Je tukubaliane na kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaaniwa?

Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari kwa nini nchi za kiafrika hasa zinazokaliwa na watu wengi wakiwa na ngozi nyeusi tuna matatizo kila kona japokuwa tuna rasilimali nyingi sana zinazoweza kutufanya tuwe matajiri wa kutupwa, mfano Tanzania na madini lakini hamna tunachofanya wakati Afrika kusini imejengwa na dhahabu za J,burg, DRC na utajiri lukuki lakini ona wanavyohangaika.

Aidha, ukiangalia mikataba tunayoingia utadhani Karl Peters na chief Mangungo enzi zile za harakati ya wajerumani kuipata Tanganyika kama koloni lao. Sasa najiuliza au kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaanika ni kweli? Naomba michango yenu waheshimiwa.

Haijalaaniwa bali ni tamaduni tu za jamii ya kiafrica
 
Nilikuwa na mawazo kama yako, mimi nasoma Archaeology. Ila ujue kuwa. Waisraeli wa kale walikuwa ni weusi/brown, wamisri walikuwa ni weusi/brown, Yesu alikuwa Brown coloured.

Aliyelaaniwa alikuwa ni Canaan na sio Ham, Ham alikuwa na watoto watatu, Canaana (aliishi kanaan), misrata (aliishi Misri), na Kush (aliishi Ethiopia). Kush ndie baba wa waafrika wa sasa. Aliyelaaniwa ni Canaan na sio Kush, Misrata au baba yao Ham.

Mtu mweusi ana nafasi kubwa katika historia za kidini, uchumi, sayansi, .

Tatizo dini, siasa, biashara, ubaguzi n.k vinatumika kumshusha mwafrika. Mfano movies za sasa hasa za kidini zinaweka wazungu wakati hakuna ushahidi wa Kiakeolojia kuwa walikuwa wazungu ila kuna picha za zamani sana zinawaonyesha brownskinned.

Jinsi sayansi inavyoendelea kuufumbua ulimwengu tunakuja kujua kuwa Afrika ndio source of humankind (Eden Garden), watu wote wametokea Africa, waafrica wa kale walikuwa Civillized n.k.

mkuu apollo yesu alikuwa brown umemuona wapi katika TV/umesoma mahali?
 
Wachangiaji wengi mna mawazo mazuri lakini kuonyesha jinsi hatuna akili naamini kati ya wachangiaji kuna ambao wanarubuniwa na kanga na t-shirt za ccm.hapa ndipo inaonekana jinsi tulivyo mbumbumbu yaani hatowanishi maisha yetu na mustakabali wa nchi....

bado si kosa lao,kwani wametayarishwa kuwa hivyo, kutohoji kutosema no, kutokuwa wadadisi toka walipokuwa wadogo, katika ngazi ya familia,shuleni, katika dini na kwa kupitia siasa chafu.
wakati mwingine njaaa mkuu inawasumbua watu sukari ya robo kilo anaona nitaikosaje hii ngoja nichukue mie
 
Hatujalaaniwa...nadhani kuna jambo la kulitazama sana 'elimu' tunayopata haitusaidii au inatuandaa kuwa watumwa... Africa ni fedheha kijana msomi kurudi kijijini (kunako rasilimali) na wengi kuishia mijini kutafuta utajiri- ufisadi...kila mtu fisadi tumekwama..wageni wanahangaika na maliasili zetu...turudishe degree zetu mashambani changes ni lazima..

kuishia mijini katika nyumba za kupanga mlo shida kazi shida mishahara haieleweki lakini tupo tu
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari kwa nini nchi za kiafrika hasa zinazokaliwa na watu wengi wakiwa na ngozi nyeusi tuna matatizo kila kona japokuwa tuna rasilimali nyingi sana zinazoweza kutufanya tuwe matajiri wa kutupwa, mfano Tanzania na madini lakini hamna tunachofanya wakati Afrika kusini imejengwa na dhahabu za J,burg, DRC na utajiri lukuki lakini ona wanavyohangaika.

Aidha, ukiangalia mikataba tunayoingia utadhani Karl Peters na chief Mangungo enzi zile za harakati ya wajerumani kuipata Tanganyika kama koloni lao. Sasa najiuliza au kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaanika ni kweli? Naomba michango yenu waheshimiwa.

Kulaaniwa kwa lipi mkuu? Naamini ni mifumo tu na viongozi wengi wa Ki- Afrika kutokuwa makini.
 
mkuu apollo yesu alikuwa brown umemuona wapi katika TV/umesoma mahali?

Sio nimeona katika TV, Mimi naamini Ethiopia Orthodox church, kanisa la kwanza la kikristu hata kabla ya Roma na huwa tangu kale hawatumii michoro ya kisasa, wao wanamichoro ya kale sana hata kabla ya michoro ya kina Leonardo Da Vinci. Pia DNA na ancient documents za zamani, pia wana wa israeli walikuwa ni brownskinned kama wa egypt na kama unasoma bible umeambiwa Iyesus alikuwa na Nyayo za rangi ya nyasi zilizochomwa. Open ure mind kutoka kwenye mental slave.

Sasa hivi kuna project mbalimbali za kufufua siri na ukweli uliofichwa kutokana na ubaaguzi wa kale wa zamani, azungu walianza kwa kudanganya kuwa wamisri ni weupe, then sasa hivi ukweli unajionyesha na ushahidi wa kusema kuwa walikuwa ni weusi upo, na sasa hivi wana akiolojia wengi tunaamini waisraeli wa kale walikuwa wanafanana na wamisri.

Yesu kuchorwa mweupe ni kutokana na sababu nyingi sana. Nyingine za kimakusudi na nyingine za bahati mbaya.

HOLLYWOOD NI WEAPON INAYOTUMIKA HIVI SASA KUPOTOSHA JAMII.
 
Sio nimeona katika TV, Mimi naamini Ethiopia Orthodox church, kanisa la kwanza la kikristu hata kabla ya Roma na huwa tangu kale hawatumii michoro ya kisasa, wao wanamichoro ya kale sana hata kabla ya michoro ya kina Leonardo Da Vinci. Pia DNA na ancient documents za zamani, pia wana wa israeli walikuwa ni brownskinned kama wa egypt na kama unasoma bible umeambiwa Iyesus alikuwa na Nyayo za rangi ya nyasi zilizochomwa. Open ure mind kutoka kwenye mental slave.

Sasa hivi kuna project mbalimbali za kufufua siri na ukweli uliofichwa kutokana na ubaaguzi wa kale wa zamani, azungu walianza kwa kudanganya kuwa wamisri ni weupe, then sasa hivi ukweli unajionyesha na ushahidi wa kusema kuwa walikuwa ni weusi upo, na sasa hiviwana akiolojia wengi tunaamini waisraeli wa kale walikuwa wanafanana na wamisri.

Yesu kuchorwa mweupe ni kutokana na sababu nyingi sana. Nyingine za kimakusudi na nyingine za bahati mbaya.

HOLLYWOOD NI WEAPON INAYOTUMIKA HIVI SASA KUPOTOSHA JAMII.

mkuu apolo, mimi sijabisha wala sitaki kubisha kuwa yesu ni mweupe au mweusi wasiwasi wangu ni chanzo cha hao waodai ni mweupe au mweusi, katika bold ya kwanza utakuwa umesoma mahali ni kweli umesoma hayo ya orthodox sasa unaamini kwa kiasi gani ukweli wa hicho ilichosoma na kufanya usiiamini kwa mengine uliyoyasoma kuwa alikuwa mweupe?

katika bold ya pili bible ipi uliyosoma? na unaaini yote yaliyoandikwa katika hizo bible kwa kiasi gani?
katika bold ya tatu project hizi zinafanywa na nani kwa lengo gani je zinafufua siri au kuzidi kupoteza watu? maana project za siku hizi zinafanywa ukweli unawekwa kwingine uongo unawekwa hadharani mfano mzuri ni maproject mengi ya UN kuhusu maendeleo ya africa na mafanikio na magonjwa mbalimbali ukiwa umebahatika kushiriki katika tafiti au kufanya kazi na makampuni ya utafiti utajua ukweli wa tafiti nyingi na kila tafiti ina lengo la nje na ndani(mficho)
najaribu tu kuwa mdadisi dont take it negative

kuhusu hollywood nakubaliana na wewe 100% kuwa inapotosha jamii na hayo pia yanafanywa kwa malengo maaalumu, hollywood is more complex than we know it.
 
Sio nimeona katika TV, Mimi naamini Ethiopia Orthodox church, kanisa la kwanza la kikristu hata kabla ya Roma na huwa tangu kale hawatumii michoro ya kisasa, wao wanamichoro ya kale sana hata kabla ya michoro ya kina Leonardo Da Vinci. Pia DNA na ancient documents za zamani, pia wana wa israeli walikuwa ni brownskinned kama wa egypt na kama unasoma bible umeambiwa Iyesus alikuwa na Nyayo za rangi ya nyasi zilizochomwa. Open ure mind kutoka kwenye mental slave.

Sasa hivi kuna project mbalimbali za kufufua siri na ukweli uliofichwa kutokana na ubaaguzi wa kale wa zamani, azungu walianza kwa kudanganya kuwa wamisri ni weupe, then sasa hivi ukweli unajionyesha na ushahidi wa kusema kuwa walikuwa ni weusi upo, na sasa hivi wana akiolojia wengi tunaamini waisraeli wa kale walikuwa wanafanana na wamisri.

Yesu kuchorwa mweupe ni kutokana na sababu nyingi sana. Nyingine za kimakusudi na nyingine za bahati mbaya.

HOLLYWOOD NI WEAPON INAYOTUMIKA HIVI SASA KUPOTOSHA JAMII.

kaka mi nakubaliana na weye kabisa asilimia 200 historia ipo wazi waafric wamehusika kwe mapinduzi mwngi ya kielimu nakidini vyuo vyakwanza duniani vilikuwa timbuktu naegypt huko,kilimo cha umwagiliaji kimeanza egypt na ethiopia ujenzi kabla hata hao wazungu hawajagundua na inaaminika falme zilizokuwa na nguvu ni ethiopoa ndo maana hata mfalme suleiman aliamua kumuoa queen of sheba na ndo maana egypt walikuwa na nguvu kutawala hadi waisraeli....tusiwe wafungwa w fikra na kujidharau...maana njia rahisi ya kutawaliwa ni hiyo
 
Acheni mambo ya laana, acheni matokeo ya ukoloni, acheni matokeo ya biashara ya utumwa ili tuangalie uhalisia uliopo kwa sasa ambao haufungamani na hayo tunayodhani ndio chanzo cha sisi kuwa nyuma kimaendeleo.

Oneni haya yafuatayo:
1. Machimbo mengi ya madini yamenguliwa baada ya ukoloni au tumeyaridhi. Sasa nani anaiba Tanzanite pale mererani? Nani anaiba kwa sasa dhahabu pale Geita, Mara, Mpanda na kwingineko?Nani anaiba almas pale mwadui?Vipi kuhusu mikataba ya kuchimba makaa ya mawe pale kiwira na linganga. Kipindi hiki tulichonacho tumegundua uranium, je itatusaidia?

Ninachojua, malalamiko hayasaidii, tuanze na rasilimali hizi nyeti tulizonazo, tuingie mikataba mizuri yenye maslahi kwa taifa, tuweke utawala bora na viongozi waache wizi wa mali ya umma na wawajibike kwenye maeneo yao ya kazi. Tuyafanye haya sisi wenyewe bila lawama kwa mkoloni, utumwa, u-ngozi nyeusi n.k. maendeleo mbona tutayapata haraka sana? Acheni mawazo mgando ya yaliyopita tuanze sasA.
 
Ni Kweli tumelaaniwa, kwa sabau ya imani zetu za kishirikina zisizompendeza Mwenyezi Mungu, USA.UK,France,Scandnavian countries,Belgium in total, 12 western countries ni decendants wa Makabila kumi na mblini ya ISRAEL ambayo Mungu aliyakarimia Baraka za Mafanikio miaka mingi iliyopita kupitia kwa Ibrahim, Isack,Yacob na zikakumbushiwa na Mussa pamoja na Joshua according to the bible.

Uzao wa Kiarabu pia,umeandikiwa baraka lakini ukawekwa chini ya Amri ya Uzao wa kizungu, refer the blessing of Ibrahim to Ishmael and Isack.

UK rank as the worlds powerful Nation followed by US to date is well explained in the bible, refer the blessings of Yakobo to Ephrahim and Manase the biological sons of Yusufu.

Ni kweli, kuna laana fulani ivi inatuzonga
 
Acheni mambo ya laana, acheni matokeo ya ukoloni, acheni matokeo ya biashara ya utumwa ili tuangalie uhalisia uliopo kwa sasa ambao haufungamani na hayo tunayodhani ndio chanzo cha sisi kuwa nyuma kimaendeleo.

Oneni haya yafuatayo:
1. Machimbo mengi ya madini yamenguliwa baada ya ukoloni au tumeyaridhi. Sasa nani anaiba Tanzanite pale mererani? Nani anaiba kwa sasa dhahabu pale Geita, Mara, Mpanda na kwingineko?Nani anaiba almas pale mwadui?Vipi kuhusu mikataba ya kuchimba makaa ya mawe pale kiwira na linganga. Kipindi hiki tulichonacho tumegundua uranium, je itatusaidia?

Ninachojua, malalamiko hayasaidii, tuanze na rasilimali hizi nyeti tulizonazo, tuingie mikataba mizuri yenye maslahi kwa taifa, tuweke utawala bora na viongozi waache wizi wa mali ya umma na wawajibike kwenye maeneo yao ya kazi. Tuyafanye haya sisi wenyewe bila lawama kwa mkoloni, utumwa, u-ngozi nyeusi n.k. maendeleo mbona tutayapata haraka sana? Acheni mawazo mgando ya yaliyopita tuanze sasA.[/QUOTE]

Kinachotufanya tushindwe kutimiza hayo yaliyo kwenye blue bold ndio laana zenyewe mkuu. Sisi ni taifa tusilomtambua wala kumtanguliza Mungu kwenye mambo yetu, hata pale tunapofanya hivyo hatuna support ya Kiimani inayotusukuma kufanya hivyo, kama kwenye wimbo wa Taifa n.k

Rais wako wa sasa kwa namna anavyotegemea waganga na wachawi nadhani akitoka ikulu na yeye ataanza kulagua watu. kwa nini tusilaanike.
 
kaka mi nakubaliana na weye kabisa asilimia 200 historia ipo wazi waafric wamehusika kwe mapinduzi mwngi ya kielimu nakidini vyuo vyakwanza duniani vilikuwa timbuktu naegypt huko,kilimo cha umwagiliaji kimeanza egypt na ethiopia ujenzi kabla hata hao wazungu hawajagundua na inaaminika falme zilizokuwa na nguvu ni ethiopoa ndo maana hata mfalme suleiman aliamua kumuoa queen of sheba na ndo maana egypt walikuwa na nguvu kutawala hadi waisraeli....tusiwe wafungwa w fikra na kujidharau...maana njia rahisi ya kutawaliwa ni hiyo

hao weusi wa egypt, ethipia hawakuwa wabantu maana naona shida kubwa sana iko kwetu wabantu tunajidharau wenyewe na hata hao cushites, hamitics, nilotes wanatudharau sijui ni hizi pua zetu pana na nyuso pana zinawaudhi! nilishaona msomali akisema yeye si mweusi loooh!
 
yalianza baada ya kuja waarabu. waarabu ndio waliotukamata watumwa wananchi wa Tanzania. Hivyo tafadhali mpende mtu mweupe aliyetuletea shule, reli ya kati na kujenga oyser bay,.
Hivi wale Waafrika weusi walioko katika bara la Ulaya na America walipelekwa na Waarabu? Hizo ni propaganda za Wazungu waliotuletea katika elimu yetu ili tuwachukie Waarabu. Sikatai kuwa Waarabu hawakuleta utumwa lakini kipindi hicho pia wazungu walichukua watumwa toka Afrika Magharibi.Je unafahamu hizo shule walizotuletea zilikuwa na malengo gani? Jikumbushe vizuri somo la Historia.Unajua Wajerumani walijenga reli kwa madhumuni gani? Kwa nini reli ya kusini kutoka Mtwara kwenda Nachingwea iling'olewa? Kama walitujengea sisi kwa nini iling'olewa?Hiyo Oster Bay walijengewa na waliishi akina nani??Unafahamu dini zililetwa kwa ajili ya kutupumbaza?? Na bado wanatuletea dini ili kuendelea kutupumbaza? Wat wanashinda Makanisani na Misikitini badala ya kwenda kuzalisha mali. Ukichunguza utaona nchi masikini sana ndio zenye waumini wengi wa dini? Kwa hili la mwisho najua nimewachokoza. HIVI NDIVYO ILIVYO>>>
 
Kuna vitu vitatu ambavyo vinamuangamiza mwanadamu navyo ni 1.prestige (kujiinua na kujioana ni bora kuliko wengine).
2. Anger (hasira). 3 Alcohol (pombe)
Katika hivi karibu Waafrika wote wana viwili au vyote vitatu. Huwa vinajionyesha sana mtu akipata vitu viwili. 1. Wealth (mali nyingi) 2. Authority (madaraka). Vitu hivyo vitatu vikitawala huwezi kuwapenda wenzako wapate mali au madaraka na badala yake kunakuwa na chuki na vita kati ya mtu na mtu au inchi na inchi.
Roho mbaya inawatawala sana Waafrika.
Ukisoma biblia utagundua kuwa Waafrika walichukua roho ya Esau na Wazungu walichukua roho ya Habili

Wenzetu Wenye rangi nyeup kwa idadi kubwa hivi vitu haviwapi shida na wakipata zaidi wanatugawia na sisi.
kaka point yako ninaikubali asilimia mia moja,bila upendo baina yetu waafrika basi hatuwezi kwenda kokote
 
Shukrani kwa kuleta hoja hiii. La kwanza ni hili: ukiwa na ngozi nyeusi si maana yake ni kwamba umelaaniwa--ni kinyume chake. Kama kuna laana yoyote mbona ingekwisha wapata wazungu siku nyingi sana zilizopita. Ukilinganisha uovu alioufanya mtu mweupe na ule alioufanya mtu mweusi utaona kwamba ktk historia ya binadamu, mtu mweupe amefanya maovu kupita mtu mweusi au mtu mwingine yeyote: ameua sana (k.m tangu warumi hadi wamarekani wa sasa), ametoa sadaka nyingi kwa njia za mauaji, ikiwa ni pamoja na kuteketeza watoto wachanga (hasa enzi za warumi na wagiriki), ameabudu sana miungu na kuwatolea sadaka (miungu kama Zeus, Cleopatra, apollo, columbia, mithra na wengine lukuki--na bado wanaabudiwa kwa njia hasa za kificho), amedharau sana mtu mweusi na kumchukua utumwani, nk nk. Maovu ya mweusi yanayomzidi mweupe na yanayomfanya huyu mweusi astahili laana ni yapi? Mtu mweusi kwa ujumla wake ni mpole na mtaratibu (sawa kuna mafisadi lakini on a larger scale, ni kitu kidogo sana). Watu weupe kwa ujumla wao wanamwelekeo wa kishirikina hasa kwa wakati huu. Niliwahi kusoma chuo kikuu pale ulaya kaskazini (jina la chuo kapuni) na niliona idara za vitivo fulani zinajitambulisha kwa majina ya miungu wao wa kale...picha kama za bundi, mwewe, nyoka nk. Nikaambiwa kuwa bundi ni alama ya hekima. Prof mmoja akaniambia kwamba hapo ulaya miungu wa kale bado wanatawala nafsi zao hata kama kuna dini za kisasa. Akasema utawala huo umo zaidi ktk ngazi ya subconscious kwa hiyo wengine hawajitambui. Kama kuna laana ambayo hutolewa na Mungu basi ulaya ingekuwa tayari imepigwa na laana hiyo zamani.

La pili, sababu ya uduni niionayo mimi ni hii. Kiasili mtu mweusi yupo wired kuiangalia dunia kama kitu ambacho amepokea na hana mamlaka ya kuibadilisha kwa namna yoyote ile. The apparent priciple is: be in the world and let the world shape you instead of you shaping the world. Let the world be the way it is...you have no right to change it...kwa mfano, ukiwa maskini maana yake Mungu kakupangia. Pia kuna dhana kwamba sisi ni watu wa kupita tu kwa hiyo hakuna haja ya kujitaabisha sana eti kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo. Kitu hiki kimo hasa kwenye subconscious ya mtu, na wasomi wa ulaya na marekani wametoa tafsiri zisizofurahisha, eti kwamba mtu mweusi wa kiafrika on average ana IQ ndogo kushinda binadamu wengine wote duniani...kwa hiyo hawezi kufanya kitu kikubwa maana kufanya mambo makubwa hayo ni nje ya capacity yake...ndiyo maana ukigundua mashine au kitu fulani chochote cha maana inakuwa big news na mshangao mkubwa kwa sababu jambo hilo halikutegemewa. Lakini ukweli ni kwamba mtu mweusi ana IQ sawa na watu wengine na anaweza kuwapita watu wengine ikiwa yupo ktk mazingira yanayoruhusu IQ yake kukua. Tafiti za Afrika kusini zimeonyesha kwamba IQ ya mtu mweusi inazidi kuongezeka kwa kasi tangu sera za ubaguzi wa rangi zilipokomeshwa. IQ hiyo iko mbioni kuwaszidi watu weupe...nadhani hii si ajabu...

Halafu baadhi ya wawekezaji toka nje (ulaya au uchina) wamewaona watanzania kama ni watu wavivu na wezi (kwa sababu wanataka njia za mkato kujipatia mapato badala ya kufuata njia ndefu zinazodai taabu na uvumilivu). Sababu ya msingi ndiyo hiyo: mindset.

La tatu, tufanye nini kujikwamua? Kinachotakiwa hapa ni kubadili mtazamo (mindset). Taasisi zilizotumika kubadili mind set kihistoria ni taasisi kama shule, makanisa na misikiti. Waingereza wakati wa Roman empire walikuwa ni watu duni sana kifikra na kimaisha...walianza kuzinduka baadaye na taasisi hizi zilitoa mchango mkubwa ktk kuzinduka huko. Shule ndiyo imekuwa kiwanda muhimu sana katika kumbadili mtoto wa kiingereza kuwa na mindset ya superiority...nimeichunguza mifumo yao toka zamani walipokuwa na makoloni duniani hadi sasa. The school is the most fundamental shaper of mindset. Vyuo vikuu vinafuata. Tanzania imelegeza uzi kwenye elimu. Ili kumbadili mtanzania kifikra kuhusu yeye mwenyewe na kuhusu ulimwengu, ni lazima kufanya mapinduzi katika sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na kurekebisha miundombinu, kuandaa walimu bora na kuwatunza vizuri, kuzingatia sana suala la lugha ya kufundishia, na kucheki malengo ya elimu kwa upya. ifike mahali kwamba mtanzania aliyehitimu ana uwezo wa kujibadili yeye mwenyewe kuwa na hali bora ya kimaisha na pia ana uwezo wa kubadili mazingira yake katika kiwango sawa na mtu mwingine ulaya au kwingineko. Halafu awe ni mtu wa kujiamini na kuipenda sana nchi yake na kuona kwamba ni kichekesho kama nchi tajiri kama Tanzania bado ni tegemezi...kwa hiyo mabadiliko ya fikra ni muhimu na taasisi muhimu katika kuleta mabadiliko ni taasisi ya elimu na mafunzo...
kaka nimekubali point yako.Yes we need to revolutionalize our education system
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari kwa nini nchi za kiafrika hasa zinazokaliwa na watu wengi wakiwa na ngozi nyeusi tuna matatizo kila kona japokuwa tuna rasilimali nyingi sana zinazoweza kutufanya tuwe matajiri wa kutupwa, mfano Tanzania na madini lakini hamna tunachofanya wakati Afri,ka kusini imejengwa na dhahabu za J,burg, DRC na utajiri lukuki lakini ona wanavyohangaika.

Aidha, ukiangalia mikataba tunayoingia utadhani Karl Peters na chief Mangungo enzi zile za harakati ya wajerumani kuipata Tatnganyika kama koloni lao. Sasa najiuliza au kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaanika ni kweli? Naomba michango yenu waheshimiwa.
Ninacoweza kukubaliana na wewe ni kulaaniwa wewe binafsi kwa kuwa na wazo Kama Hilo.
Mtu ukijidharau usitegemee wingine , utabaki chini daima.

Tatizo kubwa la fikra Kama hii ni utegemezi,na ukitegemea mtu mwingine akufanyie kitu maishani utaishia kuwa umelaaniwa kuwa maskini wa maisha yote.
 
Hakuna aliyetulaani,ni uvivu na uoga tu,kwa kiasi kikubwa Africa kama bara linaongozwa na kundi ambalo lilitakiwa kuongozwa,viongozi wako madarakani kama zombies tu,si kama binadamu kamili wenye maono na matamanio ya maendeleo.
Kuna TATIZO KUBWA SANA la kukosekana kwa uzalendo na ubinafsi wa wale wanaoongoza bara hili,hawaongozi wakiwa na malengo yanayoeleweka kila mtu ana malengo yake kichwani,hakuna makubaliaono kama bara tunataka tufike wapi,hakuna makubaliano ndani ya nchi moja moja juu ya nini dhima ya taifa kufikia ndoto fulani,ni wakati wa kujadili na kuweka mambo sawa na kuhakikisha Africa kama bala linakuwa na malengo, na nchi nazo ziwe na malengo,wakati umefika kwa watanzania kutafakari upya juu ya uwepo wa sera ya Taifa,kiuchumi,kijamii n.k,hakuna sababu ya wakati wa uchaguzi mgombea ubunge anasema yeye atafanya hiki na kile vitu ambavyo haviojaw documented kama vipaumbele ndani ya miaka mitano ya ubunge husika, Tuamue sasa kama vijiji kuwepo na vipaumbele,kama kata,jimbo hadi taifa kuwa na vipaumbele ambavyo wakati wa uchaguzi hakuna ngombea atayesema atafanya hiki au kile,bali asema namna ya kufanya na kutekeleza kile ambacho kinatakiwa kifanyike ndani ya kipindi chake cha uongozi,kama mtu kachaguliwa na kashindwa kutimiza yale yaliyotakiwa,kuwepo na mchakato wa kumsaidia kufikia malengo,kama hasaidiki inabidi tuwe serious kama CHINA,akatwe kichwa uwanja ule wa shamba la bibi na aonyeshwe kwenye TV zote.
Haiwezekani raisi amaomba kura kwa kughushi miradi ili wanachi wamchangue kwa juhudi zake za kutaja mabo ambayo atayafanya kwa kujipangia mwenyewe,ni wakati sasa raisi nae apimwe kwa yale yanayotakiwa kukamilishwa ndani ya kipindi chake cha uraisi,vinginevyo China, utaona mabadiliko ya haraka kqweli kweli
Haya yamesemwa miaka na miaka, yaleyale! kwa nini Africa isrudi katika Islamic system kama ilivyokuwa zamani na kuwa na Empires zilizokuwa na nguvu kama vile Songhai Empire.
Songhai Empire - Wikipedia, the free encyclopedia
bibi.com said:
sasa situonyeshe walimwengu kama tunaweza, mbona nchi za Asia wakoloni walienda na bado wamepiga hatua za kimaendeleo
Wamiliki wakubwa wa makampuni na viwanda vingi vilivyopo china ni Wazungu! faida mojawapo kwao wao huko China na sehemu nyingine katika Asia ni cheap labours!
Zaidi ni changa la macho tu!
 
ukifuatilia historia ya dunia utaona kuwa hatujalaaniwa ila ni kipindi tu tunapitia tumekuwa caught off guard na sema hivi kwa mifano ifuatayo
1. wakati marcopolo anaenda china alikuta china imeendelea kuliko ulaya, wachina walikuwa wanawaita wazungu barbarians(washenzi) kufika karne za 15 huko wazungu wakatake the lead wachina leo wanaonekana wasiostaarabika mbele za wazungu.
2.ottoman empire ya waturuki ilikuwa superior na kuanza kuvamia ulaya kipindi hicho wakiwaona watu wa ulaya kama waliolaaniwa au washenzi leo hii things are up side down pengine wazungu ndio wanawaona waturuki cana incapable race.
3.waingereza wenyewe walikuwa kama wanyama wa porini wakati waroma walipowatawala ilikuwa inaonekana kama hawatakuja kumake it through lakini leo wako wapi?
4.persia empire imewahi tawala the known world of those days, muslims wamewahi kuwa the most prosperous people centre ikiwa baghdad lakini leo things ni vise versa
5.wamarekani wakati wanaenda japan for the first time walikuwa wanawaita wajapan yellow monkey lakini leo wanakaa
meza moja as equal partner
my take: kila race ina mind za kuwafanya kuwa na equal chance ya kuwa tajiri tataizo linakuja kwenye mambo kama culture pengine wengine wanawork hard kuliko wengine, au wengine wanaembrace roberry kuliko wengine halafu kipindi hicho watuwalikuwa hawajaingiliana sana lakini siku hizi nchi zilizoendelea ziko very watchful kuhakikisha kwamba wanaendelea kuwa juu, lazima tuchange culture la sivyo tutakuwa kama tunaenda mpirani na moka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom