Je tukubaliane na kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaaniwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je tukubaliane na kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaaniwa?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by habi alex, Mar 16, 2012.

 1. habi alex

  habi alex Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari kwa nini nchi za kiafrika hasa zinazokaliwa na watu wengi wakiwa na ngozi nyeusi tuna matatizo kila kona japokuwa tuna rasilimali nyingi sana zinazoweza kutufanya tuwe matajiri wa kutupwa, mfano Tanzania na madini lakini hamna tunachofanya wakati Afrika kusini imejengwa na dhahabu za J,burg, DRC na utajiri lukuki lakini ona wanavyohangaika.

  Aidha, ukiangalia mikataba tunayoingia utadhani Karl Peters na chief Mangungo enzi zile za harakati ya wajerumani kuipata Tanganyika kama koloni lao. Sasa najiuliza au kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaanika ni kweli? Naomba michango yenu waheshimiwa.
   
 2. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Hakuna aliyetulaani,ni uvivu na uoga tu,kwa kiasi kikubwa Africa kama bara linaongozwa na kundi ambalo lilitakiwa kuongozwa,viongozi wako madarakani kama zombies tu,si kama binadamu kamili wenye maono na matamanio ya maendeleo.

  Kuna TATIZO KUBWA SANA la kukosekana kwa uzalendo na ubinafsi wa wale wanaoongoza bara hili, hawaongozi wakiwa na malengo yanayoeleweka kila mtu ana malengo yake kichwani, hakuna makubaliaono kama bara tunataka tufike wapi, hakuna makubaliano ndani ya nchi moja moja juu ya nini dhima ya taifa kufikia ndoto fulani, ni wakati wa kujadili na kuweka mambo sawa na kuhakikisha Africa kama bara linakuwa na malengo, na nchi nazo ziwe na malengo.

  Wakati umefika kwa watanzania kutafakari upya juu ya uwepo wa sera ya Taifa,kiuchumi,kijamii n.k,hakuna sababu ya wakati wa uchaguzi mgombea ubunge anasema yeye atafanya hiki na kile vitu ambavyo haviojaw documented kama vipaumbele ndani ya miaka mitano ya ubunge husika, Tuamue sasa kama vijiji kuwepo na vipaumbele,kama kata,jimbo hadi taifa kuwa na vipaumbele ambavyo wakati wa uchaguzi hakuna ngombea atayesema atafanya hiki au kile,bali asema namna ya kufanya na kutekeleza kile ambacho kinatakiwa kifanyike ndani ya kipindi chake cha uongozi,kama mtu kachaguliwa na kashindwa kutimiza yale yaliyotakiwa,kuwepo na mchakato wa kumsaidia kufikia malengo,kama hasaidiki inabidi tuwe serious kama CHINA,akatwe kichwa uwanja ule wa shamba la bibi na aonyeshwe kwenye TV zote.

  Haiwezekani raisi amaomba kura kwa kughushi miradi ili wanachi wamchangue kwa juhudi zake za kutaja mabo ambayo atayafanya kwa kujipangia mwenyewe,ni wakati sasa raisi nae apimwe kwa yale yanayotakiwa kukamilishwa ndani ya kipindi chake cha uraisi,vinginevyo China, utaona mabadiliko ya haraka kweli kweli.
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Matatizo ya watu weusi yalianza baada ya weupe kuja huku!Walipogundua ubora wa mtu mweusi na utajiri alionao,ndipo ulipotengenezwa mfumo wa kumfanya Mwafrika ajidharau ili aweze kutawalika vizuri!Kwa kifupi hakuna laana yoyote tena ni aibu sana mtu kusema hivyo,matatizo yote tuliyonayo ni ya kimfumo zaidi!
   
 4. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa na mawazo kama yako, mimi nasoma Archaeology. Ila ujue kuwa. Waisraeli wa kale walikuwa ni weusi/brown, wamisri walikuwa ni weusi/brown, Yesu alikuwa Brown coloured.

  Aliyelaaniwa alikuwa ni Canaan na sio Ham, Ham alikuwa na watoto watatu, Canaana (aliishi kanaan), misrata (aliishi Misri), na Kush (aliishi Ethiopia). Kush ndie baba wa waafrika wa sasa. Aliyelaaniwa ni Canaan na sio Kush, Misrata au baba yao Ham.

  Mtu mweusi ana nafasi kubwa katika historia za kidini, uchumi, sayansi, .

  Tatizo dini, siasa, biashara, ubaguzi n.k vinatumika kumshusha mwafrika. Mfano movies za sasa hasa za kidini zinaweka wazungu wakati hakuna ushahidi wa Kiakeolojia kuwa walikuwa wazungu ila kuna picha za zamani sana zinawaonyesha brownskinned.

  Jinsi sayansi inavyoendelea kuufumbua ulimwengu tunakuja kujua kuwa Afrika ndio source of humankind (Eden Garden), watu wote wametokea Africa, waafrica wa kale walikuwa Civillized n.k.
   
 5. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  Na sio waafrika tu ndio wenye ngozi nyeusi.
   
 6. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  sasa situonyeshe walimwengu kama tunaweza, mbona nchi za Asia wakoloni walienda na bado wamepiga hatua za kimaendeleo tusitafute visingizo ohh ukoloni oooh viongozu wabaya hao viongozi wabaya wametoka wapi kama sisi jamii ni nzuri? jitu linajulikana kabisa lilikuwa na historia chafu lakini ndio utakuta tunamfurahia ati awe kiongozi wetu tena tunasema kabisa personal behaviour yake haihusiani na uongozi angalia wenzetu doa kidogo unavuliwa madaraka au hata kura hupewi, tujianngalie weakness zetu na tujirekebishe na si kublame wengine kwa umaskini wetu la sivyo tutakuwa bara la giza mpk kiama!
   
 7. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  tumelaaniwa kweli naamini kabisaa. unawezaje kuuleta ujamaa katika nchi ambayo 99% hawana kazi? wakoloni wtu walitufundishs demokrasia ili watu wa kila fani na akiringi wapate kuongoza nchi. Lakini watwala wetu hawakutaka hayo. wao walitaka watawale milele na makaburi yao yazidi kuawala watu walio hai.
   
 8. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  yalianza baada ya kuja waarabu. waarabu ndio waliotukamata watumwa wananchi wa Tanzania. Hivyo tafadhali mpende mtu mweupe aliyetuletea shule, reli ya kati na kujenga oyser bay,.
   
 9. n

  naivasha Member

  #9
  Mar 18, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hakuna laana. Matatizo siyo laana. Laiti matatizo yangelikuwa laana, basi kila jamii, na kila kiumbe ni laana tupu. Hapana hakuna laana hapa. Mimi naamini laana ni kinyume na mipango ya Mwenyezi Mungu. Afrika hatujalaaniwa. Afrika tuna tatizo la uongozi tu. Viongozi na watunga sera hawajali maslahi ya umma zaidi ya kuandalia maslaho yao pamoja na ubinafsi wao uliokithiri. Vionhozi wetu wanapenda sifa za kupigiwa makofi ya kejeli. Angalia viongozi wanavyojinasibu kikasuku kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani! Kwa hiyo? Natoa mifano michache na naiongelea Tanzania yetu na viongozi wetu. Tanzania imeendesha harakati nyingi, kubwa na kwa gharama kubwa ya uhai na mali kwa faida sifuri katika umri wake wa miaka 50 ya uhuru.
  1. Tanzania imefadhili wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini, Msumbiji, Angola, Namibia na Zimbabwe kwa kuwapa chakula, makazi, matibabu, viwanja vya mafunzo ya kijeshi, elimu lakini tumepata nini. Maslkahi ya kufanya hivyo ilikwa ni nini?
  2. Tanzania imewahifadhi na kugharimia maisha na harakati za wanaharakati wa mataifa mengine hususan Museven, Obote, Garang, Kabila, Muluzi na Wanarwanda kibao kwa maslahi wanayoyajua viongozi tu.
  3. Tanzania ilipigana vita ya gharama kubwa ya damu na mali dhidi ya IDD AMINi DADA kwa minajili na maslahi tu ya kumrejesha Obote madarakani na tuliambulia anguko la uchumi hadi sasa.
  4. Tanzania tulipeleka majeshi Comorro na kwingineko kama taifa maslahi yake ni yapi?
  Hapa ni duniani. Kila mradi lazima uwe na tija vinginevyo haufai. Kwa gharama tulizolipa kwa ajili ya Uhuru wa Africa Kusini, Angola, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na mapinduzo ya DRC, Uganda; Vita ya Kagera tulitakiwa tupate mapato zaidi ya maradufu yatokanayo uthabiti na udhibiti wa siasa, uchumi na tamaduni za mataifa hayo. Lakini tulipigana vita, tukawafadhili wapigania uhuru na kuwatunza wanaharakati kwa hisani tu. Hapa ndo shida ilipo. Mimi nina swali/hoja. Hivi Tanzania kama nchi haiwezi kubargain na mataifa ya Afrika kusini, namibia, Angola, Musumbiji, DRC, Comoro, Shelisdheli, Sudan Kusini na Uganda kila nchi ikalipa fadhila kwa mali ukarimu tuliowatendea? Mi siamini kama tulitoa sadaka.
   
 10. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  I came to conclusion that, you pay a price for being black somehow.
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Upo right ila,pia kutengeneza movie inayo potray middle easterns ni rahisi kutumia rangi nyeupe kuliko Black,Ingawa pia Wayahudi nao wapo wengi waliomix na whites wa jamii tofauti, so pengine ndio wakaa assume kuchukua weupe halisi.<br>Pia kuna tatizo la black ktk kufanya tafiti nzuri, kuandaa movies za maeneno mbalimbali ya maisha ya mwanadamu.So hatuna advocates ktk history.Mtu mweusi alikuwa powerful sana kabala ya kuja ukoloni(Mzungu/Arabs/persians(Iranians)) . Until now waafrica wamejikita ktk kutetea sana tamaduni za wakoloni kwa mitazamo yao.Waislam wanapoteza muda muda kutetea everything Islamo-Arabism, wakristu the same wapo ktk dilema ya Capitalist-Europe na Christian-Europe.Debate nyingi sana hazionyeshi sisi kuukataa au hata kuujua ukoloni, ila ni kuchagua mkoloni.
  Brown skinned ni asians+mixed races throughout the world.Na african Discendant wanatazamwa km dark skinned or Black. Hao tunawaita weupe huku africa ,ni brown zaidi ya kuwa white.
  Black african walifanya biashara na watu wa mataifa na kwingine walianzisha makazi na kutawala.Kuanzia India, sehemu za china na ukanda wa middle east.Ila utumwa ulipoanza wakanguka , kila kitu kikawa kinyume chao.Hata fikra zao hadi leo zina mapungufu yanayokwanza kwenda mbele
  Sayansi bado haijafikia mwisho, wanasayansi wanaamini hiyo, kwa jinsi wanavyopata mabaki ya zamani zaidi.Ila kila siku kuna uvumbuzi unaopelekea sehemu mbalimbalia za dunia kuonekana kwa kipindi tofauti kuwa ndio chanzo cha wanadamu.Na hii uncertainty ndio inayofanya theory ya creation kuwa na Nguvu.
   
 12. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  Kama hivyo vita unavyodai ndo chanzo cha umaskini wetu naomba ujibu maswali yafuatayo:
  1. Germany imepigana vita mara 2 yani WW1 na WW2 na iliishia kupigwa na kuharibiwa vibaya lakini ina rise tena. Je kwanini sisi hatu rise na kuwa na stable economy?
  2. Rwanda imepigana vita vya wenyewe kanwe lini sasa is among of t african countries ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi na ikumbukwe kwamba wametoka vitani miaka michache tu iliyopopita compared na sisi tuliopigana vita miaka ya 70. Je ni sababu zipi zimetufanya tudorore?
  3. China ni nchi ambayo wakati tua almost sawa na sisi. Lakini leo yani kulinganisha za kiafrika ni kituko wakati china kama chresources nyingi kama sisi. Je ni kwanini wao wameendel si i nyuma?
   
 13. M

  Mr jeans New Member

  #13
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usilalamike sana coz tumetengenezewa mazingira ya kuwa hivyo, halafu tukayakubali!!!
   
 14. n

  naivasha Member

  #14
  Mar 18, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ndg yangu elmagnifico. Kwa kuwa umeuliza ni muhimu nikakujibu na naamini wengine watachangia.
  Ni kweli Wagerumani walipigana WWI na II. Suala sio kushindwa vita bali motive ya vita ilikuwa nini kama sio kusaka utajiri na makoloni zaidi. Pia pamoja na matokeo mabaya ya vita WWI na WWII kwa Ujerumani lakini kwa misingi waliyokuwa wamejenga bado liliondokea kuwa taifa kubwa hata leo. Rwanda, hawa jamaa wamepigana vita ya kuuangusha tawala dhalimu kama za CCM. Lakini hawakuishia hapo wameigia DRC kupigana vita yenye maslahi mfano madini, mbao n.k. Haya ndo maslahi niliyoongelea kuwa sisi pengine tulikuwa tunatoa sadaka vinginevyo tulipopeleka majeshi Msumbiji, Comoro, na Uganda lazima tulikuwa na malengo ya msingi. Ni yapi hayo? Kwa upande wa China nafikiri umekosea lbda ulimaanisha akina Korea siyo China. Wachina tangu enzi na enzi miaka ya 1,400 wanatengeneza vifaa vya udongo, sindano, vyereani, wembe, mapanga, majembe nk. ambazo ni zana muhimu za awali. Hadi sasa vifaa hivi tunavinunua huko!!!! Tanzania unayosema eti mlikuwa "almost sawa" mmewahi kutengeneza nini? Acha utani hapo. Mimi nilichosema ni kwamba tatizo la nchi zetu ni viongozi kutokujali maslahi ya umma/taifa. hapo ndo nikatoa mifano michache ambapo kwa shughuli zile tulitakiwa tutangulize maslahi yetu. Ina maana gani tumewasaidia, vijana wetu wakapoteza maisha, taifa likapoteza fedha zake nyingi, tukapoteza muda kwa kazi hizo na mwisho jamaa wakajikomboa wakajiondokea zao tukaambilia kuitwa taifa karimu. It counts nothing!
   
 15. pandora

  pandora Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  madameX sio kwamba watu weusi " they make themselves pay a price for being black somehow?"
   
 16. pandora

  pandora Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15

  ishu sio afrika ilikua imeendelea au la. ukisema hivi ni kama vile unataka kujipa therapy fulani au unataka kutafuta pride by self consolaton ambayo haibadilishi maisha yetu kwa namna yoyote ile. tunachotaka sisi kuona afrika inaendela sasa! hata china ilikua imeendelea katika miaka elfu kadhaa huko nyuma iliyopita na hii inaitwa ancient chinese civilisation. lakini mbona kwa sasa tunawaona wanaendelea kwa sana tu katika style ya ki -siku hizi.
  mbona bado sisi hatuendelei katika style ya ki siku hizi....matatizo chungu mzima afrika mengine hayana kichwa wala mkia yaani ni upuuzi mtupu! na kila sehemu yenye watu weusi ni vurugu.lazima utakuta hiyo jamii iko failed somehow!
   
 17. pandora

  pandora Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  nashukuru sana kwa kuliona hilo. mara nyingi sana watu wamekua hawalizungumzii kwa ukweli wote hili jambo. wanasahau kabisa kwamba waharabu ndio walioanza kuifanya na pengine kuikuza hii biashara ya kishenzi ya utumwa hapa afrika na hawakuacha chochote cha maana hapa afrika zaidi ya dini yao tu waliokuja kuieneza hapa.
  matatizo ya mwafrika always lawama ni mzungu sijui kwanini hata kama mwafrika anafanya upumbavu somehow utakuta anamlalamikia mzungu yaani mi sielewi ni kwa lipi! hata kwa matatizo madogo madogo ambayo tunaweza kujua soiurce yake ni wafrika wenyewe lakini liltahusishwa na mzungu somehow. sisemi kwamba hawa wazungu hawajawahi kutufanyia mambo mabaya la.ila somehow nasisi tuache porojo za kutaka kutafuta mchawi nani wakati hata kabla hatujajicheki sisi na makosa yetu kibao tunayofanya. let us not look for excuses.we should focus on solutions of our problems practically!

  HAKUNA CHA LAANA WALA NINI ,.,.,,,,,NI UPUUZI TU WA MWAFRIKA MWENYEWE!
   
 18. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi sizani kama tumelaaniwa bali tumejilaani wenyewe
   
 19. chiko

  chiko JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nimekupata Mkuu, kuongezea, jamii imekua na kasumba mbaya, muuza madawa ya kulevya mwizi wa mali ya umma ndie mfano bora wa kiongozi kwa sababu ya mali zake!!!, nafikiri tukitoka kwenye usingizi huu tuta-okoka!!!!
   
 20. remon

  remon JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 295
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli waafrika tumelaaniwa , soma kwenye hadithi YA NUHU WA SAFINA NA WATOTO WAKE KUNA MTOTO WA NUHU ALIYEMCHUNGULIA BABA YAKE ALIPOKUWA AMELEWA, NA AKAAMBIWA KUWA ATAKUWA MTUMWA WA WENZAKE KATIKA MAISHA YAKE.
   
Loading...