Je tukubaliane na kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaaniwa?

ukifuatilia historia ya dunia utaona kuwa hatujalaaniwa ila ni kipindi tu tunapitia tumekuwa caught off guard na sema hivi kwa mifano ifuatayo
1. wakati marcopolo anaenda china alikuta china imeendelea kuliko ulaya, wachina walikuwa wanawaita wazungu barbarians(washenzi) kufika karne za 15 huko wazungu wakatake the lead wachina leo wanaonekana wasiostaarabika mbele za wazungu.
2.ottoman empire ya waturuki ilikuwa superior na kuanza kuvamia ulaya kipindi hicho wakiwaona watu wa ulaya kama waliolaaniwa au washenzi leo hii things are up side down pengine wazungu ndio wanawaona waturuki cana incapable race.
3.waingereza wenyewe walikuwa kama wanyama wa porini wakati waroma walipowatawala ilikuwa inaonekana kama hawatakuja kumake it through lakini leo wako wapi?
4.persia empire imewahi tawala the known world of those days, muslims wamewahi kuwa the most prosperous people centre ikiwa baghdad lakini leo things ni vise versa
5.wamarekani wakati wanaenda japan for the first time walikuwa wanawaita wajapan yellow monkey lakini leo wanakaa
meza moja as equal partner
my take: kila race ina mind za kuwafanya kuwa na equal chance ya kuwa tajiri tataizo linakuja kwenye mambo kama culture pengine wengine wanawork hard kuliko wengine, au wengine wanaembrace roberry kuliko wengine halafu kipindi hicho watuwalikuwa hawajaingiliana sana lakini siku hizi nchi zilizoendelea ziko very watchful kuhakikisha kwamba wanaendelea kuwa juu, lazima tuchange culture la sivyo tutakuwa kama tunaenda mpirani na moka.
Mada imefikia sehemu ambapo kinachotakiwa ni ufumbuzi!...........pia tumeona kuwa "maendeleo" ya Asia siyo yanayotakikana kwa mwafrika na si ufumbuzi!
 
South Africa is The most developed African county. South Africa is more developed than most Eastern Europe countries but the gap between the rich and the poor made it a developing country ...Everything you can find in Europe is present in South Africa except the high rate of poverty created by the past racial segregation (apartheid).
Again, hii sio aina ya maendeleo anayoyataka Mwafrika
 
Guys c kua tumelaaniwa, mbona kuna waafrika wengi wamefanya mambo makubwa hadi leo yanaonekana e.g. computer unayotumia leo icngekua fast ka c Philip Emeagwa mnigeria ambae ndiye mgunduzi wa supercomputers, na huyu hajasoma hata sekondari alifanya homeschoolin, mic za electronics kagundua mwafrika etc.. We have the same potential na wengine sema wametuwahi na wanazidi kutudidimiza kwa kila njia startn from leaders hadi citizen wa kawaida... We cant just sit down na kusubiri viongozi wetu waanze, mtu moja anaeza leta changes.. Mbona Mark kafungua facebook ila sa hvi ana thousands of employees? Sema nchi haimjali kila raia wakisahau moja anaweza akafanya kitu kikabadilisha maisha ya maelfu watanzania ambao nao pia wanaweza wakanyanyua wengine vilevile... We got brain ila tumelala na tunazidi kupewa dawa za ucngzi... It hurts me so much.... Mtu ana degree afu anakuja ghetto kugongea ugali.....
 
Guys c kua tumelaaniwa, mbona kuna waafrika wengi wamefanya mambo makubwa hadi leo yanaonekana e.g. computer unayotumia leo icngekua fast ka c Philip Emeagwa mnigeria ambae ndiye mgunduzi wa supercomputers, na huyu hajasoma hata sekondari alifanya homeschoolin, mic za electronics kagundua mwafrika etc.. We have the same potential na wengine sema wametuwahi na wanazidi kutudidimiza kwa kila njia startn from leaders hadi citizen wa kawaida... We cant just sit down na kusubiri viongozi wetu waanze, mtu moja anaeza leta changes.. Mbona Mark kafungua facebook ila sa hvi ana thousands of employees? Sema nchi haimjali kila raia wakisahau moja anaweza akafanya kitu kikabadilisha maisha ya maelfu watanzania ambao nao pia wanaweza wakanyanyua wengine vilevile... We got brain ila tumelala na tunazidi kupewa dawa za ucngzi... It hurts me so much.... Mtu ana degree afu anakuja ghetto kugongea ugali.....

maneno mazuri sana haya. Big up.
 
Ni Kweli tumelaaniwa, kwa sabau ya imani zetu za kishirikina zisizompendeza Mwenyezi Mungu, USA.UK,France,Scandnavian countries,Belgium in total, 12 western countries ni decendants wa Makabila kumi na mblini ya ISRAEL ambayo Mungu aliyakarimia Baraka za Mafanikio miaka mingi iliyopita kupitia kwa Ibrahim, Isack,Yacob na zikakumbushiwa na Mussa pamoja na Joshua according to the bible.

Uzao wa Kiarabu pia,umeandikiwa baraka lakini ukawekwa chini ya Amri ya Uzao wa kizungu, refer the blessing of Ibrahim to Ishmael and Isack.

UK rank as the worlds powerful Nation followed by US to date is well explained in the bible, refer the blessings of Yakobo to Ephrahim and Manase the biological sons of Yusufu.

Ni kweli, kuna laana fulani ivi inatuzonga

Wee ndugu yangu wee...kumbe ndivyo mnavyohubiri makanisani ili waumini wenu waamini kwamba watabaki wamelaaniwa hadi hapo watakapotubu dhambi? Kutubu dhambi ni mhimu, lakini naomba hiyo Bible (sijui version gani) uisome vizuri, halafu pia soma context yake. Hayo makabila 12 ya Israel sio hao unaowataja...hao uliowataja asili yao ni nyingine. Hebu tembelea Vatican, District of Columbia, Inner City of London. Tafuta mwenyewe, mimi sikuambii zaidi...ila utakumbuka wakati wa september eleven G.W.Bush alitaja axis of evili kuwa ni Iraq, Iran na Korea kaskazini. In fact, axis of evil, kusema ukweli, ni Vatican (world spiritual centre), Inner City of London (world's financial centre) na District of Colombia (world' military center)...find out more on this. Na hizi centres zipo coordinated...they have the same agenda--to control the world. Hapo utajua pia kwanini kuna uhasama mkubwa kati ya mwislamu mkereketwa na mzungu wa kimagharibi...utaelewa kwanini wanawaita devils au "confederation of devils" kama Gadafi alivyowaita...there is alot going on underground.

Baadhi ya uliowataja kama ndio wenye baraka ndiyo wanaohodhi mamlaka katika miji hii mitatu na kazi yao ni kuipeleka dunia kwenye mwelekeo unaompinga Mungu. Huyo mungu aliyewapa baraka watu wanaomsaliti ni yupi? Kwa nyongeza, je umesikia chochote kuhusu New Age Movement na wafuasi wake mamilioni kwa mamilioni? Movement hii ni ya kishirikina na kama kuna weusi katika kundi hilo basi ni wachache sana...find out on this too.

Halafu yale makabila ya waisraeli unayoyataja si ya watu weupe. Ni watu wa asili ya kiasia na kiafrika, nao wamesambaa pande mbali mbali...wengine tunao humu humu Afrika lakini hatuwatambui na wao inawezekana hawajitambui...pia intermarriages zimechangia kuwafanya baadhi yao wasitambulike.

Halafu pia ifahamike kwamba kutokuwa na mali inaweza kuwa baraka, in a spiritual sense. Kiasili, binadamu ameumbwa katika mazingira kwamba roho yake iwe ni sehemu ya ufalme wa Mungu...this was the original plan. Sijui tunaelewana hapa?

Labda pia niseme kwamba wazungu waliobarikiwa wapo, sikatai. Lakini wengi wao wapo kama wengu wetu, yaani si matajiri wala hawthamini sana uwezo wa kifedha au mali...ni watu wa kawaida na wanaishi wakimtegemea Mungu huku wakijishughulisha na shughuli za kila siku...hao wapo pia. Ila si wengi.

Kwa hiyo laana haipo. Ninachoomba kwa weusi wenzangu ni kuzinduka na kuanza kusonga mbele kwa kasi. Lasivyo, ipo siku tutakiona tusichotarajia...sincerely.
 
ki ukweli wa afrika tumelaaniwa hilo halina ubishi!!!
Unachokifanya ni kum convince Mwafrika kuwa he is nothing! no matter what he tries.....it does not make sense to try either!
......hii ni moja ya njia za ki ideological warfare anayoitumia Slave Master kuwasambaratisha majeruhi wake!
Africa inahitaji Islamic System!
 
Mtu mweusi hajalaniwa kwa ujumla, ila wapo wenzetu amboa wamezama ndani ya lindi la ufisadi, ukatili uzinzi etc kina kirefu hadi kutofikiwa mapenzi ya muumba wa ardhi na bingu na hii ndio maana halisi ya kulaaniwa.
 
Eiyer sikubaliani na ww na kwa kweli hii imekuwa ni moja ya excuse kubwa sana pale viongozi wa Afrika wanapobanwa kwa kushindwa kuendeleza nchi zao! Pale VETA Dsm zamani kulikuwa na bango kubwa limeandikwa ' Fundi asiye na ujuzi siku zote hulaumu vyombo vyake' sijui bado lipo au wamelitoa sijapita siku za karibuni. Nakubaliana na mtoa mada kwamba tatizo na.1 la viongozi wetu ni kukosa uzalendo na ubinafsi, pili hata nyule ambaye anajua fika kwamba hana uwezo wa kuongoza kwa maana ya seriouly kuwaletea maendeleo watu wake bado atahakikisha anapata uongozi hata pale ambapo matokeo yake ni kuleta mateso na hata vifo kwa anaotaka kuwatawala, they simply dont care! Infact wanapokuwa kwenye vijiwe vyao na wapambe/au wenzao wa nchi nyingine wanaofanana hawana hata chembe ya muda wa kujadili mustakabali wa watu wao. Wanakuwa bize kujadili jinsi ya ku rig elections, mahali salama pa kuficha pesa,kuwekeza, kustarehe, jinsi ya kudhibiti maandamano (jinsi ya kupata magari ya kisasa ya maji ya washa washa n.k). Kwa hiyo hawana kabisa muda wa kujua shida za wanaowatawala na ndio maana wengine wanasema hawajui kwa nn wapiga kura wao ni maskini. Nyerere aliwahi kusema kuwa rais ni mzigo na matatizo makubwa mno kwani kila siku kazi yako ni kufikiria jinsi utakavyotatua matatizo mengi sana ya wananchi, na akawashangaa sana wanaokimbilia ikulu. Hivyo nimalize kwa kusema visingizio vya kuwalaumu wazungu ni sawa na fundi asiye na ujuzi anayelaumu vifaa vyake!! mbona tuilopata nao uhuru (malasia and others) wako mbali??

Matatizo ya watu weusi yalianza baada ya weupe kuja huku!Walipogundua ubora wa mtu mweusi na utajiri alionao,ndipo ulipotengenezwa mfumo wa kumfanya Mwafrika ajidharau ili aweze kutawalika vizuri!Kwa kifupi hakuna laana yoyote tena ni aibu sana mtu kusema hivyo,matatizo yote tuliyonayo ni ya kimfumo zaidi!
 
Clarion call has always been down with ukoloni mambo leo, the truth is lack of leadership has ruined most African countries. How do you explain Asian miracle , given that Asian nations were also colonized.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari kwa nini nchi za kiafrika hasa zinazokaliwa na watu wengi wakiwa na ngozi nyeusi tuna matatizo kila kona japokuwa tuna rasilimali nyingi sana zinazoweza kutufanya tuwe matajiri wa kutupwa, mfano Tanzania na madini lakini hamna tunachofanya wakati Afrika kusini imejengwa na dhahabu za J,burg, DRC na utajiri lukuki lakini ona wanavyohangaika.

Aidha, ukiangalia mikataba tunayoingia utadhani Karl Peters na chief Mangungo enzi zile za harakati ya wajerumani kuipata Tanganyika kama koloni lao. Sasa najiuliza au kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaanika ni kweli? Naomba michango yenu waheshimiwa.

ndio tumelaaniwa na na laaniwa na laana huja kwa kusikia na kuona.ili tutoke kwenye laana hii tuchague viongozi ambao hawatashiriki laana hii,pili sheria za nchi ziwabane tusisikie wala kuiona laana hii kwa kizazi cha kwanza na cha pili hata cha tatu nayo tutaipoteza.KUMBUKA TUNAJIFUNZA KWA KUONA NA KUSIKIA!
 
ndio tumelaaniwa na na laaniwa na laana huja kwa kusikia na kuona.ili tutoke kwenye laana hii tuchague viongozi ambao hawatashiriki laana hii,pili sheria za nchi ziwabane tusisikie wala kuiona laana hii kwa kizazi cha kwanza na cha pili hata cha tatu nayo tutaipoteza.kumbuka tunajifunza kwa kuona na kusikia!

having little number of educated is aproblem, and tz is an example. Sizable numble of people do not have strategies to extricate from the existing system, they support it unawares.
 
Waafrika tumelaaniwa na mungu wa kiyahudi amabye tumekuja kumjua karne ya 15?!!!

Huyo mungu amabye hana uhusiano wowote na tamaduni za kiafrika ametulaani?Hilarious!!

Kama tumelaaniwa ni mizimu ya mababu zetu kwa kuacha kuiabudu na kuwa misukule ya hizi dini zilizokuja na meli

Neo colonialism imetushika sana.Free yourself from mental slavery!!
 
Waafrika tumelaaniwa na mungu wa kiyahudi amabye tumekuja kumjua karne ya 15?!!!

Huyo mungu amabye hana uhusiano wowote na tamaduni za kiafrika ametulaani?Hilarious!!

Kama tumelaaniwa ni mizimu ya mababu zetu kwa kuacha kuiabudu na kuwa misukule ya hizi dini zilizokuja na meli

Neo colonialism imetushika sana.Free yourself from mental slavery!!

Kumbe ndiyo maana Waafrika hatuendelei! Mawazo mufilisi haya.
 
Kusema ukweli hii ngozi nyeusi ina kalaana fulani. Pamoja na dharau na manyanyaso yote tuliofanyiwa na wazungu bado kuna watu hasa viongozi wetu wanawahusudu kama miungu watu. Mabinti wanajichubua ngozi ili wafanane na wazungu. Tunalaana bwana.. Aaaaah kweli tunalaana!
 
Matatizo ya watu weusi yalianza baada ya weupe kuja huku!Walipogundua ubora wa mtu mweusi na utajiri alionao,ndipo ulipotengenezwa mfumo wa kumfanya Mwafrika ajidharau ili aweze kutawalika vizuri! Kwa kifupi hakuna laana yoyote tena ni aibu sana mtu kusema hivyo,matatizo yote tuliyonayo ni ya kimfumo zaidi!

Eiyer hii ni post yako ya zamani lakini nahisi bado unaamini kama ulivyoandika!
Sipingi ulichokiongea hapo but ningependa kukuuiliza swali hapa:

Ikiwa Muafrika ni mtu bora, kwanini walikubali kufuata mfumo huo wa kujidharau na kuweza kutawaliwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom