanayoyaita vazi la taifa ni vazi linalotumika na kabila fulani kubwa, hivyo tuangalie sana kukuza uchumi.
Na ukisema tutumie Suti n.k haya mavazi tumeyarithi tu, mfano suti zimeanzia ulaya na marekani, kuna watu wanaofata mlengo fulani watasema tuvae suti, lakini wengine watakuambia tuvae msuli na wengine watakwambia lazima tufate haki za binaada, tutembee na vimini na blauzi fupifupi, kwa hiyo labda kama ni lazima saaana tuwe na hilo vazi, tunaweza kuwa na kitambaa fulani ambacho ni vyema kingezalishwa/kutengenezwa hapahapa nyumbani kila mtu ashone anavyojua ikiwa kimini au suti, hijabu , nikaab n.k

ikiruhusiwa hali ikawa hivi kila mtu akaamua ashone anavyotaka..basi vazi hili/kitambaa hiki kitakua cha aibu sana, kwani tutegemee milegezo maalufu kama kata k za kitambaa hiki,bila kusaau vimini vya ajabuajabu sana.
 
Hii mijadala inaletwa na uvivu wetu tu wa kupenda kutumia tekinolojia, mimi nime-gugo kidogo tu, tayari nina opshenz mbili tatu

View attachment 45698 View attachment 45699 View attachment 45700

Mimi sioni haja ya mijadala, ni suala la kuingia kwenye mtandao na kuchagua. Mbona bei ya umeme haikujadiliwa kwenye runinga?

Tumeshindwa Timu ya Taifa, sasa tunataka vazi la Taifa.

hilo la vazi la chini zuri lakini rangi yake sijui kama itakubalika kwa wengi..itaitaji mjadala mwingine wa kitaifa.
 
Nina uhakika tutakuja kuishia kwenye bendera ya Taifa, yani rangi za bendera, ngoja kwanza tutumie mahela, hayana kazi.

Niko very pessimistic na hii issue, naomba mnisamehe, kwani sioni jinsi waTanzania, bara na visiwani tulivyo na culture tofauti, tupate VAZI moja, ambalo sio rangi za bendera ya Tanzania.

Huu usiwe mkakati wa kutafuta vazi, kama ningekuwa mie ningehamasisha tu wazalendo wavae kuendana na bendera yetu, au viongozi wazidishe kuivaa wakati wa shughuli za kitaifa na kimataifa.

Designers watakuja na vitambaa na trends kuendana na muda na ocassions, umri shughuli nk.

Anyway nadhani ni mtazamo zaidi, na iko mitazamo ya aina nyingi

naambiwa hata jiana TANZANIA lilipatika kwa mfumo kama huu,waliokuwepo au wenye uelewa katika hili watujuze.
 
Tuvae kimasai na kimwambao zaidi maana tutaleta vurugu mechi, vazi la taifa la kiasili au modern? iwe kama kimasai but with kaniki na shanga walizotuletea waarabu
 
vazi my arse-nal!!!
halafu tukishakuwa na vazi ndo inakuwaje sasa........
 
Nimekua nikishangazwa na mwenendo mzima wa kupata VAZI LA TAIFA..
Wahusika wakuu wa mchakato huu, kwa nyakati tofauti nimewasikia wakiongea..mara kitambaa kiwe hivi,kiwe cha rangi gani,kiwe kitambaa cha suti n.k
kibaya zaidi nimewasikia wakisema eti..kitambaa hicho kitakuwa na ubora tofauti kulingana na hadhi ya mvaaji..wakitolea mfano wabunge, eti kitambaa chao kitakua na quality tofauti pia wao wanaweza kuchagua suti waipendayo kutokana na kitambaa hicho..
Kwa ujumla mawazo yao yanajikita kwenye kitambaa na ubora wa kitambaa hicho.
Sasa wadau magreat-thinker wa jf..naomba tujadili swala hili kwa pamoja "tunataka vazi la taifa au kitambaa cha taifa" nawasilisha.

Kwa source yako ni wahusika...
Hata hivyo sikubaliani na wewe... Mi niliwahi kusuggest waende mikoa mbalimbali na kutafiti vitambaa au mavazi ya asili wanayoyatumia.. Mfano ya ngozi za wanyama,ama Wahaya wana vitambaa vya asili vinatengenezwa kwa magome ya mti wa aina fulani,Wahaya watanisaidia.. Pengine,kamati inaweza kujua ifanyeje juu ya vitambaa mbalimbali itakavyopata,maana na Hassanali yumo.
Baada ya hapo ndiyo vazi sasa dizaini yake kwa wanaume na wanawake.. Na lazima tukubali kuhusisha wabunifu wa mitindo,na ndiyo maana mavazi yenye kutambulisha utaifa huwa ghali.. Angalia Nigeria na India,hata Eritrea. Na huwa hayavaliwi mara kwa mara. Ni kitu cha heshima ya hali ya juu..
Nawasilisha..
 
Mtu anaejua nchi yenye vazi moja, au mawili official atueleze hapa mfano wake,
mimi najua nchi kama China ina mavazi mengi sana, kuendana na makabila yake au ukanda,
mchi kama Marekani, Canada, ni nguo yoyte including milegezo, mradi iwe na rangi za bendera,
manake kama nawakilisha Tanzania katika competition ya maDJ, nitavaa nini?
kama nawakilisha Watz katika umiss, nivae Tenge la mikono mikubwa? hata kidogo, hebu niambie mimi ambaye sitaki kabisa kuchanganywa na wamasai, ni mtanzania halisi nawapenda wamasai, lakini sitaki kuvaa kimasai kwani mimi si mmasai, ni mtanzania
 
kumbe ndio maana wabunge wanademand vazi lao la heshima,kwani hawawezi kuvaa vazi la aina moja na madj wapiga milegezo..!
 
Tuvae kimasai na kimwambao zaidi maana tutaleta vurugu mechi, vazi la taifa la kiasili au modern? iwe kama kimasai but with kaniki na shanga walizotuletea waarabu

pigia kura haya mavazi pia hakikisha unawashawishi wataka suti wa mjengoni.
 
mkuu..natanguliza heshima.lakini yaani kuweka matabaka yaliyopitiliza na mapya..ya kwamba ubora utofautiane? Kama hali ndio hii kule kwetu kishogo kijijini ndani watapewa vitambaa vya aina gani?

Kumbuka vitambaa havitolewi bure vitakuwa vinauzwa,kwahiyo ni hela yako tu,sasa kama watanzania wote tupo vizuri tutanunua quality ya juu,vinginevyo ni sawa tu viwepo vya style zote.
 
Kwa source yako ni wahusika...
Hata hivyo sikubaliani na wewe... Mi niliwahi kusuggest waende mikoa mbalimbali na kutafiti vitambaa au mavazi ya asili wanayoyatumia.. Mfano ya ngozi za wanyama,ama Wahaya wana vitambaa vya asili vinatengenezwa kwa magome ya mti wa aina fulani,Wahaya watanisaidia.. Pengine,kamati inaweza kujua ifanyeje juu ya vitambaa mbalimbali itakavyopata,maana na Hassanali yumo.
Baada ya hapo ndiyo vazi sasa dizaini yake kwa wanaume na wanawake.. Na lazima tukubali kuhusisha wabunifu wa mitindo,na ndiyo maana mavazi yenye kutambulisha utaifa huwa ghali.. Angalia Nigeria na India,hata Eritrea. Na huwa hayavaliwi mara kwa mara. Ni kitu cha heshima ya hali ya juu..
Nawasilisha..

tupe uzoefu wako kuhusu India n.k, wao mavazi yao yanatofautiana kulingana na hadhi? Pia kuhusu hayo magome ya miti kutoka bukoba hasahasa kiziba bado wana elimu hii..yatakubalika kwa hawa vijana wa mjini na hawa wawakilishi wetu(viongozi wapenda suti)? Pia hawa wadau watatumia mria mfumo wa kutuma meseji bure kupendekeza vazi/kitambaa..sasa mimi nina shaka kama waTanzania wa vijijini watashiriki kikamilifu..
 
Back
Top Bottom