Je tukubaliane na kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaaniwa?

Wachangiaji wengi mna mawazo mazuri lakini kuonyesha jinsi hatuna akili naamini kati ya wachangiaji kuna ambao wanarubuniwa na kanga na t-shirt za ccm.hapa ndipo inaonekana jinsi tulivyo mbumbumbu yaani hatowanishi maisha yetu na mustakabali wa nchi....
 
Sio theories zote ambazo zimetolewa zimewekwa na waafrica, kumbuka kuna wasomi weusi. Pia kuna wasomi weupe Kama Karl Max ambaye alijitahidi sana kutetea low classes na kupinga Capitalism, wewe humwamini? Kuna wasomi wa nje ambao wanatetea haki za weusi na jitihada zao zilionekana na kuna wasomi weusi nao wanatetea haki za weupe, usihukumu theory ya mtu kwa kuangalia race aliyotoka maana kuna waafrica ni ma-pupet tu. We angalia theory inasema nini.

Mi naona tukubali tu kuwa waafrika tumezidiwa akili, busara, hekima, ubunifu, uzalendo na mengine kibao.
Chanzo cha tatizo hili chaweza kuwa cha kibaolojia, historia na pengine kijamii(race).
Mi binafsi nilishajiuliza juu ya hili na nilijikuta naziondoa sababu nyingine na kubakiwa na sababu ya kijamii(race) zaidi, kwamba kulingana na chambuzi na tafiti mbali mbali inaaminika kuwa sisi waafrika ndiyo chimbuko la mwanadamu.
Baada ya sisi jamii ziliendelea mpaka kufikia wazungu.
Lakini nilipochunguza nikaona ukianzia kusini mwa afrika na kuelekea kaskazini "kwa sehemu kubwa" utaona rangi ya ngozi inabalika toka dark kuelekea white, nywele pia hubadilika kua laini.
Anglia mfano Tanzani, kenya,sudan, ethiopia, misri na kuendelea mpaka uturuki, sirya... And so on mpaka unaimaliza ulaya.
Nikiangalia trend hii naona hata mabara mengine originally yako hivyo.
Point yangu ni kuwa hii trend ilivyo ndio inaendana na akili za jamii husika. Namaanisha pengine distribution ya watu inaendana na akili zao.
Pengine tukubali tu "miafrika ndivyo tulivyo".
Labda ni kazi ya nature. Ila kwa kweli tuko chini ya kiwango.
 
Kuna watu wanasingizia wakoloni, sijui waarabu, sijuni dini ila mi naona hoja hizo hazina uzito.
Kama sisi tuna akili kwanini hatukuwapelekea wazungu na waarabu dini zetu na kuwafanya wao wa tumwa wetu kama walivyotukomesha na wanavyotutia adabu mpaka leo?
Dah! Pole mama afrika.
 
ebu tuchukulie mfano wa zimbabwe ambayo ilikuwa imeimalika kicuhumi unaotokana na settler agriculture, mgabe alipowafukuza wazungu mashamba yakarudi kwa waafrika wameshindwa kuyaendesha na wameharibu kila kitu.
Hadi najiuliza swali hivi sisi waafrika tumeumbwa kutumikishwa au nini? Tunashindwa kuwa our own bosses tukafanya kazi vizuri lakini tukiwa under another boss hapo tunafanya kazi.
Haina shaka waafrika ndio walikuwa wafanyakazi kwenye hayo mashamba na wazungu walikuwa wasimamizi tu lakini walipoachiwa mashamba wameshindwa kuyaendeleza.
I do wonder what is wrong with my black colour?
sidhan kama weupe ndiyo wanatufanya tusiendele lakin sisi wenyewe labda destiny ya hili bara letu ni kuwa kama tulivyo kwakuwa we have got everything but we dont progress kila shida iko africa.
Angalia wanafunzi toka africa wanaosoma vyuon ulaya wanakuwa so bright this proves that tuna akili lakin what is upon us yan sielewi africa tuna nini.
 
Hatujalaaniwa...nadhani kuna jambo la kulitazama sana 'elimu' tunayopata haitusaidii au inatuandaa kuwa watumwa... Africa ni fedheha kijana msomi kurudi kijijini (kunako rasilimali) na wengi kuishia mijini kutafuta utajiri- ufisadi...kila mtu fisadi tumekwama..wageni wanahangaika na maliasili zetu...turudishe degree zetu mashambani changes ni lazima..
 
mh! Maandeleo africa!!!1
Kabla hamjazungumzia hayo maendeleo lazima mkumbuke kuwa elimu ndo msingi mkubwa. leo Tanzania watu kusoma bado wanamambo eti kwanza darasa la saba, then secondary, halafu vyuo au vyuo vikuu. sasa ukiangalia huo wote ni mchujo. shule tu za primary hazitoshi. ni watanzania wangapi au asilimia ngapi wanapata Elimu? wangapi wanabaki nyumbani? Asia na nchi nyingi za ulaya lazima watu wote wasome hadi sec.school, baada ya hapo mtu sasa anafanya mitihani ya kuingia vyuoni, hapo utaona kuwa wengi tayari ubongo umeshakomaa na wanajua nini wanataka, hivyo kuelekea katika mkondo anaoutaka. lakini kwa TZ haya mambo bado ni ndoto. mfano mtu anasoma mechanical engineering wakati hata hatuna kiwanda cha gari si vichekesho hivi!! atapata kazi gani? ataleta maendeleo ganni?
viongozi wote wamesoma katika mfuo huo, wa ndio mzee.! wengi ukiangalia wamedumaa akili, lakini hilo hawataki kulitambua.
LAANA.
kusema waafrica tumelaaniwa ni kujishusha hadhi yako. lazima ujue kuwa unauwezo kama watu wengine! mbona weusiwa mabara mengine wanafanya mambo makubwa. sisi ni siasa mbovu za kubana wengine ili watu wafaidike. mfano ARUMERU baba kafa, sasa mtot anarithi UBUNGE, tutafika? Baba rais watoto mawaziri, kwani tuna ufalme ati tunalithishana?
kuna mengi ya kujifunza lakini yote hayo yanahitaji upeo mkubwa na bila woga..!
tuipende Tanzania yetu na Africa. kamwe hatujalaaniwa.
 
Asante Tibaijuka...mchawi wetu ni aidha elimu yetu au mtazamo wa wasomi wetu...hapa tz tuangalie wenzetu wenye asili ya asia, kijana akihitimu elimu yake anarudi kuimarisha/kuanzisha shughuli za kiuchumi kwao turiani,igunga,sikonge nk. Kitu ambacho sisi hatufanyi au tunaona hakina maana...kijana na degree yake ya umeme anaishia kusumbuliwa/kudhulumiwa ktk viwanda uchwala hapo mbozi road,ingekuwa safi kama angekusanya nguvu akaenda kijijini akaanzisha kahaidro plant ka kufua umeme..mito imejaa bwelele...jamani kuna utajiri wa kutisha tanzania vijijini, unakosa tu jinsi ya kuusimamia/kuuendeleza..SISI NI MATAJIRI ILA TUNAFIKIRI VIBAYA...TUNAKIMBILIA MIJINI NA ULAYA KUWA WATUMWA WA HIYARI..
 
Elimu yetu ina matatizo makubwa sana!
 
mh! Maandeleo africa!!!1
Kabla hamjazungumzia hayo maendeleo lazima mkumbuke kuwa elimu ndo msingi mkubwa. leo Tanzania watu kusoma bado wanamambo eti kwanza darasa la saba, then secondary, halafu vyuo au vyuo vikuu. sasa ukiangalia huo wote ni mchujo. shule tu za primary hazitoshi. ni watanzania wangapi au asilimia ngapi wanapata Elimu? wangapi wanabaki nyumbani? Asia na nchi nyingi za ulaya lazima watu wote wasome hadi sec.school, baada ya hapo mtu sasa anafanya mitihani ya kuingia vyuoni, hapo utaona kuwa wengi tayari ubongo umeshakomaa na wanajua nini wanataka, hivyo kuelekea katika mkondo anaoutaka. lakini kwa TZ haya mambo bado ni ndoto. mfano mtu anasoma mechanical engineering wakati hata hatuna kiwanda cha gari si vichekesho hivi!! atapata kazi gani? ataleta maendeleo ganni?
viongozi wote wamesoma katika mfuo huo, wa ndio mzee.! wengi ukiangalia wamedumaa akili, lakini hilo hawataki kulitambua.
LAANA.
kusema waafrica tumelaaniwa ni kujishusha hadhi yako. lazima ujue kuwa unauwezo kama watu wengine! mbona weusiwa mabara mengine wanafanya mambo makubwa. sisi ni siasa mbovu za kubana wengine ili watu wafaidike. mfano ARUMERU baba kafa, sasa mtot anarithi UBUNGE, tutafika? Baba rais watoto mawaziri, kwani tuna ufalme ati tunalithishana?
kuna mengi ya kujifunza lakini yote hayo yanahitaji upeo mkubwa na bila woga..!
tuipende Tanzania yetu na Africa. kamwe hatujalaaniwa.

Sasa swali ni kwamba kwanini iwe africa? Kwanini isiwe ulaya?
Kwani hao wenzetu viwanda waliletewa toka mbiguni au walitengeneza? Kwanini sisi hatujatengeneza?
Kwanini sisi tuna viongoz wabovu?
Kwanini sisi mfumo wetu wa elimu ni mbovu?
Au tumelaaniwa ndio maana ni sisi sisi sisi black coloured people
 
Ngozi yetu nyeusi na mambo yetu meusi. Shida tupu hii ngozi, mtu mweusi anaenda kuangalia mpira uwanja wa taifa halafu anashika kinyesi (sijui kama ni chake au cha mwingine) anaandikia ukutani na kukojolea masinki ya kunawa. Jamani, hv kweli mtu mweupe anaweza kufanya kitu kama hicho? Kumbe ndo maana hata shetani wanamchora mweusi kureflect laana ya hii ngozi. NGOZI GUNDU HII
 
Nyie kweli vichwa vibovu,yaani mmekaa kabisa mnajiita wajinga na kudharau rangi yenu.sa mnawafundisha nini watoto wenu au ndo mnataka wakubali misaada ya cameroon kwa kuwa ana akili zaidi yao. Dah halafu ni watu wazima kabisa nyie!!!
AM GLAD AM NOT BLACK.
 
Kwa hiyo wewe ulitaka tujisifie wakati tunafanya madudu?
Utawezaje kusonga mbele kama unashindwa kujua na kukubali kuwa some thing is wrong & u must do the right thing.
FYI, self analysiss without being bias ni vitu ambavyo vinafanywa na wanaojiamini.
Ukweli unauma lakini this is our challenge, WE must & WE will face it.
We kaa pembeni.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafakari kwa nini nchi za kiafrika hasa zinazokaliwa na watu wengi wakiwa na ngozi nyeusi tuna matatizo kila kona japokuwa tuna rasilimali nyingi sana zinazoweza kutufanya tuwe matajiri wa kutupwa, mfano Tanzania na madini lakini hamna tunachofanya wakati Afrika kusini imejengwa na dhahabu za J,burg, DRC na utajiri lukuki lakini ona wanavyohangaika.

Aidha, ukiangalia mikataba tunayoingia utadhani Karl Peters na chief Mangungo enzi zile za harakati ya wajerumani kuipata Tanganyika kama koloni lao. Sasa najiuliza au kauli kwamba ngozi nyeusi tumelaanika ni kweli? Naomba michango yenu waheshimiwa.

Shukrani kwa kuleta hoja hiii. La kwanza ni hili: ukiwa na ngozi nyeusi si maana yake ni kwamba umelaaniwa--ni kinyume chake. Kama kuna laana yoyote mbona ingekwisha wapata wazungu siku nyingi sana zilizopita. Ukilinganisha uovu alioufanya mtu mweupe na ule alioufanya mtu mweusi utaona kwamba ktk historia ya binadamu, mtu mweupe amefanya maovu kupita mtu mweusi au mtu mwingine yeyote: ameua sana (k.m tangu warumi hadi wamarekani wa sasa), ametoa sadaka nyingi kwa njia za mauaji, ikiwa ni pamoja na kuteketeza watoto wachanga (hasa enzi za warumi na wagiriki), ameabudu sana miungu na kuwatolea sadaka (miungu kama Zeus, Cleopatra, apollo, columbia, mithra na wengine lukuki--na bado wanaabudiwa kwa njia hasa za kificho), amedharau sana mtu mweusi na kumchukua utumwani, nk nk. Maovu ya mweusi yanayomzidi mweupe na yanayomfanya huyu mweusi astahili laana ni yapi? Mtu mweusi kwa ujumla wake ni mpole na mtaratibu (sawa kuna mafisadi lakini on a larger scale, ni kitu kidogo sana). Watu weupe kwa ujumla wao wanamwelekeo wa kishirikina hasa kwa wakati huu. Niliwahi kusoma chuo kikuu pale ulaya kaskazini (jina la chuo kapuni) na niliona idara za vitivo fulani zinajitambulisha kwa majina ya miungu wao wa kale...picha kama za bundi, mwewe, nyoka nk. Nikaambiwa kuwa bundi ni alama ya hekima. Prof mmoja akaniambia kwamba hapo ulaya miungu wa kale bado wanatawala nafsi zao hata kama kuna dini za kisasa. Akasema utawala huo umo zaidi ktk ngazi ya subconscious kwa hiyo wengine hawajitambui. Kama kuna laana ambayo hutolewa na Mungu basi ulaya ingekuwa tayari imepigwa na laana hiyo zamani.

La pili, sababu ya uduni niionayo mimi ni hii. Kiasili mtu mweusi yupo wired kuiangalia dunia kama kitu ambacho amepokea na hana mamlaka ya kuibadilisha kwa namna yoyote ile. The apparent priciple is: be in the world and let the world shape you instead of you shaping the world. Let the world be the way it is...you have no right to change it...kwa mfano, ukiwa maskini maana yake Mungu kakupangia. Pia kuna dhana kwamba sisi ni watu wa kupita tu kwa hiyo hakuna haja ya kujitaabisha sana eti kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo. Kitu hiki kimo hasa kwenye subconscious ya mtu, na wasomi wa ulaya na marekani wametoa tafsiri zisizofurahisha, eti kwamba mtu mweusi wa kiafrika on average ana IQ ndogo kushinda binadamu wengine wote duniani...kwa hiyo hawezi kufanya kitu kikubwa maana kufanya mambo makubwa hayo ni nje ya capacity yake...ndiyo maana ukigundua mashine au kitu fulani chochote cha maana inakuwa big news na mshangao mkubwa kwa sababu jambo hilo halikutegemewa. Lakini ukweli ni kwamba mtu mweusi ana IQ sawa na watu wengine na anaweza kuwapita watu wengine ikiwa yupo ktk mazingira yanayoruhusu IQ yake kukua. Tafiti za Afrika kusini zimeonyesha kwamba IQ ya mtu mweusi inazidi kuongezeka kwa kasi tangu sera za ubaguzi wa rangi zilipokomeshwa. IQ hiyo iko mbioni kuwaszidi watu weupe...nadhani hii si ajabu...

Halafu baadhi ya wawekezaji toka nje (ulaya au uchina) wamewaona watanzania kama ni watu wavivu na wezi (kwa sababu wanataka njia za mkato kujipatia mapato badala ya kufuata njia ndefu zinazodai taabu na uvumilivu). Sababu ya msingi ndiyo hiyo: mindset.

La tatu, tufanye nini kujikwamua? Kinachotakiwa hapa ni kubadili mtazamo (mindset). Taasisi zilizotumika kubadili mind set kihistoria ni taasisi kama shule, makanisa na misikiti. Waingereza wakati wa Roman empire walikuwa ni watu duni sana kifikra na kimaisha...walianza kuzinduka baadaye na taasisi hizi zilitoa mchango mkubwa ktk kuzinduka huko. Shule ndiyo imekuwa kiwanda muhimu sana katika kumbadili mtoto wa kiingereza kuwa na mindset ya superiority...nimeichunguza mifumo yao toka zamani walipokuwa na makoloni duniani hadi sasa. The school is the most fundamental shaper of mindset. Vyuo vikuu vinafuata. Tanzania imelegeza uzi kwenye elimu. Ili kumbadili mtanzania kifikra kuhusu yeye mwenyewe na kuhusu ulimwengu, ni lazima kufanya mapinduzi katika sekta ya elimu, ikiwa ni pamoja na kurekebisha miundombinu, kuandaa walimu bora na kuwatunza vizuri, kuzingatia sana suala la lugha ya kufundishia, na kucheki malengo ya elimu kwa upya. ifike mahali kwamba mtanzania aliyehitimu ana uwezo wa kujibadili yeye mwenyewe kuwa na hali bora ya kimaisha na pia ana uwezo wa kubadili mazingira yake katika kiwango sawa na mtu mwingine ulaya au kwingineko. Halafu awe ni mtu wa kujiamini na kuipenda sana nchi yake na kuona kwamba ni kichekesho kama nchi tajiri kama Tanzania bado ni tegemezi...kwa hiyo mabadiliko ya fikra ni muhimu na taasisi muhimu katika kuleta mabadiliko ni taasisi ya elimu na mafunzo...
 
Hatuna laana na ondoa kichwani kwako hilo neno laana.Ili uwe na laana ina maana utundikwe juu sasa nani alietundikwa juu akaning inia hadi kufa...
Kumbuka tunazaliwa weupe peeee lakini tunabadirika ukubwani kutokana na hali yetu ya hewa na nk..Pia sisi sio weusi bali ni maji ya kunde kwa kiswahili faswaa
 
Ngozi yetu nyeusi na mambo yetu meusi. Shida tupu hii ngozi, mtu mweusi anaenda kuangalia mpira uwanja wa taifa halafu anashika kinyesi (sijui kama ni chake au cha mwingine) anaandikia ukutani na kukojolea masinki ya kunawa. Jamani, hv kweli mtu mweupe anaweza kufanya kitu kama hicho? Kumbe ndo maana hata shetani wanamchora mweusi kureflect laana ya hii ngozi. NGOZI GUNDU HII

Kwanza, ngozi yako ni utajiri mkubwa sana...watu wengi weusi hawajatambua hilo. Ukiishi ktk mataifa kama ya ulaya utaona hilo. Mtu mweupe anatambua hilo na sala yake kubwa ni kwamba isifike siku ambapo mtu mweusi ataanza kujitambua. Na anajitahidi sana kuona kwamba jitu hili jeusi haliamki. Njia moja wapo ya kukoleza usingizi ni kuifanya dunia iamini kwamba mwafrika bado amelala na hataamka. Kwa mfano, likitokea tatizo kubwa afrika k.m vita unaona BBC wanalitangaza hili kufa na kupona ili kujiridhisha kwamba afrika bado haijaamka. Zile kampeni kwamba mweusi ana IQ ndogo sana zilivumishwa sana kwa lengo hilo hilo, hasa la kumfanya mweusi yeye mwenyewe aamini kwamba yupo low ili abaki pale plae. Lakini mtanzania ukionyesha umahiri wako ktk kukomesha ukoloni kusini mwa afrika, story hiyo haifiki popote maana unatisha. Zamani pale Urusi (soviet union) msomi wa kiafrika ukionyesha uwezo mkubwa katika kufikiri na kuunda mambo ulikuwa hatarini kuudhoofishwa kwa namna yoyote ile au kuuawa kinamna...nawajua walioingia ktk mkasa ule. Sijui kama hali hiyo bado ipo kwa sasa. Sababu ni kwamba wewe mweusi unapotaka kulingana na weupe unatisha...
Story ya woga huu ni ndefu...sote tunatambua kuwa mtu mweusi ndiye aliyetawala dunia zamani...misingi ya hisabati, falsafa, dini, lugha nk. ilijengwa na weusi enzi hizo. Hata wakati wa karibuni wa Roman Empire, nchi ya watu weusi ya Carthage ilikuwa tishio kubwa kwa Roman Empire na ndiyo sababu ya kufanya kila jambo kuiteka. Historia hii inafahamika sana na wasomi wengi wa ulaya na uarabuni kuliko sisi wenyewe. Mimi sikujua kwamba sisi ndiyo tuliojenga misingi ya karibu kila kitu kilichopo duniani sasa, nimeambia na wasomi wakizungu na ndipo nikaanza kufuatilia zaidi. Kwa hiyo sisi ndiyo msingi wa ustaarabu duniani, asia kidogo...mambo yaliyosababisha tuanze kurudi nyuma ni mengi....nitachangia siku nyingine kuhusu hilo...Lakini kwa ujumla, afrika itarudi katika nafasi yake ya kutawala dunia...lakini kinachoiandaa afrika kwa kazi hiyo ni wakati zaidi kuliko watu. Dalili zinaanza kuonekana.

Pili, utaalam unatuonyesha kuwa genetically, sisi tuna nguvu kuliko aina yoyote ya binadamu...biologists wanaweza kufafanua hapa. Kinachokosekana ni KUJITAMBUA na MAARIFA. That's all.

Tatu, tabia ya kutojiheshimu maliwatoni si ya mtu mweusi peke yake...kwani sijaona vitu vyaajabu sana kuliko hicho pale ulaya ya kaskazini (the so called "the most civilized part of europe?). Nenda kaone kinachoendelea ktk vyoo vya wanafunzi hasa wale wa kiume. Wanaweza kukuchora wewe mtu mweusi kwa kutumia kinyesi hichohicho na kuweka maandishi "negro". Tumeyaona hayo. Kwa kusema hayo sina maana kwamba ni mambo yanayofaa...ila nakukosoa unapodhani kwamba hiyo ni tabia ya mtu mweusi pekee.

Mwisho, michoro ya shetani inayochorwa kwa rangi nyeusi, kwa sehemu kubwa, ni katika kutafuta scapegoat. Yaani unapunguza matatizo yako ya kisaikolojia kwa kumsema vibaya kuhusu mtu mwingine. Ukishafanya hivyo basi unajisikia umepoa kidogo...suala zima la racism ni ktk kutafuta mchawi...
 
Ngozi yetu nyeusi na mambo yetu meusi. Shida tupu hii ngozi, mtu mweusi anaenda kuangalia mpira uwanja wa taifa halafu anashika kinyesi (sijui kama ni chake au cha mwingine) anaandikia ukutani na kukojolea masinki ya kunawa. Jamani, hv kweli mtu mweupe anaweza kufanya kitu kama hicho? Kumbe ndo maana hata shetani wanamchora mweusi kureflect laana ya hii ngozi. NGOZI GUNDU HII

kaka umesahau mpaka kung'oa viti na taps chooni na hata kuingiza idadi ya watu waliyozidi kiwango cha kiwanja chenyewe! sijui watu weusi tuna nini kweli?! mimi huwa najiuliza sana! halafu ukiangalia ni kila sehemu/ jamii ya mtu weusi iko shagalabagala tu.
 
Nyie kweli vichwa vibovu,yaani mmekaa kabisa mnajiita wajinga na kudharau rangi yenu.sa mnawafundisha nini watoto wenu au ndo mnataka wakubali misaada ya cameroon kwa kuwa ana akili zaidi yao. Dah halafu ni watu wazima kabisa nyie!!!
AM GLAD AM NOT BLACK.

mankind, tunachojaribu hapa nikujiuliza ni kwanini watu weusi always tuko nyuma kuliko wenzetu? hili ni swali muhimu sana kama kweli tuna nia ya kuwafikia wenzetu kimaendeleo. community zote wanazoishi watu weusi ziko nyuma kimaendeleo na zenye umaskini wa hali ya juu sana. nafikiri mtu mzima yoyote inafaa akae chini na kujiuliza hili swali.it is mandatory if he/she is really serious about africa and all africans at large.

why us? why black people? what went wrong? why can't we catch with rest of the world? by the way, ni kwanini mpaka tumefikia kupewa na kulazimishwa misaada ya watu kama cameroon?
 
Sasa ni muda mwafaka kuanza kutafuta mchawi...Usijali, subiri zamu yako itafika tu...hata wakati ule mababu zako walipokuwa wanatawala dunia, watu weupe walikuwa mbumbumbu, walidharauliwa sana na mtu mweusi, walipigwa sana kwenye vita, waliishi kwenye mapango na vijumba vyao vya kimaskini...hawakuwa na maarifa yoyote. Zamu yao ilipofika, wakaamka na kurudisha kisasi pale Carthage, Misri nk. (Ethiopia walishindwa). Kuangamizwa kwa miji yetu ya kale k.m Kilwa ni mwendelezo wa hasira zilezile. Kufuta historia ya mtu mweusi ktk vitabu, na kubadili sura za farao na miungu ionekana kama kama wao ni sehemu ya vita hiyo (Read "The black athena" written by a white american scholar). Lakini zamu yako itakurudia ya kutawala mambo mengi ktk ngazi ya kidunia...naomba ukishapata zamu ile, tumia vizuri, usiwanyanyase wengine...hapo utadumu ktk power kwa muda mrefu...use Good not evil as the only source of your power.

To catch with the rest of the world isn't an issue because the rest of most of the developed world is about to collapse....you know what I mean? The issue ni maendeleo ya aina ambayo mwafrika anayahitaji...anaweza kuchukua direction ya kwake...si lazima kuwa kama Belgium au Germany...wao wanahistoria zao. Anza na taasisi zinazotengeneza watu wanaoweza kutengeneza mabadiliko--yaani shule na vyuo---huko ndiko kwenye siri haswa. Lazima uunde kitu ili kielee.
 
hapa mnaleta mambo ya how europe under developed africa by walter rodney!!
Hata mimi nimesoma hicho ktabu ambapo rodney amejaribu kujustify kwamba matatzo tulio nayo yamesababishwa na hawa wazungu kwa kujaribu kuonesha shughuli za kiuchumi na kijamii pamoja na science iliyokuwepo afrika hata kabla ya kuja kwa wazungu.
Lakini mpaka leo kuna swali najiuliza? Ni miaka mingapi toka tupate uhuru toka kwa hao wazungu?
Ebu angalia south africa. Nadhan ingekuwa bado iko mikononi mwa makaburu (ngozi nyeupe) leo hii south africa ingekuwa iko mbali sana tena sana. Haina shaka south africa wakati wanabadili regime ya uongozi toka kwa makaburu kuja kwa waafrika ilikuwa ina uchumi na ilikuwa bora zaidi ya ilivyo sasa.
Lakini ndani ya miaka kumi na nne nadhan south africa mambo yake hayako sawa na miaka kadhaa mbeleni itakuwa nyuma zaidi maana hata kile kilichopo ni msingi uliojengwa na makuburu.
Ukiacha nchi za mashariki ya kati, nadhan africa ndilo bara linaloongoza kuwa na resources nyingi, mafuta, madini na kila kitu. Nadhan hakuna kitu kinachokosekana africa hata kama wazungu walivuna still waliacha mengine hata hajagunduliwa.
Lakini still hizo resources bado hazijaweza kumnufaisha mwafrica na bado tu masikini sana.
Kwa wanao dai kwamba tatizo ni uongozi wala hatujalaaniwa, basi mimi nawajibu laana yetu ilikuwa ya kwamba hatutakuwa na uongozi bora hivyo fact inabaki bado kuwa laana.
Kwa wanaodai kwamba weupe wanatunyonya na sasa wamekuja na neo colonialism basi mimi na conclude labda waafrica tupo kutawaliwa na kuwa supplier wa raw materials mbona asia hawanyonywi kama sisi?

Kwenye tears of the sun jamaa alisema hivi GOD HAS ALREADY FORGOTEN ABOUT AFRICA. Sitaki kuamin kama ni kweli

mkuu, labda tujiulize tena uhuru tuliopewa ni upi? ikiwa tupo katika umoja wa nchi za mataifa bei tunapangiwa viwango tunapangiwa na sheria mbalimbali za watu zatuongoza?
nakubaliana na wale waliosema kuwa baada ya kuja wao na kujua udhaifu wetu ndio maana wanaendelea kututawala kwa aina ya elimu tunayopata, na imani na vingine vingi.tutaendeleaje?
saisa ya watu democrasia, technolojia ya watu hatuwezi kugundua vyetu ikiwa tunafundishwa namna ya kugundua.
haya tukinunua vitu vya technolojia wanatuchakachua na pengine kuvitumia hatuwezi tunaharibu basi sisi ni swala katika simba tutatoka kirahisi hatuna laana yoyote hila za watu wengine wajanjanwajanja waliotuwahi, maisha kama mchezo kuwahiana ni techniques kila mtu ana zake. leo hii tazama africa itatokea mlango gani labda tufute kabisa uhusiano na hawa watu tupate changamoto na akili ya kuzitatua itapatikana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom